Friday, December 1

Mwanafunzi apewa kipigo Moshi


Moshi. Mwanafunzi wa darasa la tano Shule ya Msingi Sokoine, Wilaya ya Moshi ameshambuliwa na vijana wawili baada ya kumfungia kwenye mti na kumpa kipigo hali iliyomsababishia kupata majeraha mwilini.
Mtoto huyo anayeishi na bibi yake, mtaa wa KCMC Rau alipewa kipigo hicho leo Ijumaa baada ya bibi yake ayenaishi naye kudaiwa  kutoa maagizo kwa vijana hao kufanya hivyo.
Shuhuda wa tukio hilo, Emanuel Shirima amesema kuwa mtoto huyo alipigwa baada ya kwenda kuogelea.
Amesema kuwa mtoto huyo sio mara yake ya kwanza kupewa kipigo na huyo bibi yake huyo.
"Yaani huyu mtoto ana kama mwaka hivi anapigwa na kunyanyaswa na huyu bibi," amesema shuhuda huyo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Hamis Issah alipoulizwa kuhusu tukio hilo amesema hana taarifa yoyote.
Hata hivyo, Kamanda Issa amesema atafuatilia suala hilo kwa kuwa limetokea leo Ijumaa jioni .

Upinzani Kenya waunda kamati ya kitaifa ya "bunge la wananchi"

Kiongozi wa upinzani Kenya, Raila Odinga awahutubia wafuasi wake mjini Nairobi, Kenya, Nov. 28, 2017.
Muungano wa upinzani nchini Kenya, NASA, Ijumaa ulizindua kamati ya kitaifa ya kuratibu mikakati ya kuunda "bunge la wananchi."
Kamati hiyo ya wanachama sita imetwikwa jukumu la kuongoza na kutoa ushauri kwa mchakato ambao, NASA imesema, utapelekea mabadiliko ya mfumo wa ucghaguzi nchini humo.
Taarifa iliyosomwa na aliyekuwa gavana wa Bungoma Bonnie Khalwale mjini Nairobi, ilisema kuwa kamati hiyo itaongozwa na mchumi David Ndii, ambaye ni mshauri mkuu wa muungano huo.
"Kamati hiyo itawasilisha ripoti yake kwa vinara wa muungano wa NASA kabla ya Desemba 12," alisema Khalwale.
Aliyekuwa mgombea urais kwa tikiti ya muungano huo, Raila Odinga, alisema mapema wiki hii kwamba "ataapishwa' tarehe 12 Desemba kama 'rais wa wananchi.'
Khalwale alisema kamati hiyo aidha itatoa ratiba ya mkutano wa kumuapisha Odinga.
NASA imesema baadhi ya kaunti zitaendelea kujadili mswada wa bunge la wananchi licha ya mahakama moja mjini Kitui kuamuru usitishwaji wa mjadala kuhusu mswada huo.
Miswada hiyo tayari imejadiliwa na kupitishwa katika kaunti za Kisumu, Homa Bay, Siaya, Busia, Kakamega, Vihiga, Kituai, Kwale, Makueni na Migori, ambazo ni ngome za upinzani.
Odinga alijiondoa kama mgombea wa urais kwenye uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 26 mwezi Oktoba kwa madai kwamba haungekuwa wa huru na wa haki.
Uchaguzi huo ulikuwa umeitishwa na tume ya IEBC kufuatia auamuzi wa mahakama wa kubatilisha uchaguzi wa awali uliofanyika tarehe nane mwezi Agosti, kwa kile jaji mkuu alikieleza kuwa "kugubikwa na dosari na uvunjivu wa sheria."
Rais Uhuru Kenyatta aliapishwa kwa muhula wa pili tarehe 28 mwezi Novemba baada ya ushindi wake kuhalalishwa na mahakama ya juu.

‘WASICHANA HUJIUNGA KIDATO CHA TANO NA UJAUZITO’

