Friday, November 3

Waendesha mashtaka wataka Oscar Pistorius aongezewe kifungo

Oscar PistoriusHaki miliki ya pichaREUTERS
Waendeshaji mashtaka nchini Afrika Kusini wameiomba mahakama iongeze kifungo cha mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini Oscar Pistorius ambaye alifungwa kwa makosa ya kumuua mpenzi wake Reeva Steenkamp.
Wameambia Mahakama ya Juu ya Rufaa kwamba kifungo cha miaka sita ambacho alihukumiwa bingwa huyo wa Olimpiki ni "laini mno" na kwamba badala yake anafaa kufungwa miaka 15.
Mawakili wa mfungwa huyo wamesema kifungo hicho alichohukumiwa na mahakama ya chini kinamfaa.
Pistorius alidai kwamba alimpiga risasi Bi Steenkamp kimakosa akidhani alikuwa jambazi aliyekuwa ameingia nyumbani kwao Siku ya Wapendanao mwaka 2013.
Mahakama ya chini ilikosa kumhukumu kifungo cha miaka 15 kilichopendekezwa ikitaja baadhi ya mambo kwa mfano kumrekebisha na pia kwamba alionesha majuto. Mahakama ilisema hayo yalizidi lawama kutokana na hali kwamba hakufyatua risasi ya onyo.
Lakini mwendesha mashtaka Andrea Johnson amesema kifungo hicho hakijalingana na uzito wa kosa alilolitenda.
Pistorius, 30, hakuwa kortini Bloemfontein.
Reeva Steenkamp - 7 February 2013Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSteenkamp alikuwa mwanamitindo
Anaendelea kuzuiliwa katika gereza moja Pretoria.
Awali, alikuwa amefungwa miaka mitano kwa mauaji bila kusudia mwaka 2014 lakini akapatikana na makosa ya mauaji baada ya rufaa mwaka 2015.

Mwanamke ataka mahari kufutiliwa mbali akidai inawadhalilisha wanawake Zimbabwe

Mwanamke ataka mahari kufutiliwa mbali akidai inawadhalilisha wanawake ZimbabweHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUlipaji wa mahari ni jambo la kawaida katika tamaduni nyingi nchini Zimbabwe
Wakili mmoja wa kike nchini Zimbabwe ameanzisha kesi ya kufutilia mbali lobola au mahari akisema kuwa ni mila iliopitwa na wakati ambayo inawafanya wanawake kuonekana kama mali kulingana na gazeti la serikali la Herald.
Priccilar Vengesai anaamini kwamba iwapo utamaduni huo utaendelea ,familia zote za mume na mke zinafaa kulipa mahari kwa maslahi ya usawa wa kijinsia, gazeti hilo limeongezea.
Amewasilisha malalamishi yake katika mahakama juu, mahakama ya kikatiba akitaka kusikilizwa kwa kesi yake kwamba utamaduni huo unakiuka haki za raia.
Gazeti hilo limemnukuu bi vengesai akisema kwamba anataka kuolewa na hataki kupitia aliyopitia alipokuwa katika ndoa.
Sikushiriki katika kuuliza gharama ya mahari. Sikupewa fursa ya kuuliza kwa nini mharai ilitolewa.
Hali yote hiyo ilinifanya mimi kuonekana kama ''mali'' ambapo kiwango cha thamani yangu kilipendekezwa na wajomba zangu na mume wangu akalipa.
Hatua hii ilinivunja moyo na hali hiyo kuniweka chini ya udhibiti wa mume wangu kwa kuwa najihisi kwamba nilinunuliwa.
Mimi natoka katika kabila la Shona na ningependelea kuingia katika ndoa mara tu kesi hii itapokamilika na uamuzi kutolewa.
Chini ya utamaduni wa kabila la shona, Lobola ama mahari lazima alipiwe mwanamke kabla ya ndoa kukubalika katika familia na jamii.
Katika hali ambapo Lobola haijalipwa, wazazi na jamaa wa familia ya mwanamke hawataruhusu ndoa hiyo kuhalalishwa chini ya sheria ya ndoa.

