Saturday, October 21

Doris Wanjira: Ni wajibu wangu kulinda wanawake wakitumia matatu Kenya

Picha ya hivi karibuni ya Doris Wanjira akiwa amembeba mtoto ilisambaa sana mtandaoni
Image captionPicha ya hivi karibuni ya Doris Wanjira akiwa amembeba mtoto ilisambaa sana mtandaoni
Magari ya uchukuzi wa umma katika miji mingi duniani yamekuwa hatari kwa wanawake. Visa vya udhalilishaji wa kimapenzi pamoja na udhalilishaji wa aina nyingine vimekuwa vikiripotiwa.
Maeneo mbalimbali duniani, watu wamejaribu kutafuta suluhu.
Nchini Kenya, Doris Muthoni Wanjira, 38, ni utingo kwenye gari la uchukuzi maarufu kama matatu.
Ameambia waandishi wa makala za msimu wa Wanawake 100 wa BBC kwamba wanawake hukabiliwa na changamoto na hatari zaidi katika magari ya umma kuliko wanaume, hata katika kuajiriwa.
"Ni vigumu kupata gari la kufanyia kazi iwapo wewe ni mwanamke. Wanawake hufanya bidii tuseme mara tatu zaidi ndipo wapate kazi.
"Abiria na madereva (wa kike) katika magari ya matatu hupitia mengi: kudhalilishwa kimapenzi, na wengi kudhaniwa kuwa ni makahaba.
"Kwa utingo, baadhi (ya abiria wa kiume) huenda hatua zaidi ya hata kukataa kulipa nauli na tunapowakabili huwa wanatutusi kwa maneno na wakati mwingine hata kutushambulia."
Doris anasema changamoto hizo hata hivyo hazijamzuia kufanya kazi yake, na anahisi kwamba ni jukumu na wajibu wake kuwalinda wanawake katika magari ya uchukuzi wa umma.
"Nafikiri ni muhimu kwamba tuonekane tukifanya kazi za aina hii, inawapa wanawake wengine matumaini kwamba wanaweza kufanya kazi hii sawa na wanaume.
"Na kusema kweli, wanawake ni madereva wazuri kuliko wanaume.
Anita Nderu: Nilishtukia mkono wa mwanamume kwenye ziwa langu
"Huwa twaendesha magari kwa mwendo wa polepole lakini bado huwa twatimiza malengo ya siku na abiria wengi wa kike sasa wanatumia magari yetu kwa sababu tunajua jinsi ya kuifanya rahisi kwao kupanda au kushuka na huwa twawahudumia kwa heshima."

Kuiombea Somalia: Ni kwa nini ulimwengu uliisahau Mogadishu?

