Wednesday, June 28

NGUVU KAZI YA TAIFA INATEKETEA KWA MATUMIZI YA DAWA ZA KULEVYA- RC DODOMA


Na Chalila Kibuda, Dodoma

Vijana wengi wanaangamia kutokana na kutumia dawa za kulevya na kufanya taifa kukosa nguvu kazi ya kufanya uzalishaji.

Hayo ameyasema leo Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Jordan Rugimbana wakati wa uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square mkoani hapa, amesema kuwa vijana kuwa na familia wameshindwa kuwa wazalishaji kwa kuishia katika matumizi ya dawa za kulevya.

Amesema vita ya dawa za kulevya ilishatangazwa na Rais Dk. John Pombe Magufuli na wengine ni kufanya utekelezaji kuhakikisha linafanikiwa dhidi vita ya dawa za kulevya.

Rugimbana amesema kuwa Dodoma inalengwa na kuwindwa kutokana na vyuo vingi kuwepo hali ambayo vijana wanaweza kungeuka na kujiingiza katika matumizi ya dawa za kulevya.

Katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa amepiga marufuku matumizi ya shisha katika hoteli zilizopo katika mkoa wake kutokana na kuwa sehemu ya dawa za kulevya.

Aidha amemuomba Mkurugenzi wa Life and Hope Sober House ya Bagamoyo, Al- Karim Bhanji kujenga sober house katika mkoa wa Dodoma kutokana na kuwepo kwa kundi la vijana ambao wameathrika na matumizi ya dawa za kulevya.

Bhanji amesema kuwa wanaangalia uwezo katika kuweza kujenga kituo ili kuweza kuwarudisha vijana kutoka katika matumizi ya dawa za kulevya na kuwa wazalishaji katika taifa lao.

Amesema kuwa vijana wanaathirika sana na matumizi dawa za kulevya na kufanya familia zao kuwa na mzigo wa kuwategemea wazazi wakati wazazi hao walitakiwa kusaidiwa na vijana wao.

Katika maonesho hayo yameshirikisha umoja wa vituo vya kuhudumia walioathirika na dawa za kulevya Voice of Sober Houses (VOS).
Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini, Rogers Sianga akipeana mkono na Mkurugenzi wa Life and Hope, Sober House ya Bagamoyo, Al- Karim Bhanji jana wakati maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma Jana.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akipeana mkono na Mkurugenzi wa Life and Hope, Sober House ya Bagamoyo, Al- Karim Bhanji wakati alipotembelea banda la Life and Hope, Sober House ya Bagamoyo katika maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akipata maelezo katika banda la Kitengo cha Kupambana na Dawa za Kulevya kutoka kwa Mkaguzi wa Jeshi la Polisi Kitengo cha Kudhibiti Dawa za Kulevya, Anastazia Sauli katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma , Jordan Rugimbana akizungumza na katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma .


Kamishina Msaidizi wa Idara ya Kinga , Tiba na Utafiti ,DK. Cassian Nyadindi akitoa maelezo juu ya madhara ya matumizi ya dawa za kulevya katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.


Wananchi waktembelea mabanda mbambali juu ya huduma wanazozitoa katika uzinduzi wa maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.

 Picha ya pamoja.

Sehemu ya wananchi wakiwa katika maadhimisho ya siku ya kupiga vita dawa za kulevya Duniani yaliyofanyika katika Viwanja vya Nyerere Square Mjini Dodoma.



No comments:

Post a Comment