MKUU wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Bwiru wilayani Ilemela, Meltilda Shija, amesema wanafunzi wanaomaliza kidato cha nne wamekuwa wakijiunga sekondari na ujauzito.
Amesema kwa sababu hiyo  wameanza kuwapima kila wanapojiunga na kidato cha tano.
Alikuwa akizungumza juzi wakati wa ufunguzi wa Kiwanda cha Bwiru Girls Initiative.
Shija alisema   alichokibaini ni kuwa wanafunzi wengi huwa huru baada ya kumaliza kidatu cha nne hivyo kujikuta wakishiriki ngono na hata wanapochaguliwa kujiunga kidato cha tano baadhi yao wamekuwa wakiwa na ujauzito.
“Mwaka jana tulipopokea wanafunzi wa kidato cha tano  Julai na kuwapima tulibaini baadhi yao wana mimba za miezi tisa, nane na sita jambo hili limejirudia kwa mwaka huu inasikitisha sana.
“Naomba  uwepo   msisitizo kwa viongozi mbalimbali wa kata, mitaa na vijiji kuwabaini wanafunzi wanaohitimu kidato cha nne katika maeneo yao na kuwa nao karibu  kuwaokoa na janga la mimba,” alisema Shija.
Alisema wamekuwa wakipokea wanafunzi   lakini kumbe kipindi cha kusubiri matokeo wamekuwa wakiachwa na kujiingiza kwenye matatizo yanayowaharibia ndoto zao hivyo kujikuta wakiwa na ujauzito.
Shija alisema  mkakati wa shule yake ni kuwapima kila mara ikiwa ni pamoja na kuanzisha mpango wa kuwajengea uwezo wa kujiamini, kujisimamia na kuepuka vishawishi.
Alisema mkakati mingine  ni kujenga kiwanda hicho ambacho kitawashughulisha zaidi kupata stadi za maisha badala ya kutumia muda wao kwa mambo yasiyo na faida kwao.
Mkuu huyo wa shule  alisema ingawa kuanzishwa  kiwanda hicho pia kutasaidia kuwashughulisha hivyo kuwapunguzia muda wa kuwaza masuala ya ngono.
“Kiwanda hiki kimefanikiwa kushona sare zinazozingatia maadili ya shule na jamii kwa wanafunzi wa kidato cha tano ambazo ni sketi 700, magauni 700 na hijabu 200.
“Mauzo ya vituo hivyo yameokoa  Sh milioni 3.2 ambazo  zingetumika kama wangeshona sare hizo mtaani,” alisema na kuongeza kuwa mapato yameingizwa katika akaunti ya kujitegemea ya wanafunzi.
Akifungua kiwanda hicho kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza , John Mongella, Mbunge wa   Ilemela, Angelina Mabula, aliwapongeza wanafunzi hao kwa kubuni wazo la kuanzisha kiwanda hicho.
Aliahidi kushirikiana nao kwa kuwashirikisha  wataalamu kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) na kuangalia namna ya kuboresha vifungashio vya bidhaa zao ili ziendane na soko.
Pia alishauri kuanzishwa   kitengo maalum kwa ajili ya kiwanda hicho   waweze kufikia malengo waliojiwekea na kufanikisha lengo la kuwa washonaji wa sare za shule zote za manispaa hiyo kusaidia kuwapunguzia wazazi gharama.
Mabula ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, aliahidi kukisaidia kiwanda hicho mtaji wa Sh milioni moja.
Alisema fedha hizo  zitatumika kununulia majora ya vitambaa   na kemikali za kutengenezea sabuni za maji na kiwi na matofali yote yatakayotumika kawa ajili ya ujenzi wa jengo la kiwanda hicho.
Aliitaka halmashauri hiyo kulimalizia litakapokamilika .
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kutetea Haki za Wanawake la Kivulini, Yassin Ally, alisema azma yao ni kuwaona watoto wa kike  shuleni wanawezeshwa kuwa wanufaika na kushiriki katika Tanzania ya viwanda.

Siku ya kupambana na Ukimwi-Vijana ndio wanaotishiwa zaidi

Leo ni siku ya kimataifa ya kupambana na UKIMWI. Kenya inafanya juhudi mpya baada ya takwimu rasmi kuonyesha kuwa 51% ya maambukizi mapya yanatokea miongoni mwa vijana walio na umri wa miaka ya 15-24

Lesotho Mobile Gesundheitsversorgung: Bluttests (picture-alliance/AP Photo/D. Farrell)
Ripoti ya Baraza la kitaifa la kupambana na Ukimwi nchini Kenya, NACC inatahadharisha kuwa maambukizi ya makundi mengine ya jamii mbali na vijana, hayajaongezeka wala kupungua. Inasadikika kuwa hofu ya kupimwa na tabia za kufanya mapenzi kiholela ni baadhi ya vyanzo vya maambukizi mapya katika vijana. 
Kulingana na ripoti ya baraza la kitaifa la kupambana na ukimwi maambukizi mapya kati ya vijana yameongezeka tangu mwaka uliopita.Kwa kila watu 5 wanaoambukizwa wawili ni vijana walio na umri wa kati ya miaka 15-24. Takwimu zinaonyesha kuwa kati ya watu alfu 26 walioripotiwa kuambukizwa virusi vya HIV mwaka uliopita,alfu tatu kati yao walifariki dunia kwa sababu ya matatizo yanayotokana na ugonjwa wa Ukimwi.
Kulingana na mkuu wa mpango wa kitaifa wa kupambana na Ukimwi na magonjwa ya zinaa,NASCOP, Kigen Barmasai, takwimu hizo zinatia hofu.Inasadikika kuwa vijana wengi wanafanya mapenzi kiholela kwa sababu ya ulevi na uraibu wa mihadarati au pia kushindwa kukataa kwa sababu moja au nyengine.
Kukosekana kwa elimu ya afya ya uzazi ni tatizo
 HIV / AIDS-Test in Gaza (06.01.2017) (Provinz -sud Mosambik)
(DW/C. Matsinhe)
Bado vijana wengi wanaogopa kwenda kuchukua vipimo vya HIV
Changamoto kubwa ni ukosefu wa elimu ya afya ya uzazi na haki zinazoambatana na mazingira hayo.Vijana wanaaminika kuchelea kupimwa kujua iwapo wameambukizwa virusi vya HIV ambayo ndiyo hatua ya kwanza ya kupambana na maambukizi.Takwimu zinaashiria kuwa vijana huanza kufanya mapenzi kwa mara ya kwanza kabla ya kutimiza umri wa miaka 15.Kadhalika 67% ya wasichana ndio hutumia mipira ya kondomu kwa mara ya kwanza wanapojuana kimwili na wavulana.Wavulana ni wachache Zaidi wanaotumia mipira ya kondom kwa mara ya kwanza kwani takwimu zinaonyesha ni 58%.
Jambo jengine la kutia hofu ni kuwa vijana hawa hubadili mienendo na kuacha kutumia mipira ya kondom kadri wanavyoendelea hata wanapofanya mapenzi na watu wasiojuana nao vizuri.Suluhu ni wazazi kuwa chonjo kuwashauri na vijana wenyewe kupata elimu ya kutosha ya afya ya uzazi na haki zao.
Umasikini pia wanyoshewa kidole
Durban AIDS Konferenz Südafrika (Getty Images/R.Jantilal)
UKIMWI ni miongoni mwa magonjwa yanayowauwa watu wengi zaidi barani Afrika
Hali hii inachangia katika mimba za mapema na matatizo ya afya ya uzazi.Mtaala wa kitaifa nao pia unanyoshewa kidole cha lawama kwa kujikita zaidi kwenye masomo yanayotahiniwa pekee na kutelekeza umuhimu wa elimu ya masuala ya jamii hususan afya ya uzazi na uhusiano kati ya wavulana na wasichana. Ukosefu wa uelekezi nao pia unawapotosha vijana vilevile umasikini unawasukuma kwenye ukahaba na tabia zisoridhisha. Hata hivyo teknolojia sasa inamuwezesha aliyeambukizwa virusi vya HIV kwa bahati mbaya kupewa mchanganyiko wa dawa za kuzuwia madhara maarufu Prep.Elimu inahitajika kuepusha matumizi mabaya ya kinga hii.
Kwa sasa shirika la afya uliomwenguni WHO linaiweka idadi ya wanaoishi na virusi vya HIV kuwa milioni 36.7.Kauli mbiu ya mwaka huu ni haki ya afya: na kuwa ni wajibu wa kila mmoja kupambana na Ukimwi.Kutoka Nairobi mimi ni Thelma mwadzaya