Wasomalia wenyewe wamekuwa wakitumia uwezo wa mitandao ya kijamii kuchangisha misaada.Haki miliki ya pichaUCL BME NETWORK/UNION UCL
Image captionWasomalia wenyewe wamekuwa wakitumia uwezo wa mitandao ya kijamii kuchangisha misaada.
Ni kipi hutokea kwenye mitandao ya kijamii baada ya shambulizi la kigaidi? Vitambulisha mada busambaa ambayo huitisha maombi. Watumiaji wa mitandao mara nyingi husambaza picha za uharibifu na watu kuonyesha husuni.
Lakini baada ya shambulizi baya siku ya Jumamosi mjini Mogadishu ambalo liliwaua watu 281, baadhi ya mitandao ya kijamii wamekuwa wakiuliza ni wapi uzalendo kwa Somalia, na mbona hakuna hashi tagi sawa na za wakati wa mashambulizi nchini Marekana na Ulaya.
Shambulizi la lori la simu ya Jumamosi lilikuwa baya zaidi la kigaidi kuwai kutokea nchini Somalia tangu kundi la al-Shabab lianzishe harakati za mwaka 2007. Miili mingine ilichomeka hadi kiwango cha kutotambuliwa.
Kati ya wale waliotambuliwa, mmoja wa waathiriwa alikuwa Maryan Abdullahi, mwanafunzi anayesomea udaktari ambaye alitarajia kufuzu siku iliyofuatia.
Baba yake alikuwa amesafiri kwenda mjini Mogadishu kuhudhuria shereha za kufuzu kwake lakini badala yake akahudhuria maziko yake.
Maryam Abdullahi has been identified as one of the 267 people killedHaki miliki ya pichaANFA'A ABDULLAHI
Image captionMaryam Abdullahi ni mmoja wa watu 267 waliouawa
Hadithi kama hizi za kuvunja moyo si hazifanani na zile ambazo husambaa wakati wa mashambulizi na majanga ya kiasili kote duniani wakati watu hupoteza maisha.
Kati ya siku ya Jumamosi wakati shambulizi hilo lilitokea na mapema Jumatatu kitambulisha mada #IAmMogadishu ilikuwa na Twitter 200 na zaidi, lakini ilipotimia Jumanne kulikuwa na zaidi ya Twitter 13,000 wakati watumiaji wa mitandao ya kijamii walielezea hisia zao baada ya vyombo vya hahari kutoangazia mashambulizi hayo.
Makumbusho kadha yameandaliwa na jamii za wasomalia kote Uingerezea na Marekani yakiwemo ya siku ya Jumanne ya Kings College London's Somali society.
"Kwa sababu ya ukosefu wa uzalendo kwa Somalia, tunataka kuonyesha kuwa kuna watu walio wazalendo kwa Somalia," alisema muandalizi mmoja.
Licha ya kutokepo uzalendo wa nchi za magharibi katika mitandao ya kijamii, Wasomalia wenyewe wamekuwa wakitumia uwezo wa mitandao ya kijamii kuchangisha misaada.
Mitandao ya kijamii ni maarufu nchini SomaliaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMitandao ya kijamii ni maarufu nchini Somalia

Kifungo cha waliokamatwa wakibusu chadumishwa na mahakama Tunisia

Kifungo cha waliokamatwa wakibusu chadumishwa na mahakama TunisiaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKifungo cha waliokamatwa wakibusu chadumishwa na mahakama Tunisia
Mahakama ya rufaa nchini Tunisia imedumisha hukumu ya wapenzi wawili waliokamatwa mwezi Septemba kwa kubusu wakiwa ndani ya gari lao.
Nessim Ouadi, ambaye ni raia wa Ufaransa pia alilaumiwa kwa kupuuza maagizo ya baada ya kukamatwa pamoja na mpenzi mwanamke raia wa Tunisia.
Wawili hao walipewa vifungo vidogo ikiwa ni miezi minne kwa mwanamume na miwili kwa mwanamke tofauti na walivyopewa mwezi Oktoba.
Kesi hiyo ilisababisha malalamiko katika mitandao ya kijamii na kuzua mjadala nchini Tunisia kuhusu maadili katika maeneo ya umma na wajibu wa polisi.
Mkuu wa mshataka alisema kuwa kesi hiyo imeripotiwa kwa njia isiyofaa na vyombo vya habari vya kimataifa na kuwa wawili walikuwa uchi na walikuwa wakifanya mapenzi wakati walisimamishwa na polisi.

