Sunday, November 12

Ndovu afanyiwa upasuaji kwenye pembe Colombia

Tantor the Elephant at Barranquilla Zoo has surgery 11/11/17Haki miliki ya pichaJORGE_CHAVEZ
Image captionNdovu afanyiwa upasuaji kwenye pembe Colombia
Hifadhi moja wa wanyama nchini Colombia umemfanyia upasuaji ndovu mmoja wa uzito wa tani tano aliyepatikana katika shamba moja linalomilikiwa na walanguzi wa madawa ya kulevya.
Wati 30 walishiriki wakati ndovu huyo kwa jina Tantor alidugwa dawa ya kumpa usingizi.
Upasuaji ulifanywa kwa pembe yake iliyokuwa imepasuka.
Zaidi ya watu 100 walichanga pesa kwa upasuaji huo ambao uligharimu zaidi ya dola 8,500.
Tantor the Elephant at Barranquilla Zoo has surgery 11/11/17Haki miliki ya pichaJORGE_CHAVEZ
Image captionNdovu afanyiwa upasuaji kwenye pembe Colombia
Upasuaji huo ungefanyika miaka miwila iliyopita wakati Tantor alijeruhi pembe yake, likini shughuli hiyo ilichelewa baada ya kukosekana kwa vifaa vinavyostahili ili kufanya upasuaji.
Iibidi vifaa maalumu kutengenezwa kwa upasuaji huo.
Tantor alipekwa katika hifadhi ya Barranquilla Aprili mwaka 1991 wakati alipatwa na shirika la kupambana na madawa ya kulevya nchini Colombia kwenye shamba moja linalomilikiwa na walanguzi wa madawa ya kulevya.
Anaaminiwa kuwa na umri wa karibu miaka 50.

Waziri mkuu Uhispania aapa kumaliza mzozo wa Catalonia

Spanish Prime Minister Mariano Rajoy and Catalan People's Party (PP) president Xavier Garcia Albiol wave as they arrive at a Catalan regional People"s Party meeting in Barcelona, Spain 12 November 2017Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWaziri mkuu Mariano Rajoy (kushoto)
Waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy amesema kuwa uchaguzi wa eneo la Catalonia mwezi ujao utasaidia kumaliza mzozo wa kijitenga katika eneo hilo la kaskazini mashariki mwa nchi.
Alihutubia mkutano wakati wa ziara yake ya kwanza tangu kutangaza udhibiti kamili eneo hilo.
Viongozi kadhaa waku wa Catalonia kwa sasa wanazuiliwa kufuatia hatua hiyo.
Takriban watu 75,000 waliandamana mjini Barcelona siku ya Jumamosi kupinga kukamatwa viongozi hao.
Hali hiyo ilichochewa na kura ya maoni iliyokumbw na utata ilyofanyika Catalonia mwezi Oktoba ambayo ilikuwa imezuiwa na mahakama za Uhispania.
Protesters shine their mobile phone torches in Barcelona, 11 NovemberHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionTakriban watu 75,000 waliandamana mjini Barcelona siku ya Jumamosi kupinga kukamatwa viongozi hao.
Maafisa huko Catalonia walisema kuwa kura hiyo ilipata asilimia 92 ya kura kutoka kwa watu asilimia 43 waliojitokeza.
Wengi wa wale waliopinga kura hiyo hawakupiga kura na walikataa kutambua uhalali ya kura hiyo.
Serikali ya Catalonia hatimaye ikatangaza uhuru. Kujibu hilo serikali ya Uhispania ilivunja bunge la Catalonia na katangaza udhibiti kamili na kuitisha uchaguzi wa mapema tarehe 21 Disemba.

