Sunday, October 29
TASNIA HALISI WHATSAAP GROUP YAZINDULIWA KWA KISHINDO JIJINI DAR ES SALAAM
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
WAANDISHI wa habari ambao ni wanachama wa kundi laWhatsapp lijulikanalo kama TASNIA HALISI wamezindua kundi hilo leo Oktoba 28, 2017 kwa sherehe kabambe ya kukata na shoka iliyohanikizwa na nyama choma, vinywaji vya kila aina na muziki.
Mratibu wa shughuli hiyo, Bi. Angela Msangi amesema, kundi hilo ni mukusanyiko wa wanataaluma na wadau wa habari na linalenga kuwaleta pamoja wana tasnia kwa nia ya kubadilishana taarifa na kusaidiana kitaaluma na kijamii.
Katika uzinduzi huo uliosindikizwa na burudani ya muziki umeshuhudia waandishi kutoka sehemu mbalimbali nchini wakishiriki.
Katika sherehe hiyo, shampeni mbili zilifunguliwa ikiwa ni pamoja na kukata keki.
Puigdemont ataka upinzani wa kidemokrasia dhidi ya Uhispania
Kiongozi wa jimbo la Catalonia Carles Puigdemont ameipinga hatua ya Serikali kuu ya Uhispania kumuondoa madarakani. Amehimiza kufanywa upinzani wa kidemokrasia dhidi ya utawala wa moja kwa moja kutoka Uhispania.
Puigdemont ameilaani serikali kuu kwa kuikandamiza ari ya Wacatalonia wanaotaka uhuru. Ameongeza kuwa hatua ya Serikali ya waziri mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy kuondoa mamlaka ya ndani ya Catalonia, kwa mara ya kwanza tangu utawala wa kidikteta wa Francisco Franco kati ya mwaka 1939-1975 ni uchokozi.
Amesema upinzani wa kidemokrasia ndiyo njia pekee japo hakufafanua mkondo ambao njia hiyo itachukua. Katika taarifa aliyoitia saini kama Rais wa utawala wa Catalonia, Puigdemont amesema hatua zilizochukuliwa na Rajoy za kuvunja serikali, bunge, polisi ya jimbo hilo na kutwaa madaraka ni kinyume na mapenzi ya Wacatalonia.
Uhispania njia panda
Naibu waziri mkuu wa Uhispania Soraya de Santamaria ndiye ameteuliwa kulisimamia jimbo la Catalonia. Puigdemont ameapa kuendelea kufanya kazi kuhakikisha anajenga taifa huru akiwahimiza wafuasi wake kujibu hatua za serikali kuu kwa kutotumia ghasia, matusi na kwa njia za kuwajumuisha kila mmoja na pia kuheshimu maoni ya wanaopinga kujitenga kwa Catalonia.
Waendesha mashitaka walitangaza Ijumaa kuwa watafungua mashitaka ya uasi dhidi ya Puigdemont wiki ijayo. Kiongozi huyo huenda akafungwa gerezani kwa miaka 30 iwapo atakutikana na hatia.
Uhispania inasalia katika njia panda huku ikikumbana na mzozo mbaya wa kikatiba katika historia yake, uliosababishwa na kura ya maonii ya kutaka kujitenga na kujitawala iliyopigwa Oktoba mosi ambayo imetajwa na mahakama ya kikatiba na serikali ya Uhispania kuwa haikuwa halali.
Waziri Mkuu wa Uhispania Mariano Rajoy alitangaza kuivunja serikali ya Catalonia pamoja na bunge lake na kuitisha uchaguzi kufanywa Disemba 21 kuwachagua viongozi wapya. Uhispania imesema Puigdemont anaruhusiwa kushiriki katika uchaguzi huo.
Maandamano yanatarajiwa Jumapili
Wanaounga mkono Uhispania kusalia kuwa taifa moja wanatarajiwa kukusanyika leo katika mji mkuu wa jimbo la Catalonia, Barcelona. Maandamano hayo ya kupinga utawala wa Catalonia yanaandaliwa chini ya kauli mbiu 'Catalonia ni sisi sote'.