Blac Chyna aishtaki familia ya Kardashian

Blac Chyna ameishtaki familia ya The Kardashian kwa madai kwamba ndio iliosababisha kufutiliwa mbali kwa kipindi chake cha RuningaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBlac Chyna ameishtaki familia ya The Kardashian kwa madai kwamba ndio iliosababisha kufutiliwa mbali kwa kipindi chake cha Runinga
Blac Chyna anaishtaki familia ya The Kardashian kwa madai kwamba ndio iliosababisha kufutiliwa mbali kwa kipindi chake cha Runinga.
Anadai kwamba familia hiyo inataka kumharibia.
Wakili wa Blac Chyna aliithibitishia BBC kwamba Kris Jenner ametajwa kama mtetezi katika kesi hiyo pamoja na Kourtney, Kim na Khloe Kardashian mbali na Kendall na Kylie Jenner.
Mwakilishi wa familia hiyo hajatoa tamko lolote kufuatia ombi hilo la BBC.
Kesi hiyo inajiri baada ya Uhusiano kati ya mlalamishi huyo na Rob Kardashian kugonga mwamba , wakati ambapo walikuwa wamepata mtoto wa kike.
Black Chyna mwenye umri wa miaka 29 anadai alipigwa na kunyanyaswa na aliyekuwa mchumba wake Rob Kardashian.
Rob Kardashian na mpenziwe wa zamani Blac ChynaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionRob Kardashian na mpenziwe wa zamani Blac Chyna
Nakala za mahakama dhidi ya familia hiyo na kuchapishwa kamili na chombo cha habari cha Buzzfeed zinadai kwamba Rob Kardashian ni myanyanyasaji na anataka kumharibia Angela White {Blac Chyna}.
Chombo hicho cha habari pia kinaishutumu familia hiyo kwa kutumia umaarufu wao, utajiri na uwezo kulipiza kisasi na kuzuia kuanzishwa kwa kipindi chake cha runinga Rob na China kwa msururu wa pili.
Hatua hiyo inajiri wiki mbili baada ya Rob Kardashian kuwasilisha kesi mahakamani akisema kuwa ni yeye ndiye aliyemshambulia, madai ambayo blac Chyna amekana.

Maafisa 53 wa usalama wauawa na wapiganaji Misri

Shambulio hilo lilitokea katika eneo la jangwaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionShambulio hilo lilitokea katika eneo la jangwa
Maafisa nchini Misri wanasema kuwa takiban maafisa 53 wa usalama na wapiganaji wa kiislam kumi na watano wameuawa katika makabiliano yaliyotokea katika eneo la jangwa magharibi mwa nchi hiyo .
Wizara ya mambo ya ndani nchini humo inasema kuwa wapiganaji waliwafyatulia risasi wanajeshi wakati walipokuwa wakifanya uvamizi kwenye maficho yao, karibu na eneo lenye chemi chemi Bahariya .
Duru za usalama zinasema kuwa wapiganaji walikuwa na uelewa zaidi wa eneo hilo na afisa wa kijeshi aliyetoa maagizo ya uvamizi alishindwa kuagiza wanajeshi kuimarisha kikosi chake .
Taarifa moja inasema kuwa wapiganaji hao ni wajumbe wa kikundi kinachofahamika kama Hasm, ambacho kiliwahi kuyashambulia majeshi ya usalama awali.

WHO lamteuwa Mugabe kuwa balozi mwema wa afya

Rais Robert MUgabe ateuliwa kuwa balozi mwema wa fya na shirika la afya duniani WHOHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES/AFP
Image captionRais Robert MUgabe ateuliwa kuwa balozi mwema wa fya na shirika la afya duniani WHO
Shirika la afya duniani WHO limemteuwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe kama 'balozi mwema ' katika kusaidia kukabiliana na magonjwa yaliyosahaulika .
Akifafanua uamuzi wa uteuzi huo , Mkurugenzi mkuu mpya wa W.H.O., Dr Tedros Adha-nom Ghebre-yesus, alisifu namna Zimbabwe inavyozingatia afya ya umma.
Lakini wakosoaji wanasema katika kipindi cha miaka thelathini na saba ya utawala wa rais Mugabe, huduma za afya zimekuwa mbaya ambapo wahudumu wa afya wamekuwa hawalipwi mara kwa mara , na kumekuwa na ukosefu mkubwa wa dawa muhimu .
Wakosoaji wanasema kuwa sekta ya afya ya Zimbabwe imekuwa aiafikii viwango vya afya nchini humoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWakosoaji wanasema kuwa sekta ya afya ya Zimbabwe imekuwa aiafikii viwango vya afya nchini humo
Dr .Tedros, ni raia wa Ethiopia ambaye ni Muafrika wa kwanza kuongoza shirika la W.H.O. na alichaguliwa kwa ajili ya kukabiliana na kile kilichoaminiwa kuwa ni kugeuzwa kwa shirika hilo kuwa la kisiasa.