Watetezi wa haki wakosoa uchaguzi mdogo Tanzania


Kiongozi wa chama cha upinzani, Freeman Mbowe
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) nchini Tanzania kimesema uchaguzi mdogo wa marudio wa madiwani kwenye kata 43 uliyofanyika Novemba 26, 2017 ulikuwa na uvunjifu wa haki za binadamu.
Wakili Anna Henga, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha sheria na haki za binadamu LHRC, amesema pamoja na mambo mengine kumekuwa na ukiukwaji wa taratibu zinazo simamia uchaguzi huo ulionyesha ushindani mkali wakati wa kampeni.
LHRC imesema katika mkutano na waandishi wa habari kuwa licha ya kuwa uchaguzi umefanyika kwa uhuru na haki katika baadhi ya kata, katika maeneo mengine kumekuwepo na vitendo vya matumizi mabaya ya vyombo vya dola, matukio ya watu kutekwa na watu wasiojulikana, watu kupigwa na vitendo vya kuwatia hofi wapiga kura.
LHRC imeitaka serikali kuchukulia hitilafu katika chaguzi ndogo kama hizi za udiwani kwa uzito wa kipekee ili kuepuka athari za namna hii katika chaguzi kubwa zijazo.
Uchaguzi mdogo wa madiwani kwenye kata 43 zilizopo kwenye mikoa 19 Tanzania, ulifanyika ili kujaza nafasi zilizowazi katika kata hizo baada ya madiwani waliokuwepo kufariki, kujiuzulu na wengine mahakama kutengua uwakilishi wao.
Vyanzo vya habari nchini Tanzania vimeripoti kuwa maeneo yaliyoripotiwa kukumbwa na vurugu wakati wa uchaguzi, mengi yako Mkoa wa Arusha, hali ambayo ilifanya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwataka wagombea wake wa udiwani katika kata zote za Wilaya ya Arumeru kujitoa.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe alisema Chadema kilijitoa kwenye uchaguzi wa kata tano za jimbo la Arumeru Mashariki.
Mbowe alidai uchaguzi huo wa marudio ulikuwa na matukio ya ukikukaji sheria ikiwa ni pamoja na mashambulizi yaliyofanywa dhidi ya baadhi ya viongozi na wanachama wa Chadema.

EU, AU wakubaliana kuimarisha ushirikiano

Umoja wa ulaya na Afrika wakubaliana kuimarisha ushirikiano katika nyanja muhimu ikiwa ni pamoja na uhamiaji, usalama, uwekezaji katika elimu na maendeleo endelevu kwenye mkutano uliokamilika nchini Ivory Coast.

