Sunday, November 26

Gari la Naibu Meya lashambuliwa


Iringa. Gari la Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa, Dadi Igogo limeshambuliwa na watu wanaodhaniwa kuwa ni wafuasi wa CCM.
Igogo amesema watu waliohusika na tukio hilo anawafahamu na tayari ametoa taarifa polisi ili waweze kuchukukiwa hatua.
Akizungumza na Mwananchi leo Jumapili, Igogo amesema amekumbwa na kadhia hiyo saa  sita mchana wakati alipotembea vituo vya kupiga kura.
"Nilikuwa natembelea vituo vya kupiga kura kuona zoezi linavyoendelea, ghafla gari langu likashambuliwa kwa mawe na watu ninaowafahamu," amesema Igogo.
Kamanda wa polisi mkoani hapa, Julius Mjengi alipoulizwa kuhusu tukio hilo hakuthibitisha wala kukataa na badala  yake ametaka mwandishi kuvuta subira.
"Kuhusu jambo hilo subiri kidogo,” amesema
Kuhusu upigaji kura amesema unaendelea vizuri katika mitaa yote 23 linakofanyika zoezi hilo la kupiga kura.

Maandamano Islamabad : Jeshi la Pakistan lasema liko tayari kusaidia

Watu 200 walijeruhiwa katika mapigano ya JumamosiHaki miliki ya pichaEPA
Image captionWatu 200 walijeruhiwa katika mapigano ya Jumamosi
Jeshi la Pakistan linasema "liko tayari" kuisaidia serikali kuwatawanya waandamanaji wenye itikadi kali za kiislamu walioifunga barabara kuu wa Islamabad.
Serikali ililiomba jeshi liisaidie kurudisha utulivu baada ya polisi kushindwa kuwatawanya waandamanaji Jumamosi.
Hatahivyo taarifa ya jeshi inaonekana kuishutumu serikali kwa namna ilivyoshughulikia hali, ikieleza kuwa maafisa wa polisi hawakutumiwa vizuri.
Inaaminika kuwa takriban watu 6 wameuawa.
Wengine takriban 200 wamejeruhiwa.
Jeshi limeomba ufafanuzi zaidi kabla ya kuagiza kutumwa kwa wanajeshi.
Wengi ya waliojeruhiwa ni maafisa wa usalamaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWengi ya waliojeruhiwa ni maafisa wa usalama
Waandamanaji wamefunga barabara kwa wiki kadhaa wakitaka waziri wa sheria Zahid Hamid, afutwe kwa kazi kwa makosa ya kukufuru.
Maandamano yamesambaa hadi katika miji mingine ukiwemo Lahore na bandari ya kusini Karachi.
Siku ya Jumamosi, serikali ilifunga kwa muda vituo vya kibinfasi vya habari na kufunga baadhi ya mitandao ya kijamii ukiwemo Facebook, Twitter na Instagram - kutokana na wasiwasi kwamba matangazo ya moja kwa moja ya hatua ya polisi huenda yakachochea hisia kali za kidini.
Vyombo vya habari nchini vinasema vimesalia kufungwa siku ya Jumapili.

Ndege zaonywa kutosafiri katika anga ya Bali baada ya Volkano kulipuka

Moshi mkubwa kutoka mlima AgungHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionMoshi mkubwa kutoka mlima Agung
Kampuni za ndege zimeonywa kuhusu hatari ya jivu la volkano angani kariibu na kisiwa cha Indonesia Bali baada ya mlima wa volcano kulipuka na kusababisha kutanda kwa moshi mweusi mwingi katika urefu wa mita mia moja na kumi na tano angani.
Onyo hilo kwa sekta ya ndege inataja masalio ya volkano yaliotanda angani juu ya mlima Agung katika kisiwa hicho cha Bali.
Maafisa huko wanasema wana wasiwasi huenda mlima huwa ukalipuka kikamilifu hatua itakayo kuwa inashuhudiwa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1963, wakati takriban watu 16 walipouawa.
Maelfu ya watu karibu na mlima Agung wameyatroroka makaazi yao
Image captionMaelfu ya watu karibu na mlima Agung wameyatroroka makaazi yao
Ni tukio la pili la kuplipuka mlima wa volkano katika wiki, na watu wanaoishi kwa umbali wa kilomita nane kutoka mlima huo wameagizwa kuyahama makaazi yao.
Bali ni kivutio kikuu cha utalii.
Uwanja wake mkuu wa ndege unafanya kazi kama kawaida, licha ya kwamba baadhi ya kampuni za ndege zimesitisha safari tangu kuanza kuchemka kwa mlima mnamo September.

