Monday, September 11

Taarifa za siri za kampuni ya Apple zafuja

Apple logoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionTaarifa za siri za kampuni ya Appla zafuja
Taarifa kuhusu simu mpya za iPhone na vifaa vingine vya Apple ambavyo havijazinduliwa zimefuja.
Mitandao miwili iliruhusiwa kuona aina mbili ya tekenolojia ya iOS kabla ya siku kuzinduliwa.
Taarifa zilizofichuliwa ni za simu ya iPhone X pamoja na ya simu mbili aina ya iPhone 8.
Mwandishi mmoja wa masuala ya teknolojia huo ndio ufujaji mkubwa zaidi katika kampuniya Apple.
Apple inatarajiwa kuzindua kifaa kipya kwenye makoa yake makuu siku ya Jumanne.
Kampuni hiyo yenye makao yake huko California hujitahidi kuficha siri za teknlojia yake hadi wakati wa uzinduzi wa vifaa vyake.
Tim CookHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMkuu wa Apple Tim Cook
Hata hivyo taarifa kuhusu vigaa vipya vya Apple zlifichuliwa Agosti,
Wakati hilo likionekana kufanyika kimakosa, imedaiwa lakini ufujaji wa hivi majuzi ulikwa wa makusudi.
Hata hivyo BBC imebaini kuwa mtu asiyejulikana alichapisha anwani za iOS 11 zinazofahamika kama golden master (GM) ambazo zilifungua teknolojia katika komputa za Apple.
Apple haijasema lolote.
Hi ni mara ya pili katika kipindi cha mieiz mitatu ambapo kampuni hiyo inajipata katika hali ambapo taarifa zake za siri zinafichuka.
Mwezi Juni sauti ya saa nzima ya mkutano kuhusu njia za kuwazuia wale wanaofichua taarifa zilifichuka kwa mtandao moja wa habari.
Apple productsHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSimu za Apple huipa kampuni hiyo faida kubwa

Wakurdi wa Iraq wanasema wako tayari kujitenga na kuwa na taifa lao

The President of Iraqi Kurdistan, Massoud Barzani, during a BBC interview
Image captionRais wa eneo la Kurdistan nchini Iraq Massoud Barzani
Rais wa eneo la Kurdistan nchini Iraq amesema kuwa eneo hilo litachora mipaka ya taifa lao siku za baaadaye ikiwa Iraq haitakubali kura ya uhuru katika kura ya maoni ambayo inatarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu.
Massoud Barzani aliambia BBC kuwa alitaka kuafikia makubaliano na serikali ikiwa wakurdi wanataka kujitenga.
Waziri mkuu wa Iraq amekataa kura ya maoni akisema kuwa ni kinyume na sheria.
Bwana Barzani pia ameonya kuwa wakurdi watapigana na kundi lolote ambalo litajaribu kubadilsiha hali huko Kirkuk kwa nguvu.
Kurds take pictures with Kurdish flags at the Kirkuk Governorate Council building in Kirkuk, Iraq (6 April 2017)Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionWakurdi wa Iraq wanasema wako tayari kujitenga na kuwa na taifa lao
Vikosi vya Kurdi vya Peshmerga vimechukua udhibiti wa mji huo wenye utajiri wa mafuta ambao una waarabu wengi na sehemu zingine zinazodaiwa na Baghadad kwa zaidi ya miaka mitatu.
Wapiganaji wa kishia wanasema kuwa hawataruhusu mji wa kirkuk kuwa sehemu ya eneo huru la Kurdistan.
Wakurdi ndio jamii ya nne kwa ukubwa eneo la Mashariki ya Kati lakini bado hawajapa taifa.
Nchini Iraq ambapo wanachukua asilimia 15 hadi 20 ya watu milioni 37, wakurdi wamekumbwa na miongo kadha ya ukandamizaji wa serikali za kiarabu kabala ya kujietenga kufuatia vita vya Ghuba vya mwaka 1991.
Iraqi Kurdish men look at posters bearing images of Massoud Barzani and urging people to vote in the upcoming independence referendum in Irbil (7 September 2017)Haki miliki ya pichaAFP
Image captionWakurdi wa Iraq wanasema wako tayari kujitenga na kuwa na taifa lao

SERIKALI YATAKIWA KULINDA BARABARA ZA LAMI


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga, akitoa ufafanuzi kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu kuhusu hatua zinazochukuliwa katika ulindaji wa miundombinu ya barabara wakati walipokagua barabara ya Dodoma – Mayamaya iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Moshi Kakoso akitoa maoni kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga, juu ya ulindaji wa miundombinu na kuzingatia usalama wa mazingira wakati walipokagua barabara ya Dodoma – Mayamaya iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga, (watatu kushoto), akiwaonesha kingo za barabara baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakati walipokagua barabara ya Dodoma – Mayamaya iliyokamilika kujengwa kwa kiwango cha lami, mkoani Dodoma.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga (katikati), wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu wakitoka kukagua daraja la Kelema linalounganisha Wilaya ya Chemba na Kondoa, mkoani Dodoma. Daraja hilo limekamilika kwa asilimia 98.




Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga, akitoa maelekezo kwa Mhandisi wa mradi wa barabara ya Mayamaya – Mela yenye urefu wa KM 99.3, Eng. Leornado Licari, wakati walipokagua Daraja Kelema lililopo katika barabara hiyo lenye urefu wa mita 205, mkoani Dodoma.




Mhandisi Mshauri wa mradi wa barabara ya Mayamaya – Mela yenye urefu wa KM 99.3, Eng. Leornado Licari akifafanua jambo kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga na wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu katika ziara ya ukaguzi wa daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205 lilipo katika barabara hiyo mkoani Dodoma.




Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu Mhe. Moshi Kakoso (wanne kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Joseph Nyamhanga, (wanne kushoto), katika picha ya pamoja na wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya miundombinu katika picha ya pamoja chini ya Daraja la Kelema linalounganisha Wilaya za Chemba na Kondoa mkoani Dodoma.


…………………….

Serikali imetakiwa kuweka mkakati wa kuzilinda, kutunza na kuhifadhi barabara zote zinazojengwa kwa kiwango cha lami nchini ili kuziwezesha kudumu kwa muda uliokusudiwa na hivyo kuepuka gharama za ukarabati wa mara kwa mara.

Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu mheshimiwa Moshi Suleman Kakoso amesema hayo mara baada ya kukagua barabara ya Dodoma – Babati yenye urefu wa kilomita 263, ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami umekamilika.

“Hakikisheni ujenzi wa barabara unaendana na uboreshaji wa huduma na maisha ya wananchi sehemu ambapo barabara hizo zinapita ili kuchochea maendeleo”, amesema mheshimiwa Kakoso.

Makamu mwenyekiti huyo amesema Kamati yake imeridhishwa na hatua zilizofikiwa za ujenzi wa barabara Dodoma –Babati KM na daraja la Kelema linalounganisha Wilaya za Chemba na Kondoa ambalo litawezesha barabara hiyo kupitika kwa uhakika wakati wote.

“Nimefurahishwa na taarifa aliyoitoa Meneja mradi wa barabara hii kwamba pamoja na kujenga barabara pia mkandarasi amechimba visima vya maji katika maeneo haya kwa ajili ya kusaidia wananchi jambo ambalo ni jema na la kuigwa na makandarasi wengine”, amesisitiza Makamu Mwenyekiti Kakoso.

Aidha, Makamu Mwenyekiti ameitaka Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (sekta ya ujenzi), kuwa na mpango endelevu wa kuweka kingo zinazoonesha mipaka ya hifadhi ya barabara mapema na kwa uwazi ili kuepusha migogoro kwa wananchi na ulipaji wa fidia zinazoweza kuepukika.

Ameongeza kuwa Serikali ihakikishe inasimamia ipasavyo sheria zinazolinda barabara ikiwemo kuweka alama za vivuko vya wanyama mahala panapostahili ili kudhibiti mifugo kukatiza ovyo katika barabara.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), Mhandisi Joseph Nyamhanga amesema katika kuhakikisha kuwa Serikali inailinda barabara ya Dodoma – Babati tayari imeagiza uongozi wa Wakala wa Barabara (TANROADS), mkoa wa Dodoma na Manyara kuhakikisha wanatenga eneo kwa ajili ya ujenzi wa mizani ili kudhibiti madereva wanaozidisha uzito usiokubaliwa kisheria.

Ameongeza kuwa Wizara inaendelea kutoa elimu kwa umma ili kuhamasisha utunzaji wa miundombinu ya barabara kama kutomwaga mafuta barabarani,kutopitisha mifugo na kutoiba alama za barabarani.

Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Miundombinu imefanya ziara katika mradi wa barabara ya Dodoma – Babati (Km 263), na daraja la Kelema lenye urefu wa mita 205 lililopo wilaya ya Chemba mkoani 

Dodoma na kuridhishwa na miradi hiyo ambapo wameitaka Serikali kupitia wizara ya ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi), kuhakikisha inalinda na kutunza miundombinu hiyo ili idumu muda mrefu.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

UFUNGUZI WA UCHUNGUZI WA KINYWA NA MENO WAFANYIKA ZANZIBAR

Jamii inatakiwa kuweka utaratibu wa kupima afya ikiwemo afya ya kinywa na meno ili kupatiwa uchunguzi wa awali pamoja na elimu sahihi ya afya angalau mara mbili kwa mwaka .