Mradi wa maji Moshi kugharimu Sh400 milioni


Mradi wa majisafi na salama katika vijiji vya Mweka, Sungu na Chuo cha Wanyamapori Mweka unaotarajiwa kukamilika Februari mwakani utagharimu Sh400 milioni na kunufaisha zaidi ya kaya 3,500.
Akizungumza katika mahojiano na mwandishi wa gazeti hili, Kaimu mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Moshi (Muwsa), John Ndetiko alisema: “Kiutendaji eneo hili la Kibosho siyo letu, ila kwa kuwa wizara ya maji imetuomba tushirikiane na Halmashauri ya Moshi, Bonde la Pangani na Sekretarieti ya Mkoa, tukaona ni vyema tuutekeleze ili tuwasaidie wananchi hawa ambao wanaoumia zaidi ni wanawake.”
Mhandisi wa maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi, Elifadhili Mrutu alisema wakati wanaanza walikutana na changamoto ya hitaji kubwa la wananchi wa eneo hilo.
Mrutu alimuomba mkuu wa mkoa huo kuwaeleza wananchi hao kuwa mradi huo ni mali yao na wanapaswa kuupokea na kuutunza.
“Wakati wa upimaji wananchi walipinga sisi kuendelea, lakini tulivyomshirikisha mkuu wa wilaya, alifika na kuitatua changamoto hiyo...nazidi kuwaomba wananchi waupokee na kuutunza kwa manufaa ya vizazi vijavyo,” alisema Mrutu.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Sungu, William Kiwale alisema baada ya wataalamu kutoka Bonde la Maji la Pangani kufika na kupima kiwango cha maji waligundua kuwa yaliyopo yanatosheleza kaya 3,600 kijijini hapo.
“Wataalamu walipofika kwenye chanzo cha Mto Lombanga waligundua kuwapo kwa kiasi cha kutosha cha maji, wakapendekeza kutoa lita 10 kwa sekunde. Tunaomba Serikali iendelee na mradi huu,” alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira aliwataka wananchi kushirikiana na wataalamu wanaoendelea na mradi huo.

Ng’ombe 900 wakamatwa Pori la Akiba la Muyowosi


Serikali wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma imekamata ng’ombe 928 katika Pori la akiba ya Muyowosi wanaodaiwa kuingizwa nchini kwa njia haramu kutoka nchi jirani ya Rwanda.
Ng’ombe hao walikamatwa baada ya kufanyika operesheni ya kuzuia mifugo kuingizwa nchini kwa njia ya magendo.
Kati ya idadi hiyo, ng’ombe 572 wapo Kijiji cha Kumuhasha na 350 wapo Kijiji cha Busunzu.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari katika Kijiji cha Kumuhasha, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo, Louis Bura alisema walibaini ng’ombe hao kwa kuwa wamepigwa chapa ya nchi hiyo.
Alisema wamiliki wa ng’ombe hao walilazimika kutafuta sehemu nyingine ya malisho ili kuokoa mifugo yao.
“Ndipo wamiliki hao walipovamia pori la akiba la Muyowosi na kuanza kuchungia ng’ombe humo, lakini hawakujua kwamba mkono wa Serikali ni mrefu na hatimaye tuligundua wameficha ng’ombe kwenye pori hilo, tumewakamata na tunashikilia mifugo yao,” alisema Bura.
Ng’ombe hao walipitia pori la Burigi lililopo mkoani Kagera kabla ya kutoroshwa huko na kuingizwa pori la Muyowosi lililopo Kibondo.
Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Juma Mnwele alisema hawapo tayari kuona wafugaji wakiigeuza halmashauri kama kichaka cha kuficha mifugo kutoka nchi jirani na mikoa mingine nchini.
Alisema endapo wamiliki wa ng’ombe hao watashindwa kulipa fidia ndani ya siku tatu mifugo hiyo itauzwa kwa mnada.
Makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo, Hamisi Kapukii alisema kuingiza mifugo kiholela kunasababisha mapigano baina ya wakulima na wafugaji kwa vile mifugo huharibu mazao.
Mkazi wa Kijiji cha Kumuhasha, Noel Joel alisema mifugo imekuwa ikiharibu mazao yao.