Adakwa na polisi kwa kubaka watoto wadogo 14


Singida. Jeshi la Polisi mkoani Singida linamshikilia mganga wa kienyeji mkazi wa mtaa wa Minga, Daud Idd (74), kwa tuhuma ya kunajisi watoto 14 wenye umri kati ya miaka saba na 12 na kuwasababishia maumivu makali katika sehemu zao za siri.
Mgonga huyo maarufu kama Babu Karatu ameelezwa kuwa alikuwa akishirikiana kutenda vitendo hivyo na mtoto wa mdogo wake aitwaye Abdallah Yahaya (31).
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo Jumamosi, kaimu kamanda wa polisi mkoani hapa Isaya Mbughi amesema mtuhumiwa anadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti kati ya Desemba mwaka jana, hadi Oktoba mwaka huu.
Amesema kuwa mwathirika mmoja mwenye umri wa miaka saba siku ya Oktoba 16 mwaka huu saa 11.45 jioni wakati akiogeshwa na mama yake alilalamika kuwa anasikia maumivu makali katika sehemu yake ya siri.
Amesema baada ya binti kuyo kulalamika kwa mama yake mama huyo aliweza kumchunguza kwenye sehemu zake za siri na kubaini kuwa michubuko inayotokana na kuingiliwa kimwili.
“Mama huyo baada ya kuona michubuko hiyo kwenye sehemu za siri za binti yake alimhoji mtoto wake na mtoto huyo aliweza kumtaja mganga wa kienyeji Karatu. Mwaathirika huyo alienda mbele zaidi na kumweleza mama yake kuwa si yeye pekee hufanyiwa vitendo hivyo, bali wapo watoto wengi wamefanyiwa.” 
Kaimu kamanda huyo amesema baada ya hapo mama huyo alitoa taarifa kwa mwenyekiti wa mtaa wa Minga na kisha yeye na mwenyekiti wa mtaa waliweza kuongozana hadi kituo cha kati cha polisi mjini hapa.
“Jeshi la polisi liliweza kuwakamata watuhumiwa hao ambao wanaishi katika nyumba moja, kwa tuhuma ya ubakaji. Uchunguzi wa awali umebaini kuwa watoto waliofanyiwa unyama huo wanasoma katika Shule za Msingi Singidani, Nyerere na Mughanga,” amesema.
Mbughi amesema mbinu iliyokuwa inatumika kuwanasa watoto hao wa ni kuwarubuni na kisha kuwaonyesha video/movie, kwenye kompyuta mpakato.
“Wakati watoto hao wa kike wakiendelea kuangalia video sebuleni, mtuhumiwa huyo alikuwa akichomoa mmoja na kuingia naye chumbani na kumwingilia kimwili. Wachache alikuwa akiwachezea sehemu zao za siri. Baada kuingiliwa kimwili watoto hao walikuwa wakipewa zawadi ya shilingi mia mbili au shilingi 2,000,” amesema.