Mwanamume ampata mamba mkubwa nje ya nyumba yake India

The 3m (12ft) long crocodileHaki miliki ya pichaKISHORE DASH
Image captionMwanamume ampata mamba mkubwa nje ya nyumba yake India
Mwanamume mmoja katika kijiji kilicho jimbo la mashariki mwa India la Orissa, alipigwa na mshangao baada ya kumpata mgeni ambaye hakumtarajia nje ya nyumba yake - mamba wa urefui wa mita 3
Dasharath Madkami alimpata mamba huyo baada ya kuamshwa na sauti zisizo za kawaida usiku.
Alipiga kamsa na wanavijiji wakafika ambao walimfunga mamba huyo kwa mti.
Mamlaka za wanyamapori kisha zikafika kumuokoa mnyama huyo.
CrocodileHaki miliki ya pichaKISHORE DASH
Image captionMwanamume ampata mamba mkubwa nje ya nyumba yake India
Hata hivyo kulikuwa na mzozo kuhusu ni wapi mambaohuyo angepelekwa.
Maafisa wa misitu walitaka kumuachilia myama huyo kwenda kwa bwagwa lililoku karibu ambapo alitoka, lakini wanavijiji wakakataa wakohofia kuwa angerudi tena.
Mamba huyo hata hivyo aliachiliwa kwenda mto Balimela ulio umbali wa kilomita 60.

Keisha atoa ushahidi wenye utata ndoa ya Dogo Janja, Uwoya


Dar es Salaam. Mwanamuziki Keisha amejichanganya kuhusu suala la ndoa kati ya Dogo Janja na mwigizaji, Irene Uwoya akitoa maelezo tofauti kuhusiana na ushiriki wake katika kufanikisha shughuli hiyo.
Awali Keisha akihojiwa mwanzoni mwa kipindi cha Leo Tena cha leo Ijumaa kinachorushwa na kituo cha Redio Clouds amesema alishiriki kumfuata bibi harusi nyumbani kwao baada ya watangazaji kutaka kufahamu kwa nini ndoa haikufungwa huko.
Keisha akimsaidia Dogo Janja kujibu swali hilo alisema: “Nilikuwa mmoja wa waliokwenda nyumbani kwa kina Irene kumfuata kisha tulimpeleka katika eneo la siri ilipofungwa ndoa, unajua mimi ni kama mama au dada mkubwa wa Abdul ( Dogo Janja) kwa sababu Madee ni kama baba yake asingweza kwenda peke yake.”
Lakini watangazaji walipoendelea na mahojiano Keisha alibadilisha kauli yake akisema hata yeye hakuwa akifahamu anayeolewa ni nani na pia hakuamini iwapo ni tukio la kweli mpaka aliposhuhudia tendo zima.
“Nilipofika nilimuuliza Johari (mwigizaji) ambaye alikuwa mmoja wa mashahidi iwapo ni ndoa kweli na siyo filamu. Johari alisema siwezi kukudanganya hii ndoa kweli. Mimi nimeolewa kwa hiyo niliposhuhudia tukio zima nikajiridhisha kuwa ile ndoa haswa,” amesema Keisha.