Hayo aliyaeleza na Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya Dr Fadhil Mo’hd Abdalla huko katika Kituo cha Afya Rahaleo, wakati akifungua zoezi la uchunguzi wa afya ya kinywa na meno linaloendeshwa na Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno kutoka Tanzania .

Alisema afya hiyo ni muhimu kufanyika awali kabla ya madhara, kwa kupatiwa ushauri wa mapema kabla ya athari kujitokeza na kusababishwa kupoteza meno .Alifahamisha kuwa katika miaka ya nyuma elimu ya afya ya kinywa na meno zilikuwa zikitolewa katika maskuli ,wataalamu hutoa elimu kwa wanafunzi pamoja na kung’oa meno kwa wale ambao meno yao yameadhirika .

Aidha alisema mpango huo wa uimarishaji afya ya jamii iko haja kurejea utaratibu wa kizamani , wataalamu wa afya ya kinywa na meno kutoa huduma za matibabu katika maeneo mbali mbali ikiwemo maeneo ya maskuli na vijijini .

“Huu usiwe mwanzo wa kuonyesha njia kwa jamii na wala msisubiri kuumwa kila muda mujiwekee utaratibu wa kujichunguza afya zenu ikiwemo afya ya kinywa na meno pamoja na maradhi yasioambukiza ili muweze kupata ushauri mapema kwa Madaktari ,”alisema Mkurugenzi Kinga.

Alieleza kutoa elimu na uchunguzi wa afya kwa jamii itasaidia kupunguza gharama za matibabu na kuimarisha kinga ya awali na kujiepusha na matumizi ya vyakula ambavyo vinachangia kuleta madhara ikiwemo vyakula vya sukari kuchangia uozeshaji wa meno hasa kwa watoto .

Nae Mwenyekiti wa Chama cha Madaktari wa Afya ya Kinywa na Meno ( TBA) Dr Lorna Carneiro alisema mara hii wamepata fursa ya kuja Zanzibar kwa kufanya uchunguzi wa afya ya kinywa na meno ili kujua wale wagonjwa  ambao wanamatatizo na kuwapatia tiba pamoja na kuwapa elimu ya afya .

Alisema Chama hicho kinahimiza umuhimu wa afya bora kwa jamii na kutoa ushauri wa maradhi mbalimbali ikiwemo ukimwi ,saratani ,Kifua kikuu,afya ya kinywa na meno pamoja na maradhi yasioambukiza kwa kuifanya jamii ipate uelewa na kujikinga na maradhi ambayo yanauwezo wa kuepukika .

“Hali ya idadi ya Wagonjwa ni kubwa wakati ya kuwa magonjwa haya yanakingika kwa haraka na kupona lakini kikwazo ni kuwa na uchache wa madaktari ,“alisema Dr Lorna .

Alifahamisha kila ifikapo tarehe 20 machi ya kila mwaka huadhimisha siku ya afya ya kinywa na meno kwa mwaka ujao wanatarajia uzinduzi wa zoezi hilo litafanyika Zanzibar .

Nae Mgonjwa BI Nargisi Uzia ambae alifika kupatiwa huduma ya matibabu katika kituo hicho alisema anaishukuru Serikali kwa kuwaletea wataalamu wa kuchunguza afya zao lakini pia iko haja ya zoezi hilo liwe endelevu kwani matatizo yako mengi yanahitaji uchunguzi.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dokt,Lorna Carneiro kulia akitoa hotuba ya makaribisho katikaUfunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.

Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil Abdalla akitoa hotuba ya Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Kinga na Elimu ya Afya katika Hospitali ya Mnazi mmoja Dkt,Fadhil Abdalla katikati akiwa katika picha ya pamoja na Madaktari kutoka Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).pamoja na madaktari wa Zanzibar katika Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.
Daktari wa Kinywa na Meno kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt,Ismail Amour akitoa Elimu ya kujikinga na maradhi hayo katika Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.


Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania Dokt,Lorna Carneiro kushoto akifanya mahojiano na Muandishi wa Habari kutoka ITV Farouk Kariym pamoja na muandishi wa Habari Maelezo Zanzibar Khadija Khamis katika Ufunguzi wa Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.