Libyen Flüchtlinge in Sabratha (Reuters/H. Amara)
Suala la uhamiaji ni mojawapo ya masuala mazito yaliyojadiliwa kwa kina katika mkutano huo na kufikiwa maamuzi. Rais wa baraza la Umoja wa Ulaya Donald Tusk akizungumzia suala zima la uhamiaji ametaja juu ya biashara ya utumwa nchini Libya akiitaja ripoti hiyo kuwa ya kuogofya huku akitilia mkazo kwamba suala la uhamiaji ni jukumu la pamoja baina ya serikali za Ulaya na Afrika.
Wasafirishaji haramu wa binadamu wachemshiwa muarobaini
Katika mkutano huo mjini Abidjan, viongozi kwa pamoja wamekubaliana kuhusu mpango wa dharura wa kuyaangamiza makundi yanayofanya biashara ya binadamu na kuwarejesha nyumbani wahamiaji katika jitihada za kupunguza janga la ukiukaji haki za binadamu nchini Libya.
Elfenbeinküste | Gipfel AU und EU in Abidjan | Conde (Reuters/L. Gnago)
Alpha Conde rais wa Guinea ambaye nchi yake ndiye mwenyekiti wa kupokezana wa Umoja wa Afrika ameweka wazi juu ya kile kilichofikiwa kuhusu wahamiaji.
“Tumechukua uamuzi juu ya kuwahamisha haraka  wakimbizi, na kuunda kamati inayoongozwa na tume  ya umoja wa afrika juu ya haki za binadamu, ikisaidiwa na umoja wa Ulaya, wanaowatafuta wafanyabiashara ya binadamu. na tunaona ukiukwaji huu kuwa uhalifu dhidi ya ubinadamu. Na hivyo, nchi mbalimbali lazima ziweke vikosi maalum vya kupambana  dhidi ya mtandao wa kusafirisha watu kwa njia za magendo.”
Makala ya televisheni yawafumbua watu macho
Picha zilizooneshwa hivi karibuni nana kituo cha Televisheni cha CNN mapema mwezi huu zilizoonyesha wahamiaji wakipigwa mnada kama watumwa na walanguzi wa binadamu  huko nchini Libya na hivyo kuibua hamaki barani  Ulaya na ghadhabu barani  Afrika.
Taarifa hiyo iliangazia juu ya ukiukwaji uliofanywa dhidi ya wahamiaji wa Afrika wanaotaka kuingia Ulaya, ikilazimisha suala hilo kuwa ajenda kuu ya mkutano huo ambao ulilenga kuzingatia maendeleo ya vijana wa Afrika.
Elfenbeinküste EU-Afrika-Gipfel in Abidjan (Reuters/P. Wojazer)
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron alisema Jumatano kuwa mpango huo ulihusisha uanzishwaji wa "jopokazi" ikijumuisha polisi wa Ulaya na Afrika pamoja na maafisa wa kijaasusi.
Serikali ya Libya yawajibika
Mpango huo uliibuka kutoka mkutano wa viongozi wa Umoja wa Mataifa, viongozi wa muungano wa ulaya  na wawakilishi wa serikali kutoka Chad, Niger, Morocco, Congo na Libya ambao uliitishwa na Ufaransa Jumatano.
Umoja wa Ulaya, Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa walikubaliana kuzuia  mali pamoja na kuweka vikwazo vya kifedha dhidi ya walanguzi wanaojulikana.
Serikali ya Libya, iliyoahidi kuchunguza  ripoti za mnada wa watumwa, ilikubali kuyaruhusu mashirika ya umoja wa mataifa kufikia kambi za wahamiaji katika maeneo yaliyo chini ya udhibiti wake, viongozi wa Ujerumani walisema.
Nchi za Umoja wa ulaya, wakati huo huo, zimeridhia  kufadhili mpango wa kuwarudisha  wahamiaji kutoka Libya, mchakato ambao tayari unaandaliwa na shirika la kimataifa la uhamiaji,IOM.
Wahamiaji walio na matatizo ambao hatimaye wanaweza kuhifadhiwa watapelekwa  nchini chad au Niger kabla ya kuhamishwa kwenye nchi ya tatu inayoweza kuwa nchi ya  Ulaya au kanda nyingine.

Wakuu wa jeshi wateuliwa kuwa mawaziri Zimbabwe

Rais Emmerson Mnangagwa amewateua wakuu wa jeshi katika baraza lake jipya la mawaziri
Image captionRais Emmerson Mnangagwa amewateua wakuu wa jeshi katika baraza lake jipya la mawaziri
Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amelitaja baraza lake la mawaziri akimteua afisa mkuu wa jeshi kwa wadhfu mkuu katika serikali yake.
Waziri mpya wa fedha ni Sibusiso Moyo , jenerali aliyetangaza katika runinga ya taifa hilo wiki mbili zilizopita kwamba jeshi limechukua udhibiti.
Mkuu wa jeshi la angani Perence Shiri ataongoza wizara ya fedha na kilimo.
Kiongozi mmoja wa upinzani Tendai Biti amesema kuwa fungate iliokuwa ikisherehekewa Zimbabwe imeisha kabla ya kuanza.
Bwana Mnangagwa aliapishwa wiki moja iliopita kufuatia kujiuzulu kwa Robert Mugabe ambaye alikuwa mamlakani kwa takriban miaka saba.
Upinzani umelaumu mabadiliko hayo kama usaliti wa matumaini miongoni mwa raia na thibitisho kuwa vikosi vya usalama vilivyokuwa na nguvu nyingi wakati wa utawala wa Mugabe vinaendelea kuthibiti taifa hilo.
Hali ya kuleta uwiano na umoja ilioonekana katika siku za karibuni huenda ikabadilishwa na makabiliano ya uongozi katika uchaguzi wa mwaka ujao.