Serikali yakimbilia tena mahakama ya Rufaa


Moshi. Maagizo ya jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufaa ya kutaka kesi ya mauaji ya polisi PC Michael Milanzi inayowakabili raia wawili wa Kenya na Mtanzania, yanaonekana kuwatesa mawakili.
Baada ya Jaji John Mgeta aliyepangiwa kuisikiliza kesi hiyo upya kutoa uamuzi mdogo wa mabishano ya kisheria juu ya uamuzi huo wa majaji, bado upande wa Jamhuri umeamua kukata rufaa.
Raia wa Kenya, Samwel Saitoti na Peter Kimani wamehukumiwa kunyongwa wakati mshitakiwa Calist Kanje akihukumiwa kifungo cha miaka mitano kwa kuwasaidia wakenya hao wasikamatwe na polisi.
Mauaji hayo ya Julai 11, 2007 yaliambatana na uporaji wa Sh239 milioni mali ya benki ya NMB tawi la Mwanga na PC Milanzi alikuwa lindo siku hiyo ya uporaji na kupigwa risasi hadi kufa.
Hata hivyo, walikata rufaa kupinga hukumu hiyo ya mwaka 2014 lakini jopo la majaji watatu wa mahakama ya rufaa, Mbarouk Salum,Benard Luanda na Mussa Kipenga wakaamuru isikilizwe upya.
Majaji hao wamesema wamebaini katika mwenendo wa kesi hiyo iliyosikilizwa Moshi, wazee washauri wa mahakama hawakupewa nafasi inayostahili ili kuiwezesha mahakama kufikia maamuzi sahihi.
Wamesema katika shauri hilo, wamebaini makosa kadhaa ya kisheria na hivyo, wameagiza kufutwa mwenendo wote wa kesi na kesi hiyo kuanza upya kwa washitakiwa watatu waliokata rufaa.
Hata hivyo wakati kesi hiyo ikipangwa kuanza kusikilizwa upya jumanne iliyopita, kuiibuka hoja za kisheria kutoka kwa mawakili wa Serikali na wa utetezi na kuiomba mahakama kutoa mwongozo.
 Upande wa Jamhuri ulihoji juu ya utata wa maagizo hayo ya majaji wa mahakama ya Rufaa kwa vile hayaelezi kama iwasilishwe hati mpya ya mashitaka au ibaki ile ya zamani yenye washitakiwa 12.
 Pia akasema majaji walifuta mwenendo wa kesi tu lakini kutiwa kwao hatiani na adhabu waliyopewa hivyo hukumu ya awali bado inasimama na hivyo mahakama kuu haina tena mamlaka ya kuisikiliza.
 Wakili wa Serikali mwandamizi Ladslaus Komanya, akasema kutokana na utata huo, haieleweke kesi hiyo ianze katika hatua ipi na kwa kutumia hati ipi wakati hukumu ya awali haikubatilishwa.
 Wakili Majura Magafu anayemtetea Kanje kwa kusaidiana na wakili Erasto Kamani, alisema mteja wao alishamaliza kifungo chake Desemba 2016 na hakuna hati mpya ya mashitaka iliyowasilishwa kortini.
Kwa mujibu wa wakili Magafu, njia pekee ya kutatua mkwamo huo wa kisheria ni kwa Jaji Mgeta kuirudisha kesi hiyo kwa majaji watatu waliotoa maagizo hayo ili waipitie upya hukumu yao.
 Hata hivyo wakili  Allen Godian anayesaidiana na wakili Faustine Materu wanaowatetea raia hao wa Kenya, alikubaliana na amri ya majaji wa mahakama ya rufaa kuwa kesi hiyo ianze upya.
Katika hoja yake, wakili Godian alisema hukumu ya wateja wake ilitokana mwenendo wa kesi ambao umefutwa na mahakama ya rufani hivyo moja kwa moja hukumu nayo inakuwa imeondoka.

Akitoa uamuzi wake jana kuhusiana na mabishano hayo ya kisheria, Jaji Mgeta alikubaliana na hoja za wakili Godian akisema hakuna hukumu iliyosimama baada ya mwenendo wa kesi kufutwa.
 Jaji Mgeta ametolea mfano wa nyumba akisema huwezi kuondoa msingi na paa likabaki hivyo akaagiza kesi hiyo ianze kusikilizwa upya kwa hati ya mashitaka ambayo tayari washitakiwa wanaijua.
 “Nakataa pia wazo la mawakili la kupeleka kesi hii kwa majaji wa mahakama ya rufaa ili waipitie. Naagiza usikilizwaji upya uanze kwa kuanza kuchukua ushahidi wa mashahidi wa Jamhuri,”amesema.
Mara baada ya Jaji kutoa uamuzi huo, wakili Komanya alisimama na kumueleza Jaji kuwa hawajaridhishwa na maamuzi hayo hivyo wameamua kuyakatia rufaa maamuzi yake madogo.
Wakili Magafu naye amesema nao walikuwa na nia ya kukata rufaa kuhusu kama mahakama ina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, lakini watatoa hoja zao kupitia rufaa itakayokatwa na Jamhuri.
 Jaji Mgeta amesema kukata rufaa ni haki ya kisheria hivyo nakala ya mwenendo wa shauri hilo na uamuzi wake mdogo zitakuwa tayari hiyo leo saa 9:00 jioni na kesi itatajwa Jumatatu.

