Haki miliki ya pichaAFPImage captionWapiganaji wa Al- Shabaab nchini Somalia
Polisi watano wa Kenya wameuawa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya katika shambulio linaloaminika kutekelezwa na wanamgambo wa Kiislamu wa al-Shabaab katika eneo la Fino, katika kaunti ya Mandera kaskazini mwa nchi hiyo.
Naibu kamishena mkuu wa eneo hilo Eric Oronyi, anakisia kuwa kati ya wapiganaji 70 au 100 hivi, waliokuwa na silaha kali, walivamia kambi ya polisi mapema leo alfajiri na kuiteketeza kabisa.
Amesema kuwa maafisa wengine watatu walijeruhiwa, na mmoja wao yuko katika hali mbaya, shirika la habari la Reuters limeongeza.
Bwana Oronyi amesema kwamba washambuliaji hao waliharibu mtambo wa mawasiliano, kabla ya kuvamia kambi hiyo.
"Mnara wa mawasiliano, ambao ulikuwa ukilindwa na polisi wa akiba, ulipigwa bomu na kwa sasa, hakuna mawasiliano yoyote ya simu hata ya rununu katika eneo hilo", amesema Bw Oronyi.
Kundi hilo la wapiganaji, ambalo limekuwa likitekeleza mashambulio mara kwa mara kutokea nchi jirani ya Somalia, mara kwa mara limekuwa likiwalenga maafisa wa usalama na magari ya umma, kuvamia maskani ya watu na matimbo ya mawe na kuwauwa watu wengi kwa kuwapiga risasi.
Image captionRamani ya Kenya
Kaunti ya Mandera, inapakana na nchi ya Somalia, jambo ambalo limewaacha wapiganaji hao kutekeleza maovu yao kwa urahisi.
Katika mwaka mmoja uliopita, kundi hilo la wapiganaji wa Kiislamu, limekiri kutekeleza mauaji ya watu kadha eneo la Mandera.
Haki miliki ya pichaMITEGOImage captionEmmanuel Elibariki mwanamuziki wa Tanzania
Mwanamuziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki, alimaarufu kama Ney wa Mitego amesema yeye ndio chanzo cha maamuzi ya nyimbo kufungiwa Tanzania.
Nyimbo zaidi ya kumi zilitangazwa na Mamlaka ya Mawasiliano kupigwa marufuku kuchezwa katika radio nchini Tanzania.
Ney wa mitego akiongea na BBC,amesema
Haki miliki ya pichaMITEGOImage captionMwanamuziki wa Tanzania
'Wakati mwingine naona kuwa sababu ya kufungiwa kwa miziki hii ni mimi na wengine wanawekwa kama chambo kwa kuwa kati ya nyimbo zote hizo,nyimbo mpya peke yake ni yangu tu ambayo imetoka wiki mbili zilizopita na video ina wiki moja tu" Ney wa Mitego.
Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa mwanamuziki huyo kupata misukosuko katika muziki wake.
Mnamo mwezi machi mwaka jana Ney wa Mitego aliwahi kukamatwa na jeshi la polisi la Tanzania kwa kosa la kuimba wimbo unaokashifu serikali lakini inakumbukwa kuwa mwanamuziki huyo aliwahi kupewa onyo kuhusiana na mavazi yake.
Huku wanamuziki wengine bado hawakuwa tayari kutoa maoni yao.
Wakati huo huo , hii leo, msanii wa bongo fleva, Roma Mkatoliki aliyefungiwa wimbo wake mpya wa 'kibamia' kwa sasa amefungiwa na Naibu Waziri wa habari,sanaa,utamaduni na michezo Juliana Shonza kutojihusisha na tasnia ya muziki kwa takribani miezi sita mara baada ya kukiuka kurekebisha wimbo huo .
Baadhi ya wananchi walioongea na BBC,walikuwa na maoni tofauti.
Image captionMaoni ya watanzaniaImage captionMaoni
Meneja wa mawasiliano wa TCRA,Semu Mwakyanjala amelizungumzia suala la muda na kusema kuwa 'wakati wa kufungia haujalishi kikubwa ni nyimbo hizo zilizofungiwa ni hazina maadili.'
