Monday, October 30

Raila: Uhuru hakubaliki, anatawala kwa mabavu


 Wakati wanafunzi wa darasa la nane wakitarajia kuanza mitihani ya kuhitimu kuanzia kesho, kiongozi wa muungano wa upinzani wa Nasa, Raila Odinga ameendelea kumshambulia Rais Uhuru Kenyatta akimtaka kuachia madaraka.
Wanafunzi nchini humu wanatarajia kuanza mitihani hiyo huku hali ya usalama ikiwa bado tete kufuatia uchaguzi wa urais wa marudio uliofanyika wiki iliyopita.
Akizungumza kwenye ibada ya Jumapili iliyofanyika katika kanisa la Gatina PAG, Odinga alisema mauaji ya watu watatu juzi katika eneo la Kawangware mjini Nairobi hayakubaliki. Watu watatu waliuawa na wanaodaiwa kuwa ni polisi baada ya kutokea sintofahamu kati ya polisi na waandamanaji.
Mwanasiasa huyo aliyesusia uchaguzi wa marudio alisema kwamba siasa za Kenya zimehamia katika uhasama wa kushambuliana baina ya raia na vyombo vya usalama.
Siku ya Ijumaa, watu watatu waliuawa na wengine kujeruhiwa baada ya makundi mawili pinzani kupigana mgogoro unaohusishwa na kuibuka kwa kundi la Mungiki.
Hata hivyo, Odinga alisema katika hotuba yake kanisani jana kuwa, umaarufu wake ni wa nchi nzima na kwamba Rais Kenyatta anatumia ‘nguvu ya kutawala’.
“Wakenya wanataka haki si utawala wa nguvu. Tuko katika barabara ya Kanaani na safari bado inaendelea. Kenya inahitaji kiongozi asiye na ubinafsi ili kukabiliana na ubaguzi ambao Jubilee haiwezi kuutatua,” alisema,
Watu 49 wanadaiwa kuuawa na vyombo vya dola nchini humo vifo vinavyohusishwa na uchaguzi huo ambapo vimetokea kati ya Agosti 8 na juzi wengi wakiuawa katika maeneo ya Kawangware, Kibera, Mathare na Kisumu.
Vifo vilivyotokea Kawangware juzi vimeelezwa kutokea kutokana na ‘vita’ ya kawaida kati ya polisi na waandamanaji vilivyosababisha kuibuka kwa makundi mawili yenye mrengo wa kikabila.
Pande zote zilikuwa na silaha kama mapanga, visu, marungu na mawe, ambapo polisi walisema walimuua mtu mmoja, lakini wananchi wanadai watu wengi walikufa au kupotea kutokana na mapigano.
Nini kilichosababisha?
Kila upande unaulaumu mwingine, lakini ukabila ndio unaoelezwa kusababisha mapigano hayo ikielezwa kwamba yaliongozwa na ufuasi wa kisiasa ulioegemea katika mrengo huo.
“Tulidhamiriwa kwa sababu hili ni eneo la Wakikuyu,” anasema Geoffrey Mbithi (42) anayejishughulisha na shughuli za hoteli ambaye nyumba yake ya wageni iliharibiwa.
Machafuko hayo ingawa yalikuwa ya kipekee na yaliyodumu kwa saa chache yalikumbushia ukatili wa kikabila uliosababishwa na siasa ambao huchochea vurugu zilizosababisha vifo vya watu zaidi ya 1,100 miaka 10 iliyopita.
“Mimi nilikuwa ndani ya nyumba nikasikia watu wakisema, ‘moto, moto, moto,” alisema Rose Kiema mwenye umri wa miaka 50 ambaye ameishi na kufanya kazi katika eneo la Congo Junction tangu miaka ya 1980.
Mama huyo alikimbia na kurejea kesho yake asubuhi na kukuta moshi ukiendelea kufuka katika makazi yake.
Karibu na sehemu hiyo kuku watatu na mbuzi walichomwa moto wakiwa hai.
Kiema na wenzake wanasema vijana ambao ni wafuasi wa Nasa walichoma moto huo wakichagiza lengo la viongozi wao la kutoshiriki uchaguzi.
“Tulifanyiwa unyama huu kwa sababu hatuiunga mkono Nasa. Tulipiga kura, ndiyo sababu pekee tunayopata tabu,” anasema Josphat Gatimu (62).
Hakukuwa na huruma kwa wachuuzi wa bidhaa mbalimbali raia kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambao walishuhudia bidhaa zao zikichomwa moto.
“Mahali hapa ni ngome ya Nasa,’’ alisema mtu mmoja mwenye umri wa miaka 20 ambaye hakutaka kutaja jina lake.
“Ni nini kinachoendelea hapa? Ni Serikali inajaribu kulazimisha vikundi vingine vibaya kutoka katika jumuiya zingine kuja na kutishia usalama wetu,” alisema akimaanisha ‘Mungiki’, kikundi kinachohusishwa na Wakikuyu kinachojulikana kwa harakati za kikabila.
Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2007, Rais Kenyatta alishutumiwa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kuchochea vurugu za kisiasa jambo ambalo alitumia muda mwingi kulikanu