Mwongozo mpya wa matumizi ya dawa mbioni kutolelewa



Naibu Waziri wa Afya Dk Faustine Ndugulile
Naibu Waziri wa Afya Dk Faustine Ndugulile 
Serikali kupitia Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto inatarajia kutoa mwongozo mpya wa matumizi ya dawa kabla ya mwaka huu kumalizika.
Naibu Waziri wa Afya Dk Faustine Ndugulile ameyasema hayo leo Novemba 3 wakati wa uzinduzi wa  cheti cha mfumo wa uhakiki ubora wa huduma katika kiwango cha kimataifa cha ISO 9001:2015 kilichotolewa kwa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA).
Amesema mwongozo huo utasaidia kupunguza matumizi holela ya dawa ambayo mara nyingi huchangiwa na kampuni zinazozalisha dawa.
Amesema Serikali imeshaorodhesha jumla ya dawa muhimu 135 na inahakikisha dawa hizo zinapatikana kwa asilimia 80.
Dk Ndugulile  amesema serikali imeongeza bajeti ya fedha katika sekta ya afya kutoka Sh40 bilioni hadi Sh290 bilioni kuhakikisha zinakuwepo dawa za kutosha.
"Wafanyabiashara hasa wenye kampuni wamekua wakipita kwenye mahospitali kuhamasisha dawa ipi itumike, wao lengo lao ni kufanya biashara matokeo yake linakuja tatizo la usugu wa dawa,”
Amesema serikali itaendelea kusimamia kuhakikisha upatikanaji wa dawa haupungui.
Aidha Dk  Ndugulile ameitaka TFDA kuendelea kusimamia kwa ukamilifu uingizwaji wa dawa na vipodozi nchini.
"Hakuna asiyejua kuwa wote tunaguswa na kazi zinazofanywa na TFDA katika maisha ya kila siku. Hivyo kufanya vizuri kwa taasisi hii ni kuhakikishia umma kuwa afya zetu zinalindwa,"
"Niwasisitize msiridhike na mafanikio mliyoyapata mpaka sasa mnapaswa kukumbuka kuwa afya za watanzania zipo mikononi mwema, endeleeni kuboresha mifumo ya utendaji kazi,"
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TFDA, Hiiti Sillo amesema mamlaka hiyo imekuwa ya kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki na ya pili Kusini mwa jangwa la sahara kupata cheti hicho.
Amesema cheti hicho imekipata baada ya kukidhi kiwango  kufuatia kufanyiwa ukaguzi na kampuni ya ACM Limited ya Uingereza.
Amesema mfumo wa uhakiki wa ubora wa huduma umesaidia kutengeneza, kufanya marejeo na kusimamia matumizi ya nyaraka, kufanya ukaguzi za ndani na kuratibu marejeo ya mfumo.

Papa ataka kubadili mfumo ili mapadri waoe


Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis amependekeza kubadili mfumo wa utumishi wa mapadre akisema itakuwa vyema iwapo makasisi hao wakaruhusiwa kuanza kuoa.
Hata hivyo, imefahamika kuwa pengine pendekezo hilo likawaruhusu mapadre wa Brazil pekee kutokana na mjadala unaoendelea nchini humo. Hivi karibuni Askofu wa Brazil, Kadinali Claudio Hummes alimwomba Papa Francis kufikiria kuondoa sheria inayowakataza makasisi kufunga ndoa.
Ingawa pendekezo hilo la Papa Francis huenda likapunguza tatizo la uhaba wa wanaume wanaojiunga kwenye utumishi huo, lakini linatarajiwa kukabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa waumini wenye msimamo mkali na hata pia kusababisha mgawanyiko ndani ya kanisa.
Ombi hilo linatarajiwa kujadiliwa katika kikao cha baraza la kanisa kinachotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu nchini Brazil.
Kanisa Katoliki linahubiri mafundisho ambayo yanapiga marufuku makasisi wake kufunga ndoa ingawa kumekuwa na baadhi wanaovunja mwiko huo na kuisha maisha ya ndoa. Hata hivyo, wale wanaochukua uamuzi huo hujitenga na kanisa.
Kasisi moja aliyetambulika kwa jina la Paddy O’Kane amenukuliwa na baadhi ya magazeti akielezea uwezekano wa Papa Francis kuchukua uamuzi wa kuwafungulia mapadre kifungo cha kutokua wakati wowote mwezi huu.
“Hivi karibuni nilimsikia Papa anataka kutekeleza ombi alilolipata toka Brazil kama jaribio lake la kwanza,” alisema.
Papa Francis na mtangulizi wake, Benedict XVI wamekuwa wakieleza kuwa suala la makasisi kutoruhusiwa kuoa siyo jambo lisiloweza kubadilika na kwamba jambo hilo linajadilika.