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionRobert Mugabe aliitawala Zimbawe tangu mwaka 1980
Wakati Robert Mugabe aliondolewa madarakani mwaka uliopita, alikuwa ameitawala Zimbabwe kwa karibu miongo minne.
Swali ni kwa njia gani madikteta wanafanikiwa kubaki madarakani kwa muda mrefu. Mchambuzi James Telly, professor wa masuala ya siasa katika chuo cha Oxford anachanganua mbinu wanazotumia madikteta kubaki madarakani.
Wanawadhibiti vipi watu wa kawaida na kuzuia mapinduzi? Ni vipi wanawazui wapinzani kuwashinda nguvu? Na ni vipi wanavuruga masuala kama uchaguzi kuweza kuendelea kutawala?
Professor James Tilley anachambua baadhi ya mikakati ambayo mara nyingi hutumiwa na madikteta.
Kudhibiti watu
Jambo la kwanza ambalo kila dikteta hufanya ili abaki madarakani ni kuwadhibiti watu. Tunaweza tukafikiria kuhusu njia za kutumia dhuluma, mateso na kuwaua watu lakini pia kuna njia zingine za kutumia dhuluma ambazo huzuia watu kuungana kuipinga serikaki.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionRais wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi alipinduliwa mwaka 2011 na kuuawa
Kwenye ulimwengu wa sasa hii mara nyingi humaanisha kudhibiti mitandao.
Mara nyingi serikali ndiyo hufaidika na watu kuwepo kwa wingi katika mitandao.
Serikali ya China imetumia mfumo huu kwa njia kubwa.
Kudhibiti wapinzani
Ni madikteta wachache hupinduliwa kwa njia ya maandamano. Hatua ya pili kila dikteta anachukua ili kubaki madarakani si kukandamiza watu bali kudhibiti watu wachache wenye ushawishi.
Ili dikteta kubaki madarakani watu ambao wanaweza kuwa wapinzani ni lazima wafurahishwe siku zote.
"Kwa mfano nchini Korea Kaskazini, watu muhimu ni majenerali wa jeshi. Watu wachache wa familia na watu wenye vyeo vya juu serikalini huwa ni wale husimamia masuala ya fedha na hao ni kati ya watu wachache hadi mamia ya watu." Anasema Bruce Bueno de Mesquita profesa wa masuala ya siasa katika chuo cha New York.
Haki miliki ya pichaKCNA/URIMINZOKKIRIImage captionKiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un
Sasa uzalendo wa watu hawa unaweza kununuliwa. Hii inamaanisha kutenga pesa kutoka kwa kodi au kutokana na mauzo ya mafuta ambazo zingeweza kutumiwa kwa huduma kwa watu kama mahospitali, kuwazawadi watu wachache kwa magari mengi na makasri.
Madikteta pia hufanya uchaguzi
Madikteta mara nyingine wana mikakati chungu nzima ya kusalia madarakani kama vile kuwadhibiti mahasimu wa kisiasa pamoja na wafuasi wao.
Mbinu ya tatu katika orodha ya kuendelea kutawala ni ya kustaajabisha mno, inajulikana kama ''uchaguzi''.
Mataifa mengi sasa yana uchaguzi mkuu, lakini mara nyingi madikteta huiba kura.
Leo hii, wizi wa kura una mbinu kali sana na ya kisasa, badala ya ile ya zamani ya kujaza makaratasi ya ziada ndani ya masanduku ya kupigia kura. Dkt Brian Klaas, ni mtafiti katika Chuo kimoja kikuu cha Uchumi Jijini London:
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionObiang Nguema ndiye kiongozi ameongoza kwa miaka mingi zaidi barani Afrika
"Chaguzi nyingi duniani, huwahusisha viongozi wa kiimla ambao mara nyingi, wanawazuia wapinzani wao wakuu wasigombee kiti cha urais kwa kutumia mbinu potovu za kisheria. Mfano mzuri ni uchaguzi mkuu wa Madagascar wa mwaka 2006, ambapo kiongozi wa upinzani alitakiwa kufika mwenyewe katika tume ya uchaguzi mkuu kujiandikisha kibinafsi, (wakati huo alikuwa uhamishoni nje ya nchi).