Alipua vilipuzi mahakamani na kujiua pamoja na mshukiwa

Magurunedi hayo yalilipuliwa wakati wa kusikizwa kwa kesi ya mauajiHaki miliki ya pichaDP.NPU.GOV.UA
Image captionMagurunedi hayo yalilipuliwa wakati wa kusikizwa kwa kesi ya mauaji
Mwanamume mmoja amelipua maguruneti mawili katika mahakama moja mashariki mwa Ukraine , akijiua pamoja na mmoja wa washukiwa wa mauaji ,kulingana na maafisa wa polisi.
Mlipuko huo ulitokea wakati wa kikao cha kusikizwa kwa kesi hiyo mjini Nikopol katika jimbo la Dnipropetrovsk.
Mtu huyo ni baba ya mmoja wa waathiriwa waliouawa kulingana na maafisa wa polisi.
Takriban watu tisa walijeruhiwa, ikiwemo washtakiwa wawili , walinzi wawili afisa mmoja wa mahakama na raia.
Washtakiwa hao watatu wanatuhumiwa kuifyatulia risasi gari moja na kuwaua abiria wawili mnamo mwezi Februari 2016 akiwemo mwana wa mtu ambaye alilipua vilipuzi hivyo , kulingana na vyombo vya habari.
Kulingana na ripoti za awali mtu mmoja alitoa maguruneti mawili na kuyalipua wakati wa kusikizwa kwa kesi ya mauaji kulingana na mtandao wa Ukrainska Pravda ambao ulimnukuu msemaji wa polisi Yaroslav Trakalo akisema.
Mtu huyo alichukua hatua hiyo baada ya kusikia kwamba kesi hiyo inaahirishwa na kwamba washukiwa wanafungwa mikono.
Uchunguzi sasa umeanzishwa.
Mzozo unaoendelea mashariki mwa Ukraine unamaanisha kwamba kuna umiliki wa silaha miongoni mwa raia.
Zaidi ya watu 10,000 wamefariki katika mzozo huo uliotokea mnamo mwezi Aprili 2014, muda mfupi baada ya Urusi kulinyakua eneo la kusini la rasi ya Crimea.

Apigwa faini kwa kuchora alama zake za barabarani China kurahisisha usafiri wake

Apigwa faini kwa kuchora alama zake za barabarani China
Image captionApigwa faini kwa kuchora alama zake za barabarani China
Mtu mmoja raia wa China amepigwa faini baada ya kupatikana katika kamera akipaka rangi ishara mpya za barabarani ili kurahisisha safari yake kuwa rahisi.
Gazeti la Modern Express limeripoti kwamba mtu mwenye umri wa miaka 28 kwa jina Surnamed Cai, alipigwa faini ya Yuan 1000 mashariki mwa mji wa Lianyungang mkoani Jiangsu .
Alipatikana katika kamera mnamo mwezi Septemba 27 akiwa na mkebe wa rangi akipaka mistari mipya katika barabara ili kubadilisha mwelekeo wa trafiki na kuwaambia maafisa wa polisi kwamba alichukua hatua hiyo ili kupunguza tatizo la milolongo mirefu ya magari swala ambalo limekuwa likimchelewesha kila siku anapoelekea kazini.
Niliona kwamba barabara iliokuwa ikielekea moja kwa moja ilikuwa na mlolongo mrefu wa magari , huku barabara inayoelekea upande wa kushoto ikiwa na nafasi kubwa., aliambia maafisa wa polisi.
Nilidhani kubadilisha ishara hizo za babarabara kutarahisisha usafiri wangu kuelekea kazini.
Maafisa wa idara ya trafiki waliambia gazeti hilo kwamba walidhani kwamba tabia ya bwana Cai ilikuwa hatari na kwamba ingesababisha ajali.
Tayari wametuma wafanyikazi kuhadilisha ishara hizo za trafiki.
Hii sio mara ywa kwanza kwamba raia ametumia ujuzi wake wa sanaa kuweka ishara zao za barabara.
Mnamo mwezi Mei ,dereva mmoja mashariki mwa mji wa Zhejiang alipigwa faini baada ya kamera kumpata akichora eneo lake la kuegesha gari kwa kutumia chaki.

Jeshi la Argentina lasitisha zoezi la kutafuta manowari iliyopotea

Matumaini ya kuioata manowari hii iitwayo ARA San kwa sasa yamekufa
Image captionMatumaini ya kuioata manowari hii iitwayo ARA San kwa sasa yamekufa
Jeshi la wana maji la Argentina limesitisha jitihada za kutafuta Monowari iliyopotea kusini mwa bahari ya Atlantiki wiki mbili zilizopita ikiwa na watu 44.
Msemaji wa kikosi cha jeshi la wana maji, Keptein Enrique Balbi amesema kwa sasa shughuli hiyo imeitishwa rasmi.
Kaptain Enrique Balbi, anasema kuwa kikosi cha uokoaji chenye idadi ya watu 4000 kilikwenda kufanya uokoaji mara mbili.
Enrique Balbi amesema hakuna dalili inayoonyesha uwepo wa manowari hiyo
Image captionEnrique Balbi amesema hakuna dalili inayoonyesha uwepo wa manowari hiyo
Balbi anasema kuwa pamoja na jitihada za uokoaji zilizofanyika lakini,hakujawa na mafanikio ya kufanikiwa.
Hata hivyo matumaini ya kuwapa waliokuwa nadani ya nyambizi hiyo wakiwa hai, yalitoweka baada ya kudaiwa kusikika mlipuko mkubwa karibu na eneo ambalo ilikuwa inasadikika kwamba ndipo ilipo manuari hiyo iliyozama.
Manowari hiyo ilikua na watu 44
Image captionManowari hiyo ilikua na watu 44
Nyambizi hiyo ya ARA San Juan ilikumbwa na mkasa huo ilipokuwa ikirejea kutoka katika shughuli zake za kawaida keneo la Ushuaia.

