Tuesday, May 19
SPIKA JOB NDUGAI AONGOZA KIKAO CHA KAMATI YA UONGOZI, AZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DODOMA
Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na waandishi wa habari katika kikao kilichofanyika leo nyumbani kwake uzunguni Jijini Dodoma. Mmoja ya agenda ya kikao hicho ilikuwa ni kupokea Mapendekezo ya Mabadiliko ya Ratiba ya Mkutano wa 19 wa Bunge.
Wajumbe kamati ya uongozi wakimsikiliza Spika wa Bunge, Mhe. Job Ndugai wakati wa kikao cha kamati hiyo kilichokaa ili kupokea Mapendekezo ya Mabadiliko ya Ratiba ya Mkutano wa 19 wa Bunge leo nyumbani kwake uzunguni Jijini Dodoma.
Monday, May 18
FIHIR MVUNGI: DIWANI ALIYEONGOZA KATA YA MSANGENI KWA MIAKA 55, BADO ANATAKA KUENDELEA AKIWA NA UMRI WA MIAKA 80
*Hajawahi kung'atuka wala kuondolewa, afikiria kugombea tena mwaka huu, azungumzia thamani ya Mzee Msuya wilayani Mwanga
Charles James, Michuzi TV
JINA lake ni Fihir Mvungi, umri wake ni miaka 80. Ameongoza kwa miaka 55 kama Diwani wa Kata ya Msangeni iliyopo wilayani Mwanga, Kilimanjaro.
Ndio. Unaweza kusema Mvungi ndiye kiongozi wa kuchaguliwa ambaye amehudumu kwenye nafasi yake kwa muda mrefu bila kung'atuka wala kuondolewa na wananchi.
Katika mahojiano maalum ambayo amefanya na Michuzi Blogu, Mvungi anaeleza kuwa moyo wa utumishi alionao, upendo kwa wananchi wake ni sababu zinazomfanya aendee kuwa Diwani wa kata hiyo ya Msangeni kwa muda mrefu.
Diwani huyu aliingia kwa mara ya kwanza kwenye nafasi yake mwaka 1965 akiwa kijana mdogo wa miaka 25 baada ya kugombea nafasi hiyo kwa mara ya pili baada ya kugombea 1962 na kuikosa.
" Kwanza niligombea mwaka 1962 lakini nilikosa nafasi hiyo, lakini nilipogombea tena 1965 nilipita bila kupingwa. Toka hapo nimekua diwani wa kata hii toka kipindi hicho.
Lakini wakati nachaguliwa Wilaya ilikua ni moja tu, bado wilaya ilikua ni Same. Haikua imegawanywa kama sasa ambavyo ni Same na Mwanga. Hivyo nimeongoza kwa kipindi chote hicho hadi leo," Anaeleza Mvungi.
Diwani huyu pia ameweka rekodi yake ya kufanya kazi na marais wa awamu zote tano kuanzia Mwalimu Nyerere hadi sasa chini ya Rais Dk John Magufuli ambaye yeye Mvungi anamuona kama kiongozi mwenye maono mengi ya kiuongozi.
SIRI YA KUDUMU MUDA MREFU
Mvungi anasema uwezo wake wa kushirikiana na watu wake katika Matatizo na raha, kuwasaidia kupata maendeleo na kuwaletea pindi inapobidi ni sababu zingine zinazomfanya aendelee kuongoza kwa kipindi kirefu tofauti na madiwani wengine.
Anasema kazi ya uongozi haijawahi kumletea fedha lakini yeye anaifanya kwa moyo mmoja bila kunung'unika kwani anaamini nafasi aliyopewa na wananchi wa kata yake imetokana na moyo wa uaminifu walionao kwake.
" Ningeweza kuitumia nafasi yangu kujinufaisha lakini inamaana gani kama wewe unaishi maisha mazuri ilihali watu waliokuchagua wanalalamika? Mimi ni mtu ambaye naitazama kesho yangu zaidi kuliko leo.
Unadhani ningekua mtu wa kujinufaisha mwenyewe ningekaa kwenye uongozi tena wa kupigiwa kura kwa muda wote huu bila kuondolewa?
Kuna watu wana kipato kikubwa kuliko mimi, ingekua ishu ni fedha wangeshanitoa. Lakini wananchi wangu wamewekeza uaminifu kwangu. Wananiamini na mimi nawafanyia kazi yao ipasavyo," Anasema Mvungi.
Anasema ndani ya miaka 55 aliyodumu amesaidia upatikanaji wa Shule Nne za Sekondari zenye mahitaji karibu yote kwa asilimia 90 pamoja na Zahanati ambazo zinawahudumia wananchi wake bila matatizo.
Anaeleza Zahanati Moja ya Sungo ndio inayomuumiza kichwa maana haina nyumba ya Daktari lakini anaamini mwaka huu hautoisha atakua imeshajengwa.
Kuhusu Miundombinu Mvungi anasema hakuna barabara ambayo haijajengwa kwenye Kata yake. Tena anaeleza suala la barabara sio ajenda kabisa kwenye Wilaya ya Mwanga.
Anasema Wilaya ya Mwanga licha ya kuwa milimani lakini ina Lami kutokea Barabara kuu ya Moshi-Dar es Salaam hadi vijijini huko na wala hapajawahi kuwa na changamoto hiyo.
Kata yake pia kila kaya inawasha umeme. Hakuna nyumba ambayo ina changamoto ya umeme wala haipo ambayo inawasha kibatari kwa kukosa umeme.
Hii inaonesha jinsi gani miaka 55 aliyodumu amemaliza changamoto zinazogusa maisha ya binadamu Moja kwa Moja.
Kutokua na changamoto ya Maji, Afya, Elimu, Miundombinu na Umeme ni uthibitisho tosha kwamba miaka 55 aliyoongoza kata hiyo amelet maendeleo ya kuridhisha kwa wananchi wake.
ANAMUONGELEAJE MSUYA.
Wilaya ya Mwanga ni mojawapo ya Wilaya ambazo zimebarikiwa kutoa viongozi wakubwa nchini ambao wamewahi kushika nafasi za juu za kiuongozi nchini.