Ndege yake ilizuiwa kutua mara tu ilipokuwa imabakisha dakika kumi hivi itue kwa kufunga viwanja vya ndege.
Motisha ya kukaa madarakani
Hadi sasa, mbinu za madikteta za kusalia madarakani, sio ngumu hata kidogo. Kuchunguza na kudhibiti raia ambao ndio wapigaji kura, kuwalipa mlungula, baadhi ya watu mashuhuri miongoni mwao na kutumia uchaguzi mkuu kuonyesha tu wana nguvu ya kusalia mamlakani.
Mara tu baada ya watawala hao wa kiimla wanapotawala kwa miaka michache na kubaini mbinu ya kijanja ya kuendelea kukwamilia madaraka, wanakita mizizi na kuwa vigumu mno kuwang`oa uongozini.
Haki miliki ya pichaVODAFONEImage captionMtambo wa kutua kwenye Mwezi (kushoto) na mtambo wa kupeleleza (chini kulia)
Kampuni maarufu za simu za mkononi Vodafone na Nokia zimetangaza mpango wa kuweka huduma ya mtandao wa 4G kwenye mwezi.
Mpango huo unatarajiwa kukamilishwa mwaka 2019.
Mtandao huo utatumiwa na mitambo ya kupeleleza anga za juu kutuma picha, video na maelezo hadi duniani.
"Tunatuma mitambo hii miwili kwenye Mwezi na tutakusanya data, video za HD na picha nyingi zenye maelezo na umuhumu kisayansi. Tatizo ni kwamba hatuwezi kuzituma moja kwa moja kutoka kwa mitambo hiyo hadi duniani. Hii ni kwa sababu itatumia nishati nyingi," amesema Kate Arkles Gray wa shirika la PTScientists.
"Kwa hivyo, kutumia mtandao wa 4G kwenye Mwezi kutatuwezesha kutuma data, video na picha hizo hadi kwenye mtambo wa kutua kwenye Mwezi ambao una nishati nyingi, na unaweza basi kuvituma hadi duniani."
"Kwa kufanya hivyo, tutaweza hata kuzitazama video hizo za HD moja kwa moja kutoka kwenye Mwezi tukiwa hapa duniani.
Haki miliki ya pichaHISANI
Wengi wameshangaa ni kwa nini kampuni hizo zimeangazia mradi huo badala ya kuangazia zaidi kufikisha huduma ya simu katika maeneo mengi duniani ambayo bado hayana huduma hiyo.
"Naam, ni kweli naegemea upande mmoja kwa sababu mimi hufanyia kazi kampuni inayoangazia upelelezi wa anga za juu lakini kuna mambo na vitu vingi sana ambavyo tunavitumia kwa sasa duniani kila siku ambavyo vilianza kama teknolojia ya kutumiwa anga za juu," anasema Bi Gray.
Haki miliki ya pichaHISANI
Anatoa mfano wa teknolojia inayotumiwa kwenye kamera za sasa kwenye simu ambazo hutumia sensa ambayo iliundwa kwa ajili ya kutumiwa anga za juu.
Mmoja wa mashuhuda, Omar Zombre, ameiambia runinga moja nchini humo kuwa: "tuliwaona watu wanne ambao walijaribu kuingia kwa nguvu ndani ya ubalozi huu kutokea eneo la Mashariki. Walikuwa na mavazi ya kiraia, na aina fulani ya vazi maalum na mzigo mgongoni, huku wakibeba bunduki za Kalashnikov (AK-47), zilizoonekana bayana.
"Walijaribu lakini hawakufaulu, kisha wakaelekea upande wa Magharibi wa jumba hilo. Tuliwaona wakiliteketeza moto gari. Tulipokwenda juu {katika paa la jumba} tulisikia milio ya risasi kutoka kwa gari la rashasha, [ilikuwa] hali ya kutisha."
Wanajeshi wa Ufaransa walioko nchini humo pia wametumwa huko.