Wawakilishi wa serikali ya Syria na upinzani wakutana

Vita imeacha makovu makubwa Syria
Image captionVita imeacha makovu makubwa Syria
Wawakilishi wa serikali ya Syria na upande wa upinzani waliopo katika mazungumzo ya amani mjini Geneva, wamekalishwa mbali mbali katika mwanzo wa siku za awali, jambo ambalo baadhi yao hawalikulitarajia na kudhani wangeweza kukutana uso kwa uso.
Msuluhishi wa umoja mataifa ,Staffan de Mistura, amesema pamoja na pande hizo mbili kutonana uso kwa uso lakini mazungumzo yameanza.
Mashirika ya kibinadamu ya umoja wa mataifa yaliyopo Syria yanasema kuwa watu wapatao 500 waliopo katika maeneo yanayoshikiliwa na wapiganaji wana mahitaji makubwa kiafya.
Jan Egeland anasema kuwa kumeripotiwa vifo vya watu tisa, kati ya watu wanaosubiria kupata namna ya kutoka katika eneo la mashariki la Ghouta.
Raia kadhaa pia wameuawa katika mashambulio ya anga ya hivi karibuni yaliyofanywa na vikosi vya serikali.
Mapigano hayo nchini Syria hadi sasa yamesababisha vifo vya Zaidi ya watu laki tatu tangu mwaka 2011 huku umoja wa mataifa ukisaka suluhu ya kisiasa kutokana na mzozo huo.

MAMA WEMA ATOA MSIMAMO HATIMA YAKE CHADEMA

MAMA mzazi wa Miss Tanzania mwaka 2006, Wema Sepetu, Miriam Sepetu amekanusha taarifa zilizombazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa yeye na mwanawe wana mpango wa kurudi katika Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Februari 25 mwaka huu Wema na mama yake Miriam walijivua uanachama wa CCM na kujiunga na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa madai ya kwenda kupigania demokrasia ya kweli.
Juzi katika mitandao ya kijamii zilianza kusambaa taarifa kuwa Wema na mama yake wana mpango wa kurudi CCM kwa madai kuwa wameahidiwa kutobomolewa nyumba yao na Wema kufutiwa kesi inayomkabili mahakamani ya matumizi ya dawa za kulevya.
Akiandika katika mitandao ya kijamii jana, mama Wema alieleza yeye na mwanaye wataendelea kuwa wanachama wa Chadema na mwanaye.
“Mimi ninachoona CCM wana akili ya kutaka kuvuruga Chadema. Na tuwe makini kwa maneno ya kutuvuruga kwa kipindi hiki tujenge chama.
“Kuna watu ambao si waelewa kabisa na CCM wanajua nguvu ya Wema na yangu zilivyo, waje  wabomoe nyumba. ‘Notes’ wametoa lini ya kubomolewa hii nyumba? Basi kifo cha wengi ni harusi.
“Mimi nitakuwa Chadema pamoja na mwanangu na mimi ndiye msemaji mkuu. Wao waje wabomoe tu nipo tayari. Kwanza hawanibomoi mimi. Wana bomoa nyumba ya marehemu Sepetu,”alisema mama Wema.
Wakati wakijiunga na Chadema, walisema wamejiunga na chama kilichoisumbua CCM wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Naye Wema alisema alijiunga Chadema bila kulipwa chochote na iwapo ikibainika kinyume kaburi la baba yake Zanzibar lipasuke katikati.

DAKTARI: HOMA YA INI HATARI ZAIDI YA UKIMWI

 

