Kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi amesema tukio hilo limetokea jana Agosti 21 saa mbili asubuhi katika kitongoji hicho.
Amesema kwamba mtuhumiwa huyo alipigwa fimbo na mawe sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kumchomwa moto.
Kwa mujibu wa Kamanda inadaiwa marehemu aliiba kuku hao katika kijiji cha Ngulla kisha kukimbia nao katika kijiji jirani cha Mwabomba ambapo walimshuku kisha kumkamata na baadaye walitoa taarifa kijiji cha Ngulla ambapo mwenye kuku hao alifika na kuwatambua.
Inadaiwa kuwa baada ya marehemu kukabidhiwa kuku hao wananchi walimchukua kwenda naye kituo cha polisi lakini wakiwa njia walianza kumshambulia kwa kumpiga fimbo na mawe kisha kumchoma moto.
Amesema wakati polisi wakiendelea na uchnguzi na kuwasaka watu wengine mwili wa marehemu tayari umekabidhiwa kwa ndugu tayari kwa mazishi.
No comments:
Post a Comment