Miongoni mwa watakaoshiriki maandamano hayo ni wawakilishi wa vyama vitatu vya upinzani vya Catalonia, kikiwemo chama cha kihafidhina kinachoongozwa na Rajoy. Maandamano hayo yanaonekana kuwa mwanzo wa kampeini kuelekea uchaguzi wa Desemba 21.
Wabunge 70 wa Catalonia siku ya Ijumaa walipiga kura kuidhinisha uhuru wa kujitawala wa jimbo hilo tajiri lenye idadi ya watu milioni 7.5.
Wachambuzi wanaonya huenda wiki ijayo, mzozo huo wa kisiasa na kikatiba ukashuhudia wakati mgumu wakati wafanyakazi wa umma katika jimbo la Catalonia watakaporejea makazini na huenda wakakataa kuchukua maagizo kutoka kwa viongozi waliotumwa kutoka Madrid kuiongoza Catalonia kwa muda.
Watu milioni 3 wamo hatarini ya kufaa nja DRC

Umoja wa mataifa unasema kuwa zaidi ya watu milioni tatu wamo katika hatari ya kufa njaa katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Kiongozi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia mpango wa chakula Duniani- WFP, ametoa wito wa msaada wa dharura wa kimataifa, ili kumaliza matatizo ya baa la njaa, nchini DR Congo.
David Beasley, ambaye anafanya ziara yake ya kwanza kabisa, katika jimbo linalokumbwa na msukosuko wa mapigano na uasi la Kasai, ameiambia BBC kuwa, zaidi ya watu milioni tatu, wanakabiliwa na baa la njaa.
Anasema kwamba, timu ya wafanyikazi wake, wameshuhudia watoto ambao wanakabiliwa na matatizo ya utapia mlo, huku mamia kwa maelfu yao, wakiwa katika hatari ya kufa, katika kipindi cha miezi kadhaa ijayo, ikiwa msaada hautawafikia.

Mapigano mabaya yalianza katika jimbo hilo la Kasai mwezi Agosti mwaka 2016, baada ya kiongozi mmoja wa kitamaduni kuuwawa, katika mapigano na wanajeshi wa kulinda amani.
Ghasia mpya imesababisha mauwaji ya watu elfu tatu na kuwafurusha zaidi ya watu milioni moja, wengi wao wakiwa ni watoto kutoka nyumbani kwao.
'Mazombi wa simu' kupigwa faini wakivuka barabara Honolulu
Haki miliki ya pichaAFP
Honolulu limekuwa jiji la kwanza kubwa nchini Marekani kuifanya kuwa haramu kwa "mazombi wa simu" kuvuka barabara wakitumia au kutazama simu zao.
Serikali katika jiji hilo la Hawaii wameidhinisha sheria ya kutotekwa fikira ukitumia kivuko cha barabarani.
Hii ina maana kwamba ni marufuku hata kuitupia jicho skrini ya simu yako kwa muda mfupi ukivuka barabara.
Ukipatikana na kosa hilo utapigwa faini ya $15-$35 (£11-£27).
Ukirudia kosa hilo, unaweza kutozwa faini ya hadi $99 (£76), shirika la habari la KHNL Hawaii News Now limeripoti.
"Ni jambo la kimsingi, kwamba macho yako huwa hayatazami pale unapotakiwa kutazama na hilo huweka kila mtu hatarini. Kutazama chini kidogo hata muda mfupi kuangalia ujumbe kwenye simu, unaweza kukosa kuangalia barabara kwa sekunde tano," afisa wa polisi wa Honolulu James Shyer ameambia KHNL.
Wanaotembea kwa miguu hata hivyo bado wataweza kutumia simu zao wakitembea maeneo yaliyotengewa abiria barabarani.
Aidha, unaweza kusamehewa iwapo utatazama simu yako kupiga simu ya dharura, shirika la habari la NPR limesema.
Sheria hiyo iliidhinishwa kuwa sheria Julai lakini kulikuwa na miezi mitatu ya kuwahamasisha raia kabla ya kuanza kutekelezwa rasmi.
Wakati huo, meya Kirk Caldwell alisema Honolulu ni mji ambao ulikuwa na sifa mbaya ya watu wengi kugongwa na magari kwenye vivuko vya barabara - hasa watu wazima - kuliko mji wowote ule Marekani.