Waziri Mkuu Mstaafu, Cleopa David Msuya ambaye ana rekodi ya kuongoza katika Serikali mbili ya awamu ya kwanza chini ya Mwalimu Nyerere na ya pili chini ya Alhaji Hassan Mwinyi kwao ni Mwanga.
Mwanamke wa kwanza kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ni Asha-Rose Migiro ambaye kwa sasa ni Balozi wa Tanzania nchini Uingereza. Huyu nae kwao ni Mwanga.
Profesa Uruma wa Makinikia, Waziri wa zamani wa Habari, Phenela Mkangala, Waziri wa zamani wa Utalii na Elimu, Prof Jumanne Maghembe. Ni baadhi ya viongozi wanaotoka Mwanga.
Turudi kwa Msuya: Napenda kujua namna ambavyo Jamii ya Wapare ambao ndio hasa wazawa wa Mwanga wanavyomtazama lakini pia Mkoa wa Kilimanjaro kwa ujumla.
Mvungi anasema mafanikio yote ya Mwanga na Kilimanjaro yalichangiwa na Msuya akiwa Mbunge na Waziri Mkuu.
Namna ambavyo Mwanga usiku inapendeza kwa mwanga wa Umeme na siyo kibatari, namna ambavyo licha ya Milima ya Usangi na Ugweno ilivyo mikubwa na barabara inapitika tena ya lami ni wazi heshima na sifa vinapaswa kurudi kwa Msuya.
Anasema simu za mikononi kwao zilikuepo toka zamani, changamoto ya Shule, Afya na miundombinu mingine ilimalizwa na Msuya katika utumishi wake.
" Kama Nyerere ni Baba wa Tanzania, kwa hakika Mzee Msuya ni Baba wa Mwanga. Wanasema Nabii hakubaliki kwao lakini Msuya anakubalika kwenye kila moyo wa mwana-Mwanga.
Ukitaka upigwe n uchakae zungumza maneno mabaya ya kumhusu Msuya hapa Mwanga. Tunafahamu yeye ni binadamu na ana makosa yake lakini hapa Mwanga Msuya ni Baba hasemwi hadharani," Anasema Mzee Mvungi.
Anasema Msuya ni vile aliamua kung'atuka mwenyewe lakini tofauti na hapo angeiongoza Mwanga pengine hadi leo. Maana kwa mambo aliyoyafanya hakuna ambaye angethubutu kugombea nae.
" Ukitaka kujua Msuya alikua kichwa tazama ameweka rekodi ya kuwa Waziri Mkuu kwa awamu mbili. Kwa Mwalimu Nyerere na Mzee Mwinyi. Hii ni sifa kubwa na ya kipekee sana. Kuaminiwa na marais wawili haiji hivi hivi," Anasema Mvungi.
JE ANA MPANGO WA KUGOMBEA MWAKA HUU?
2020 huu ni mwaka wa uchaguzi na tayari wanasiasa mbalimbali nchini washaanza kupigana vikumbo kwenye nafasi mbalimbali. Udiwani, Ubunge na Urais.
Mvungi ambaye yeye hajawahi kutamani hata kuwa Mwenyekiti wa Halmashauri anatueleza kama bado anahitaji kuendelea kuongoz kwa kipindi kingine.
" Ujue mimi sikujichagua mwenyewe kuwa Kiongozi, mimi nilifuatwa na watu kuombwa kugombea. Nikagombea na wakanipa kura. Na hata kila uchaguzi huwa siamui mwenyewe kwa utashi wangu nafuatwa kuambiwa nigombee.
Hivyo mwaka huu pia wananchi wangu wakisema endelea nitaendelea, wakisema Mvungi imetosha kaa pembeni nakaa pembeni. Binafsi naamini katika Demokrasia ya kuwaacha wananchi kuamua nani wanataka awaongoze," Anasema Mvungi.
Pamoja na umri wake wa miaka 80 bado Diwani huyu ana kumbukumbu nyingi za mambo ya zamani, ana uwezo wa kusoma bila kutumia miwani lakini hata gari anayoendesha ni 'Manual' jambo ambalo ni tofauti na wazee wengine wa umri wake.
ANAMZUNGUMZIAJE RAIS MAGUFULI?
Ni Kiongozi mzuri, jasiri ambaye akiamua jambo lake basi litatimia bila kujali watu wanasema nini. Ameonesha kwamba anaweza kuleta mabadiliko zaidi ya kimaendeleo ndani ya muda mfupi aliokaa.
Kafufua shirika letu la Ndege, miundombinu ya barabara inajengwa kila kona nchini, elimu bure ambayo inampa fursa kila mtoto sasa kusoma imerejea. Huu ni uzalendo ambao ameuonesha.

Diwani wa Kata ya Msangeni, Fihir Mvungi ambaye amedumu kwenye nafasi hiyo kwa miaka 55 ambapo alianza kuhudumu nafasi hiyo mwaka 1965 akiwa kijana wa miaka 25 na sasa ana miaka 80.
BOB MAKANI- MTANZANIA KIPANGA ALIYEKUWA NA TALANTA LUKUKI NA KUCHEZEA TIMU YA TAIFA YA UGANDA 'GOSSAGE CUP'.
By MZEE WA _ATIKALI ✍️✍️✍️
1. Usuli
Bongolanders walimjua marehemu BOB NYANGA MAKANI kama Mwanasiasa mahiri. Lakini, wengi hawajui kwamba BOB alikuwa ni kipanga aliyejaaliwa talanta lukuki na alifanya mambo mengi ya kipekee na yasiyo mfanowe ikiwemo kuichezea Timu ya Taifa ya Uganda kwenye michuano ya "Gossage Cup" kabla ya Uhuru, licha ya kuwa Mtanzania!.
Hivyo, ATIKALI hii inammyambua marehemu BOB NYANGA MAKANI toka anazaliwa hadi umauti unamfika huku ikitanabaisha talanta zake hizo mujarab.
2. Kuzaliwa kwa BOB
BOB alizaliwa mwaka 1939 huko hospitali ya Kolandoto, Wilaya ya Kishapu, Shinyanga, baba yake akiitwa ALLY MAKANI @"Wakili" kutokana na kujua Lugha 7 ikiwemo Kiingereza na Kiarabu.