Vifaa vya mionzi kuzalishwa nchini


Serikali imesema baadhi ya vifaa tiba vya matibabu ya mionzi vitaanza kuzalishwa nchini baada ya kuingia makubaliano ya ushirikiano na Kampuni New Soft ya China.
Baadhi ya vifaa hivyo ni Ultrasound, CT-scan, MRI na Digital X-Ray.
Hata hivyo, Serikali haikueleza uzalishaji huo utaanza lini ambao umelenga kuboresha huduma kwa Watanzania.
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo, Jinsia ya Watoto na Wazee, Dk Faustine Ndugulile alitoa kauli hiyo jana katika hotuba yake iliyosomwa na James Boyi ambaye pia ni Mkuu wa Huduma za Radiolojia kutoka wizara hiyo.
Dk Ndugulile alieleza hayo wakati akifungua mkutano wa Chama cha Wateknolojia wa Matumizi ya Mionzi katika Uchunguzi na Tiba ya Magonjwa (Tara), uliokwenda sambamba na kuadhimisha siku ya 122 kimataifa ya ugunduzi wa mionzi duniani.
“Vifaa hivi vitakuwa vikizalishwa hapa hapa. Pia wataalamu watapata fursa ya kupewa mafunzo ya utengenezaji na uendeshaji wa vifaa hivyo nchini,” alisema Dk Ndugulile.
Awali, mwenyekiti wa Tara, Stephen Mkoloma aliwahikikisha Watanzania kuwa mionzi ya hospitali ni salama na aliwataka kujitokeza mapema kwa ajili ya uchunguzi na wakigundulika wana matatizo waanze matibabu haraka.
“Mfano kama una tatizo la saratani nenda hospitali usiende kwa mganga wa kienyeji, hakuna mganga wa kienyeji anayeweza kutibu saratani. Pia hakuna utafiti uliofanyika kwamba mtu ametumia dawa za kienyeji amepona,” alisema.
Mkoloma alifafanua kuwa wao kama wataalamu wapo tayari kuwahudumia Watanzania huku akisisitiza kuona umuhimu wa kwenda hospitali kwa ajili ya kufanya uchunguzi dhidi ya afya zao.

Nyalandu akwama kuhutubia mkutano wa Chadema


Aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu aliyejiondoa CCM siku 12 zilizopita ameshindwa kupanda jukwaani mjini Mtwara katika mkutano wa Chadema.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe jana Jumamosi Novemba 11,2017 akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni ya uchaguzi mdogo wa udiwani katika Kata ya Saranga jijini Dar es Salaam alisema amempokea Nyalandu na leo Jumapili Novemba 12,2017 angeungana naye kwenye mkutano wa kampeni mjini Mtwara.
Hata hivyo, kukosekana kwa ndege inayofanya safari kati ya Dar es Salaam na Mtwara kumemsababishia Nyalandu kushindwa kuhudhuria mkutano huo.
Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amesema Nyalandu aliyekuwa Nairobi nchini Kenya kumjulia hali Tundu Lissu amekosa ndege ya kwenda Mtwara.
Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki anaendelea na matibabu ya majeraha ya risasi katika Hospitali ya Nairobi, Kenya. Alishambuliwa akiwa maeneo ya makazi yake Area D mjini Dodoma Septemba 7,2017.
Mrema amesema Nyalandu amefika Dar es Salaam lakini kwa bahati mbaya hakuna ratiba ya ndege ya Mtwara kwa leo Jumapili Novemba 12,2017.
"Tunaomba radhi, tukio hilo tunaliandalia mahali pengine na wakati ukifika tutakuwa pamoja naye," amesema Mrema.
Nyalandu baada ya kujiondoa CCM, aliiomba Chadema imfungulie “malango”.
Alipomtembelea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ofisini kwake Mikocheni, Dar es Salaam hivi karibuni, Nyalandu alimshukuru “kwa kuonyesha njia kwa wengine kuwa kuna maisha nje ya CCM”.
Viongozi wa juu wa Chadema wamejipanga kuongoza kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata 43 nchini.
Chama hicho kimeunda kamati za kitaifa 10 zitakazokwenda kuongeza nguvu, hamasa na mikakati ya kampeni za uchaguzi huo utakaofanyika Novemba 26.

