Baada ya taarifa kuenea kwamba mwigizaji Ray anahusika moja kwa moja na kifo cha mwigizaji marehemu Steven Kanumba, mwigizaji huyo amezungumza kwenye AMPLIFAYA ya CLOUDS FM na Millard Ayo na kusema yafuatayo:
“...nimekuqa nikizisikia sana hizi tuhuma, sio kweli kwa sababu Kanumba ni mdogo wangu wa karibu sana tumetoka mbali sana kimaisha mimi na yeye, nimekua na mazoea ya kuona vitu kila siku vinaandikwa ambapo juzi nilipigiwa simu na kuambiwa nitazame kwenye blog ya U-Turn ambayo anaimiliki huyu dada ambaye simfahamu anaitwa Mange Kimambi”
“...alikuwa ameandika kwamba amepata taarifa kutoka kwa polisi mmoja wa Oysterbay kwamba Ray ndio aliyepiga simu kwa Lulu siku ya kifo cha Kanumba kwa hiyo Lulu ametumika kufanya mauaji bila kujijua, na pia kukawa kuna swali kwamba kwa nini Ray alikua wa kwanza kufika kwa marehemu Kanumba. Mungu ndie anaejua...”
“...kwa hiyo anataka kuwadhihirishia Watanzania kwamba Ray ndiyo anahusika na hicho kifo, baada ya hilo nimeshirikiana na polisi na kushitaki na kufungua kesi ambapo hivi sasa ninapozungumza yupo polisi Oysterbay akihojiwa kwa sababu ameandika kitu ambacho bado kipo ndani ya uchunguzi, hana uhakika nacho sijui Lulu amekamatwa Coco Beach which is not true, sijui hizi habari kaipata wapi...”
“...sasa hii ni kutaka kunivunjia heshima, mimi nafanya kazi ya kuigiza ndio maisha yangu unapoandika kitu kama hicho kwenye internet inafika sehumu kubwa dunia nzima, sasa unategemea watu wanichukuliaje kama sio kunivunjia heshima, kunipotezea mashabiki wangu… nasema hili sitoweza kuliacha, nitalifanyia kazi na nitalifikisha mahakamani ili iwe fundisho, sitolichekea...”
Kwenye sentensi nyingine Ray amesema baadhi ya maoni yaliyotolewa na watu mbalimbali kwenye hiyo habari iliyoandikwa kwenye blogu hiyo, “maoni niliyoyasoma mengine yanamwambia yule dada kwamba anachokiandika kinaweza kum-cost kwenye maisha yake, na nyingine zinasema kwamba tuko tayari kumvamia Ray na kumuua, sasa hichi kitu ni hatari sana kwenye maisha yangu kwa hiyo nimemshitaki polisi na kuandika kwa kusema chochote kitakachonikuta hata nikipigwa jiwe na kuanguka mimi na-deal na huyo mwanamke kwa sababu yeye ndio mtu aliye-publish hivyo vitu watu wanichukulie mimi vinginevyo kabisa tofauti jinsi nilivyo na sihusiki kabisa na hicho kifo, kimsingi maisha yangu yapo hatarini lakini nasema haya ni maisha nitaendelea kuvumilia...”
No comments:
Post a Comment