3. Elimu ya BOB
3.1 Elimu ya Msingi
Mwaka 1942 akiwa na miaka 6, BOB alianza masomo ya msingi katika shule ya msingi Ibadakuli iliyoko wilayani humo. Alikuwa kijana hodari sana darasani.
3.2 Elimu ya Sekondari
BOB alipohitimu elimu ya msingi alichaguliwa kujiunga na shule maarufu na iliyokuwa bora kuliko zote Tanganyika wakati huo ya "Tabora Boys" baada ya kufaulu vizuri mitihani yake.
4. BOB Awika Tabora Boys
4.1 BOB:- Mwanafunzi Kipanga
BOB alikuwa genius kwani tofauti na wanafunzi wenzake waliokuwa wanalazimika kukesha wakibundi, yeye alielewa darasani na hivyo alihitaji kusoma kidogo tu. Daima aliongoza darasani na mwisho wa kila temu alikuwa akisomba zawadi zote za masomo!.
4.2 BOB-: Mwanamichezo Hodari
4.2.1 BOB-: Bingwa wa Long Jump & High Jump
BOB alikuwa mwembamba mrefu hivyo michezo hii miwili aliimudu vilivyo huku akishikilia rekodi ya Taifa ya Long jump akiwa Mwanafunzi! Aidha, BOB alikuwa pia ni hodari sana wa kufukuza upepo!.
4.2.2 BOB-: Mwanasoka Hodari
BOB alichaguliwa timu ya mpira wa miguu ya shule mara tu alipojiunga ba Tabora Boys kutokana na kipaji chake cha kipekee cha gozi la ng'ombe!.
4.2.3 BOB Aichezea Tabora Michuano ya Sunlight Cup
BOB, licha ya kuwa Mwanafunzi, alichaguliwa timu ya mkoa wa Tabora kwenye michuano ya Sunlight Cup au Taifa Cup kutokana na kuupiga mpira mwingi michuano ambayo Tabora Boys ilikuwa ikishiriki mkoani Tabora. Marehemu MATHIAS KISSA ambaye mwaka 2000 alichaguliwa na TFF kuwa "Mwanasoka Bora wa Karne TZ" pia aliichezea Tabora kwenye michuano hiyo ya Sunlight Cup akiwa mwanafunzi.
4.2.4 BOB & KISSA-: Vipenzi vya Headmaster Mzungu
Headmaster wa shule wa Tabora Boys enzi hizo, mzungu Crabbe, aliwapenda sana BOB na KISSA kwa umahiri wao kwenye kabumbu uliopelekea kuiletea, mara kwa mara, heshma kubwa shule hiyo.
5. BOB Aenda Makerere University
5.1 BOB Apasua paper
BOB alifaulu vizuri sana mtihani wake wa mwisho Tabora Boys na kuchaguliwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda kusomea Uchumi.
5.2 BOB Aendeleza Ukipanga Makerere
BOB, alipojiunga Makerere, aliendelea kuwatimulia vumbi wanafunzi wenzake kimasomo na kufaulu vizuri sana mitihani yake.
5.3 BOB Akonga Nyoyo Michezoni
BOB alikuwa Mwanafunzi maarufu sana Makerere kutokana na ukipanga, wajihi wake na uhodari michezoni kwani talanta zake zliijiweka bayana.
5.3.1 BOB-: Mwanasoka Bora Makerere
Katika michuano mbalimbali ambayo Chuo cha Makerere kilishiriki, BOB alitia fora na bila ubishi akawa ndiye mwanasoka bora kabisa chuoni hapo.
6. KABAKA WA BAGANDA Ampangishia BOB Presidential Suite Hotel ya Kifahali
KABAKA wa BAGANDA ie Sir EDWARD FREDRICK WLLIAM DAVID WALUGEMBE MUTEBI LUWANGULA MUTEESA II, alivutiwa mno na uhodari wa BOB kwenye kabumbu. Hivyo, KABAKA akamtoa BOB bwenini Makerere na kumpangishia chumba maalum Presidential Suite kwenye hotel ya Grand Imperial Hotel iliyokuwa nzuri kuliko zote jijini Kampala enzi hizo. KABAKA akampatia BOB Coupon ambapo BOB aliweza kula na kunywa chochote alichokitaka hotelini hapo bila kulipa!. BOB, kwa hakika, licha ya kuwa mwanafunzi, akaishi maisha ya anasa sana!.
7. BOB Achaguliwa UGANDA CRANES
BOB alichaguliwa timu ya Taifa ya Uganda (Uganda Cranes) ambapo KABAKA alimwezesha kupata passport na hivyo akashiriki michuano ya Gossage Cup iliyoshirikisha Uganda, TG, Kenya na ZNZ.
Katika hali ya kustaajabisha, Mtanzania BOB akawa anaichezea Uganda ambayo ilikuwa ikiionea mara kwa mara Tanganyika iliyokuwa chovu na kutwaa ubingwa mara lukuki wa Gossage Cup!.
8. BOB Ahitimu Makerere
BOB alimaliza kwa kufaulu vizuri masomo yake ya Uchumi Makerere na kisha akarejea Tanganyika.
9. BOB Aenda Masomoni LIVERPOOL, UK
Mwaka 1961, BOB alienda Chuo Kikuu cha Liverpool, UK ambako alisomea Sheria. Alifaulu vizuri masomo hayo vizuri ikiwa pia na mitihani ya mafunzo ya sheria (Middle temple), London.
10. BOB Arejea TZ
Mwaka 1965, BOB akarejea nchini na kuajiriwa kama Mwanasheria wa Serikali.
11. BOB Awa Meneja BOT
Mwaka 1968, BOB aliteuliwa kuwa Meneja BOT wa "Exchange Control" . Alihudumu nafasi hiyo hadi 1971. Wakati huo, Gavana alikuwa Mh. EDWIN MTEI ambaye alimpenda sana BOB kwa uchapakazi na Uzalendo wake, kama anavyotiririka:-
"Bob Makani alikuwa Mzalendo na mchapakazi hodari mimi nilipokuwa Gavana BOT. Mara kwa mara nilikuwa namsifia kwa Rais Nyerere. Hii ilipelekea Rais aninyang'anye hazina hiyo na kumteua kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu".