Miji mingine imekuwa pia ikifikiria kuchukua hatua sawa.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Baraza la jiji la Toronto lilipiga kura kuomba serikali ya jimbo la Ontario kufanyia marekebisho sheria za trafiki kulifanya kuwa kosa mtu akitembea akiwa hisia zake zimetekwa.
Lakini serikali ya jimbo iliamua zaidi kuangazia kuhamasisha raia kuhusu hatari ya kufanya hivyo.
- Simu ambazo hazifanyi kazi tena na WhatsApp
- Mkono 'huathiri' mawimbi ya simu
- Mwizi wa simu Marekani anaswa kwa kutumia App
Afisa wa polisi wa Toronto Clint Stibbe aliambia CBC mnamo 25 Oktoba kwamba badala ya kupitisha sheria, abiria wanafaa kuwajibikia zaidi usalama wao.
Abiria asafiri katika ndege akiwa pekee

Mwanamke aliyelipa nauli ya ndege ya £46 kuelekea Crete ameshangazwa baada ya kujipata kuwa abiria wa pekee katika ndege.
Karon Grieve kutoka Dunlop mjini Ayrshire aliitaja ndege hiyo aina ya Jet2 inayosafiri kutoka Glasgow hadi kisiwa cha Ugiriki ambayo kwa kawaida huwabeba abiria 189 kuwa ya kushangaza.
Alihudumiwa kama mtu muhimu sana VIP baada ya abiria wawili waliotarajiwa kuabiri ndege hiyo kukosa kufanya hivyo.
Jet2 ilisema kuwa sio jambo la kawaida kwa ndege ya mwisho ya msimu kuwa na abiria wachache.
Bi Grieve aliyekuwa akisafiri kuelekea Crete ili kuandika riwaya alisema kuwa ilikuwa wazi kwamba kulikuwa na abiria wachache wakati alipowasili katika uwanja wa ndege ili kuabiri ndege hiyo siku Jumapili.
Aliambia BBC kwamba: Niliwasili katika eneo la kukaguliwa na kwa mzaha nikawauliza wafanyikazi wa ndege , ni watu wangapi waliabiri ndege hiyo.
Tulianza na watu 10 hadi kufikia watu wanne na akasema huwezi kudhania kuna watu watatu pekee.
Lakini nilipoingia katika lango la mwisho la kwenda kuabiri ndege , watu wengine wawili hawakujitokeza.

Bi Grieve alisema kwa kuwa yeye ni abiria wa pekee wafanyikazi wote wa ndege hiyo walikuwa wakilijua jina lake.
Alisema: Tulikuwa marafiki wakubwa hata kabla ya mimi kuingia katika ndege.Rubani wa ndege alikuwa mzuri.
Baada ya ndege kupaa angani bi Griev aliniita kwa jina langu akiwa katika chumba cha urubani.
Alisema hujambo Karon, utaona Croatia upande wako wa kushoto na tutasafiri katikati ya kimbunga hiki na baadaye alikuja na kusema.
Tafadhalini Karon na wafanyikazi jaribuni kwenda upande mwengine wa ndege na mutazame ''ni kitu cha kushangaza''.
Bi Grieve alisema kuwa alipanga kusalia mjini Crete kwa mwezi mmoja akiandika kitabu chake kabla ya kurudi Uskochi.
Hatahivyo amesema ni vigumu kujipata katika hali kama hiyo atakaropejea Uskochi.
Msichana wa shule aliyelazimishwa kupaka nywele rangi ashtaki
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Msichana wa shule mwenye umri wa maiaka 18 nchini Japan anaishtaki manispaa ya mji baada ya shule yake kumlazimisha mara kwa mara kuipaka nyele yake rangi nyeusi nywele ambayo kwa kawaida ni ya rangi ya udhurungi.
Msichana huyo anasema aliambiwa kuwa atalazimika kuihama shule hiyo iliyo karibu na mji wa Osaka iwapo hangefuata agizo lililotaka nywele za wanafunzi kuwa nyeusi.
Inaripotiwa kuwa alisena rangi aliyokuwa akipaka iliharibu nywe yake.
Shule ya upili ya Kaifukan ilisema kuwa sera zake ni za kuwazui wanafunzi kupaka nyele zao rangi tofauti.
