Mbeya. Wakati ugonjwa wa kipindupindu ukiendelea kuwatesa wananchi wa Wilaya ya Mbarali mkoani hapa, ugonjwa huo umepiga hodi ndani ya jiji la Mbeya na hadi leo Alhamisi wagonjwa watano waligundulika.
Meya wa jiji hilo, Mchungaji David Mwashilindi amebainisha hilo leo kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Madiwani la jiji hilo la linaloketi kwa ajili ya kupitia taarifa mbalimbali za mwaka wa 2016/2017.
Meya Mwashilindi alisema tayari ugonjwa upo kwenye kata za Iyela, Ilemi na Iganjo na wagonjwa hao wametoka katika kata hizo, hivyo aliwataka madiwani kuhakikisha wanatoa ushirikiano kwa wataalamu na wananchi kudhibiti ugonjwa huo.
“Ndugu zangu tayari ugonjwa huu umeingia ndani ya jiji letu na wagonjwa watano wamegundulika kupata kipindupindu. Hivyo basi ninaona madiwani tuhakikishe tunatoa kila aina ya ushirikiano kwa wataalamu wetu wanaofika kwenye maeneo yenu kuchukua hatua mbalimbali dhidi ya ugonjwa huu kwa wananchi,” alisema meya huyo.
No comments:
Post a Comment