Upinzani kuandaa mkutano siku ya kuapishwa kwa Uhuru Kenyatta

Viongozi wa upinzani wa NASA nchini Kenya wakiongozwa na Raila OdingaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionViongozi wa upinzani wa NASA nchini Kenya wakiongozwa na Raila Odinga
Upinzani nchini Kenya Nasa umesema kuwa utaandaa mkutano sambamba siku ambayo rais Uhuru Kenyatta anatarajiwa kuapishwa.
Mkutano huo utafanyika katika uwanja wa Jacaranda katika eneo la Embakasi mjini Nairobi.
Kongamano hilo ambalo maafisa wa polisi wanasema sio halali huenda likasababisha makabiliano makali kati ya wafuasi wa upinzani huo na maafisa hao wa polisi
Tayari viongozi wa upinzani wamesema kuwa hawatambui ushindi wa Uhuru Kenyatta kwa madai kwamba uchaguzi wa marudio uliofanyika tarehe 26 mwezi Novemba ulikuwa haramu.
Vilevile kiongozi wa muugano huo Musalia Mudavadi amesema kuwa watatumia njia halali zilizopo kupinga ushindi wa rais Uhuru Kenyatta licha ya kuidhinishwa na mahakama ya juu.
Mudavadi pia amewaambia Wakenya kutohudhuri sherehe ya kuapishwa kwa rais Uhuru Kenyatta katika uwanja wa Kasarani siku ya Jumanne na badala yake kuhudhuri mkutano wa upinzani huo ili kuomboleza mauaji ya waathiriwa waliouawa na maafisa wa polisi.
Mapema katika taarifa na vyombo vya habari kamanda wa polisi mjini Nairobi Japhet Koome alisema kuwa muungano huo haujaarifu afisa wa polisi kuhusu mkutano huo.
''Hatujui kwamba kuna mkutano kama huo.hatujaarifiwa.
Kwa hivyo mtu yeyeto ambaye anadhani anaweza kufanya mkutano mkutano huo bila kuarifu polisi, mwambieni mtu huyo kwamba sheria itakabiliana na hali hiyo, alisema Koome''.

2 wafariki katika mlipuko mkubwa China

Mlipuko huo umesbaabisha uharibifu wa mali ikiwemo nyumba na magariHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMlipuko huo umesbaabisha uharibifu wa mali ikiwemo nyumba na magari
Maafisa nchini China wanasema watu wawili wamefariki na 30 wakajeruhiwa katika mlipuko kwenye kiwanda kimoja mjini Ningbo, kusini mwa Shanghai.
Mlipuko huo umesababisha vifo vya wawili na wengine wengi wakajeruhiwa.
Madirisha ya majengo yaliyo umbali wa hadi kilomita moja kutoka eneo la mlipuko yamepasuka.
Inakisiwa kuwa mitungi ya gesi imesababisha mlipuko huo, japo polisi wanaendelea na uchunguzi.
Picha zilizotolewa zinaonyesha wafanyikazi wa mjego wakiondoa watu kutoka kwenye eneo la mlipuko ambapo majengo yameharibiwa na magari yamebondwa.
Ambulensi zimeonekana zikiondoa watu kutoka kwenye eneo la mlipuko hadi kwenye hospitali zilizo karibu.
Mji wa Ningbo unajulikana kwa viwanda vya kutengeneza magari.

Mnangagwa amwita Mugabe baba wa taifa

Wananchi wa Zimbabwe waliohudhuria kwa wingi katika sherehe za kuapishwa Rais Emmerson Mnangagwa Harare, Zimbabwe, Novemba 24, 2017.
Rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa Ijumaa amemsifia Rais mstaafu Robert Mugabe na kuahidi kufanya uchaguzi mkuu mwaka 2018 kama ilivyokuwa imepangwa.
Mnangagwa amemwagia sifa Mugabe kwa kumwita "baba wa taifa letu" na kukiri kuwa rais mstaafu alifanya "makosa ya kukusudia na kutokusudia."
Kiongozi huyu mpya aliwaambia watu kwenye uwanja wa mpira wa taifa wenye viti 60,000 mjini Harare kuwa "jukumu kubwa mbele yetu ni kulijenga taifa letu kubwa mara nyingine.
Mnangagwa amesema kuwa yuko tayari kuwalipa wakulima ambao walipoteza ardhi yao chini ya utawala wa Mugabe.
Wapinzani wa Mugabe wamesema kuwa mgogoro wa programu ya marekebisho ya ardhi katika nchi hiyo iliwalazimisha wafanyabiashara wa kilimo wengi wao wenye uzoefu kuachia ardhi zao, na hilo kupelekea kuwepo njaa katika taifa hilo, nchi ambayo ilikuwa inazalisha chakula cha kutosha kusini mwa Afrika.
Mnangagwa alifukuzwa kutoka katika wadhifa wake wa naibu rais na aliyekuwa rais wa nchi hiyo na kuashiria kumuachia madaraka mkewe Grace. Sherehe hizo za kuapishwa kwake zilifanyika kwenye uwanja wa michezo mjini Harare na kuhudhuriwa na maelfu ya Wazimbabwe.
Kwa mujibu wa historia ya Zimbabwe, Mnangagwa anajulikana kama mamba ana uhusiano wa karibu na jeshi la nchi hiyo.
Pia duru za siasa zinaripoti kuwa Rais Mnangagwa atakabiliwa na mitihani mingi ya kuujenga tena uchumi wa nchi hiyo ambao umeharibika vibaya kutokana na utawala wamiongo minne ya Mugabe. Hata hivyo Mugabe pamoja na mkewe Grace Mugabe wamepewa kinga ya kutoshitakiwa.