Kaanzia Azam FC Academy, sasa anakipiga Marekani


Siri ambayo Neymar wa Brazil aliisema kwa vijana wanaochipukia kwenye soka ni kuamini kupitia ndoto zao; kuna uwezekano wa kuwa kama nyota wanaowahusudu, kikubwa ni kujituma kwa kutafuta mafanikio, inawezekana bila kukata tama.
Adolf Bitegeko ni Kinda la Kitanzania ambalo leo tunalo kwenye rada zetu za Spoti Mikiki ambazo huwa zinawanasa wachezaji wa Kitanzania wanaotafuta maisha ya soka nje ya nchi, nyota huyo anamhusudu sana Paul Pogba wa Manchester United akisema anaweka bidii na anaamini siku moja atafikia kiwango chake.
Tukurejeshe nyuma kabla ya kuendelea mbele na Bitegeko, wiki iliyopita tulikuwa na Aman Kyata ambaye ni Mtanzania wa tatu kuwa naye kati ya wengi wanaocheza Ligi Kuu Kenya. Kyata anaichezea Chemelil Sugar F.C alielezea anavyotamani kuichezea timu ya Taifa Stars.
Leo tunaye Bitegeko ambaye yupo nchini Marekani kwenye Kituo cha Lassen Soccer ambako pia yupo Aboud Doud ambaye tuliwahi kuwa naye miezi kadhaa iliyopita katika ukurasa huu wa wachezaji wa Tanzania wanaokipiga nje ya nchi.
Bitegeko anaamini kupitia siri ambayo amewahi kuisema nyota wa PSG ya Ufaransa, Neymar na ndiyo maana kila siku amekuwa akipambana kuhakikisha anayafikia malengo yake.
Kabla ya kuzungumzia alivyopata nafasi ya kujiunga na kituo cha Lassen Soccer ambacho pia huwajenga wachezaji kwa kuwapatia elimu ya darasani kama kipaumbele cha kwanza alianza kwa kusema ataona fahari siku moja kama akipata nafasi ya kuichezea timu ya Taifa.
“Kuichezea timu ya Taifa ni lengo langu la pili, kwanza kufanikiwa kucheza mpira wa kulipwa, siwezi kuwa mchezaji wa Taifa Stars kama sitokuwa nacheza mpira kwenye ngazi ya ushindani.
“Najua kuwa haitoshindikana kwa sababu ninamwamini sana Mungu, kupitia yeye hakuna jambo ambalo linaweza kumshinda, wote ambao walikuwa na dhamira ya kweli Mungu naye amewasaidia.
“Tanzania sio nchi kubwa kwenye soka hivyo hakuna idadi kubwa sana ya wachezaji wa Kitanzania wanaocheza nje hivyo hata kwenye ufuatiliaji haitokuwa mgumu sana,” alisema mchezaji huyo ambaye anacheza nafasi ya kiungo mkabaji.
Kupata nafasi kwa Bitegeko ya kujiunga na Lassen Soccer haikuwa kwa ujanja na uwezo wake binafsi wa kucheza soka kwa sababu kama uwezo kuna kundi kubwa la wachezaji wa Kitanzania wenye uwezo zaidi yake.
“Nina bahati niseme hivyo kwa kifupi, Mungu amekuwa akinisimamia kuanzia hatua yangu ya kwanza mpaka hapa nilipofika, nimezaliwa 26 Februari 1999 na kukua kisoka nikiwa Karume jijini Dar es Salaam tangu nikiwa darasa la tatu.
“Waliokuwa wakinisimamia ni Eugene Mwasakami, Rogasian Kaijage pamoja na Maalim Salehe. Nimekulia pale mpaka nilipofikakidato cha nne, lakini nilipata nafasi kuchezea timu ya ligi daraja la kwanza ya Ashanti united ila kutokana na shule sikuwa na muda wa kutosha kuwa pamoja na timu.
“Baada ya kumaliza kidato cha sita nikapata nafasi kule Azam FC na nilijiunga na kituo chao na nilikaa kwa takriban mwaka mzima. ni sehemu bora zaidi Tanzania kwa kijana kukaa na kujifunzia soka kutokana na mazingira.
Alijifunza mengi akiwa na Azam na kilichompa nguvu zaidi ya kujengeka, Bitegeko amesema ni ushindani uliokuwepo baina ya wachezaji kwa wachezaji kwa kuwa kila mtu alikuwa anataka kuonyesha uwezo zaidi na kumshawishi kocha wa vijana.
“Ni kwa neema tu ya Mungu nilipata nafasi ya kuchaguliwa kuja kujiunga na hiki chuo ambacho kwa sasa hivi kimetufanya kuwa bize sana na masomo,kila mtu anasomea anachopenda kisha na kucheza mpira.
“Wamerekani hawapendi ujinga kama unakipaji alafu huna elimu ni sawa na bure kama unapenda kucheza mpira basi lazima usome ili maisha ya mpira yakimalizika uweze kumudu kuendesha maisha binafsi nje ya soka.
“Nina miezi minne sasa tangu nijiunge nao, haikuchukua muda kwangu kuendana na mazingira yao japo ni tofauti sana na mazingira ambayo nilikuwa nimezoea kuishi nikiwa Tanzania, kuanzia mwakani nitakuwa kwenye hatua nyingine,” anasema Bitegeko.
Marekani wamelijenga soka lao la chini kwenye mfumo wa vyuo ambao umekuwa ukitambulika sio soka pekee bali hata kwenye upande wa mpira wa kikapu na kwenyewe wanatambua uwepo wa vyuo.
Kuna ngazi tofauti ambazo zimekuwa zikitumika kabla ya mchezaji kuhitimu na kupata timu ya kuichezea ligi (MLS), Ronald Mkaramba naye yupo kwenye mpangilio huo lakini yeye kidogo ni tofauti na wakina Daud na Bitegeko ambao wapo chini yake.
. “Kucheza soka Marekani kunauhitaji wa mambo manne ambayo nimeyaona kupitia vyuoni, usajiliwe kama mchezaji wa kulipwa na timu husika, uanzie kwenye kituo husika cha timu au upitie vituo vichache vilivyopo ambavyo hutoa elimu ya soka tu. “Ubaya wa vile vinavyotoa elimu ya soka pekee sio rahisi mtu kupata timu za MLS pekee.