Pikipiki, bastola na risasi 30 zapokewa kortini kama kielelezo


Moshi. Vielelezo zaidi vya kesi ya mauaji ya mfanyabiashara tajiri wa Mererani, Erasto Msuya vimeendelea kupokewa mahakamani ikiwamo pikipiki inayodaiwa kutumika.
Uamuzi wa kupokea pikipiki hiyo kama kielelezo cha kesi hiyo, ulitolewa jana na Jaji Salma Maghimbi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, anayesikiliza kesi hiyo inayowakabili washtakiwa saba.
Jaji Maghimbi alilazimika kutoa uamuzi mdogo baada ya kutokea mabishano ya kisheria wakati mawakili wa utetezi wakiongozwa na wakili Emanuel Safari kupinga kupokewa kwa kielelezo hicho.
Katika hoja zake, wakili Safari alisema shahidi wa tisa, Samwel Maimu hakuwa shahidi sahihi kutoa kielelezo kwa vile hakueleza namna alivyoipata hiyo pikipiki.
Maimu ambaye alikuwa mkuu wa operesheni katika tukio hilo, alitoa ushahidi wake akisema pikipiki hiyo ni moja ya vitu alivyovikusanya siku ya tukio na kuvitunza katika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi (RCO).
Hata hivyo, katika hoja yake, wakili Safari alisema shahidi huyo kwa sasa sio mtunzaji wa vielelezo hivyo kisheria, ilitakiwa ionekane mnyororo wa tangu alipovihifadhi na alipokabidhiwa hiyo jana.
Jaji Maghimbi alikataa pingamizi hilo akisema shahidi huyo ni sahihi kwa kuwa aliweza kutambua na kuzitaja alama za kipekee zilizopo katika pikipiki hiyo aina ya Toyo yenye nambaT.316 CLG.
Baada ya kupokewa kwa kielelezo hicho, shahidi huyo aliendelea kutoa ushahidi wake kwa kuongozwa na Wakili mwandamizi wa Serikali, Omary Kibwana na mahojiano yalikuwa kama ifutavyo:-
Wakili Kibwana: Umeeleza kuwa tarehe 7.8.2013 ulipofika eneo la tukio ulikusanya pia maganda ya risasi, yalikuwa mangapi?
Shahidi: Yalikuwa 22.
Wakili Kibwana: Yalikuwa vipi kama ukiyaelezea?
Shahidi: Yana rangi ya grey (kijivu) na mengine yalikuwa na namba. Ninaweza kukumbuka chache kama 77 na 61 lakini siwezi kukumbuka namba zote.
Wakili Kibwana: Ulivyoyakusanya, uliyarudisha kuyahifadhi wapi?
Shahidi: Nilikwenda kuyahifadhi kwenye kasiki iliyopo ofisi ya RCO Kilimanjaro.
Wakili Kibwana: Ulimkabidhi nani ayahifadhi?
Shahidi: Kwa kipindi hicho mimi ndiyo nilikuwa mtunza stoo.
Wakili Kibwana: Hebu tueleze, ulitunzaje?
Shahidi: Niliyaweka kwenye bahasha nyeupe nikaandika exhibit (kielelezo), maganda 22 ya SMG au SAR yaliyokutwa eneo la tukio.
Wakili Kibwana: Kingine ulichoandika?
Shahidi: Niliandika namba ya kesi BMG/IR2786/2013
Wakili Kibwana: Hiyo bahasha uliyohifadhia hayo maganda ya risasi, ukipewa nafasi unaweza kuitambua?
Shahidi:Ndiyo
Wakili Kibwana: Vitu gani vitakufanya uitambue?
Shahidi:Ni kutokana na mwandiko wangu, jinsi nilivyoifunga na rangi ya bahasha.
Wakili Kibwana: (akimpa shahidi bahasha) Naomba uiangalie.
Shahidi: Ndiyo bahasha yenyewe niliyoweka maganda 22.
Wakili Kibwana: Naomba ionyeshe Mahakama hayo maandishi unayosema uliandika?
Shahidi: (akatoka kizimbani na kwenda kumuonyesha Jaji)
Wakili Kibwana: Ulisema bahasha hii uliiweka kwenye kasiki?
Shahidi: Ndiyo
Wakili Kibwana: Na kipindi hicho wewe ulikuwa mtunzaji wa stoo?
Shahidi: Ndiyo
Wakili Kibwana: Baada ya kuyaweka kuna wakati yaliwahi kupelekwa mahali pengine?
Shahidi: Sikumbuki kama yaliwahi kupelekwa sehemu nyingine.
Wakili Kibwana: Umesema ulikusanya pia bastola eneo la tukio?
Shahidi: Ndiyo
Wakili Kibwana: Ulikusanya bastola na nini?
Shahidi: Bastola moja na magazini mbili
Wakili Kibwana: Hiyo bastola ukipewa nafasi ya kuitambua utaweza?
Shahidi: Ndiyo nitaweza.
Wakili Kibwana: Utaitambuaje?
Shahidi: Kwa rangi yake, aina yake na namba zake
Wakili Kibwana: Ilikuwa na namba gani?
Shahidi: ELS 417
Wakili Kibwana: Kitu kingine unachoweza kukitambua?
Shahidi: Ni kwamba ilitengenezwa Australia
Wakili Kibwana: Hizo magazini mbili unaweza kuzitambua?
Shahidi: Zina rangi nyeusi, moja ni ndefu na moja ni fupi na zote zina namba.