WATU wanane kati ya 100 nchini wana maambukizi ya virusi vya homa ya ini (Hepatit B), ambavyo vinatajwa kuwa hatari zaidi ya virusi vya Ukimwi (VVU).
Uwezekano wa mtu kupata maambukizi ya virusi vya homa ya ini ikiwa atajamiiana na mtu mwenye virusi hivyo, ni mara 10 zaidi ikilinganishwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Daktari bingwa wa magonjwa ya mfumo wa chakula na ini wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), John Rwegasha, alisema hayo jana alipozungumza na MTANZANIA katika mahojiano maalumu.
“Homa ya ini ni hatari, na njia za maambukizi ni kama zile za maambukizi ya VVU na ikiwa mtu hatapata matibabu mapema, huweza kuvisambaza virusi hivi kwa kasi kubwa mno kwa wengine,” alisema.
Daktari huyo ambaye ni miongoni mwa wataalamu saba wa hospitali hiyo wanaoondoka kwenda nchini India kujifunza jinsi ya kufanya upasuaji na upandikizaji wa ini, alisema wanaume ndio kundi ambalo lipo katika hatari zaidi ya kupata maambukizi ya ugonjwa huo kuliko wanawake.
“Ni kundi ambalo lipo kwenye ‘risk’ kubwa, kulingana na takwimu zetu hapa hospitalini, kati ya wagonjwa wanaolazwa wodini tunaowatibu magonjwa ya ini, asilimia 60 ni wanaume na 40 ni wanawake,” alibainisha.
Alisema hiyo inatokana na baadhi ya wanaume kuwa na tabia hatarishi zinazowasababisha kupata magonjwa hayo, ikiwa ni pamoja na unywaji pombe, hasa zile zisizothibitishwa ubora wake.
“Baadhi ya wanaume wana tabia ya kuwa na mahusiano na wanawake zaidi ya mmoja, ni hatari, ikiwa anakutana na ambaye ana maambukizi ya virusi hivi, basi hupata maambukizi hayo,” alibainisha.
Alisema katika kitengo hicho, asilimia 60 ya wagonjwa wamepata matatizo ya ini kutokana na kupata maambukizi ya virusi vya homa ya ini.
Akizungumzia hali ya ugonjwa huo nchini, Dk. Rwegasha ambaye pia ni mkuu wa kitengo hicho, alisema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), Tanzania imepewa kiwango cha asilimia tano cha maambukizi.
“Tunacho kiwango cha kitaifa pia, ambacho ni asilimia tano hadi 17 na kuna makundi ambayo yapo kwenye hatari ya kupata maambukizi, wakiwamo wenye VVU ambao kiwango chao ni asilimia 17, wajawazito asilimia tano,” alisema.
Aliongeza: “Makundi mengine ambayo tunapendekeza wapewe chanjo ili kudhibiti kiwango cha maambukizi ni wanaojidunga dawa za kulevya, wanaofanya biashara ya ngono na mengineyo.
“Duniani takwimu zilizotolewa na Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonyesha kati ya watu bilioni mbili waliogundulika na kutibiwa virusi vya homa ya ini, 450 bado wanaishi navyo duniani.”
Alisema kwa mujibu wa WHO kila mwaka watu milioni 1.5 hufariki dunia kwa maambukizi ya virusi vya homa ya ini na kila mwaka kunagundulika kesi mpya milioni nne za watu wenye virusi hivi.
Alisema tafiti zinaonyesha asilimia 60 hadi 80 ya saratani ya ini zinazogundulika duniani huwa zimetokana na maambukizi ya virusi hivyo.
“Changamoto tunayoiona ni wakati unatibu wagonjwa, bado kunajitokeza maambukizi mapya, vifo na kuna makundi ya watu ambayo huwa ni ‘carrier’ (wabebaji) wa virusi hivi ambao huvisambaza kwa kasi kwa wengine,” alisema.
Kwa mujibu wa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Wateja wa MNH, Aminiel Aligaesha, jopo la wataalamu linalokwenda India, lina madaktari bingwa wanne wa magonjwa ya mfumo wa chakula na ini, wauguzi wawili wanaosimamia mifumo ya hadubini na mhandisi wa vifaa tiba anayesimamia mitambo ya hadubini.
Alisema mafunzo hayo yatachukua miezi mitatu na wataalamu hao watarejea nchini wiki ya kwanza ya mwezi Machi, mwakani.

WATOTO 1,300 WALIOPOTEA KIBITI WANA ZAIDI YA MWAKA

Kamanda wa Polisi nchini, Simon Sirro amewataka wazazi ambao watoto wao hawakuhamishwa shule na hawajui mahali walipo kuripoti polisi.
Hatua hiyo inatokana na kusambaa kwa taarifa ya kupotea kwa watoto 1,300 wilayani Kibiti, Mkoa wa Pwani kupotea kusikojulikana.
“Ni taarifa ya muda mrefu, kipindi cha mwaka jana na mwaka huu, ni zaidi ya mwaka mmoja niliipata Wizara ya Elim kule ndiyo maana nimeelekeza wazazi ambao hawawaoni watoto wao kutoa taarifa.
“Maana kama mtoto humuoni shuleni wala nyumbani si lazima uripoti,” amesema Kamanda Sirro.
Kupotea kwa watoto hao kumezua sintofahamu kutokana na wazazi wa watoto hao kutiripoti tukio hilo polisi.

Kenya: Vikao vya bunge vyaanza tena

Bunge la kitaifa nchini Kenya limerejea vikaoni baada ya mapumziko yaliyoupisha uchaguzi mpya wa mwezi wa Oktoba.Agenda kuu ni kuteua kamati itakayowapiga msasa mawaziri wapya watakaochaguliwa na Rais Uhuru Kenyatta