Spika Ndugai ameiandikia NEC kuwa jimbo la Singida Kaskazini liko wazi


Dar es Salaam. Spika wa Bunge, Job Ndugai ametangaza kuwa jimbo la Singida Kaskazini lililokuwa likishilikiwa na Lazaro Nyalandu liko wazi baada ya mbunge huyo kufutwa uanachama na CCM.
Taarifa iliyotolewa leo Ijumaa na Ofisi ya Bunge imeeleza kuwa Spika Ndugai amemuandikia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi(NEC), Jaji Semistocles Kaijage kumfahamisha kuwa jimbo hilo liko wazi.
Barua hiyo imeandikwa na Spika kwa mujibu wa kifungu 37(3) cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi 2015 kinachoeleza kwamba, pale ambapo mbunge atajiuzulu, atakufa au sababu nyingine yeyote tofauti na zilizoainishwa katika kifungu cha 113, Spika atamjulisha Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi na kutangaza kwenye Gazeti la Serikali kwamba kiti hicho cha ubunge kiko wazi.
“Kufuatia barua hiyo Tume ya Taifa ya Uchaguzi inaweza kuendelea na mchakato wa kumpata mbunge wa kujaza nafasi hiyo iliyo wazi,” imeeleza taarifa hiyo

Mitandao yajitetea haikutumika vibaya

MarekaniHaki miliki ya pichaEPA
Image captionkutoka kushoto muwakilishi wa Facebook Colin Stretch , Sean Edgett kutoka Twitter, na muwakilishi wa kampuni ya Google Richard Salgado wakitoa ushahidi wao mbele ya kamati ya bunge la seneti nchini Marekani
Wawakilishi wa mitandao mikubwa duniani ya Google, Facebook na Twitter wanatoa ushahidi mbele ya bunge la Seneta wa Marekani ili kuthibitisha kama Urusi ilitumia huduma zao kujaribu kujaribu kuingilia uchaguzi wa rais wa Marekani mwaka 2016.
Makamu mwenyekiti wa Kamati ya Ushauri wa Seneti, Mark Warner, aliwaambia waandishi habari alitarajia makampuni hayo kujieleza endapo huduma zao zilitumika vibaya.
Kampuni ya Facebook imeeleza mapema wiki hii kuwa Wamarekani milioni moja na ishirini na sita milioni wamegawanyika kufuatia maoni waliyotoa kuwa urusi inahusika .
Serikali ya Urusi imekanusha madai ya kujaribu kuingilia kati uchaguzi wa Marekani.

Rapa aonyesha sehemu nyeti 'kimakosa' katika Instagram Live

Rapa wa Afrika Kusini Emtee alikuwa akizungumza na mashabiki wake akiwa katika haja ndogoHaki miliki ya pichaINSTAGRAM
Image captionRapa wa Afrika Kusini Emtee alikuwa akizungumza na mashabiki wake akiwa katika haja ndogo
Kumekuwa na hisia katika vyombo vya habari vya Afrika Kusini baada ya mwanamuziki mmoja wa taifa hilo Emtee kwa bahati mbaya kuonyesha uume wake katika mtandao wa Instagram Live.
Chombo cha habari cha Times Lives kinasema kuwa rapa huyo ambaye jina lake kamili ni Mthembeni Ndevu hakukubali kudhalilika na kitendo hicho baada ya picha hizo zilizoonyesha sehemu yake nyeti kusambazwa.
Huku mtandao wa burudani wa Zalebs ukisema kuwa watu wamekuwa wakichochea hali hiyo kwa kutumia alama ya reli #emteechallenge.
Mtandao huo unasema kuwa hatua hiyo ni nzuri kwa msani huyo.
''Unajua kwamba umefanya makosa na kupewa changomoto'', unaelezea.
Emtee aliambia Times Lives:Nilikuwa chooni nikijibu maswali ya mashabiki moja kwa moja.Nilitaka kujisaidia haja ndogo lakini bila kufikiria nikatumia mkono huohuo niliokuwa nikishikilia simu yangu wakati nilipokuwa nikiendelea na haja ndogo na kutumia mkono huohuo kupiga picha.Sikufikiria kuhusu kilichofanyika hadi nilipogundua kwamba kile nilichofanya na nikaomba msamaha.