Wekundu wa Msimbazi ‘Lunyasi’ kama Yanga tu


Juzi tulishuhudia mtanange wa kufa mtu wa Simba na Yanga. Sitaki kurudia kilichotokea ninaamini kila mmoja amekiona na wengine wamekisikia.
Leo nitazisema hizi timu kwa kuwa ni siku zao na majina yao hayajayeyuka midomoni mwa mashabiki,
Niliwahi kuyasema haya lakini leo ninarudia kwa ili yawaingie. Unaweza kusema, Simba ni klabu kongwe na kubwa isiyo na maendeleo kama klabu ya Yanga!.
Ndiyo, Simba au Wekundu wa Msimbazi, ukipenda waite Lunyasi au Taifa Kubwa ni miongoni mwa timu mbili zenye mashabiki wengi zaidi siyo tu hapa nchini, lakini katika ukanda mzima wa Afrika Mashariki. Timu nyingine yenye mashabiki wengi ni Yanga, lakini Simba na Yanga hazina maendeleo.
Ukongwe wa klabu hizi mbili na hadhi zao haziendani kabisa na maendeleo yao. Ninasema klabu hizi hazina maendeleo kwa sababu ni kweli hazina viwanja vya mazoezi (Uwanja wa Kaunda haufai licha ya kuzuga kuwa unawekewa vifusi na ule wa Simba Bunju haueleweki), viwanja vya kuchezea mechi zinakodi, hazina wadhamini wengi (klabu inatakiwa kuwa na mdhamini mkuu, washirika katika udhamini, wadhamini kutoka sehemu mbalimbali, wadhamini wa mechi husika), hazina mabalozi wa klabu (zinatakiwa ziwe na angalau wachezaji nyota wanne kwa mwaka waliowahi kufanya vizuri katika klabu hizo, ili wawe wanafanya kazi ya kuwa mabalozi wa klabu hizo), hazina mifuko maalumu kwa ajili ya kuwasaidia wachezaji wao wa zamani (klabu inatakiwa kuwa na harambee za kutafuta fedha kwa ajili ya kulinda historia yake kwa kuwasaidia wachezaji wake wa zamani na wafanyakazi wake), hazina mpango wa kuwawezesha wachezaji wake kupata fursa mbalimbali za kutangaza biashara za makampuni (klabu za Simba na Yanga zina wachezaji wengi wanaochezea timu za taifa na wanaocheza mashindano mbalimbali ya Afrika hivyo zinaweza kuwatumia wachezaji hao kuingia mikataba na makampuni kwa ajili ya kutangaza bidhaa za makampuni hayo), hazina mipango ya bora ya kuibua vipaji na fursa mbalimbali, hazina mipango iliyo wazi ya kibiashara, hazina mipango bora ya kuwasaidia walemavu na watu wenye uhitaji, hazina vituo bora vya kutoa habari (kazi za vituo hivi ni kuelezea matukio mapya ya klabu na mikutano ya habari inayofuata, kutoa taarifa za mechi za klabu, kuelezea mazoezi ya klabu, kuelezea wachezaji n.k), hazitangazi ajira ilizonazo hivyo kuwanyima fursa wanachama na mashabiki wenye uwezo kuomba ajira hizo katika mfumo ulio rasmi, hazina maduka ya bidhaa zao, bidhaa kama Jezi za wachezaji, fulana, skafu, track suit na vitu vingine vingine kwa ajili ya mashabiki wanaume, wanawake na watoto (baadhi ya bidhaa zao zinazouzwa hivi sasa kama vile jezi zinauzwa na wajanja wachache na siyo klabu), hazina rekodi mbalimbali za wachezaji, viongozi n.k.
Hakika kuna vitu vingi vya kimaendeleo ambavyo klabu hizi za Simba na Yanga hazifanyi na hivyo kukosa maendeleo kulingana na umri na mashabiki zilionao.
Ndiyo, Yanga ilianzishwa mwaka 1935 kwa hiyo ina miaka 82 wakati Simba ilianzishwa mwaka 1936 kwa hiyo ina umri wa miaka 81.
Kwa mtazamo wangu, ninawashauri wanachama na mashabiki wa Simba kuwasimamia na kuwafuatilia viongozi wao waweze kuwajibika vya kutosha, wawe na mipango ya muda mfupi na mrefu inayotekelezeka ili klabu ipate maendeleo ya msingi yanayoonekana ili ijitofautishe na watani wao wa jadi Yanga.
Ukweli klabu hazina maendeleo, zinashindwa na Azam!