Daktari wa Kinywa na Meno kutoka Haspitali ya Arrahma Zanzibar akimfanyia Uchunguzi wa mardhi ya Kinywa na Meno Kauthar Vuai mkaazi wa meli nne, katika Zoezi la Uchunguzi wa Maradhi ya Kinywa na Meno katika Kituo cha Afya Rahaleo Mjini Unguja.Zoezi linalofanywa na Chama cha madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania(TDA).wakishirikiana na madaktari wa Zanzibar.PICHA NA YUSSUF SIMAI/MAELEZO ZANZIBAR.

Sunday, September 10

China katika mipango ya kupiga marufuku magari yanayotumia mafuta

Heavy air pollution above cars driving in BeijingHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionChina katika mipango ya kupiga marufuku magari yanayotumia mafuta
China ambaye ni nchi yenye soko kubwa zaidi la magari ina mipango ya kupiga marufuku uundaji na uuzaji wa magari yanayotumia mafuta ya diesel na petroli
Naibu waziri wa viwanda nchini humo alisema wameanaa utafiti lakini badoo hawajaamua ni lini marufuku hiyo itaanza kutekelezwa.
"Hatua hizo bila shaka zitalea mabadiliko makubwa katika sekta yetu ya magari," alisema Xin Guobin.
China iliunda magari milioni 28 mwaka uliopita, takriban thuluthi moja ya magari yote yaliyoundwa duniani.
Volvo car, Shanghai Auto ShowHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionKampuni ya kichina ya kuunda magari ya Volvo, ilisema mwezi Julai kuwa magari yake yatatumia umeme ifikapo mwaka 2019.
Uingereza na Ufaransa tayari wametangaza mipango ya kupiga marufuku magari mapya yanayotumia mafuta ya diesel na petroli ifikapo mwaka 2040 kama sehemu ya njia za kuzuia uchafuzi wa hewa.
Kampuni ya kichina ya kuunda magari ya Volvo, ilisema mwezi Julai kuwa magari yake yatatumia umeme ifikapo mwaka 2019.
Makampuni mengine duniani yakiwemo Renault-Nissan, Ford na General Motors yote yanashughulikia mipango ya kuunda magari yanayotumia umeme.

Amnesty:Burma yatega mabomu ya ardhini kuwazuia Rohingya

Vikosi vya usalama BurmaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionVikosi vya usalama Burma vyasema vinapambana na wanamgambo
Amnesty International linasema lina ushahidi kuwa vikosi vya usalama Myanmar vimetega mabomu ya ardhini yaliopigwa marufuku katika mpaka na Bangladesh.
Hilo ni eneo ambako idadi kubwa ya waislamu wa Rohingya wanatoroka ghasia.
Shirika hilo la kimataifa la kutetea haki za binaadamu linasema raia wapatao watatu wamejeruhiwa kwa milipuko hiyo ya kutegwa ardhini katika wiki iliyopita, na inaarifiwa mwananmume mmoja aliuawa.
Watu walioshuhudia wameliambia shirika hilo kwamba waliwaona maafisa wa usalama wa Burma wakitega mabomu hayo.
Umoja wa mataifa unasema zaidi ya waislamu laki mbili na nusu wa Rohingya wametoroka Myanmar tangu jeshi lianze operesheni dhidi ya wanamgambo huko wiki mbili zilizopita.
Shirika la Umoja wa mataifa linalowashughulikia wakimbizi UNHCR linasema idadi hiyo imeongezeka baada ya ukaguzi wa kina wa maeneo ambayo awali hayakujumuishwa katika hesabu.
Waislamu wengi wa Rohingya wametembea kwa siku kadhaa wakipitia jangwani na milimani .
Baadhi wamepanda maboti wakivuka bahari ya Bengal.

Wapiganaji wa Rohingya watangaza kusitisha mapigano, Myanmar

Wa Rohingya wanaishutumu jeshi la Myanmar kwa kuteketeza vijiji vyao - Lakini utawala nchini Myanmar, unasema wanajeshi wake wanakabiliana na "magaidi"Haki miliki ya pichaEPA
Image captionWa Rohingya wanaishutumu jeshi la Myanmar kwa kuteketeza vijiji vyao - Lakini utawala nchini Myanmar, unasema wanajeshi wake wanakabiliana na "magaidi"
Katika taarifa nyingine Asubuhi hii ya leo, waasi wa kiislamu wa kabila la Rohingya nchini Myanmar wametangaza upande mmoja makubaliano ya kusitisha mapigano leo Jumapili, ili kujaribu kupunguza mgogoro wa kibinadamu magharibi mwa taifa hilo.
Mashambulio dhidi ya jeshi la taifa hilo yanayotekelezwa wapiganaji wa Arakan Rohingya Salvation Army, yalisababisha mapigano makali ya wiki mbili, ambapo zaidi ya watu laki tatu wa jamii ndogo ya Warohingya wamekimbilia nchi jirani la Bangladesh.
Image caption
Kundi hilo la waasi, yameiomba jeshi la nchi hiyo pia kuitisha wito wa kusitisha mapigano, huku likiomba mashirika ya utoaaji misaada ya kibinadamu kurejelea kazi zao za kusambaza misaada.
Waziri mmoja wa serikali ya Myanmar ameiambia BBC kuwa, wengi wa Wa-Rohingya waliokimbia nchi hiyo na kuelekea Bangladesh, hawataruhusiwa kamwe kurejea Myanmar.