Kenya yaimarisha ulinzi sherehe za kuapishwa Kenyatta

Uhuru Kenyatta
Matayarisho ya sherehe za kuapishwa kwa Rais Uhuru Kenyatta siku ya Jumanne yamekamilika na tayari vyombo vya usalama vimeimarisha ulinzi wa kutosha kwa wale watakao hudhuria sherehe hizo, kamati ya maandalizi imesema.
Sherehe hizo zitagharimu kiasi cha shilingi milioni 300, na habari za ndani zinasema kuwa kiwango kikubwa cha fedha hizo zitatumika kwa ajili ya ulinzi.
Mnamo mwaka 2013, wakati Rais Kenyatta alipokuwa anaapishwa kwa awamu ya kwanza, kamati hiyo ilikuwa inahitaji shilingi bilioni 1.2, ambazo ofisi ya Hazina baadae ilipunguza kiwango hicho kufikia shilingi milioni 374, na shilingi milioni 64 zilitolewa na Mahakama.
Katika bajeti ya mwaka 2017, hazina imetoa shilingi milioni 384 kwa ajili ya sherehe hizo, ambazo ni shilingi milioni 10 zaidi kuliko ilivyokuwa 2013.
Siku ya Ijumaa, kamati hiyo, inayoongozwa na mkuu wa wafanyakazi wa ikulu na mkuu wa wafanyakazi wa Umma, Joseph Kinyua haikutoa mchanganuo wowote wa shilingi milioni 300 vipi zitatumika. Alisema tu kiwango hicho ni cha “kati na kinatosheleza”.
Kamati ya maandalizi ya kuapishwa kwa Rais kuchukua wadhifa wake imesema kuwa imemwalika kiongozi wa Muungano wa Upinzani, Nasa, Raila Odinga na wagombea wengine sita wa kinyang’anyiro hicho cha urais, pamoja na wagombea wenza wao.
Kinyua pia amemtaka Odinga kusitisha mpango wa maandamano ya Nasa uliopangwa siku ya Jumanne.
Ni lazima sote tushikamane katika kujenga umoja wa taifa la Kenya,” amesema Kinyua kuwaambia waandishi wa habari katika kituo cha kimataifa cha michezo cha Moi, Kasarani, ambapo rais ataapishwa hapo.
Aliendelea kusema kuwa: “Tukio la kuapishwa Rais siku ya Jumanne ni la kihistoria.

Gavana asema uchumi wa Kenya uko imara

Rais Uhuru Kenyatta na Rais Raila Odinga
Uchumi wa Kenya umeonyesha ustahamilivu wa hali ya juu wakati nchi ikikabiliwa na hali tata ya kisiasa, Gavana wa Benki Kuu Kenya amesema Ijumaa.
Amesema nguvu ya uchumi huo inatokana na vyanzo mbalimbali vya uchumi huo na biashara ndogo na za kati nchini humo.
Pia amekadiria kuwa kukua kwa uchumi huo unaweza kufikia asilimia 5.1 mwaka huu—ambacho ni kiwango cha chini kilichofikiwa wakati wa utawala wa Rais Uhuru Kenyatta.
Lakini amesema bado ukuaji huo ni juu ya asilimia 2.6 ya makadirio ya Shirika la Fedha Duniani (IMF) katika nchi za Afrika zilizoko kusini mwa Jangwa la Sahara.
Kenya ilikabiliwa na kipindi kirefu cha ukame kabla ya kutumbukia kwenye mzozo wa kisiasa wa muda mrefu, baada ya Mahakama ya Juu kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa urais, uliofanyika tarehe nane mwezi Agosti 2017.
Kenyatta, anatarajiwa kuapishwa Jumanne wiki ijayo, baada ya kutangazwa mashindi wa marudio ya uchaguzi, ambao ulisusiwa na mpinzani wake wa karibu, Raila Odinga.