Nairobi Kenia Abgeordnete Parlament Debatte Sicherheitsgesetz 18.12.2014 (Reuters/T. Mukoya)
Bunge la kitaifa nchini Kenya limerejea vikaoni baada ya mapumziko yaliyoupisha uchaguzi mpya wa mwezi wa Oktoba.Agenda kuu ni kuteua kamati itakayowapiga msasa mawaziri wapya watakaochaguliwa na Rais Uhuru Kenyatta. Wakati huohuo wanasiasa wa vyama vya muungano wa NASA hatimaye wamewasilisha orodha ya majina ya washirika wao wa kamati za bunge za utendaji. Hata hivyo wabunge wanaotokea eneo la pwani wa NASA wanatishia kukwamisha shughuli za chama kwa madai ya kutengwa. Rais Uhuru anakabiliana na kibarua kigumu kuinganisha nchi kwasababu ya tofauti za kisiasa zilizoko.
Kikao cha bunge kilianza rasmi asubuhi baada ya mapumziko ya wiki tatu yaliyoupisha uchaguzi mpya wa rais. Rais Uhuru Kenyatta aliapishwa jana uwanjani kasarani jijini Nairobi kufuatia kipindi cha mvutano wa kisiasa na wenzake wa upinzani wa NASA. Wabunge hao walikuwa na ajenda nzito ya kuiteua kamati itakayowapiga msasa mawaziri wapya watakaoteuliwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Kibarua cha kuwa na baraza la mawaziri lenye sura ya kitaifa
Rais Kenyatta ana kibarua kigumu cha kuhakikisha kuwa baraza lake jipya linapata sura ya kitaifa pasina kuwasogeza karibu wafuasi wa upinzani waliomuunga mkono katika uchaguzi mkuu uliopita. Kadhalika huu ndio wakati wa kuanza kuandaa mikakati ya kuwajumuisha washirika wapya kabla uchaguzi mkuu wa 2022.
Tetesi zimezagaa kuwa nusu ya idadi ya mawaziri waliohudumu katika serikali iliyopita huenda wakatimuliwa kwa sababu ya utendaji wao. Ifahamike kuwa katiba inampa rais uwezo wa kuwateua mawaziri wasiopungua 14 na wasiozidi 22. Kulingana na kigezo hiki Rais Uhuru analazimika kuwabadilishia nyadhifa mawaziri walioko, kuzigawa baadhi ya wizara na kujaza nafasi zote 22 ili kuonekana kuwa na taswira ya kitaifa na kuwashirikisha waliofanikisha harakati za chama cha Jubilee katika awamu mbili za uchaguzi zilizofanyika. Kwa sasa baraza lina wizara 20 na mawaziri 19.
Wabunge wa NASA kutoka Pwani wahisi kutengwa
Wakati huo huo mapema bungeni kulizuka sokomoko baada ya wabunge wanaotokea eneo la pwani wa vyama vya muungano wa upinzani wa NASA kutishia kukwamisha shughuli za chama kwa madai ya kutengwa kwenye uteuzi wa washirika wa kamati za bunge.
Wabunge wa upinzani wametishia kutoshiriki kwenye mipango yoyote ya kuunda kamati za utendaji bungeni
Wabunge wa upinzani wametishia kutoshiriki kwenye mipango yoyote ya kuunda kamati za utendaji bungeni
Kiongozi wa wachache bungeni aliyeteuliwa ni Mbunge wa Suba Kusini John Mbadi na kiranja ni Mbunge wa Suna Mashariki Junet Mohammed.Wawili hao ni wa chama cha ODM kinachoongozwa na Raila Odinga.Manaibu wao ni Mbunge wa Kiminini Chris Wamalwa wa Ford Kenya na Robert Mbui wa chama cha Wiper anayetokea eneo bunge la Kathiani. Kwa sasa tayari upande wa upinzani wa NASA umewasilisha kwa spika wa bunge la taifa Justin Muturi orodha ya majina ya wawakilishi wake katika kamati za bunge.
Spika wa Bunge la kitaifa Justin Muturi alikiri kuwa ameipokea orosha ya wabunge wa upinzani kushiriki kwenye kamati za bunge na sasa inasubiri ridhaa yake.Hata hivyo upinzani bado haujafikia mwafaka kuhusu wanachama watakaowawakilisha kwenye kamati ya Uwekezaji wa Umma na Uhasibu wa umma .Mchakato huo ulisuasua kwasababu ya mivutano kati ya vyama vinanvyounda muungano wa NASA vya ODM, Wiper,ANC na Ford Kenya mintarafu jinsi ya kugawanya nafasi hizo.
Kadhalika wabunge wa upinzani walikuwa wanatishia kutoshiriki kwenye mipango yoyote ya kuunda kamati za utendaji bungeni kwani wanashikilia hawaitambui serikali inayoongozwa na Jubilee. Je ipi athari ya wabunge wa upinzani kususia shughuli za bunge? Hilo ndilo suali nililomuuliza Joy Mdivo, mkurugenzi mkuu wa Kituo cha Sheria cha Afrika Mashariki,EACLJ.
Bunge la 12 lilianza kazi rasmi mwezi wa Septemba ila hakuna kamati ya utendaji iliyoundwa kwasababu ya tofauti za kisiasa zilizokuwako. Kibarua kinachomsubiri Rais Uhuru Kenyatta ni kuwaunganisha wakenya wakati mpasuko wa kisiasa bado unashuhudiwa kwani wafuasi wa upinzani wanashikilia kiongozi wao Raila Odinga ataapishwa tarehe 12 mwezi ujao wa Disemba ambayo ni sikukuu ya kitaifa ya Jamhuri.