Kumekuwepo na upotoshaji wa mafunzo ya utarajali (Internship programme) bila malipo yaani fedha za kujikimu wakati wa mafunzo hayo kwa baadhi ya wanaotarajia kuanza mafunzo kwa vitendo mapema mwaka huu.
Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto inapenda kuwajulisha kwamba kwa sasa hakuna ‘intern’ aliyepangiwa kuanza mafunzo hayo kwani tunasubiri watoke waliopo kwenye mafunzo.
Barua iliyodukuliwa na kusambaa kwa lengo la kupotosha wataraji hao ilikuwa ni kwa ajili ya wataraji (intern) kutoka nje ya nchi ambao kwa sheria hawalipiwi na Serikali ya Tanzania.
Aidha wapo ‘intern’ wawili ambao wanasoma nchini China na mwingine Algeria masomo yao yalihitaji mafunzo kwa vitendo kabla ya kumaliza na kwa kuwa ilikua lazima warudi vyuoni mwezi Oktoba waliomba kufanya mafunzo hayo kwa kujigharimia pamoja na kuwa ni watanzania na wazazi wao walikuwa wameridhia hilo kwa maandishi ili warudi mapema kumalizia program yao ya udaktari.
Hivyo ni watanzania wawili tu wameshapata barua yenye kuwataka kujilipia kwa mazingira hayo hakuna wengine waliyepewa barua ya kuruhusiwa kwenda mafunzo ya utarajali (internship) bila malipo.
Imetolewa na;
Nsachris Mwamwaja
Mkuu Kitengo cha Mawasiliano Serikali-Afya
30/7/2017
No comments:
Post a Comment