Wakili Kibwana: Zina namba gani?
Shahidi: Ile ndefu ina namba 7151 na ile fupi namba 3206.
Wakili Kibwana: Kingine kwenye hiyo magazini?
Shahidi: Magazini ndefu ilikuwa na risasi 23 na fupi ilikuwa na risasi saba.
Wakili Kibwana: Hii bastola na magazini ulifanya nazo nini?
Shahidi: Nilizihifadhi kwenye kasiki ofisi ya RCO.
Wakili Kibwana: Ulizihifadhije?
Shahidi: Niliziweka kwenye bahasha nikaandika bastola za marehemu Erasto Msuya na nikaandika namba ya kesi.
Wakili Kibwana: Hiyo bahasha uliyohifadhia bastola na magazini mbili unaweza kuitambua?
Shahidi: Ndiyo ilikuwa na rangi ya kaki na ina mwandiko wangu.
Wakili Kibwana: Mheshimiwa Jaji tunaomba tumuonyeshe hiyo bahasha
Shahidi: (Baada ya kukabidhi na kuitizama) ndiyo bahasha niliyohifadhia bastola na magazini
Wakili Kibwana: Naomba ufungue hiyo bahasha utuonyeshe vilivyopo.
Shahidi: (akifungua na kutoa bastola) Hii ndiyo bastola aina ya Glock19 na namba zake kama nilivyozitaja ni ELS 417, rangi yake ni nyeusi na imetengenezwa Australia.
Wakili Kibwana: Hebu endelea.
Shahidi: (akatoa magazini) Hii ndiyo magazine niliyosema ni nyeusi, ina risasi 23 na namba yake ni 7151.
Wakili Kibwana: Naomba utuhakikishie hizo risasi.
Shahidi: (akizitoa kwenye magazini na kuzihesabu) ziko 23.
Wakili Kibwana: Na magazini ndogo?
Shahidi: (akiionyesha) ndiyo hii namba zake ni 3206, ina risasi saba.
Wakili Kibwana: Naomba utuhakikishie
Shahidi: (akazitoa na kuzihesabu) ziko saba.
Wakili Kibwana: Umetambua bastola kwa namba zake na sehemu ilipotengenezwa na umetambua magazini zote mbili. Naomba ionyeshe Mahakama hizo namba kwa ukaribu.
Shahidi: (akaenda kwa Jaji na baadae kwa wazee washauri wa Mahakama na mawakili wa utetezi na kuwaonyesha kwa ukaribu)
Wakili Kibwana: Baada ya kutambua bastola hii na magazine mbili, uko tayari kuzitoa kama kielelezo?
Shahidi: Ndiyo niko tayari kutoa bastola na magazini mbili zenye jumla ya risasi 30 kama kielelezo.
Hata hivyo, Wakili John Nundu alisimama na kupinga kupokewa kwa bastola na magazini hizo akisema sababu za kupinga zitatolewa na wakili Safari.
Katika hoja zake, wakili Safari alisema shahidi huyo katika ushahidi wake alidai kwa wakati huo alikuwa akifanya kazi kituo cha Himo na alisema vitu hivyo alivihifadhi katika kasiki ya RCO.
“Juzi alituambia badala yake, sasa kuna mtunza stoo mwingine aliyemtaja kwa jina la Hashimu. Kwa kuwa shahidi huyo siyo mtunza stoo, siyo competent (sahihi) kuvitoa kama kielelezo. Wala hajatueleza vielelezo hivi ambavyo havihifadhi tena yeye vilifikaje mikononi mwake leo (jana) hadi avitoe kama kielelezo kwa vile ile chain of custody (mnyororo) hauonekani.”
“Kuna mashaka makubwa na kwa maoni yetu hivi siyo authenticity (sio vyenyewe) na vinaweza kuwa vilichezewa. Katika mazingira haya tunaweza kupokea vitu vya kutunga, kuungaunga na kupandikiza,” alisema wakili Safari.
Hoja hiyo ilipingwa na wakili Kibwana anayesaidiana na Wakili Mwandamizi Abdalah Chavula na mawakili Lucy Kyusa na Kassim Nassiri akisema hazina mashiko.
Wakili Kibwana alisema kulikuwa hakuna haja ya kuwapo kwa mnyororo wa makabidhiano kwa kuwa shahidi wake alitambua vielelezo hivyo kwa alama za kipekee.
Baada ya kusikiliza mabishano hayo, Jaji Maghimbi aliahirisha kesi hiyo kwa muda ili kuandaa uamuzi mdogo na iliporejea, Jaji alitupilia mbali pingamizi hilo na kuvipokea vielelezo hivyo.
Msuya aliyekuwa akimiliki vitega uchumi kadhaa ndani na nje ya Arusha, aliuawa kwa bunduki ya kivita ya Sub Machine Gun (SMG) Agosti 7, 2013 katika eneo la Mijohoroni wilayani Hai.
Kesi hiyo inawakabili washtakiwa saba ambao ni Sharifu Mohamed, Shaibu Jumanne (Mredii), Musa Mangu, Jalila Zuberi, Karim Kihundwa, Sadick Mohamed (Msudani au Mnubi) na Ally Mussa. Jaji Maghimbi aliahirisha kesi hiyo hadi Jumatatu kwa ajili ya mawakili wa utetezi kumhoji shahidi.