Bodi ya Mikopo yatangaza orodha mpya ya mikopo


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetangaza orodha nyingine yenye wanafunzi 1,775 wa mwaka wa kwanza waliopata mikopo.
Kwa orodha hiyo, jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza waliopangiwa mikopo hadi sasa imefikia 31,353.
Katika awamu ya kwanza, wanafunzi 10,196 wa mwaka wa kwanza walipangiwa mikopo; awamu ya pili (11,481) na ya tatu (7,901).
Taarifa ya HESLB iliyotolewa leo Jumapili Novemba 12,2017 na Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Abdul-Razaq Badru, imesema orodha kamili ya wanafunzi hao inapatikana katika tovuti ya bodiwww.heslb.go.tz na pia imeshatumwa kwa vyuo husika ili kuwawezesha wanafunzi kufanya usajili na kuendelea na masomo.
“Tumekuwa tukifanyia kazi orodha za udahili ambazo tumekuwa tukipokea, na kila tunapokamilisha tunatoa orodha za wanafunzi waliopangiwa mikopo ambao wana sifa,” amesema Badru.
Badru katika taarifa kwa vyombo vya habari amesema Sh427.54 bilioni zimetengwa kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi kwa mwaka 2017/18 na tayari Serikali imeshatoa Sh147.06 bilioni kwa ajili ya robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2017/18.
Fedha hizo, Sh427.54 bilioni amesema ni kwa ajili ya wanafunzi 122,623 wa mwaka wa kwanza na wanaoendelea na masomo.
Wakati huohuo, HESLB imetangaza kufungua dirisha la rufaa kuanzia kesho Jumatatu Novemba 13,2017 hadi Novemba 19, 2017 ili kuwapa fursa waombaji ambao hawajaridhika na upangaji wa mikopo kuwasilisha rufaa kupitia vyuo walivyopata udahili. 
Badru amesema lengo la HESLB ni kuhakikisha wanatangaza orodha ya majina ya waombaji mikopo waliofanikiwa katika rufaa ifikapo au kabla ya Novemba 30,2017.
“Tunatoa wito kwa uongozi wa vyuo vyote kupokea maombi ya rufaa za wanafunzi na kuwasilisha kwa Bodi kabla ya Novemba 22,2017 ili kuiwezesha Bodi kutoa orodha ya waombaji waliofanikiwa katika rufaa zao ifikapo Novemba30, 2017,” amesema Badru.