Abiria wapanda mabasi ya Udart kwa kugombea

Abiria wakiwa wamejaa katika Kituo cha Kimara
Abiria wakiwa wamejaa katika Kituo cha Kimara Mwisho jijini Dar es Salaam cha Mabasi yaendayo haraka kutokana na madai ya mabasi hayo kuwa machache tangu iliponyesha mvua wiki iliyopita. Picha na Salim Shao 
Abiria wanaotumia mabasi yaendayo haraka ya kampuni ya Udart  wamepata adha ya usafiri baada ya magari  zaidi ya 20 kuharibika kutokana na mvua iliyonyesha wiki iliyopita.
Kwa mujibu wa Udart, mvua iliyonyesha Jumatano Oktoba 25 na Alhamisi Oktoba 26,2017 imesababisha mabasi 29 ya kampuni hiyo kuharibika.
Mwandishi wa Mwananchi  ameshuhudia leo Jumatatu Oktoba 30,2017 asubuhi  abiria wakitumia nguvu kupanda mabasi ili kuwahi kwenye shughuli zao.
Waliokuwa wakihangaika zaidi ni wanafunzi wa kidato cha nne ambao wameanza mitihani yao ya Taifa leo.
Baadhi ya vituo ambavyo abiria wamekuwa wakigombea mabasi ni vya Kimara, Mbezi na Ubungo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Selemani Jafo ameshaagiza watoa huduma ya mabasi hayo kuhakikisha yaliyoharibika yawe yametengenezwa ifikapo Alhamisi Novemba 2,2017 ili kuwaondolea adha abiria.

Magufuli azuia bomoabomoa Mwanza


Mwanza. Rais John Magufuli ameagiza kusitishwa kwa ubomoaji wa nyumba za wananchi zaidi ya 2,000 wanaodaiwa kuvamia eneo la Uwanja wa Ndege Mwanza, kituo cha polisi na Jeshi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ).
Akizungumza na wananchi wakati uzinduzi wa daraja la juu la waenda kwa miguu eneo la Furahisha jijini Mwanza leo Jumatatu, Rais Magufuli ameagiza ubomoaji huo usitishwe hadi atakapotolea uamuzi suala hilo.
“Rais ndiye msimamizi mkuu na mwenye mamlaka juu ya ardhi yote nchini; hawa (wananchi) ndio walionipa urais," amesema Rais Magufuli.
Agizo la Rais Magufuli anayefanya ziara ya siku mbili mkoani Mwanza limetokana na mabango ya wananchi kutoka maeneo ya Kayenze, Muhoze na Kigoto wakielezea kero zinazowakabili ikiwemo tishio la nyumba zao kubomolewa kwa madai ya kuvamia maeneo ya ndege, jeshi la polisi na JWTZ
Rais amewaagiza mawaziri wanne kutoka Wizara za Ujenzi,  Mawasiliano na Uchukuzi, Mambo ya Ndani, Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa pamoja na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kukutana kujadili na kutoa mapendekezo ya namna ya kutatua mgogoro huo ndani ya siku 21 kunazia leo Jumatatu.
Amesema baada ya mapendekezo ya vikao vya  mawaziri hao, ataangalia namna ya kushughulikia suala hilo, hata kama itabidi kubadilisha sheria  kulinda maslahi ya wananchi ambao baadhi wameishi maeneo hayo kwa zaidi ya miaka 30.
Katika hotuba yake, Rais pia ameahidi kukamilisha malipo ya Sh9 bilioni yanayodaiwa na mkandarasi anayetekeleza mradi wa upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwa kiwango cha kimataifa ili ukamilike kabla ya mwaka 2020.