Mwalimu ajiua kwa kujichinja


Sumbawanga. Mwalimu wa Shule ya Sekondari ya Mtenga wilayani Nkasi, Leonard Mwipugi (29) amejiua kwa kujichinja koromeo akiwa nyumbani kwake.
Taarifa zilizotolewa na Mratibu wa Elimu Kata ya Mtenga, Hebron Mwafungo zimeeleza kuwa mwalimu huyo amekutwa akiwa amekufa baada ya kujichinja nyumbani kwake muda wa  saa sita mchana leo Jumamosi.
Amesema kuwa mwalimu huyo alikwenda kazini kwake na saa  5 asubuhi alirejea nyumbani na hakumkuta mkewe  na baada ya muda walipata taarifa kuwa mwalimu huyo amekutwa amekufa baada ya kujichinja koromeo chumbani kwake.
Amesema kuwa mwalimu huyo alikua akiishi na mdogo wake nyumbani hapo na alipofika alimtuma mdogo wake  mbali kidogo ya nyumba hiyo na baada ya kurudi aliona damu na baada ya kuchungulia chumbani alikuta kaka yake amefariki dunia kwa kujichinja koromeo na kutoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji hicho.
Amesema baada ya kumdodosa mdogo wa marehemu huyo alidai kuwa kaka yake  siku za nyuma alikua na mgogoro na mkewe lakini ulikwisha ila anahisi kitendo cha mkewe kuondoka nyumbani na kwenda mjini Namanyere huenda jambo hilo lilimkasirisha na kuchukua hatua hiyo ya kujichinja.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Rukwa, George Kyando amesema chanzo cha kifo hicho bado hakijajulikana lakini polisi wanaendelea na uchunguzi ili kubaini kilichomsibu mwalimu huyo kiasi cha kuchukua maamuzi ya kujiua kikatili namna hiyo.