Wednesday, August 2

Mkurugenzi wa FBI apatikana



Christopher Wray

Christopher Wray 
Washington.Bunge la Seneti nchini Marekani limepiga kura ya kumthibitisha Christopher Wray kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Kijasusi la Marekani la FBI.
Nafasi hiyo ilikuwa wazi tangu James Comey alipoondolewa kwenye wadhifa huo na  na Rais Donald Trump  Mei.
Aliondolewa baada ya  uchunguzi aliokuwa akiufanya kuhusu Urusi kuingilia uchaguzi wa nchi hiyo uliompa ushindi   Trump.
Christopher Wray ni mmoja wa maofisa wa ngazi za juu wa mahakama ya nchi hiyo ambaye amefanya kazi chini ya Rais George Bush.

No comments:

Post a Comment