Agizo la shule kwa mwanafunzi lilitolewa liocha ya mama yake kuiambia shule kuwa msichana huyo alizaliwa akiwa na nyele ya rangi ya udhurungi.
Ripoti zinasema kuwa msichana huyo hajahudhuria masomo tangu mwezi Septemba mwaka uliopita.
Mwalimu mkuu wa shule ya Kaifukan Masahiko Takahashi hajazungumzia kesi hiyo.
Zaidi ya watu 20 wauwawa katika mlipuko wa Bomu Somalia
Haki miliki ya pichaREUTERS
Habari zinazotufikia zinasema kuwa, makabiliano makali na hali ya kuzingirwa kwa hoteli moja mjini Mogadishu- Somalia na magaidi, imemalizika.
Duru zinasema kuwa idadi ya watu waliouwawa katika shambulio la kigaidi mjini humo, imepanda na kufikia 20, huku kukiwa na hofu kuwa hienda idadi hiyo ikaongezeka, baada ya kupatikana kwa maiti zaidi, pale walinda usalama watakapomaliza kazi yao.
Hoteli hiyo mjini Mogadishu, ilishambuliwa na kundi la kigaidi la kiislamu, la Al- Shabaab.
Haki miliki ya pichaTWITTER
Wanamgambo hao wanasemekana kuvamia jumba la Hoteli hiyo, mara tu baada ya mabomu mawili kulipuka nje ya majengo hayo.
Inasemekana afisa mmoja mkuu wa kiusalama katika kanda hiyo ameuwawa.
Milipuko miwili imetokea mjini Mogadishu nchini Somali chini ya wiki mbili baada ya shambulio kubwa la bomu kuwaua watu 350.
Mlipuko wa kwanza ulitokea baada ya gari lililokuwa limetegwa bomu kuvurumishwa na kuingizwa kwa nguvu hotelini.
Wanamgambo wenye silaha kisha walifuata na kuingia ndani ya jengo hilo.
Milio ya risasi ingali ikiendelea kusikika ndani ya hoteli moja katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu, ambao ulishambuliwa na kundi la kigaidi la kiislamu, la Al- Shabaab. Yamkini watu 17 wanasemekana kuuwauwa kufikia sasa. Wanamgambo hao wanasemekana kuvamia jumba la Hoteli hiyo, mara tu baada ya mabomu mawili kulipuka nje ya majengo hayo.
Duru zinasema kuwa watu kadhaa wamepigwa risasi ndani ya hoteli hiyo, wakiwemo watoto na mbunge mmoja wa zamani.
Hoteli hiyo ilipangiwa kuandaa mkutano wa kiusalama leo Jumapili.
Majuma mawili yaliyopita, mji wa Mogadishu, ulikumbwa na shambulio baya zaidi la bomu kuwahi kutokea nchini Somalia, amabapo zidi ya watu 350 waliuwawa.
Mlipuko wa pili ulitokea karibu na majengo ya zamani ya bunge ambayo yamo hapo karibu.
Bado haijabainika idadi ya waliofariki.
Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la al-Shabaab ambalo lililaumiwa kwa shambulio hilo la wiki mbili zilizopita, ingawa halikujitokeza kukiri, limejitokeza na kusema lilitekeleza mashambulio hayo ya leo.
Afisa wa polisi Mohamed Hussein ameambia shirika la habari la Reuters kwamba: "Watu zaidi ya saba wamefariki wakiwemo wanajeshi na raia."
Shirika la huduma ya dharura la Aamin mjini humo limesema tayari limesafirisha majeruhi 15 hadi hospitali na kwamba kulikuwa na "miili mingi ya waliofariki".

Afisa wa polisi Ibrahim Mohamed ameambia AFP kwamba katika mlipuko wa pili, gari lililokuwa limejazwa vilipuzi lililipuka karibu na makutano ya barabara.
Shambulio hilo limetekelezwa huku viongozi wa mkoa wakikutana mjini Mogadishu kwa mkutano Jumapili kukubaliana kuhusu mkakati wa pamoja wa kukabiliana na al-Shabab.
Shambulio lililotekelezwa tarehe 14 Oktoba lilisababisha vifo vya zaidi ya watu 358.
Watu 56 bado hawajulikani walipo.
Subscribe to:
Posts (Atom)























