* Niwakati mwingine tena Vodacom Tanzania imewaletea wateja wake na watanzania wote kwa ujumla promosheni mpya kabambe kabisa inayojulikana kama Tusua Mapene. Promosheni hii itawawezesha wateja wetu na wananchi wote kwa wale ambao watajiunga na mtandao wetu kushiriki katika bahati nasibu na kujishindia vitita mbalimbali mpaka kiasi cha shilingi milioni 150 ndani ya siku 150.
* Promosheni hii inampa mteja wa vodacom fursa ya kushiriki kupitia ujumbe mfupi wa maneno, huduma ya M-pesa au mitandao ya kijamii.
*Vodacom itatoa mshindi mmoja wa Sh. 100M/-, washindi watano wa Sh. 20M/- na mshindi moja wa Sh. 15M/- KILA SIKU na mshindi wa mwisho wa promosheni(Grand draw) atajishindia kitita cha shilingi Million 150/-
*Jinsi yakushiriki katika promosheni hii ni rahisi sana mteja anachotakiwa kufanya ni kutuma neno “CHECK” au “VODA” kupitia ujumbe mfupi wa maneno kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu ikijumuisha kodi kwa kila ujumbe.
Meneja huduma za Ziada na Tehama wa Vodacom Tanzania,Mathew Kampambe(kushoto) na Msimamizi wa michezo ya kubahatisha nchini,Abdallah Hemed(kulia)wakimsikiliza Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu(katikati)alipokuwa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya Tusua Mapene inayoendeshwa na kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam leo ambapo mkazi wa mkoa wa singida Munira Jumanne alijishindia Tsh. Laki 5/- Ili Mteja wa Vodacom aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.
Meneja huduma za Ziada na Tehama wa Vodacom Tanzania,Mathew Kampambe(kushoto) na Msimamizi wa michezo ya kubahatisha nchini,Abdallah Hemed(kulia)wakionyeshwa na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu(katikati) namba ya simu ya mshindi aliejishindia Tsh. Laki 5/- Munira Jumanne Mkazi wa Singida wakati wa Uzinduzi wa Promosheni mpya ya Tusua Mapene inayoendeshwa na kampuni hiyo uliofanyika jijini Dar es salaam leo. Ili Mteja wa Vodacom aweze kushiriki kwenye promosheni hii anatakiwa kutuma neno “CHECK” au “VODA” kwenda namba 15544, kwa gharama ya shilingi 300 tu.
No comments:
Post a Comment