Kuugua kwa wakili kwasababisha kesi ya bilionea Msuya kuahirishwa


Moshi. Usikilizwaji wa kesi ndogo ndani ya shauri la mauaji ya bilionea Erasto Msuya umekwama baada ya wakili mmoja kati ya wanne wa upande wa utetezi, John Lundu kuugua.
Lundu anayemtetea mshitakiwa wa nne, Jalila Zuberi, wa sita, Sadick Mohamed na wa saba Ally Mussa Majeshi, ndiye aliyekuwa amuhoji shahidi wa kwanza wa mashitaka, Koplo Seleman Faraji.
Mawakili wenzake, Hudson Ndusyepo, Majura Magafu na Emanuel Safari walishamaliza kumuhoji shahidi huyo katika kesi ndogo Ijumaa Oktoba 27,2017 na leo Jumatatu Oktoba 30,2017 alikuwa amalizie Lundu.
Hata hivyo, baada ya Mahakama kuanza, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Abdallah Chavula alimjulisha Jaji Salma Maghimbi anayesikiliza kesi hiyo kuwa Lundu  amepata dharura.
Chavula ameiomba Mahakama iahirishe kesi hiyo hadi kesho Jumanne Oktoba 31,2017, ombi lililoungwa mkono na wakili Safari kwa niaba ya mawakili wenzake wa utetezi na Jaji Maghimbi ameliridhia.
Kesi hiyo ndogo iliibuka baada ya mawakili wa utetezi kupinga kupokewa maelezo ya kukiri kosa ya mshitakiwa wa pili, Shaibu Jumanne wakidai aliyatoa baada ya kuteswa na polisi.
Koplo Seleman ameieleza Mahakama kuwa Agosti 16,2013 baada ya kumkamata mshtakiwa eneo la Mirerani wilayani Simanjiro alipewa jukumu la kuandika maelezo yake katika Kituo cha Polisi Mirerani.
Katika maelezo hayo ambayo alidai aliyatoa kwa hiari na bila kulazimishwa, mshitakiwa alikiri kushiriki tukio la kumuua mfanyabiashara huyo.
Hata hivyo, shahidi huyo alipoiomba Mahakama ipokee maelezo hayo kama kielelezo cha kesi hiyo, jopo la mawakili wa utetezi likiongozwa na Majura Magafu lilipinga na kutoa sababu nne.
Magafu alisema mshitakiwa amemweleza kuwa hakuandika maelezo polisi Agosti 16,2013 kwa kuwa siku hiyo hakuwa amekamatwa na polisi.
Pia, alisema anachojua ni kuwa Agosti 18,2013 ndipo alipoteswa na polisi na kulazimishwa kusaini maelezo ambayo hakuyatambua.
Wakili Magafu alisema maelezo aliyolazimishwa mteja wake kusaini na kuweka dole gumba hakuwahi kusomewa wala kujua kilichoandikwa na hajui chochote kuhusu tukio hilo.
Magafu alisema baada ya mshitakiwa kuteswa na kuumizwa, polisi waliingiwa woga angeweza kufia Kituo cha Polisi Moshi hivyo Agosti 21,2013 walimpeleka hospitali.
Amesema mshitakiwa alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kilimanjaro ya Mawenzi na baadaye kuendelea kutibiwa katika zahanati ya Gereza la Karanga hadi alipozidiwa akapelekwa KCMC.
Baada ya kutoa hoja hiyo, wakili Chavula alisema msimamo wa kisheria linapojitokeza suala la iwapo mshitakiwa alitoa maelezo kwa hiari au la, ni lazima kuwe na kesi ndani ya kesi.
Akitoa ushahidi katika kesi ndogo, Koplo Seleman alisisitiza kuwa wakati akichukua maelezo ya mshtakiwa alikuwa na afya njema na hakuwa na jeraha lolote. Kesi itaendelea kesho Jumanne Oktoba 31,2017

