Thursday, August 24

RAIS DKT MAGUFULI AMUAPISHA NAIBU KAMISHNA MKUU WA TAKUKURU IKULU DAR ES SALAA LEO


 Brigedia Jenerali John Julius Mbungo aliyeapishwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi  Brigedia Jenerali John Julius Mbungo baada ya kumuapisha kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Brigedia Jenerali John Julius Mbungo akila kiapo cha maadili ya Viongozi wa serikali baada ya kumuapisha kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Brigedia Jenerali John Julius Mbungo wakati akiongea machache  baada ya kumuapisha kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipeana mikono na Brigedia Jenerali John Julius Mbungo baada ya kuongea machache  baada ya kumuapisha kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Mhe. Angela Kairuki  baada ya kuongea machache  baada ya kumuapisha  kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Mwenyekiti wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela baada ya kumuapisha Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsikiliza  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Takukuru Bw. Alex Mfungo akiongea machache  baada ya kuapishwa kwa  Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea machache baada ya kumuapisha Brigedia Jenerali John Julius Mbungo kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan,  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Mhe. Angela Kairuki, Waziri wa sheria na Katiba Profesa palamagamba Kabudi, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. George Masaju, katibu Mkuu Kiongozi Balozi  John Kijazi, wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama pamoja na Brigedia Jenerali John Julius Mbungo baada ya kuapishwa kuwa Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Ikulu jijini Dar es salaam leo.

PICHA NA IKULU

Utumishi


Katibu Msaidizi wa Sekretarieti ya ajira kwa utumishi wa umma Bw. Malimi Muya akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani ) mapema leo Jijini Dar es Salaam kuhusu upatikanaji wa fursa za ajira kwa walemavu kulia ni Mkuu wa kitengo cha mawasiliano katika sekta hiyo Bi.Riziki Abrahamu
Picha Na Paschal Dotto-MAELEZO

Na. Georgina Misama, Agness Moshi - MAELEZO
Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Sekretariati ya Ajira Katika Utumishi wa Umma imewashauri walemavu kuchangamkia fursa za ajira zinazotolewa Serikalini kwani ni haki yao ya msingi kama ilivyo kwa watanzania wengine.

Akiongea na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Msemaji wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi Wa Umma Riziki Abraham amesema Serikali inawahamasisha walemavu kuchangamkia fursa za ajira zinazotangazwa na Ofisi hiyo kwa sababu ni wachache wanaojitokeza.

“Mwamko wa walemavu katika uombaji wa ajira ni mdogo, ninawahamaisha kutuma maombi yao endapo wametimiza vigezo bila kuogopa changamoto zinazowakabili kwa sababu mchakato wote wa ajira unafanywa kwa kufuata kanuni na Sheria za Nchi ambayo inampa kila mtu haki ya kupata ajira”,Alisema Riziki.

Sheria namba 9  ya Ajira ya mwaka 2010 inasema “ Mwajiri yoyote awe wa Umma au Binafsi mwenye waajiriwa kuanzia 20 na kuendelea lazima asilimia 3 ya waajiriwa hao iwe kwa ajili ya watu wenye ulemavu” hii  inaonyesha kuwa walemavu wana haki ya kuajiriwa mahali popote.

Bi.Riziki amesema ni vyema walemavu kuzitaja changamoto zao kweye fomu za maombi ili Ofisi iweze kuwaandalia mazingira rafiki kwa ajili ya mchakato mzima wa upatikanaji wa ajira na baada ya kupata ajira waweze kupangiwa sehemu ambazo hazitakua changamoto kwao.

Aidha Serikali inawapa kipaumbele walemavu kuanzia wakati mchakato wa usajili hadi wakati wa kupanga ajira hivyo basi walemavu wenye vigezo vilivyoanishwa kwenye matangazo ya ajira wajitokeze kutuma maombi ya nafasi hizo.

Naye, Katibu Msaadizi wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi Wa Umma Malimi Muya amesema kuwa Walemavu wanahaki kisheria hivyo waachane na mawazo ya kudhani wakitaja changamoto zao kwenye maombi hawatapatiwa nafasi.

“Serikali yetu haina ubaguzi kwenye utoaji ajira ukiwa na vigezo tutakuchukua, kuna upendeleo tunawapa walemavu kulingana na changamoto zao kama vile kuwaongezea muda wakati wa usaili, kuwatafutia wataalam wa mawasiliano na kuwaandalia mazingira rafiki wakati wa usaili kwa kuzingatia changamoto zao”, alisema Malimi.

Aidha Bw.Muya ameongeza kuwa Serikali inatambua nafasi ya Walemavu katika kuchangia maendeleo ya Nchi na ina wahamasisha kutumia fursa mbalimbali zinazojitokeza ili kujikwamua kiuchumi.

Ofisi ya Rais, Sekretariati ya Ajira Katika Utumishi wa Umma ina jukumu la msingi la kuendesha mchakato wa ajira kwa niaba ya waajiri mbalimbali na hatimaye kuwapangia vituo vya kazi wanaofaulu usaili.