Mahakama Marekani kusikiliza kesi bila mshukiwa Reza Zarrab

Mchoro wa sura ya Reza Zarrab, kulia, akiwa mahakamani.
Kesi inayofungamana na mgogoro wa kisiasa inayomhusisha mfanyabiashara mwenye asili ya Uturuki na Iran itaanza kusikilizwa wiki ijayo nchini Marekani lakini inategemewa kufanyika bila ya kuwepo mshukiwa mkuu: Reza Zarrab.
Mfanyabiashara huyo anatuhumiwa kuendesha biashara ya mabilioni ya pesa kwa minajili ya kukwepa vikwazo vya uchumi vilivyowekwa dhidi ya nchi ya Iran.
Zarrab ni mwenye kumiliki mamilioni ya fedha, umri miaka 33, mwenye uraia pacha wa Iran na Uturuki na ambaye anamaslahi ya kibiashara nchini Uturuki na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), na pia mafungamano na serikali ya Uturuki na Iran.
Mfanyabiashara huyu alikamatwa katika jimbo la Florida Machi 2016 akiwa katika ziara pamoja na familia yake kwenye eneo la starehe la Disney World na baadae kuhamishiwa New York.
Mfanyabiashara huyo anakabiliwa na tuhuma za jinai kwa kuisaidia Iran kukwepa vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa na Marekani kati ya mwaka 2010 na 2015 kwa kuzungusha fedha katika mifumo ya kifedha ya Marekani na kuwahonga maafisa wa Uturuki.​
Kesi hiyo ambayo inasubiriwa kufanyika imekuwa ndiyo kiini cha kuendelea kuzorota kwa mahusiano kati ya Marekani na Uturuki.
Rais wa Uturuki Recept Tayyip Erdogan yeye binafsi amekuwa akijaribu kuibembeleza Marekani kumwachia Zarrab, ambapo maswali mengi yameibuka kuwa huenda Erdogan na maafisa wa Uturuki wanawasiwasi kuwa Zarrab anaweza kuwahusisha na tuhuma hizo za rushwa na ufisadi.

KORTINI KWA KUKUTWA NA SEHEMU ZA SIRI ZA WANAWAKE

SERIKALI imemfikisha mahakamani mkazi wa Ipililo, Maswa, Salum Nkonja ama Emmanuel Nkonja (22), aliyekuwa akishikiliwa na Jeshi la Polisi kwa kukutwa na sehemu za siri za wanawake.
Nkonja alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana na kusomewa mashtaka ya kumuua kwa kukusudia mtu asiyejulikana.
Akisoma mashtaka, Wakili wa Serikali, Nassoro Katuga mbele ya Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha, alidai mshtakiwa huyo alifanya kosa hilo kati ya Oktoba mosi na 30, mwaka huu.
“Mshtakiwa anadaiwa kumuua mtu asiyejulikana kwa kukusudia maeneo ya kati ya Kahama mkoani Shinyanga na Ubungo, Dar es Salaam,” alidai.
Hakimu Mkeha alimfahamisha mshtakiwa kwamba hatakiwi kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.
Katuga alidai upelelezi haujakamilika na kesi iliahirishwa hadi Desemba 8, mwaka huu.
Katika hatua nyingine, taarifa kutoka vyanzo vya uhakika zinasema mshtakiwa huyo alikutwa na viungo vya binadamu zikiwamo sehemu za siri za wanawake ambazo zimekaushwa.

EU: ZINGATIENI HAKI ZA BINADAMU MAPAMBANO DHIDI YA UFISADI

SERIKALI imeshauriwa kuzingatia misingi ya utawala bora na haki za binadamu katika mapambano yake dhidi ya vitendo vya rushwa na ufisadi.
Ushauri huo ulitolewa Dar es Salaam jana na Balozi wa Umoja wa Ulaya (EU), Roeland Van der Geer, katika hafla ya uzinduzi wa mradi wa ‘Tuungane Kutetea haki’ unaofadhiliwa na EU, wenye lengo la kuongeza uelewa wa wananchi katika kukabiliana na tatizo la rushwa na kuongeza uwajibikaji katika ngazi za halmashauri.
Balozi Van Geer pamoja na kutambua mchango wa Rais Dk. John Magufuli na Serikali yake katika kupambana na rushwa, alitaka jitihadi hizo zizingatie uwazi na uwajibikaji.
“Rushwa ni adui mkubwa wa maendeleo na dawa yake ni uwazi, tunatambua mchango wa Rais Dk. Magufuli katika kushughulikia vitendo vya rushwa hivyo mapambano hayo yawe endelevu na yafuate sheria, utawala bora na kuzingatia haki za binadamu.
“Pia kitendo cha Serikali kuanzisha mahakama maalumu kwa ajili ya kushughulikia kesi za rushwa na mafisadi na kupitishwa kwa mpango mpya wa kupambana na rushwa, hizo ni jitihada kubwa sana na EU inaahidi kuendelea kuunga mkono mapambano hayo,” alisema Van der Geer.
Kwa upande wake Meneja wa Mradi unaotekelezwa na Taasisi ya Konrad Adenauer Stiftung (KAS), Maria Kayombo, alisema mradi huo unalenga kuongeza ulewa wa wananchi kukabiliana na rushwa na kuwa na uwezo wa kuhoji masuala mbalimbali kwa viongozi hivyo kuongeza uwazi na uwajibikaji kuanzia ngazi ya mitaa hadi halmashauri.
“Mradi utawajengea wananchi uwezo wa kushiriki kwenye michakato ya maendeleo kama vile kuibua, kupanga, kutekeleza na kusimamia miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kuhakikisha Serikali inatoa taarifa mbalimbali za miradi ya maendeleo,” alisema Maria.
Alisema mradi huo utatekelezwa ndani ya miaka miwili kuanzia 2017 hadi 2019 ukihusisha zaidi ya kata 1,000 kwenye wilaya 40 na mikoa 7 ya Tanzania Bara na kugharimu Sh bilioni 2.5.