Tume kumtangaza rais mpya Kenya leo


Nairobi, Kenya. Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatarajiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi wa marudio kwa kura ya utais uliofanyika Oktoba 26 na kutangaza ikiwa itaandaa uchaguzi katika majimbo 25 ambako uliahirishwa.
Makamu wa Rais wa tume hiyo, IEBC, Consolata Nkatha alisema jana jioni kwamba walikuwa wamepokea matokeo kutoka majimbo sita kati ya saba yaliyokuwa yamesalia na kwamba kufikia Jumatatu asubuhi matokeo yote yatakuwa yamejumlishwa.
“Tumepokea matokeo kutoka majimbo sita sasa na tutakuwa katika nafasi ya kutangaza matokeo ya mwisho kesho (leo) asubuhi. Tutafanya kazi usiku kucha kuhakikisha uhakiki na ujumlishaji unakamilika. Pia tutatangaza ikiwa tutaendesha uchaguzi katika majimbo 25 ambako uliahirishwa au la,” alisema Nkatha.
Majimbo hayo yaki kwenye kaunti ambazo tume iliahirisha uchaguzi ambazo ni Kisumu, Migori, Siaya na Homa Bay.
Mawasiliano na IEBC yamekuwa haba lakini inafahamika kwamba makamishna wa tume walifanya kikao cha saa kadhaa na wanasheria wao juzi kufikiria kama wajaribu kuitisha uchaguzi katika majimbo 25.
Jana jioni Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alisema tume yake ilikuwa imehakiki matokeo ya majimbo 259 kati ya 265, yakiwemo ya nchi za nje.
Kutoka katika majimbo hayo, Chebukati alisema watu 7,447,014 walijitokeza kupiga kura sawa na asilimia 43.04. Matokeo yaliyokuwa yakitangazwa moja kwa moja kutoka jengo la Bomas of Kenya Rais Kenyatta alijikusanyia kura 7,393,405 sawa na asilimia 98.3 ya kura halali.
Wagombea wengine wote wamepata kura chini ya 100,000 akiwemo Raila Odinga aliyejiondoa japokuwa amepigiwa kura 70,425.

Rais Magufuli atuma salamu mabadiliko ya CUF


Dar es Salaam. Rais John Magufuli amepongeza mabadiliko yanayofanywa na Chama Cha Wananchi(CUF) akisema mabadiliko hayo yanaungwa mkono na CCM.
Bila kutaja mabadiliko ya aina gani, Rais Magufuli ambaye alikuwa akizunguza wakati wa ufunguzi wa daraja la furahisha litakalotumiwa na waenda kwa miguu jijini Mwanza amesema,“ tunawapongeza kwa mabadiliko mnayofanya.”
Rais Magufuli amesema hayo wakati akikamilisha hotuba yake na kumtambua Mbunge wa Liwaled, Zuberi Kuchauka(CUF), ambaye awali alipanda jukwaani na kusifia utendaji kazi wa Serikali ya Awamu ya Tano. Mbunge huyo ni mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu.
Kuchauka ambaye alikaribishwa na mwenyekiti wa kamati hiyo  Profesa Norman Sigalla King kuwasalimia wananchi mbali ya kumwagia sifa Rais Magufuli pia amesema anamuombea dua ili awe na afya njema kusudi atimize lengo lake na kukuza viwanda na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya kipato cha kati.
“Mheshimiwa Rais sisi sote tunatambua kazi nzuri unayoifanya ya kuwaletea maendeleo Watanzania na mimi napenda nikupongeze sana kwa hilo na ndiyo maana nakuombea dua uzidi kuwa na afya njema,” amesema.
Hivyo wakati akikamilisha hotuba yake, Rais Magufuli alimwita Kuchauka jukwaani na kumshukuru kwa namna alivyotambua utendaji wa Serikali yake.
“Yuko wapi yule mbunge wa CUF...njoo hapa. Huyu ni mbunge wa CUF tena ni kaaafu,” alicheka kidogo na kuendelea “hii ndiyo Tanzania ninayoitaka, tofauti za chama siyo uadui. Siyo kila wakati wewe unakuwa wa kupinga tu, kupinga tu huu ni uzito wa mawazo fulani fulani kichwani,” amesema.
Amesema kwa vile mbunge huyo ametoa pongezi kutokana na utendaji mzuri wa Serikali ya CCM basi akamtaka awafikishie salamu wana CUF wenzake kwa yale wanayoendelea kufanya.
“Tunawapongeza sana kwa mabadiliko mnayofanya na ukawafikishie salamu zetu,” amesema Rais Magufuli.
Ingawa Rais Magufuli hakubainisha bayana ni mabadiliko yapi alikuwa akiyazungumzia lakini CUF imekuwa ikikabiliwa na msuguano wa uongozi kiasi kujikuta kikigawika katika pande mbili, ile inayotambulika kama CUF inayoungwa mkono na Maalim Seif na ile nyingine inayojulikana CUF ya Profesa Ibrahim Lipumba.