12. Rais NYERERE Amteua BOB kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu
Mwaka 1971, Rais NYERERE alimteua BOB kuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
13. Rais NYERERE Amteua BOB Naibu Gavana BOT
Mwaka 1974, Rais NYERERE alimteua BOB kuwa Naibu Gavana wa Benki Kuu ambapo alikuwa chini ya Gavana CHARLES NYIRABU ambaye waliteuliwa pamoja mwaka huo.
14. BOB Ahudumu kwa utumishi Uliotukuka
BOB akiwa Naibu Gavana, alishiriki kwa karibu sana kwenye maamuzi na mageuzi ya kiuchumi nchini, akifanya kazi hiyo kwa uaminifu na Uzalendo wa hali ya juu kwa Taifa lake.
15. BOB Awa Mjumbe Bodi Lukuki
Katika utumishi wake wa Umma, BOB alihudumu kwenye Bodi mbalimbali mf. Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ndege, Mkurugenzi wa Bodi ya Williamson Diamonds, Mkurugenzi Bodi ya TZ Breweries, Mkurugenzi Bodi ya NBC nk.
16. BOB Awa Wakili wa Kujitegemea
BOB alihudumu kama Naibu Gavana kwa miaka 12 toka 1974 hadi 1986. Tarehe 4.4.1986, BOB aliapishwa kuwa Wakili wa kujitegemea na kupewa namba ya Uwakili 131 na mara moja akanzisha kampuni yake "Bob Makani & Co. Advocates".
17. BOB-: Mpenzi Kindakindaki wa LIVERPOOL FC
Kutokana na kusomea Sheria jijini Liverpool, BOB alilipenda sana Chama Kubwa Liverpool FC, na hilo lilikuwa wazi.
18. BOB Amfanya MZEE WA ATIKALI Kushabikia LIVERPOOL FC
MZEE WA ATIKALI alipata fursa kumtembelea Wakili BOB kwenye ofisi zake za uwakili zilizokuwa eneo la Co-cabs, Mnazi Mmoja, Dsm. BOB alimsimulia MZEE WA ATIKALI jinsi alivyochezea Uganda Cranes na jinsi alivyoihusudu Liverpool FC na toka siku hiyo "MZEE WA ATIKALI akawa shabiki mkubwa wa Liverpool FC ie MZEE WA ALLEZ ALLEZ ALLEZ LIVERPOOL FC!!!.
19. BOB Awa Mmoja wa Waasisi wa CHADEMA
Baada ya mfumo wa vyama vingi kuanzishwa nchini mwezi Julai 1992 kupitia Sheria ya Vyama vya Siasa, 1992, BOB alikuwa ni mmoja wa Waasisi wa CHADEMA iliyosajiliwa Januari 1993 na kupewa Hati ya Usajili Na. 0000003. BOB kadi yake ya uanachama ilikuwa ni Na.3 akitanguliwa na Mh. EDWIN MTEI Kadi Na.1 na Mh. BROWN NGWILULUPI Kadi Na.2.
Waasisi wengine walikuwa VICTOR KIMESERA, PHILEMON NDESAMBURO, GEORGE WASIRRA, COSTA SHINYANGA, MARY KABIGI, EVARIST MAEMBE na MEDARD MUTUNGI.
20. BOB Amfanya MWALIMU Aisifu Katiba ya CHADEMA
BOB, akitumia weledi wake wa Sheria na uzoefu wake wa Uchumi, kwa kushirikiana na Waasisi wenzake, waliisuka vizuri sana Katiba ya CHADEMA. Mh. MTEI akampelekea Katiba hiyo Mwalimu NYERERE huko Butiama. MWALIMU, bila kumung'unya maneno, aliisifu sana Katiba hiyo hadharani.
21. BOB Awa Katibu Mkuu wa Kwanza wa CHADEMA
BOB alichaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa kwanza wa CHADEMA na Mh. MTEI akawa Mwenyekiti. Viongozi hawa walifanya kazi kubwa sana "kukiuza" chama mikoani ambako walipata changamoto mf Morogoro walipigwa mawe, lakini hawakukata tamaa bali walikomaa hadi chama kikasimama.
22. BOB Awa Mwenyekiti CHADEMA
Mwezi Agosti 1998, BOB alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA na kuhudumu hadi Machi 2003. Baada ya hapo, BOB alibaki kuwa mshauri wa chama huku aliendelea na kazi zake za uwakili.
23. Afya ya BOB Yaanza Kutetereka
Mwaka 2009, BOB aliugua na mwaka uliofuata alipelekwa India kwa matibabu. Mwanzoni mwa mwaka 2012, BOB alipelekwa Nairobi, Kenya kwa matibabu pia.
24. BOB Aaaga Dunia
Majira ya saa 5 usiku, siku ya Jumamosi, tarehe 9.6.2012, BOB aliaga dunia akiwa njiani akikimbizwa Aga Khan hospitali. BOB aliagwa ukumbi wa Karimjee tarehe 11.6.2012 ambapo Rais KIKWETE aliongoza maelefu ya wakazi wa Jiji la Dsm kutoa heshma zao za mwisho. BOB alizikwa tarehe 12.6.2012 wilayani kwake Kishapu ambapo aliacha mke, watoto Dr. JULIE, GRACE, TUME, MOHAMED nk na wajukuu kadhaa.
25. TAMATI
Huyu ndiye marehemu BOB NYANGA MAKANI ambaye Bongolanders wengi walimtambua kwa umahiri wake kama Mwanasiasa tu. ATIKALI hii imetanabaisha bayana kuwa BOB alikuwa ni Kipanga aliyejaaliwa talanta lukuki ambazo alizitumia vizuri katika maisha yake. Kipaji chake cha hali ya juu cha kabumbu kilipelekea BOB aweze kuichezea Timu ya Taifa ya Uganda wakati yeye alikuwa Myanganyika! Hakuna raia mwingine yeyote wa Afrika Mashariki aliyeweza kufanya hivi hadi leo, ukimwondoa BOB.
KONGOLE KWAKO BOB NYANGA MAKANI!!!