JPM, BUNGE WAOMBOLEZA KIFO CHA MBUNGE WA SONGEA MJINI

RAIS Dk. John Magufuli, ametuma salamu za rambirambi kwa Spika wa Bunge, Job Ndugai, kutokana na kifo cha Mbunge wa Songea Mjini (CCM), Leonidas Gama (58), kilichotokea juzi usiku baada ya kusumbuliwa kwa maradhi ya moyo.
Gama anayetarajiwa kuzikwa keshokutwa katika Kijiji cha Likuyu Fusi kilichopo Manispaa ya Songea Mjini, alikutwa na umauti katika Hospitali ya Mtakatifu Joseph ya Peramiho iliyopo wilayani Songea baada ya kufikishwa kwa matibabu kutokana na kuugua ghafla.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano-Ikulu, Gerson Msigwa, ilieleza kuwa Magufuli ameshtushwa na taarifa ya kifo cha mbunge huyo.
“Nimepokea kwa mshtuko na majonzi taarifa za kifo cha ghafla cha Leonidas Gama, nakupa pole Spika Ndugai, wabunge na wafanyakazi wa ofisi yako.
“Kupitia kwako, naomba ufikishe salamu zangu za pole kwa familia ya marehemu, wananchi wa Songea Mjini na mkoa mzima wa Ruvuma, ndugu jamaa na marafiki walioguswa na msiba huu,” alisema.
Pia amempa pole Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Ruvuma, Odo Mwisho na wanachama wote kwa kumpoteza kada aliyekiwakilisha vema chama hicho katika nafasi ya ubunge.
Alisema mbali na ubunge, pia aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali za uongozi zikiwamo mkuu wa wilaya na mkoa akifanya kazi kwa kujiamini na kupigania masilahi ya wananchi bila kuchoka.
Katika hatua nyingine, Ofisi ya Bunge kupitia Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano, kimeeleza masikitiko yake kuhusu kifo hicho.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyomnukuu  Ndugai, ilieleza kuwa Novemba 11, mwaka huu, Gama, alirejea nchini kutoka India alikokuwa anatibiwa.
“Novemba 21 alitokea Dar es Salaam na kurejea Songea kupitia mkoani Dodoma ili kushiriki mapokezi na ziara ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, iliyoanza jana Ruvuma,” alisema Ndugai.
Alisema Novemba 22, mwaka huu saa sita usiku aliugua ghafla na alikimbizwa Hospitali ya Peramiho kwa matibabu.
Alisema baada ya Ofisi ya Bunge kupata taarifa hizo iliandaa ndege maalumu kwa ajili ya kumsafirisha kwenda Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa matibabu zaidi.
Alisema madaktari wa Peramiho walishauri asisafirishwe hadi hali yake itakapotengemaa lakini jana alifariki dunia.
Alisema Ofisi ya Bunge inaendelea kuratibu taratibu za mazishi ikishirikiana na Serikali na familia yake na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.
Pia taarifa kutoka Songea zinaeleza kuwa wakazi wa Songea Mjini wamepokea kwa mshtuko msiba wa Gama.
Akizungumza na gazeti hili, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Songea Mjini, Hamis Ally, alisema chama na wakazi wa jimbo hilo wamepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa za kifo cha Gama kwa kuwa siku chache zilizopita alipita maeneo hayo kufanya ziara katika baadhi ya kata za jimbo hilo.
Alisema juzi usiku alipokea taarifa za ugonjwa wa mbunge huo kutoka kwa mmoja wa wanafamilia akimweleza kwamba Gama amezidiwa na homa akiwa nyumbani kwake na walifanya jitihada za kumpeleka hospitali.
“Baada ya kupata taarifa hiyo, niliondoka usiku huo saa tano na kuelekea nyumbani kwake Likurufusi na kuungana na wanafamilia kumpeleka Hospitali ya Peramiho,” alisema Ally.
Alisema baada ya kuwasili hospitalini hapo madaktari walimpeleka katika chumba cha uangalizi maalumu (ICU).
Alisema kwa mujibu wa wanafamilia waliokuwa karibu naye usiku ule walimwambia kuwa Gama alitoka kuoga baada ya kuingia chumbani alianza kujisikia vibaya na alikuwa akitokwa na jasho na mwili wake kuishiwa nguvu.
Naye msemaji wa familia ya mbunge huyo, Issa Fusi, alisema mazishi yake yatafanyika keshokutwa katika Makaburi ya Likurufusi.
Kabla ya mauti hayajamkuta, inadaiwa Gama alisumbuliwa na ugonjwa wa moyo uliomsababisha kwenda India kutibiwa na safari ya mwisho alitokea huko na aliwasili hapa nchini kisha akaenda Dodoma na safari ya jimboni kwake ilikuwa ni kuiwahi ziara ya Majaliwa lakini hakufanikiwa.