Rugimbana: Hakuna kilichobadilika


Dodoma. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wa zamani, Jordan Rugimbana amesema hakuna kilichobadilika kwake kwa sababu mtumishi wa umma ni kama askari ambaye hachagui uwanja wa kupigana vita.
Rugimbana aliyeachwa katika mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa yaliyofanywa na Rais John Magufuli amesema hayo leo Jumatatu Oktoba 30, 2017 alipokabidhi ofisi kwa mkuu mpya wa mkoa huo, Dk Binilith Mahenge.
Akizungumza kuhusu mabadiliko hayo, Rugimbana amesema, "Mtumishi wa umma ni kama askari, hachagii uwanja wa kupigana vita, kwa lugha nyingine hakuna kilichobadilika nipeni muda mtaelewa."
Amesema anakwenda uraiani lakini jukumu lake sasa litakuwa ni kulipa fadhila kwa Rais Magufuli kwa kumchagua kuwa miongoni mwa wasaidizi wake wa kwanza katika Serikali aliyoiunda mwaka 2015.
Rugimbana amesema anachomuahidi Rais ni kuwa atakuwa raia mtiifu, mwaminifu na ataendelea kuwa timu Magufuli.
Amewasifu wakuu wa wilaya akisema ni watiifu, wamekuwa wakiuliza na kupokea ushauri wanaopewa.
Kuhusu utendaji wake, Rugimbana amesema mchakato wa Serikali kuhamia Dodoma unakwenda vizuri.
Mrithi wake, Dk Mahenge amesema atasimamia na kufuatilia mambo yote yaliyofanywa na Rugimbana kwa sababu ni maelekezo ya timu aliyokuwa akifanya kazi nayo.
"Nitasimamia na kufuatilia yote uliyoyafanya kwa sababu ni maelekezo ya timu yako. Wewe ni hazina uendelee kutushauri," amesema.

Nyalandu aachia ubunge, ajivua uanchama CCM


Dar es Salaam. Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amejivua uanachama wa CCM na nyadhifa zake zote, akisema haridhishwi na mwenendo wa siasa nchini.
Nyalandu, ambaye alikuwa Waziri wa Maliasili na Utalii katika Serikali ya Awamu ya Nne, aliiambia Mwananchi  Jumatatu mchana kuwa ameamua kujiondoa CCM na ameiomba “Chadema wafungue malango yao” ili aweze kuungana nao.
"Nimeamua kujiuzulu nafasi yangu ya ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017," alisema Nyalandu ambaye video ya uamuzi huo imesambaa mitandaoni.
"Hali kadhalika, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya ubunge wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.
"Aisha, nimechukua uamuzi huu kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa haki za binadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya Watanzania."
Kwa uamuzi huo, Nyalandu, ambaye aliomba ridhaa ya kugombea urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi uliopita, amejivua ubunge na nafasi nyingine zote alizokuwa akishikilia ndani ya CCM, ikiwa ni pamoja na ujumbe wa Halmashauri Kuu.

Kim Jong-un azuru kiwanda cha bidhaa za urembo Pyongyang

Kim Jong Un holds a hairspray canHaki miliki ya pichaKCNA VIA REUTERS
Image captionKim Jong-un azuru kiwanda cha bidhaa za Urembo Pyongyang
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un ametembelea kiwanda ya bidhaa za urembo mjini Pyongyan akiandamana na mke wake Ri Sol-ju na dada yake Kim Yo-jing.
Vyombo vya habari vilichapisha picha za ziara hiyo siku ya Jumapili.
Kuoneka hadharani kwa Kim Yo-jong, kunakuja muda mfupi baada ya kupandishwa cheo ndani serikali ya Korea Kaskazini.
Bidhaa za urembo kutoka nchi za kigeni zimekuwa adimu nchini Korea Kaskani kutokana na vikwazo.
Kim Jong Un smiles toward electronic device in newly renovated facility with senior officials and his wife in the backgroundHaki miliki ya pichaKCNA VIA AFP
Image captionKim Jong-un azuru kiwanda cha bidhaa za Urembo Pyongyang
Korea Kaskazini inaonekana kujenga sekta yake ya bidhaa za urembo ambapo bidhaa kama Bomhyanggi na Unhasu vimepata umaarufu.
Licha ya umaarufu wake wa kupigwa picha akiwa katika vituo vya kijeshi na maeneo ya kufanyia majiribio makombora, ziara ya Kim katika kiwanda cha bidhaa za urembo ni moja ya propaganda ya kuhalalisha utawake wake kwa watu wa Korea Kaskazini.
Kim Jong Un holds clear liquid samples in bottles at factory visitHaki miliki ya pichaKCNA VIA REUTERS
Image captionKim Jong-un azuru kiwanda cha bidhaa za Urembo Pyongyang
Ziara hiyo "ni ya kuonyesha kuwa Korea Kaskazini inaweza kuwatunza watu wake na kuleta maendeleo kwa kiwango sawa na cha China na Korea Kusini," mdadisi wa masuala ya Korea Kaskazini Ankit Panda aliiambia BBC.
"Licha ya sisi kujua kuwa sio ukweli, ni muhimu kwa utawaka huo kuonyesha watu wake kuwa unaweza kuwapa bidhaa wanazozihitaji,"
Wakati wa ziara hiyo , Kim alikisifu kiwanda hicho kwa kuzalisha bidha za kiwango cha kimataifa, kwa mujibu wa shirika la habari la serikali la KCNA.
Kim Jong Un smiles near a pink-branded selection of cosmeticsHaki miliki ya pichaKCNA VIA REUTERS
Image captionMr Kim was reportedly pleased with the factory's products and recent upgrade