BY MZEE WA ATIKALI ✍️✍️✍️

Rais Magufuli Atoa Salamu Baada Ya Kusali Ibada Ya Jumapili Katika Kanisa La KKKT Usharika Wa Chato

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mkewe Mama Janeth Magufuli wakiwa katika Ibada ya Jumapili ya Tano baada ya Pasaka katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chato mkoani Geita leo tarehe 17 Mei 2020.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Waumini wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chato mkoani Geita leo tarehe 17 Mei 2020 mara baada ya Ibada.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikabidhi Mchango wake kwa ajili ya Ujenzi wa Kanisa la (KKKT) Usharika wa Chato kiasi cha Shilingi milioni 10 kwa Mchungaji wa Jimbo la Kusini c (Biharamulo) Dayosisi ya Kaskazini Magharibi Kanisa hilo Mch. Thomas Pascal Kangeizi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika Ibada ya Jumapili ya Tano baada ya Pasaka katika Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Chato mkoani Geita leo tarehe 17 Mei 2020. PICHA NA IKULU
Saturday, May 16
Mtaalamu wa chanjo aliyefutwa kazi asema Marekani itakabiliwa na hali mbaya zaidi ya corona majira ya baridi
WASHINGTON, MAREKANI
OFISA wa zamani wa ngazi ya juu wa afya nchini Marekani ameliambia bunge la congresi kuwa Marekani inaweza kukabiliwa na hali mbaya kuwahi kushuhudiwa wakati wa majira ya baridi kwa sababu ya virusi vya corona.
Rick Bright aliongoza shirika la serikali kujaribu kutengeneza chanjo, lakini akaondolewa katika kazi hiyo mwezi uliopita.
Awali alisema aliondolewa kazini kwa kuelezea hofu juu ya tiba zinazotangazwa na rais Donald Trump.
Rais Trump alimfuta kazi kwa madai kuwa alikua mtumishi asiyeridhika.
Bright pia aliiambia kamati ya Bunge la wawakilishi ya masuala ya afya kuwa maisha yanapotea kwa sababu ya serikali kutochukua hatua katika hatua za mwanzo za mlipuko wa virusi vya corona.
Alisema kuwa kwa mara ya kwanza alizungumzia juu ya ukosefu wa zana za matibabu mwezi Januari, na kufikisha suala hilo katika ngazi za juu za Wizara ya Afya na huduma za binadamu (HHS), lakini hakujibiwa.
Wakati wa ushahidi, Bright alionya kwamba dirisha la kushughulikia virusi vya corona linakaribia kufunga.
“Kama tutashindwa kuboresha jinsi tunavyokabiliana na ugonjwa huu sasa, kwa misingi ya sayansi, ninaogopa janga litakua baya sana na kuendelea kwa muda mrefu,” alisema.
“Bila mpango bora, 2020 unaweza kuwa na kipindi kibaya zaidi cha majira ya baridi kuwahi kushuhudiwa katika histioria ya sasa”.
Bright pia ameiambia kamati hiyo ya bunge la wawakilishi kuwa mwezi Januari alipokea barua pepe ambayo hawezi kusahau, kutoka kwa wasambazaji wa barakoa za hospitali ambao walioonya juu ya upungufu mkubwa wa vifaa hivyo.
“Alisema… tunahitaji kuchukua hatua.Na nikaituma barua hiyo kwa ngazi ya juu ya HHS – na sikupata jibu.
Alisema a kuondolewa kwake kazini kulikua ni matokeo ya kuendelea kwake kusisitiza kwamba fedha zilizotengwa na congress za kupambana na mlipuko wa virusi zinapaswa kuwekwa katika suluhu salama na zilizochunguzwa kisayansi na sio katika dawa, chanjo au teknolojia nyingine ambazo hazijathibitishwa kisayansi.
“Nilizungumza wazi wakati ule, na ninatoa ushahidi leo, kwa sababu sayansi sio siasa au upendeleo -lazima iongoze katika njia ya kupambana na virusi,” aliongeza.
Malalamiko yaliyowasilishwa mapema mwezi huu, yanasema Bright aliondolewa kwenye wadhfa wake kama Mkurugenzi wa taasisi ya utafiti wa kimatibabu – Biomedical Advanced Research and Development Authority (Barda) kwa sababu za kisiasa.Bright anasema aliondolewa muda mfupi baada ya taarifa kuhusu chloroquine, ambayo alisema alikuwa chanzo chake.
Rais Trump alikua amesema kuwa hydroxychloroquine, dawa ya malaria ina uwezekano wa “kuleta mabadiliko “ katika tiba ya Covid-19-ingawa wataalmu wengi wamesema kuwa huenda isiwe ya ufanisi, au hata ikawa hatari.
Malalamiko ya Bright yalikua ni kwamba aliamua kuzungumza na waandishi wa habari kwa sababu maofisa wa serikali walikataa kusikia tahadhari zake. Alisema alikua na jukumu la kujaribu na kulinda umma kutoka kwa madawa ambayo anaamini ni ya hatari kwa usalama na afya ya umma.
MAJIBU YA TRUMP
Baada ya kusikia, Rais Trump aliwaambia waandishi wa habari : “Simfahamu.Sijawahi kukutana nae.Sitaki kukutana nae.”
“Lakini nilimtazama , na anaonekana kama mtu mwenye hasira, mtumishi asiyeaminika , ambaye kusema kweli kwa mujibu wa baadhi ya watu hakufanya kazi nzuri sana .”
Waziri wa afya, Alex Azar alidai kuwa maofisa walifuata mapendekezo ya Bright.
“Kila alichokilalamikia kilifanikiwa-anachokizungumzia kilifanyaka ,” alisema Azar
“Alisema alizungumzia kuhusu haja ya kupata vifaa vya kusaidia kuongeza oksijeni kwenye mapafu.Tuliagiza vifaa hivyo(respirators) kutokana na maagizpo ya rais.
Alisema tunahitaji mradi wa Manhattan wa chanjo. Tukawa na Mradi wa Manhattan.”
Zoom yashtakiwa na kanisa baada ya mafunzo ya bibilia kuvamiwa kwa picha za ngono
CALIFONIA, MAREKANI
WAKATI watumiaji wa mtandao wa Zoom wakiongezeka kutoka milioni 10 kwa siku hadi milioni 200, Kanisa moja huko Califonia linashtaki kampuni hiyo baada ya mvamizi mmoja kuvamia darasa la mafundisho ya bibilia yaliokuwa yanaendelea mtandaoni na kutuma picha za unyanyasaji wa watoto kingono.
