Arusha. Binti wa Waziri mkuu wa zamani, Edward Sokoine, Namelock Sokoine ameshinda kura za maoni kugombea ubunge Jimbo la Monduli kupitia CCM huku mkwe wa Lowassa, Siyoi Sumari akishindwa Jimbo la Arumeru Mashariki.
Namelock ambaye ni mbunge wa Viti Maalumu (CCM) alipata kura 29,582 akifuatiliwa na Loota Sanare aliyepata kura 8,809 na nafasi ya tatu, ilichukuliwa na Lolinyu Mkoosu aliyepata kura 235 na Payani Leyani akipata kura 226.
Arumeru Mashariki: Sumari aliyewania jimbo hilo kwa mara ya kwanza baada kifo cha baba yake Jeremia Sumari na kushindwa na Joshua Nassari wa Chadema alipata kura kura 3,664 dhidi ya 12,071 za John Pallangyo. Mshindi wa tatu alikuwa ni William Sarakikya ambaye alipata kura 3,552 na wagombea hao waliwaacha mbali wapinzani wao wengine wanne.
Arusha Mjini: Katika Jimbo la Arusha Mjini, mfanyabiashara Philemon Mollel ameshinda kwa kura 5,320, akifuatiliwa na mfanyabiashara mwingine Justine Nyari aliyepata kura 1,894 na nafasi ya tatu, ilichukuliwa na Moses Mwizarubi aliyepata kura 1,205.
Karatu: Dk Willibrod Lorry alishinda baada ya kupata kura 17,711, Rajabu Malewa (911), John Dado (745) na Joshua Mwambo (67).
Masele ambwaga Mlingwa
Naibu Waziri, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Steven Masele amembwaga waziri mwingine wa zamani, Dk Charles Mlingwa baada ya kupata 70,900 dhidi ya 669 za mpinzani wake. Wagombea wengine Abdallah Seni alipata kura 391, Erasto Kwilasa (232), Hassan Athuman (164), Mussa Ngangala (116), Hatibu Malimi (69), Wille Mzava (65) na Tara Omari (43).
Ushetu: Elias Kwandikwa (11,554) Isaya Sino (5,241) na Elfaidi Sikuli (2,007).
Kahama Mjini: Jumanne Kishimba (9,754), Kintoki Godwin (433), Nkuba Charles (389), Bundala Maiko (284), Sazia Robert (257), Kapela Robert (135), Ngalawa Adamu (126), Luhende Jerard (106), Malele Charles (91), Tunge John kura (78), Mpangama Deogratias (57), Machunda Eliakimu (56), Masanja Andrew (48) na Kambarage Masusu (28).
Msalala: Ezekiel Maige (11,575), Emmanuel Kipole (1,197), John Sukili (962), Nicholas Mabula (668), Maganza Mashala (597), John Lufunga (29) na Wankia Welema (14).
Solwa: Mbali ya matokeo ya kata moja ambayo imerudia uchaguzi, Ahamed Salum alikuwa akiongoza kwa kura 17,485 akifuatiwa na Amos Mshandete (2,028), Cyprian Mhoja (1,586), Luhende Richard (1,273), Kasile Paul (637), Gabriel Shija (361), Renatus Chokala (357) na Hosea Somi (255).
Kishapu: Kabla ya matokeo ya kata tatu, Suleiman Nchambi alikuwa akiongoza kwa kura 13,443, William Bonda (6,143), Kishiwa Kapale (500), Limbe Moris (393), Heke Bulugu (356) na Timoth Ndanya (193).
Mawaziri watamba Kanda ya Ziwa
Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, Dk Titus Kamani ameshinda kura za maoni Jimbo la Busega baada ya kupata kura 10,697 dhidi ya mbunge wa zamani wa jimbo hilo, Dk Rafael Chegeni aliyepata kura 9,661. Buchosa: Naibu Waziri wa Uchukuzi, Dk Charles Tizeba ameibuka mshindi kwa kupata kura 26,368 dhidi ya Eston Majaliwa aliyepata 9,213.
Misungwi: Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Charles Kitwanga ameibuka mshindi kwa kura 26,171, akimwangusha Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Jacob Shibiliti aliyepata kura 7,009. Shomari Chalamila alipata kura 1,840, Dk Makene Doshi (1,339), Cleophace Jerome (1,051).
Ilemela: Mkuu wa Wilaya ya Iringa Angelina Mabula ameibuka mshindi katika Jimbo la Ilemela kwa kupata kura 6,324 mbele ya Barnabas Mathayo (3,562), John Buyamba (1,167) na wagombea wengine 16.
Tabora Kaskazini: Almasi Maige (9,466), Shaffin Sumari (6,392) na Joseph Kidawa (5,965).
Bariadi: Andrew Chenge (20,200), Masanja Kadogosa (2,986) na Cosmas Manula (270).
Meatu: Salum Mbuzi (13,180), Oscar Maduhu (2,988), Romano Thomas (358) na Donard Jinasa (350).
Itilima: Njallu Daudi (44,486), Simon Ngagani (2,759) na Danhi Makanga (814).
No comments:
Post a Comment