Wabunge wataka wawekezaji wazawa wasaidiwe


Wabunge wameicharukia Serikali kuacha kuwakatisha tamaa wawekezaji wazalendo kwa kuwapiga vita katika biashara na badala yake iwasaidie waweze kukua kiuchumi.
Wakizungumza katika semina ya wabunge iliyoandaliwa na kampuni ya Maxcom Afrika  leo Novemba 12, wamesema baadhi ya watumishi wa Serikali wamekuwa wakipiga vita kampuni zinazomilikiwa na wazawa.
Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe amesema baadhi ya watumishi wameanza utamaduni wa kushusha ubora  kazi zinazofanywa na wazalendo.
“Kuna kampuni moja ya kizalendo ilikuwa inahusika na E-migration (uhamiaji mtandao) imeendelea kwa miaka sita lakini wakubwa wanawanyang’anya na wanaleta watu wengine,” amesema
Amewataka watendaji kuacha wivu kwa wazawa wanapopata fursa za kukuza uchumi wa nchi.
Mbunge wa Ileje (CCM), Janet Mbene ameeeleza kusikitishwa na vita inayopigwa kwa kampuni ya Maxcom. Alisema baadhi ya idara za Serikali zimewanyang’anya baadhi ya huduma akiitaja Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
“Kama kuna sehemu wamekosea warekebishwe na si kunyang’anywa, adui lazima wawepo sasa tusirudi nyuma, tusiingize vitu binafsi kwenye masilahi ya Taifa, vitu hivi vinawakimbiza vijana nje,” amesema Mbene.
Mbunge wa Singida Magharibi, (CCM), Elibariki Kingu alisema inashangaza Serikali inawekeza fedha kuibua vipaji vya Watanzania lakini wakikua na kuanzisha kampuni baadhi ya watendaji wanawapiga vita.
“Acheni kuwavunja moyo wazawa na kuwawekea vikwazo, wasaidieni wakue zaidi Afrika Mashariki na kuna madai Serikali inawawekea vikwazo hata kuwalipa madeni yao,” amesema.
Akizungumzia mauzo ya hisa, Mtendaji Mkuu wa Zan Securities ambao ni washauri wa masuala ya hisa wa Maxcom, Raphael Masumbuko alisema kampuni hiyo inatarajia kuuza asilimia 25 ya hisa zake kwenye Soko la Hisa Dar es Salaam (DSE).
 Amesema kwa sasa thamani ya kampuni hiyo ni Sh68 bilioni, hivyo baada ya mauzo ya hisa thamani itafikia Sh90 bilioni.
Mkurugenzi wa kampuni hiyo ambayo ni ya kwanza kutoa huduma za ununuzi wa umeme wa Luku kwa njia ya mtandao, Jamson Kasati amesema kwa siku kampuni hiyo inapitisha miamala 600,000, huku uwezo wake kwa sasa ni kupitisha miamala milioni tano kwa siku.
Ahmed Lusasi ambaye ni ofisa mwandamizi wa Maxcom amesema kampuni hiyo inayotoa huduma pia Uganda, Msumbiji, Burundi, Rwanda na Zambia inatarajia kutoa huduma katika nchi 10 ifikapo mwaka 2020. Kodi inayolipa nchini ni Sh6.5 bilioni.

Mkuu wa mkoa kuwachukulia hatua wasioshiriki mazoezi ya viungo


Mkuu wa Mkoa wa Lindi kuwachukulia hatua watumishi wa umma ambao hawajajitokeza kufanya mazoezi ya viungo  kwa madai kwamba wamekiuka agizo la Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu la kuwataka kushiriki mazoezi kila Jumamosi ya pili ya mwezi.
Mkuu huyo wa mkoa huo  Godfrey Zambi amemwagiza Katibu tawala wa mkoa huo kuwachukulia hatua watumishi wote wa ofisi yake pamoja na watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi  ambao wamekiuka  agizo  la  Makamu  wa  Rais.
Ametoa agizo hilo jana  Jumamosi   baada    ya  watumishi   wa  ofisi  hizo  kutohudhuria   mazoezi  hayo ambayo  alikuwa anayasimamia yeye mwenyewe.
Zambi amesema kitendo cha watumishi hao kutohudhuria mazoezi ni kupuuza agizo la Makamu wa Rais  la kutaka kila Jumamosi ya pili ya mwezi watumishi pamoja na  wananchi wote kujumuika kwa pamoja na kufanya mazoezi ya  viungo.
Katika mazoezi hayo yaliyofanyika kwenye  fukwe za bahari ya Lindi mkoani hapo watumishi walioshiriki mazoezi hayo walikuwa 15.
Zambi pia amewapongeza wananchi wa Mkoa wa Lindi kwa kujitokeza kwa wingi katika mazoezi hayo pamoja na kumuunga mkono Makamu wa Rais.
Pia amewaasa wananchi hao kama walivyojitokeza katika mazoezi lakini pia wajitokeze  siku ya  usafi ambayo hufanyika  mwisho wa mwezi.

PITIA VICHWA VYA HABARI KATIKA MAGAZETI YA LEO NOVEMBA 12,2017