Mvamizi huyo alivamia mkutano huo na kuchezesha picha za video zenye kutatiza akili”, kulingana na kesi iliyowasilishwa na Kanisa la Lutherani la Saint Paulus.
Viongozi wa kanisa la San Francisco waliwasiliana na kampuni ya Zoom kutafuta usaidizi lakini kampuni hiyo haikuchukua hatua yoyote.
Katika taarifa, msemaji wa kampuni ya Zoom ameshtumu tukio hilo baya na la kiovu.
“Tunahuzunika pamoja na wale walioathirika,”kampuni hiyo imesema, “Siku hiyo hiyo tulipogundua tatizo hili, tulimtambua aliyetekeleza kitendo hicho, tukachukua hatua kwa kumfungia asiweze kuingia kwenye mtandao wetu na kuwasilisha taarifa kwa mamlaka husika.”
Kampuni hiyo imezungumzia hatua za kiusalama walizochukua hivi karibuni katika mtandao wao”, na kuongeza kwamba watumiaji wa kampuni ya Zoom hawastahili kushirikisha watu wengi sana namba zao za siri za kuwawezesha kufanya mkutano kama ilivyoonekana kwa kundi hilo la kanisa.
Umaarufu wa mikutano kwa njia ya video kupitia mtandao wa Zoom umeongezeka sana katika miezi ya hivi karibuni hasa kwa wafanyakazi na hata kwa shughuli za kibinafsi wakati ambapo nchi kadhaa zimechukua hatua ya kusalia ndani kama njia ya kukabiliana na virusi vya corona.
Utumiaji mkubwa wa mtandao huo wa zoom umekumbwa na mashaka ya kiusalama na faragha ya watu, ambapo wavamizi wamekuwa wakivamia mikutano ya watu bila kualikwa na wakati mwingine wakituma ujumbe wa chuki, kibaguzi, unyanyasaji au hata picha za ngono.
Kanisa la Saint Paulus – moja ya makanisa ya zamani huko San Francisco – limesema kwamba kesi hiyo iliyowasilishwa katika mahakama moja iliyopo San Jose Jumatano, inalalamikia tukio la Mei 6 wakati wa mafundisho ya bibilia ambayo yalivamiwa na mtu aliyefahamika – ambaye pia ameripotiwa kwa mamlaka mara kadhaa.
Wanafunzi wanane wanaojifunza mafundisho ya bibilia, wengi wao wakiwa wale wanaopokea malipo ya uzeeni, mfumo wao wa kompyuta ulikatishwa wakati mvamizi huyo alipocheza video za ngono.
Wakati ambapo programu ya zoom imeendelea kupata umaarufu, imekumbwa na ukosoaji mkubwa kwasababu za kiusalama.
“Video hizo zilikuwa mbaya na ilikera zaidi kuonesha watu wakubwa wakijihusisha na vitendo vya ngono miongoni mwao, kufanya vitendo vya ngono dhidi ya watoto na wale wachanga, pamoja na kuwanyanyasa kimwili,” kesi hiyo inasema
Wakati wanafunzi hao walipojaribu kufunga video hiyo na kuanza tena, mvamizi huyo alivamia tena, kesi hiyo inaongezea.
Kanisa hilo limewasilisha mashtaka likitaka hatua kuchukuliwa dhidi ya kampuni ya Zoom yenye makao yake San Jose.
Katika kesi hiyo, waliowasilisha mashtaka wanataka kufidiwa kwa madai ya kupuuzwa, kukiukwa kwa mkataba, ukosefu wa haki na tabia zisizofaa katika biashara.
Kampuni ya Zoom iliandika kwenye blogu kwamba imechukua hatua zaidi za kiusalama wiki hii na kuahidi hatua za kuimarishaji usalama ikiwemo mipango ya kumzuia mtu wa kando kuingilia mawasiliano ya mtumiaji.
Awali, kampuni hiyo ilikosolewa kwa kudai kwamba tayari hatua za kumzuia mtu wa kando kuingilia data ya mtumiaji zipo kumaanisha kuwa ni mtumiaji pekee anayeweza kufikia ujumbe wake na video zake.
Kile kilichoikumba kanisa hilo ndicho kilichotokea katika kikao cha bunge cha Afrika Kusini wiki moja iliyopita.
Mkutano wa kamati ya bunge kwa njia ya mtandao Afrika Kusini uliwahi kuvamiwa na wadukuzi na spika kudhalilishwa.
Kikao hicho kilikuwa tu ndio kimeanza picha za ngono zilipojitokeza kwenye skrini huku sauti ya mwanamume ikisikika kumtusi Spika Thandi Modise, ambaye alikuwa mwenyekiti wa kikao hicho.
Spika huyo aliyeshikwa na hasira alipaza sauti akisema hiyo ndio sababu anapinga mikutano ya mitandaoni.
“Hiki kilichotokea ni kilekile nilichokuwa ninakisema kuhusu kufanya mikutano kwa njia ya Zoom!” Modise amenukuliwa akisema hivyo na tovuti ya Times Live.
Wabunge walielezea tukio hilo kama lenye kukera na kutatiza akili, kulingana na Tovuti ya habari ya Eyewitness.
Iliwalazimu wahandisi wa Bunge kutuma kiunganishi kingine ambapo wabunge waliungana tena na kuendelea na kikao chao.
Kampuni ya mtandao wa Zoom imekuwa ikikosolewa kimataifa kwa taarifa kwamba kuna wavamizi wanaotuma picha za ngono au maudhui ya matusi wakati wa mikutano.
Kuvamiwa kwa mtandao kwa njia ya Zoom kumekuwa kukifanyika mara kwa mara katika wiki za hivi karibuni wakati ambapo watumiaji wengi wapya wameanza kutumia mtandao huo kama njia moja ya kukabiliana na kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19 na kuahirishwa kwa mikutano na matukio ambayo awali ilikuwa ifanyike ana kwa ana.
KEYDOLI; MREMBO KUTOKA KENYA AMWAGIA SIFA HARMONIZE
MOMBASA, KENYA
ONGEZEKO la wasanii wapya halipo Bongo pekee bali mpaka nchini Kenya, mashabiki wameendelea kushuhudia vipaji vipya kila siku.