Mourinho afika mahakamani kujibu madai ya kukwepa kulipa kodi Uhispania

Mkufunzi wa Chelsea Jose MourinhoHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho
Mkufunzi wa Man United Jose Mourinho amewasili katika mahakama ya Uhispania kujibu madai ya kukwepa kulipa kodi wakati alipokuwa mkufunzi wa klabu ya Real Madrid.
Wawakilishi wake wamekana kuwa anadaiwa Yuro milioni 3.3 kupitia haki za matangazo ambazo hakuzitangaza.
Bwana Mourinho alionekana akiingia mahakamani katika makaazi ya mjini Madrid Pozuelo de Alarcon.
Kusikizwa kwa kesi hiyo kunajiri siku mbili kabla ya Manchester United kucheza dhidi dhidi ya Chelsea katika ligi ya Uingereza.
Mkufunzi huyo alizungumza na vyombo vya habari siku ya Alhamisi kama ilivyo ada.
Utawala wa Uhispania ulianzisha kesi dhidi ya Mourinho mnamo mwezi Juni.

Hoteli yakalia kuti kavu Kahama


Kahama. Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Fadhil Nkurlu ametishia kuifunga Hoteli ya Kahama Gold ya mjini Kahama iwapo mmiliki wake hatalipa kodi ya mauzo ya Sh30 milioni ifikapo Novemba 9.
Uongozi wa hoteli hiyo pia umuagizwa kuwalipa fidia wateja, akiwemo Mwandishi wa habari wa Kituo cha Luninga cha ITV Mkoa wa Shinyanga, Frank Mshana aliyeibiwa kamera na kompyuta mpakato wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Elias Kwandikwa.
Nkurlu ametoa maagizo hayo leo Ijumaa baada ya kutembelea hoteli hiyo kutokana na uongozi kukaidi agizo la Mamlaka ya Mapato(TRA) la kulipa kiasi hicho kabla au ifikapo Julai 5.
“TRA walitoa siku 90 zilizomalizika Julai 5 kodi hii iwe imelipwa. Naona mlipuuza; sasa nawapa siku saba kuanzia leo mlipe, la sivyo nitaifunga huku hatua zingine za kisheria ikiwemo kuipiga mnada zikifuata,” ameagiza Nkurlu
Kabla ya kuuzwa na kubadilishwa jina kuwa Kahama Gold, hoteli hiyo ilikuwa ikiitwa Mongo Hotel.
Meneja wa TRA Mkoa wa Kodi wa Kahama, Jacob Mtemang’ombe amethibitisha hoteli hiyo kudaiwa Sh30 milioni inayotokana na kodi ya asilimia 10 ya mauzo yaliyofanyika zaidi ya mwaka mmoja uliopita.
“Tayari tumekamilisha taratibu kadhaa za kiofisi ikiwemo kuwaandikia wahusika kuwakumbusha kulipa deni hilo; hatua zingine zitafuata kwa mujibu wa sheria,” amesema Mtemang’ombe
Akizungumzia suala hilo, meneja wa hoteli hiyo, Obedi Hussein amesema wanapitia nyaraka, kumbukumbu na sheria kubaini iwapo mmiliki mpya au wa zamani ndiye anastahili kulipa kodi ya mauzo.
“Ikibainika sisi wamiliki wapya ndiyo tunapaswa kulipa kodi hiyo, tutalipa mara moja,” ameahidi Hussein
Kuhusu wizi wa mali za wateja, meneja huyo amesema tayari uongozi umechukua hatua kadhaa kudhibiti hali hiyo anayodaiwa waliikuta waliponunua hoteli hiyo.

JAFO: Wafanyakazi Mzigo Hawahitajiki

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo akiongea kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali za mitaa na kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini Mhandisi Victor Seif akieleza majukumu ya TARURA kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali za mitaa na kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini Bw.Abdul Digaga akiongea kwenye kikao cha kamati ya kudumu ya bunge ya utawala na Serikali za mitaa na kamati ya kudumu ya bunge ya hesabu za Serikali za Mitaa kilichofanyika katika ukumbi wa Hazina mjini Dodoma.

……………

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Seleman Jafo amesema hatavumulia kuwa na watumishi mizigo ambao hawatimizi majukumu yao kikamilifu na kuleta mabadiliko katika sekta ya barabara ambayo ni nguzo ya uchumi nchini.