ZIARA YA RAIS DK.SHEIN WILAYA YA MKOANI PEMBA


 Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Chokocho Nd,Abdalla Mohamed Abdalla akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(katikati) alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Sekondari ya Chokocho leo kufungua  Jengo la  madarasa manne na Chumba cha Maabara leo akiwa katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo Mkoa wa Kusini Pemba (kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma
  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akisalimiana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd.Khadija Bakari Juma alipowasili katika viwanja vya Skuli ya Sekondari ya Chokocho leo kufungua  Jengo la  madarasa manne na Chumba cha Maabara  akiwa katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo Mkoa wa Kusini Pemba.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(wa pili kushoto) alipokuwa akifungua pazia kuashiria ufunguzi wa Jengo la Skuli ya Sekondari ya Chokocho Wilaya ya Mkoani lenye madarasa manne na Chumba cha Maabara leo akiwa katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo Mkoa wa Kusini Pemba (kushoto) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipoku wa akikata utepe kama ishara ufunguzi wa Jengo la Skuli ya Sekondari ya Chokocho Wilaya ya Mkoani lenye madarasa manne na Chumba cha Maabara leo akiwa katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo Mkoa wa Kusini Pemba.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipoku wa akiuliza suala na kutoa maelekezo kwa Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari ya Chokocho Maalim Abdalla Mohamed Abdalla (kushoto) wakati alipoikagua maabara katika skuli hiyobaada ya kuifungua rasmi pamoja na madarasa manne ya kusomea (kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma,Rais akiwa katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba.
  Pichani ni jengo la Skuli ya Sekondari ya Chokocho lililofunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa katika ziara yake ya Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba,kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo katika Wilaya hiyo.
Baadhi ya Wananchi wa Kijiji cha Chokocho Wilaya ya Mkoani wakimsikiliza Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma alipokuwa akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) ili kuzungumza na Wazee,Wananchi hao pamoja na Walimu katika uzinduzi wa jengo la madarasa manne (4) na Chumba cha maabara leo katika Skuli ya Sekondari ya Chokocho  akiwa katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo Mkoa wa Kusini Pemba.
 Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma alipokuwa akimakaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(hayupo pichani) ili kuzungumza na Wazee,Wananchi na Walimu katika uzinduzi wa jengo la madarasa manne (4) na Chumba cha maabara leo katika Skuli ya Sekondari ya Chokocho Wilaya ya Mkoani akiwa katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo Mkoa wa Kusini Pemba leo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein(kulia) alipokuwa akizungumz na Wazee,Wananchi na Walimu katika uzinduzi wa jengo la madarasa manne (4) na Chumba cha maabara katika Skuli ya Sekondari ya Chokocho Wilaya ya Mkoani leo akiwa katika ziara ya kukagua na kutembelea Miradi mbali mbali ya Maendeleo Mkoa wa Kusini Pemba leo.
[Picha na Ikulu.] 24/08/2017.

Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai


 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akizungumza na Rais wa Umoja wa Mabunge ya Afrika ambaye pia ni Spika wa Bunge la Guine-Bissau Mheshimiwa Cipriano Cassama Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam. Spika huyo wa Guine-Bissau alitembelea Mhe Ndugai kwa lengo la kumpa mwaliko wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania wa kujiunga na Umoja wa Mabunge ya Africa (African Parliamentary Union). Kushoto ni Katibu Mkuu wa Umoja huo Mheshimiwa N’ZI Koffi.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akipokea mwaliko wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa  Tanzania wa kujiunga na Umoja wa Mabunge ya Africa (African Parliamentary Union) kutoka kwa  Rais wa Umoja huo ambaye pia ni Spika wa Bunge la Guine-Bissau Mheshimiwa Cipriano Cassama Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam anayeshuhudia kushoto  ni Katibu Mkuu wa Umoja huo Mheshimiwa.  N’ZI Koffi.

  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai akimueleza jambo na Rais wa Umoja wa Mabunge ya Africa (African Parliamentary Union) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Guine-Bissau Mheshimiwa Cipriano Cassama Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam mara baada ya kupokea mwaliko wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa kujiunga na Umoja huo.
 Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (katikati) katika picha ya pamoja na Rais wa Umoja wa Mabunge ya Africa (African Parliamentary Union) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Guine-Bissau Mheshimiwa Cipriano Cassama (kushoto) na  Katibu Mkuu wa Umoja huo Mheshimiwa.  N’ZI Koffi (kulia).


 Rais wa Umoja wa Mabunge ya Africa (African Parliamentary Union) ambaye pia ni Spika wa Bunge la Guine-Bissau Mheshimiwa Cipriano Cassama (kushoto) akimkabidhi zawadi  Spika wa Bunge Mhe Job Ndugai (kulia) mara baada ya mazungumzo Ofisi Ndogo za Bunge Jijini Dar es Salaam. Picha na Ofisi ya Bunge

Watumishi wa umma Zanzibar wapigwa msasa kutekeleza Mipango ya Serikali.




Watumishi wa umma Zanzibar wapigwa msasa kutekeleza Mipango ya Serikali.