Swaggaz tumekutana na KeyDoli, mrembo kutoka Mombasa nchini Kenya anayefanya vyema kwa sasa na wimbo, Infinity aliomshirikisha rapa Country Boy akitumia staili ya Afro Arabic Soul.
Swaggaz: KeyDoli ni nani na lini ulianza kujihusisha na muziki?
KeyDoli: Jina langu halisi ni Yusriyah Ahawa, nilianza muziki nikiwa mdogo sana kama miaka 14 hivi, ilikuwa mwaka 2002.
Nilipata kutambulishwa na prodyuza mmoja anayeitwa Bruce Othiambo ambaye alikuwa rafiki wa baba yangu kwa sababu walikuwa wanafanya kazi sehemu moja.
Prodyuza Bruce ambaye sasa ni marehemu alikuwa kwenye studio zinaitwa Johari Cleff na ndio ilikuwa inasimamia wasanii wakubwa kutoka Kenya.
Ngoma yangu ya kwanza iliitwa Nipe na baba yangu ndio alirekodi akishirikiana na prodyuza Bruce, wimbo huo ulinipa umaarufu sio tu hapa Kenya bali na Afrika Mashariki na Uingereza.
Swaggaz: Wanamuziki gani walikuvutia mpaka ukaingia kwenye muziki?
KeyDoli: Nilizaliwa kwenye familia ya muziki ndiyo maana nikajikuta napenda kuimba kwa kuwa hata baba yangu alikuwa anapenda muziki.
Nikawa nasikiliza muziki wa Yondo Sister, Mbilia Bel na Franco huku Madonna akiwa ni msanii wangu pendwa na haipiti siku sijamsikiliza.
Swaggaz: Kwanini uliamua kutangaza muziki wako Tanzania kwa kumshirikisha rapa Country Boy?
KeyDoli: Toka zamani ilikuwa ndoto yangu nifike Tanzania. Kwa hadithi za mama aliniambia amezaliwa Bongo pia nilikuwa nikiwasikia kina Juma Nature, Lady Jay Dee na Ray C kwahiyo nilikuwa natamani nifike.
Nilitamani kufika Tanzania nikiwa mdogo ila kwa sababu nilikuwa shule nilishindwa lakini nashukuru Machi 1, mwaka huu nilifika Dar es Salaam na kuweza kutimiza ndoto yangu kufanya kazi na Country Boy.
Swaggaz: Ukiwa kama msanii wa kike na mrembo sana, changamoto zipi unapitia kwenye muziki wako?
KeyDoli: Sio rahisi ila mimi nilifunzwa toka nikiwa mdogo kuwa wakati wa biashara ni biashara tu, ukiwa na mazungumzo ya biashara hakuna mtu anaweza kukutongoza ndio maana nikiwa nakwenda kwenye studio kurekodi au redioni au kwenye Tv huwa nakuwa na mtu kando yangu ili kukwepa hizo changamoto.
Swaggaz: Mbali na Country Boy, wasanii gani wengine wa Tanzania unatamani kufanya nao kazi?
KeyDoli: Harmonize au Darassa lakini Harmonize zaidi maana mashallah yuko na moyo mweupe na nilipata bahati ya kumwona hana dharau wala kiburi na uimbaji wake ni mzuri pia Darassa navutiwa na floo zake.
Swaggaz: Changamoto zipi zipo kwenye tasnia ya muziki hapa Kenya?
KeyDoli: Mimi naona sapoti hamna sana lakini siwezi kulaumu vyombo vya habari kwa sababu kuna wengine hawajafikishiwa kazi pia mashabiki nao hawajafikishiwa muziki kwa usahihi ili waweze kuusapoti.
Swaggaz: Baada ya kuachia ngoma yako na Country Boy, mashabiki watarajie nini kutoka kwako?
KeyDoli: Niko na ngoma mpya nitaiachia Mei 21, mwaka huu nikiwa nimemshirikisha msanii mkubwa wa Tanzania. Huo wimbo upo kwenye albamu yangu yenye jumla ya nyimbo 12.
Pia niko na EP yenye nyimbo nne ambazo zote nimeshirikisha Country Boy na tayari zina video ambazo nilifanyia Tanzania.
Mashabiki waendelee kunitafuta kwenye mitandao ya kijamii kama Facebook, Instagram, YouTube naitwa Keydoli ili wapate kunifahamu zaidi nawapenda sana Watanzania.
Pia nawakumbusha tuendelee kuvaa barakoa na kunawa mikono na kutumia sanitaiza mara kwa mara ili Mungu atulinde na ugonjwa wa corona.
Mashine ya kupima virusi vya corona iliyotolewa na Rostam yawasili Zanzibar
MASHINE ya kupima virusi vya corona yenye uwezo wa kutoa majibu ndani ya saa nane ambayo iliagizwa nchini Korea Kusini kwa ufadhili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Mfanyabiashara maarufu nchini, Rostam Aziz, hatimaye imewasili visiwani humo.
Mashine hiyo ina uwezo wa kutoa majibu ndani ya saa nane kwa vipimo vya watu 96 na kwa saa 24 ina uwezo wa kutoa majibu kwa watu 496.
Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Zanzibar, Juma Mohammed Salum jana ilieleza kuwa mashine hiyo ni miongoni wa tatu zilizokuwa zimeagizwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Itakumbukwa Machi 25 Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein aliiagiza Wizara ya Afya kuhakikisha ndani ya miezi mitatu wanakamilisha maabara ya kupima magonjwa ya mripuko.
Shein alikuwa amefanya ziara ya kuangalia ujenzi wa Maabara ya Uchunguzi ya Microbiology katika kijiji cha Binguni na kuagiza Wizara ya Afya kuanza mara moja ujenzi wa maabara itakayochunguza maradhi yanayosababishwa na virusi (Virology Laboratory).
Zaidi alitaka ujenzi wa maabara hiyo ukamilike haraka iwezekanavyo ili Zanzibar iweze kuwa na mashine za kupima virusi vya corona.
Polisi yaeleza sababu za kumwita Mbowe
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe jana aliitwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano na kisha kuachiwa.
Hatua ya kuitwa kwa Mbowe ilikuja saa chache kabla ya kufanya mkutano mubashara kupitia mitandao ya kijamii ya Chadema kuwasilisha ujumbe kwa Watanzania.