Saturday, November 25

MAJALIWA: TANESCO KAWAHUDUMIENI WANANCHI VIJIJINI


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ameliagiza Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) liwafuate wananchi walioko katika vijiji vinavyotarajiwa kuunganishiwa umeme kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) na kuwahudumia.

Amesema Serikali imetenga shilingi trilioni moja kwa ajili ya kusambaza umeme katika vijiji vyote ambavyo bado havijaunganishiwa nicety hiyo nchini, hivyo ni vema wakawatembelea wananchi katika maeneo yao na kuwahudumiahuko huko.

Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo jana jioni (Ijumaa, Novemba 24, 2017) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika uwanja wa michezo Tunduru, ambapo aliwasisitiza watumishi wa TANESCO kutokaa maofisini na badala yake wakawahudumie wananchi katika vijiji vyao.

Alisema katika kipindi hiki ambacho Serikali inatekeleza miradi ya kusambaza umeme vijini kupia REA, TANESCO wanatakiwa kwenda vijijini na kuwaandikisha wananchi wanaohitaji huduma hiyo pamoja na kufungua vituo vya muda vya malipo.

Waziri Mkuu alisema hatua hiyo itawapunguzia wananchi gharama za kusafiri hadi kwenye makao makuu ya wilaya kufuata huduma mbalimbali ikiwemo ya kulipia gharama za kuunganishiwa umeme katika nyumba zao.

Alisema Serikali imedhamiria kusambaza huduma ya nishati ya umeme katika vijiji vyote nchini vikiwemo vya wilaya ya Tunduru ambapo wananchi hao wataunganishiwa umeme huo kwa gharama ya sh. 27,000 tu.

Pia Waziri Mkuu aliesema wananchi hawatowajibika tena katika kulipia gharama za nguzo wala fomu za maombi ya kuunganishiwa umeme, kwa sababu tayari gharama hizo zimeshabebwa na Serikali.

Waziri Mkuu aliongeza kwamba lengo la Serikali ya awamu ta tano chini ya Rais Dkt. John Magufuli ni kufikisha umeme kwenye vijiji vyote Tanzania na kwa vile ambavyo viko kwenye maeneo yaliyo mbali na gridi vitafungiwa sola, jambo ambalo litafungua fursa za ajira na kukuza uchumi kwa wananchi na Taifa.

Waziri Mkuu alisema huduma hiyo ni muhimu kwani mbali ya kutumika katika matumizi ya majumbani, pia kwa kusogezwa karibu na maeneo ya pembezoni itawezesha zahanati, shule ,viwanda na vituo vya afya kuwa na umeme.

Awali Waziri Mkuu alitembea na kukagua shughuli za ujenzi wa mradi wa kituo cha afya kinachojengwa katika eneo la Nakayaya wilayani Tunduru pamoja na kukagua ghala la kuhijfadhia korosho na kisha kupokea taarifa ya kiwanda cha kubangulia korosho cha Korosho Afrocan Limited.


IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU, 
JUMAMOSIni, NOVEMBA 25, 2017.

Kanzi Data Ya Kuhifadhi Taarifa Za Wadau Wa Tasnia Ya Filamu Kuleta Maslahi Katika Tasnia


Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Cogsnet Bw. Nkundwe Moses Mwasaga akielezea namna kampuni hiyo itakavyohifadhi data za wanatasnia ya filamu wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo akifafanua jambo wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe akizungumza wakati wa kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam
Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba (wapili kushoto waliokaa) pamoja na mwanasheria wa kampuni ya Cogsnet Bw. Thomas Herman (katikati waliokaa) wakisaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam. Waliosimama katikati ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe
Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba (kulia) akikabidhiana mkataba na mwanasheria wa kampuni ya Cogsnet Bw. Thomas Herman (kushoto) baada ya kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe (waliokaa katikati) katika picha ya pamoja na wadau wa tasnia ya filamu baada ya kusaini mkataba wa kutengeneza Kanzi Data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu kati ya kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam. Wapili kulia ni Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo.Picha na: Genofeva Matemu – WHUSM


Na: Genofeva Matemu – WHUSM

Wadau wa tasnia ya filamu nchini wametakiwa kujitokeza kwa wingi kujiunga katika vyama vilivyopo chini ya Shirikisho la filamu ili waweze kuingia katika mpango wa Kanzi Data inayolenga kuhifadhi taarifa za wasanii na kuinua maslahi ya tasnia kupitia tuzo na mashindano mbalimbali yatakayoandaliwa.