Waziri wa Mashauri ya nchi za kigeni wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian, ameiambia ameiambia runinga ya ICI kwamba hakuna "raia yeyote wa Ufaransa aliyejeruhiwa au kuuwawa".
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionReuters wamepakia mtandaoni picha hii ya wanaume wawili wanaoonekana wakijificha
Kambi hiyo ya jeshi na majengo ya ubalozi wa Ufaransa- ambayo pia iko karibu na Ofisi ya Waziri mkuu- yako katika eneo la kilomita moja kutoka nyingine.
Runinga ya taifa hilo inasema kuwa, Waziri mkuu yuko salama.
Ubalozi wa Marekani mjini humo, umewashauria raia kutahadhari na kujificha.
Katika miaka miwili ya nyuma, mji wa Ouagadougou umeshambuliwa na wapiganaji wa kiislamu.
Taifa hilo lililoko Afrika Magharibi, pia lilikabiliwa na jaribio la mapinduzi, lililotibuka mwaka 2015. Mapema wiki hii, kesi ya waliopanga jaribio hilo la mapinduzi ilianza, lakini ikaahirishwa baada ya mawakili wao walipoondoka nje ya mahakama hiyo, wakilalamika kupinga mahakama ya kijeshi.
Image captionEdgar Edmund Tarimo,17, ni mshindi wa Anzisha Prize 2017
Akiwa na umri mdogo tu chini ya miaka 17, Edgar Edmund Tarimo ameweza kubuni na kutengeneza mashine ya kutengenezea vigae vya sakafu, (Paving Blocks), kwa kutumia taka za plastiki na mchanga.
Kupitia ubunifu wake huo, ameweza kupunguza kiasi kikubwa cha taka za plastiki mitaani na kusaidia kupunguza uchafuzi wa mazingira zinazotokana na taka hizo.
Na Kupitia kampuni yake ya Green Venture tayari ameajiri wafanyakazi sita na kuweza kutoa kipato kwa takriban watu themanini, ambao hufanya kazi ya kumkusanyia taka za plastiki.
Edgar anasema alianza ujasiriamali akiwa na mtaji wa shilingi za Kitanzania elfu 40, na tayari ameweza kushika mpaka kiasi cha milioni nne za Kitanzania.
Image captionVigae (paving Blocks) vilivyotengenzwa na plastiki
Edgar Edmund ambaye amehitimu kidato cha nne mkoani Arusha mwaka uliopita, alikanza kutengeneza mashine hiyo aliyoivumbua miaka mitatu iliyopita, kutokana tatizo la mafuriko lililowahi kutokea na baadhi ya watu nyumba zao zilisombwa na maji, kutokana na kuokuwa imara na pia uchafu wa plastiki ulikuwa ukiathiri mazingira, kutokana na kusombwa na kutawanywa na maji kutoka maeneo mbalimbali wakati wa mafuriko hayo.
''Nilifikiria jinsi ya kutatua matatizo mawili kwa suluhisho moja ndio nikafikiria jinsi gani naweza kutumia taka kutengeneza bidhaa za ujenzi ambazo zinaweza kuwa za bei rahisi ili watu watumie kujengea katika nyumba zao ziwe imara, na pia kupunguza uchafu wa mazingira kwa kukusanya taka hizo za plastiki na kuzitumia.''
Kwa upande wa mama yake, Emiliana Tarimo anasema hakutegemea mwanae kufikia mafanikio hayo, kutokana na jinsi alivyoanza na changamoto alizokutana nazo.
Hata hivyo anasema kutokana na umri wake mdogo, anamshauri aendelee na masomo yake na kuhitimu vizuri, ili aweze kupata mafanikio zaidi ya kazi yake.
Ameiomba serikali kuweza kusaidia mtoto huyu, kutopoteza kipaji chake na kuweza kuilinda kazi yake hiyo, kutokana na umri wake mdogo, wa chini ya miaka 18.
Mwaka jana wa 2017, Edgar Edmund alifanikiwa kupata tuzo ya Anzisha Prize baada ya wazo lake la kibiashara la kubadilisha taka za plastiki, kuwa malighafi ya kutengenezea vigae (paving Blocks) kwa kuchanganya na mchanga, kushinda.