Taarifa kutoka ndani ya Chadema ilieleza kwamba Mbowe akiwa nyumbani kwake Dar es Salaam, alifuatwa na maofisa wa Jeshi la Polisi, lakini wasaidizi wake waligoma kufungua mlango.
Hata hivyo, saa chache kabla ya kuanza kwa mkutano wake, alipokea wito wa polisi na kutakiwa kwenda kuripoti ofisi ya Upelelezi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni katika Kituo cha Oysterbay.
Mbowe aliitikia wito huo na kwenda polisi huku akiwa na jopo la wanasheria wake.
KAULI YA POLISI
MTANZANIA ilipomtafuta Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Mussa Taibu, alisema kuwa alimwita Mbowe ili kufahamiana.
“Ni kweli nilimwita tufahamiane kwa sababu yeye ofisi yake ya Chadema iko maeneo haya haya ya Kinondoni, hivyo baada ya kufahamiana yeye ameendelea na ratiba zake,” alisema Kamanda Taibu.
Jana, muda mfupi baada ya Mbowe kutaka kufanya mkutano na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya kitaifa na kimataifa, Msemaji wa Chadema, Tumaini Makene alitoa taarifa kupitia mitandao ya kijamii akisema mkutano huo hautafanyika tena.
“Mkutano wa Mwenyekiti Mbowe uliokuwa ufanyike mubashara kuzungumza na umma, hautafanyika kama ilivyopangwa baada ya Jeshi la Polisi kumhitaji akaripoti ofisi ya RCO Kinondoni, Kituo cha Oysterbay,” ilisema taarifa hiyo ya Makene.
Awali gazeti hili lilipomtafuta Makene kutaka kujua kuhusu kuitwa kwa Mbowe, alisema polisi hawakusema sababu ya kumwita mwenyekiti huyo.
“Kweli alikwenda polisi kitambo, tangu muda ule wa saa tano na polisi hawakusema sababu, nadhani mkiwauliza kwa sasa wanao wajibu wa kusema hilo,” alisema Makene.
MAAMUZI YA CHADEMA
Mbowe ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, kwa wiki za hivi karibuni aliendesha kikao cha Kamati Kuu ya Chadema kwa njia ya mtandao ambacho kiliazimia kuwavua uanachama wabunge wake wanne.
Wabunge waliofutwa uanachama ni pamoja na Joseph Selasini (Rombo), Antony Komu (Moshi Vijijini) ambao wote kwa nyakati tofauti walitangaza kujiunga na Chama cha NCCR-Mageuzi mara baada ya Bunge kumaliza muda wake.
Wengine ni Wilfred Lwakatare (Bukoba Mjini) na David Silinde (Momba).
Mbali na wabunge hao, Mbunge wa Viti Maalumu, Mariam Msabaha ambaye alikuwa Mjumbe wa Kamati Kuu alivuliwa nyadhifa zake zote ndani ya chama na kutakiwa kujieleza kwanini asichukuliwe hatua.
Uamuzi huo umefikiwa kutokana na wabunge hao kukiuka maelekezo ya chama ya kuwataka wabunge wote wa chama hicho
wasishiriki vikao vya Bunge vinavyoendelea Dodoma na kukaa karantini kwa siku 14.
Wabunge wengine ambao wanaendelea kuhudhuria vikao vya Bunge na kutakiwa kujieleza kwa kukiuka makubaliano hayo ni Suzan Masele, Joyce Sokombi, Latifa Chande, Lucy Mlowe, Sware Semesi, Jafari Michael, Peter Lijualikali, Willy Kambalo, Rose Kamili, Sabrina Sungura na Anne Gideria.
Siku 14 za wabunge hao kujiweka karantini zilikamilika juzi.
SPIKA AWAZUIA
Hata hivyo juzi Spika Bunge, Job Ndugai aliwazuia wabunge 15 wa Chadema kuhudhuria bungeni, iwapo hawatakamilisha masharti mawili muhimu.
Wabunge hao watatakiwa kutimiza masharti hayo kwa kuwa hawajulikani waliko na wamekuwa wakihesabiwa kama watoro tangu walipoacha kuingia bungeni Mei 1.
“Ofisi ya Bunge inatoa taarifa kwamba katika siku za hivi karibuni baadhi ya wabunge wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wamekuwa watoro kwa kutohudhuria vikao vya Bunge bila ruhusa ya Spika kwa muda wa wiki mbili kinyume na masharti ya Kanuni ya 146 inayosisitiza wajibu wa kila mbunge kuhudhuria vikao vya Bunge.
“Aidha, tunapenda ifahamike kwamba wabunge hao walisusia vikao vya Bunge huku wakiwa wamelipwa posho ya kujikimu ya kuanzia Mei 1-17, 2020.
“Kwa mujibu wa masharti ya Kanuni ya 5 ya Kanuni za Bunge, Spika alitoa masharti mawili kwa wabunge hao,” ilieleza taarifa hiyo.
Ilieleza kuwa sharti la kwanza ni kuwataka wabunge hao kurejea bungeni au kurudisha fedha walizolipwa mara moja na sharti la pili ni kwa kuwa haijulikani wabunge hao walipo, watalazimika kuwasilisha ushahidi kwamba wamepimwa na hawana maambukizi ya virusi vya corona kabla ya kuruhusiwa kuingia bungeni
Iliwataja wabunge hao kuwa ni Freeman Mbowe, Ester Bulaya, Halima Mdee, John Heche, Joseph Mbilinyi, Peter Msigwa, Rhoda Kunchela, Pascal Haonga, Catherine Rage, Devotha Minja, Joyce Mukya, Aida Khenan, Upendo Peneza, Grace Kiwelu na Joseph Haule.
“Hivyo basi, kwa taarifa hii, na kwa mujibu we Kanuni ya 144 ya Kanuni za Kudumu za Bunge inayohusu usalama katika maeneo ya Bunge, Spika ameagiza Kitengo cha Usalama cha Bunge kutowaruhusu wabunge waliotajwa hapo juu kuingia katika maeneo ya Bunge kuanzia leo (juzi) Jumatano Mei 13, 2020 mpaka watakapotimiza masharti tajwa hapo juu,” ilieleza taarifa hiyo ya Bunge.
Subscribe to:
Posts (Atom)