Rai hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Harrison Mwakyembe wakati wa kusaini mkataba wa kanzi data itakayohifadhi taarifa za wasanii wa filamu kati ya Kampuni ya Cogsnet na Shirikisho la Filamu leo Jijini Dar es Salaam.

“Ni wajibu wetu kuhamasisha wadau wa tasnia ya filamu kuingia katika mfumo wa kanzi data kwani mpango huu umedhamiria kuboresha na kuendeleza maslahi ya tasnia ya filamu na kuleta maendeleo ya msanii mmoja mmoja” amesema Mhe. Mwakyembe

Awali Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Bibi. Joyce Fissoo amesema kuwa tasnia ya filamu imekua ikikosa fursa nyingi kutokana na wadau kutokua katika kanzi data inayowatambua vizuri hivyo ujio wa kanzi data hii utakua mkombozi kwa tasnia.

Bibi. Fissoo amesema kuwa suala la kanzi data limilikiwe na wadau wote kwa kupata uelewa na kila litakalofanyika katika kanzi data hiyo lifanywe kwa maslahi ya sekta ya filamu kwani filamu ni uchumi, filamu ni ajira na filamu ni kwa maendeleo endelevu.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kampuni ya Cogsnet Bw. Nkundwe Moses Mwasaga amesema kuwa kampuni yake inaingia mkataba wa kuunda kanzi data ya wanatasnia ya filamu na shirikisho la filamu kwa ajili ya kuongeza msukumo wa kuifanya tasnia ya filamu kukua na kuendelea kwa kasi zaidi.Aidha Bw. Mwasaga amesema kuwa kanzi data hiyo itasaidia kujua mapato yanayopatikana kupitia kazi za filamu lakini pia namna tasnia ya filamu inavyochangia katika pato la taifa.

Naye Rais wa Shirikisho la Filamu Bw. Simon Mwakifwamba amesema kuwa mchakato wa kufanikisha kanzi data itakayohifadhi taarifa za wanatasnia ya filamu unahitaji wanachama wasiopungua laki tano kwa kuanzia, na wanachama hao ni lazima wawe ndani ya vyama vilivyopo chini ya shirikisho la filamu huku kila mwanachama atakayekuwepo katika kanzi data hiyo atatakiwa kuchangia shilingi elfu moja kwa kila mwezi.

Serikali kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora


Naibu Waziri Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile(katikati)akiongea na Viongozi na Watendaji wa Afya Afya Mkoa na Wilaya ya Mtwara wakati wa zoezi la kutoa ngao na vyeti kwa vituo vya afya vilivyo na ubora wa huduma za afya.Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Mhe.Evod Mmanda na kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Dkt.Wedson Sichalwe
Mkuu wa Wilaya MHE.Evod Mmanda akiongea wakati wa mkutano huo
Mkurugenzi wa Idara ya Ubora na Uhakiki wa Huduma za Afya toka Wizara ya Afya Dkt.Mohamed Mohamed akielezea tathimini ilivyofanyika katika Mkoa huo mwaka 2016 na Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Kuibuka mshindi kwa kupata ngao na cheti
Dkt.Ndugulile akimkabidhi Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu Dkt.Furaha Mwakafyila Ngao baada ya kuibuka mshindi wa Huduma za afya katika vituo vya afya
Afisa Tawala wa Wilaya ya Nanyumbu Salumu Palango akimpongeza Kaimu Mganga Mkuu wake baada ya kupokea ngao


Naibu Waziri akimpongeza Kaimu Mganga Mkuu wa Wilaya ya Nanyumbu baada ya kuibuka mshindi.Dkt.Ndugulile aliipongeza Wilaya hiyo kwa mpangilio mzuri wa utoaji huduma pamoja na utunzaji wa kumbukumbu kwenye stoo ya dawa katika kituo cha afya cha Mtambaswala ambacho kimeanza miezi miwili iliyopita lakini kimeonyesha ufanisi wa hali ya juu.
Picha ya pamoja mara baada ya Naibu Waziri kutoa ngao na vyeti kwa washindi kwa Mkoa wa Mtwara
Dkt.Ndugulile akisoma taarifa ya dawa katika Zahanati ya Ziwani iliyopo Manispaa ya Mtwara,ambapo Naibu Waziri huyo alichukizwa hali ya miundombinu na uwajibikaji wa Zahanati hiyo na kuwapa miezi miwili wawe wamefanya marekebisho kama walivyoelekezwa.
Mkuu wa Zahanati ya Shangani akipokea cheti kutoka kwa Naibu Waziri wa Afya



Serikali inatarajia kutoa leseni kwa hospitali na vituo vya afya vya Umma vitakavyokidhi vigezo vya ubora wa kutoa huduma za afya ili mwananchi wajue kituo atakachoenda kina ubora gani wa huduma hivyo nchini

Hayo yamesemwa jana na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Dkt.Faustine Ndugulile wakati akiongea na Viongozi na Watendaji wa afya wa Mkoa na Wilaya zake kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mtwara wakati wa zoezi la kutoa ngao kwa wilaya iliyofanya vizuri na vituo vya afya vilivyofanya vizuri wakati wa zoezi la tathimini ya kutoa nyota kwa vituo vya kutolea huduma za afya.