Waziri Jaffo ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wabunge wa Kamati ya kudumu Serikali za mitaa(TAMISEMI) sambamba na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) kuhusu majukumu ya Wakala wa barabaraza vijijini na mijini(TARURA) iliyofanyika katika ukumbi wa Hazina Mjini Dodoma

Mhe. Jaffo amesema Serikali ilishatoa muongozo wa malengo ya utendaji kazi katika utumishi wa umma na kuwapima kulingana na malengo yao hivyo watumishi ambao watashindwa kutekeleza na kufikia malengo waliyopangiwa Serikali haitasita kuwachukulia hatua za kiutumishi.

Amesema kuwa Serikali haitavumilia suala zima la ubadhilifu kwa watumishi wa umma, kwa kuwa Serikali haiwezi kumbeba mtu ambaye ni mbadhilifu kwa kuwa Serikali inahitaji kuleta mabadiliko katika utendaji kazi na kuleta maendeleo kwa jamii.

Amesema kuwa Taruara ni chombo kipya hivyo haitaji kuajiri watumishi ambao ni mzigo ambao waleta sura mbaya kwa jamii kabla chombo hiki hakijafanya kazi ya kuwahudumia wananchi katika kutatua kero ya miundombinu ya barabara vijijini na mijini.

Amewataka Wabunge wa kamati zote mbili (LAAC&TAMISEMI) kusimamia utekelezaji wa miradi iliyoko chini ya TARURA na kuhakiki ubora wa miradi hiyo na kukosoa pale wanapoona miradi haitekelezwi kwa viwango vinavyotakiwa ili wahusika waweze kurekebisha makosa kabla ya kukabidhi miradi hiyo kwa wahusika.

Aidha aliwahisi Wabunge kuendelea kuishauri TARURA kwa kuwa chombo hiki kimeundwa kwa ajili ya kutoa majibu ya changamoto za Wananchi hivyo ni wajibu wetu kuwasilisha yale yote ambayo tunaona yanawakwaza wananchi katika majimbo yetu.

Mhe Jafo amemuuagiza Mkurugenzi wa TARURA Mhandishi Victor Seif kuhakikisha Mameneja katika ngazi ya Wilaya wanasaini Mkataba wa Makubaliano ya kazi “Performance contract”na kuwafuatilia utendaji wao kwa mujibu wa Mkataba na atakeyeshindwa kufikia malengo yaliyowekwa atolewe bila kigugumizi ili kupisha watendaji wengine watakaofanya kazi kulingana na matakwa ya Serikali.

Wakati huohuo Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seif amesema kulingana na muundo na majukumu ya Wakala wa Barabara mahitaji halisi ya watumishi ni 3,222 lakani mpaka sasa ni watumishi 1,147 wameshapatikana ambapo 47 wako Makao Makuu, 103 Mikoa na 997 katika halmashauri, na pia kuna upungufu wa watumishi 2,075 katika kada mbalimbali.

TARURA ina majukumu ya Msingi ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya mtandao wa barabara zenye urefu wa Km 108,946.2 za vijini, mijini pamoja na madaraja, na kati ya hizo barabara 56,000 zinafanyiwa uhakiki ili ziweze kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali ili zitambulike kisheria na Km 52,946.2 tayari zimeshatambulika na kutangazwa kwenye Gazeti la Serikali.

CECAFA SASA YARUDISHA MICHUANO YA CHALENJI, KUANZA NOVEMBA 25-9DEC


Baada ya kupita miaka miwili bila kuchezwa kwa mashindano ya kuwania Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki, michuano hiyo imerejea tena msimu huu na Tanzania imethibitisha kushiriki.


Nchi wanachama Tanzania Bara, Zanzibar, Uganda, Kenya, Burundi, Rwanda, Somalia, Sudan, Sudan Kusini, Eritrea na Ethiopia.

Kaimu Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Kidao Wilfred amethibitisha kikosi cha kwanza cha ‘Taifa Stars’ kushiriki na matarajio ya kufanya vema michuano hiyo itakayofanyika kuanzia Novemba 25, 2017 hadi Desemba 9, mwaka huu.

Kidao amesema kwamba uteuzi wa timu za kwanza kwa kila nchi mwanachama wa Baraza la Mpira wa Miguu la Afrika Mashariki ni makubaliano ya viongozi wa CECAFA waliokutana kwa pamoja huko Sudan, Septemba, mwaka huu.

