Tuesday, August 15

Mrithi wa Mugabe apelekwa Afrika Kusini kwa matibabu

Makamu wa rais wa Zimbabwe Emmerson MnangangwaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMakamu wa rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangangwa
Mmoja ya watu wanaotarajiwa kumrithi rais Mugabe wa Zimbabwe amekimbizwa nchini Afrika Kusini kwa matibabu kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Emmerson Mnangangwa ambaye ni makamu wa rais wa Zimbambwe alikuwa mgonjwa ghafla wakati wa mkutano wa hadhara siku ya Jumapili.
AFP imemnukuu waziri wa Afya David Parirenyatwa akisema: Anaendelea kupata nafuu.
''Alikuwa akitapika na kuharisha na kukosa maji mwilini. Amefanya vipimo vingi''.
Rais Mugabe mwenye umri wa miaka 93 amesema kuwa atatetea wadhfa wake wakati wa uchaguzi wa mwaka ujao.

No comments:

Post a Comment