Dkt.Ndugulile alisema hivi sasa serikali inasisitiza kuweka ubora wa huduma za afya katika vituo vyote vya afya vya umma ili kukidhi ubora unaotakiwa wa kutoa huduma kwa wananchi”tunakwenda mbali zaidi usipokuwa na vigezo hospitali yako na kituo chako hutopewa leseni”

Hata hivyo amewataka wale wote waliopewa maelekezo ya nini wafanye basi viongozi wawajibike kwa kurekebisha changamoto zilizopo na wasingoje idara ya uhakiki ubora kutoka wizarani waje kukagua kwani Lengo liliowekwa na wizara ni kila kituo cha afya kupata nyota tatu hadi kufikia mwezi juni mwakani.

“Nyinyi wengine wote hamkustahili kupata cheti hata kimoja hapa,Mkoa wa Mtwara asilimia 3 za vituo vyenu vina nyota mbili na asilimia 51 vina nyota moja na zaidi ya nusu mna nyota 1 na asilimia 46 mna nyota sifuri hali ya utoa huduma bado”Nimetoka hapo zahanati ya Ziwani,kwakweli hapana,ubora wa kutoa huduma pale hapana wakati mpo mjini.

Kwa upande mwingine amewataka kamati za afya ngazi ya Mkoa na Wilaya kufanya kazi na kusimamia katika kuyafanyia kazi maelekezo yote waliyopatiwa kwani maboresho mengine hayahitaji fedha hivyo kamati hizo zitimize wajibu wao”Niwaombe mbadilike kwani mambo madogo madogo yatakuja kuwagharimu hivyo msimamie hali ya utoaji wa ubora na huduma za afya kwa mkoa wa mtwara ni mbaya,nikirudi wakati mwingine sitoongea kirafiki hivi”alisisitiza

Aidha,aliwataka watendaji hao kubadilika katika utendaji wao na hivyo kusimamia upatikanaji wa dawa katika vituo vyao vya afya ili kusiwepo na malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba wamekosa dawa

“Dhama imebadilika,hivyo kila mmoja awajibike,awamu hii ni nyingine,hatutaki kusikia dawa hakuna na mwananchi analalamika amekosa dawa kwenye kituo cha afya,Mhe.Rais anaipenda sekta ya afya na ameongeza bajeti ya dawa na anatoa pesa zote,sitaki kusikia dawa hakuna na Wilaya itakayoshindwa basi viongozi wake nao hawatoshi”aliongeza Naibu Waziri

Naye Mkurugenzi wa Idara ya Uhakiki Ubora toka Wizara ya afya Dkt. Mohamed Mohamed alisema wizara ilingia kwenye mpango wa kuboresha huduma kwenye vituo vinavyotoa huduma za afya ya Msingi mwaka 2014 kwa kuhusisha kufanya tathimini vituo vyote vya afya nchini na kuvipa kategoria ya nyota moja hadi tano ikiwemo wa kuandaa mipango ya kuimarisha ubora katika vituo hivyo.

“Tathimini ya awali ilifanyika katika vituo vyote vya kutolea huduma za afya ya msingi nchini mwaka Aprili,2015 na Desemba 2016”

Alitaja maeneo yaliyoangaliwa na kufanyiwa tathimini ni uendeshaji wa vituo ,utendaji wa wafanyakazi,uwajibikaji,miundombinu ya kituo,mkataba kwa mteja pamoja na mazingira salama ya kutolea huduma na ubora wa huduma wenyewe.

Jumla ya vituo 6997 vilifanyiwa tathimini nchini na katika Mkoa wa Mtwara tathimini ya awali ilifanyika mwezi mei 2016 na vituo 221 vilifanyiwa tathimini na matokeo ya awali yalikua vituo 6 vilipata nyota 2(3%),vituo 112 vilipata nyota 1(51%) na vituo 103 vilipata nyota 0(47%).

Katika zoezi hilo Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu iliibuka mshindi kwa kupata ngao,na kituo cha afya Nanyumbu kilipata cheti.Kituo kingine cha afya kilichopaya cheti ni kituo cha Nagaga cha Masasi pamoja na za zahanati ya Nanjota na Nambaya zote za Halmashauri ya Masasi zilifanya vizuri.Pia zahanati ya Shangani ya halmashauri ya Manispaa ya Mtwara ilipata cheti