Aliyekuwa kiongozi wa Catalonia "atawania kama hatakuwa gerezani"

People wave Spanish and Catalan Senyera flags during a pro-unity demonstration in Barcelona on October 29, 2017.Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionMaandamano ya kuunga mkono umoja yalifanyika Barcelona
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Uhispania, amesisitiza msimamo wa serikali yake, kuwa kiongozi wa Catalonia ambaye alifutrwa anaweza kuwania tena uchaguzi wa Disemmba ikiwa hatakuwa gerezani.
Alfonso Dastis alizunguamza wakati wa mkutana wa kuunga mkono umoja wa Uhispania ambao ulifanyika katika mji mkubwa zaidi huko Catalonia wa Barcelona.
Carles Puigdemont aliondolewa ofisini baada ya Madrid kulivua eneo la Catalonia usimamizi wake baada ya eneo hilo kutangaza uhuru.
Serikali kuu ya Uhispania kwa sasa imechukua udhibiti kwa idara za Catalonia
Sacked Catalan leader Carles Puigdemont greets supporters at the entrance of a restaurant in Girona, 28 October 2017Haki miliki ya pichaEPA
Image captionAliyekuwa kiongozi wa Catalonia atawania kama hatakuwa gerezani
Mkuu wa mashtaka nchini Uhispania anaandaa kumfungulia mashtaka Bw. Puigdemont na maafisa wengine wa Catalonia kwa kukiuka sheria ya Uhispania.
Bw. Puigdemont anasema hatambui amri ya kutoka Madrid ambayo ilimundoa madarakani.
Wakati huo huo waziri wa mambo ya nadani nchini Uhispania amewaandikia polisi wote huko Catalonia akiwataka kuonyesha uzalendo kwa awamu mpya ya uongozi.
Aliwashauri polis wote ambao sasa wako chini ya udhibiti kutoka Madrid kuhusu wajibu wao wa kufuata maagizo.

Kiongozi wa wakurdi nchini Iraq ameondoka madarakani

Iraqi Kurdish leader Massud Barzani speaks during a press conference on September 24, 2017Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionRais wa wakurdi nchini Iraq Massoud Barzani amewacha wadhifa huo
Rais wa wakurdi nchini Iraq Massoud Barzani amewacha wadhifa huo wakati eneo hilo linapambana na serikali kufuatia uhuru wake.
Kupitia barua iliyosomwa kwa bunge la Kurdi, Bw. Barzani alisema kuwa hataomba kuongezwa muhula wake ambao unakamilika siku nne zinazokuja.
"Ninaomba bunge kukutana ili kujaza nafasi hiyo," alisema.
Wakurdi walikipiga kura mwezi uliopita kuitenga Kurdistan lakini Iraq inasema kuwa kura hiyo ilikuwa kinyume na sheria.
Kisha jeshi la Iraq likaanzisha oparesheni ya kuukomboa mji uliokuwa chini ya wakurdi wa Kirkuk na kuteka vituo vya mafuta vya mji huo.
Map showing control of northern Iraq and Kurdistan Region (23 October 2017)
Image captionRamani inayoonyesha Kurdistan
Bwana Barzani alisema atasalia mpiganiaji wa kurdi na atazidi kutetea mafanikio ya watu wa Kurdistan.
Bw Barzani aliingia ofisini mwaka 2005 baada ya kuhusika katika wajibu mkubwa wa kunda eneo huru la Kurdistan lililo kaskazini mwa Iraq baada ya Saddan Hussen kuondolewa madarakani.
Barzani alishinda uchaguzi mwingine wa urais mwaka 2009 na muhula wake ukaongezwa mwaka 2013.
Baada ya kupoteza maeneo yanayozunguka mji wa Kirkuk kwa serikali ya Iraq, alishinikizwa na wapinzani katika eno la Kurdistan kuondoka madarakani.