Mugabe aagiza usajili mpya wa wapiga kura Zimbabwe

MugabeHaki miliki ya pichaREUTERS
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameagiza usajili mpya wa wapiga kura wakati nchi hiyo inajitayarisha kwa uchaguzi mkuu mwaka ujao.
Chini ya agizo jipya la serikali, raia wote Zimbabwe watakuwana miezi minne kujisajili upya katika daftari la usajili.
Zimbabwe itafanya uchaguzi mkuu mwaka ujao kwa kutumia dafatri hiyo mpya ya usajili wa wapiga kura , ikiwa ni mojawapo tu ya mageuzi ya uchaguzi yalioitishwa na upinzani kwa muda mrefu.
Agizo hilo la rais linasema usajili unapaswa kuanza September 14 hadi Januari mwaka ujao.
Mfumo huu mpya unaidhinishwa kwa kutumia vifaa vilivyonunuliwa hivi karibuni kutoka China.
Usajili utajumuisha kunakiliwa alama za vidole na ithibati ya ukaazi.
Dafatari hilo la usajili limekumbwa na mzozo katika uchaguzi wa siku za nyuma Zimbabwe.
Mnamo 2008 vyama vya upinzani vilisema waligundua makosa ikiwemo kusajiliwa kwa wapiga kura wengi waliokuwa wanasemekana kuishi katika eneo moja, na wengine katika maenoe yasioishi watu.

Miili iliyohifadhiwa kwenye kaburi karne ya 16 yagunduliwa Misri

An Egyptian antiquities worker works on a coffin in the recently discovered tomb of Amenemhat, a goldsmith from the New Kingdom, at the Draa Abu-el Naga necropolis near the Nile city of LuxorHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMiili iliyohifadhiwa kaburini karne ya 16 yagunduliwa Misri
Wana akiolojia wamegundua kaburi lenye miili ya mwanmke na watoto wake waliokuwa wamehifadhiwa karne kadhaa zilizopita.
Kaburi hilo linaloaminika kuwa la karne ya 16 hadi 11 BC lilipatikana karibu na mji wa Luxor kilomita 70 kutoka Cairo.
Kati ya vifaa vilivyo patikana ndani ya kaburi hilo ni sanamu ya mfua viuma Amenemhat akiketi kando na mke wake.
Egyptian archaeologists work on mummies at a recently discovered tomb in the Draa Abul Nagaa necropolis, Luxor's West Bank, 700km south of Cairo, Egypt, 9 September 2017Haki miliki ya pichaEPA
Image captionKaburi lilipatikana eneo la Draa Abul Naga
Kulingana na wana akiolojia mama alifariki akiwa na miaka 50, na uchunguzi ulionyesha kuwa alifariki kutoka na ugonjwa wa mifupa.
Watoto wawili wa kiume walikuwa na umri wa kati ya miaka 20 na 30 na walikuwa wamehifadhiwa katika hali nzuri,
Skulls and hands are seen next to coffin in the recently discovered tomb of Amenemhat, a goldsmith from the New Kingdom, at the Draa Abu-el Naga necropolisHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMiili hiyo ilitajwa kuwa katika hali nzuri
A carved sandstone statue depicting the tomb's owner Amenemhat sitting on a high back chair beside his wife at a recently discovered tomb in the Draa Abul Nagaa necropolis, Luxor's West Bank, 700km south of Cairo,Haki miliki ya pichaEPA
Image captionKati ya vifaa vilivyo patikana ndani ya kaburi hilo ni sanamu ya mfua viuma Amenemhat akiketi kando na mke wake.
Egyptian antiquities worker brushes a coffin in a recently discovered tomb of Amenemhat, a goldsmith from the New Kingdom at the Draa Abu-el NagaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMiili iliyohifadhiwa kaburini karne ya 16 yagunduliwa Misri