Kutokana na makubaliano hayo ya kuita timu za kwanza, michuano hiyo itaathiri kidogot ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) kwa kuwa wachezaji wengi wanaounda kikosi hicho, wanatoka timu za VPL.

Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi (TPLB), Boniface Wambura amesema: “Tutakaa kama kamati na kuangalia siku ya Jumatano na Alhamisi baada ya michuano hiyo na kupanga ratiba ya mechi ambazo zitapanguliwa wakati wa michuano ya Chalenji.”

Mbali ya michuano hiyo, Tanzania imethibitisha kushiriki michuano ya Chalenji ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 itakayofanyika Bujumbura nchini Burundi kuanzia Desemba 12, 2017 hadi Desemba 22, mwaka huu.

Kadhalika, Tanzania imethibitisha kushiriki michuano ya Chalenji kwa wanawake ikienda kutetea taji katika michuano itakayofanyika Rwanda mwezi Desemba, mwaka huu. Tarehe rasmi itatajwa baadaye.

CECAFA imeamua kurejesha hadhi yake kwani mara baada ya michuano ya Chalenji ya vijana huko Burundi, mwakani itakuwa ni zamu ya Tanzania ambako michuano hiyo inatarajiwa kuanza Agosti 11, 2018 hadi Agosti 25, mwakani.

Wakati huo huo Kidao amethibitisha Tanzania kuwa wenyeji wa mashindano ya Vijana ya Chalenji ya CECAFA/CAF kwa vijana chini ya miaka 17 mwakani na mashindano hayo yatatumika kama sehemu ya kufanya maandalizi Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 (AFCON – U17).

Michuano ya mwakani ina baraka za Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kwa sababu shirikisho hilo linataka kutumia michuano hiyo ya vijana ya Kanda mbalimbali za Afrika kupata timu saba katika michuano AFCON – U17 ya mwaka 2019.


Kanda hizo ni CECAFA (Afrika Mashariki), COSAFA (Nchi za Kusini mwa Afrika), WAFU – UFOA (Afrika Magharibi); UNAF (Afrika Kaskazini) na UNIFFAC (Afrika ya Kati).

MAVUNDE AWACHARUKIA WAAJIRI MKOANI KILIMANJARO JUU YA MIKATABA NA VIBALI VYA WAGENI KUFANYA KAZI NCHINI

 Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akikagua nyaraka mbalimbali alipotembelea Kiwanda cha China Paper Corporation.
  Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akikagua kiwanda cha China Paper Corporation.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde akizungumza katika kiwanda cha China Paper Corporation..


Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu(Kazi,Vijana na Ajira) Mh Anthony Mavunde leo amefanya ziara ya ukaguzi wa masuala ya kazi na kusikiliza kero na changamoto mbalimbali zinazowakabili wafanyakazi mkoani Kilimanjaro.

Mavunde alianza ziara hiyo katika shule ya Kimataifa ya Moshi (ISM) ambapo alisikiliza kero za wafanyakazi na kutoa maagizo kwa Menejimenti ya Uongozi wa Shule hiyo kutoa mikataba kwa wafanyakazi kwa mujibu wa kifungu cha 14 cha Sheria ya Ajira na Mahusiano kazini kinavyoelekeza ikiwa ni pamoja na kuagiza Taasisi za Serikali kuchunguza malalamiko juu ya unyanyasaji kwa wafanyakazi unaodaiwa kufanywa na baadhi ya viongozi wa menejimenti.

Mavunde pia alitembelea Kiwanda cha China Paper Corporation ambapo alisikiliza kero za wafanyakazi na kuiagiza Menejimenti ya Kiwanda hicho kuhakikisha sheria za Kazi zinafuatwa kwa kutoa Mikataba kwa wafanyakazi wote na kuhakikisha haki za wafanyakazi zinalindwa ikiwemo usalama wa mazingira ya kufanyia kazi.Pamoja na maagizo hayo kwa kiwanda,Naibu Waziri Mavunde aliwataka wafanyakazi nao kutimiza wajibu wao na kutumia njia sahihi za malalamiko yao bila kuvunja sheria za nchi.

Wakati huo huo,Naibu Waziri Mavunde amewaaguza Afisa Kazi Mfawidhi na Afisa wa Uhamiaji wa mkoa wa Kilimanjaro kuzishikilia hati za kusafiria za raia wa kichina 9 mpaka watakapowasilisha Vibali vya kufanya kazi nchini na Vibali vya makazi.