Taasisi za Umma zimeshauriwa kujikita zaidi katika utekelezaji wa mipango iliyojiwekea badala ya kutumia muda mwingi kupanga mipango isiyotekelezwa.
Ushauri huo umetolewa leo kwenye warsha ya kuwajengea uwezo watendaji wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kuingiza Mpango kazi wa utelezaji wa APRM kwenye mipango ya maendeleo ya nchi kama vile Dira ya Zanzibar 2020, MKUZA III na Mipango ya Matumizi ya Muda wa Kati. 

Warsha hiyo ya siku mbili imeandaliwa na APRM Tanzania na inafanyika katika Hoteli ya Golden Tulip mjini Zanzibar tarehe 24 na 25 Agosti 2017.
Mgeni Rasmi kwenye warsha hiyo, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Kubingwa Mashaka Simba ambaye alimwakilisha Waziri wa Wizara hiyo, Mhe. Haroun Ali Suleiman aliwahakikishia washiriki kuwa Serikali ya Zanzibar imejipanga vema kutekeleza changamoto zote zilizobainishwa kwenye ripoti ya APRM iliyowasilishwa rasmi kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan mwanzoni mwa mwezi Agosti 2017.
Bw. Simba alieleza kuwa tayari Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ilishachukua hatua za kuimarisha Utawala Bora ikiwemo kuunda taasisi za kusimamia suala hilo ambazo baadhi yao ni Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Tume ya Kupambana na Rushwa pamoja na ugatuzi wa madaraka.
Wadau wanaoshiriki warsha hiyo walibainisha kuwa changamoto kubwa katika taasisi za umma ni utekelezaji wa mipango iliyowekwa, Hivyo kuna umuhimu wa APRM kuangalia namna ya kujenga uwezo wa watumishi katika kutekeleza mipango ya Serikali kwa kuzingatia namna ya kupata rasilimali zinazohitajika na zenye uwezo wa kutekekeza mipango iliyopo pamoja na muda wa kutekeleza mipango hiyo.
Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa APRM, Tanzania, Bi. Rehema Twalibu alisema warsha hiyo ni muhimu kwa watumishi wa Serikali ya Zanzibar kwa kuwa itawapa uwezo wa kuandaa taarifa ya utekelezaji wa changamoto zilizoainishwa kwenye ripoti ya APRM iliyowasilishwa miaka mitano iliyopita kwa Wakuu wa Nchi zilizoridhia Mpango wa APRM. 

Taarifa ya utekelezaji itakayoandaliwa na Serikali ya Zanzibar itajumuishwa na taarifa ya Tanzania Bara ili kupata ripoti moja ambayo inatarajiwa kuwasilishwa na Mhe. Rais kwa Marais wenzake wanaounda APRM baadaye mwaka huu.
-->

-Mwisho-
 
Imetolewa na:
 
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
 
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki,
 
Zanzibar, 24 Agosti 2017


Katibu Mtendaji wa Mpango wa Afrika wa Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM) Tanzania, Bi. Rehema Twalib akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Bw. Kubingwa Mashaka Simba (hayupo pichani) kwenye ufunguzi wa Warsha ya kuunganisha mipango ya APRM na Mipango ya Serikali inayofanyika katika Hoteli ya Golden Tulip, mjini Zanzibar. 
Naibu Katibu Mkuu, Bw. Kubingwa Mashaka Simba akitoa hotuba kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora katika ufunguzi wa Warsha ya ya kuunganisha mipango ya APRM na Mipango ya Serikali
Sehemu ya viongozi waliohudhuria kwenye Warsha hiyo wakimsikiliza kwa makini Mhe. Simba.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar, Bw. HAji Kombo (katikati), wa kwanza kushoto ni Mratibu wa Utawala APRM, na kulia ni Amani A.M. Shein nao wakifuatilia kwa makini ufunguzi wa Warsha  hiyo.
Mjumbe wa Jopo la Watu Mashuhuri na Kiongozi wa Mchakato wa Tanzania toka APRM, Mhe. Bridget Mabandla naye akizungumza kwenye ufunguzi huo.
Sehemu ya washiriki wa ufunguzi huo wakisikiliza kwa makini.
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wa kwanza kulia ni Halima Salim Abdallah, na katikati ni Hamida Makame Juma.
Watumishi wa APRM Tanzania, Bi. Stella William (kushoto`) na Bi. Elizabeth Ngereza nao wasikiliza hotuba iliyokuwa ikiendelea kutolewa na mgeni rasmi (hayupo pichani).
Bw. Max Ochai kutoka (UNECA), akitoa mada ya kwanza mara baada ya kumalizika kwa zoezi la ufunguzi
Sehemu ya washiriki wakifuatilia kwa kumsikiliza Bw. Ochani (hayupo pichani) alipokuwa akiwasilisha mada ya kwanza.
Bw. Ochani akiendelea kutoa mada yake kwa washiriki
Picha ya pamoja mara baada ya kumaliza ufunguzi wa Warsha hiyo.

ZAIDI YA SH BILIONI 200 KUWANUFAISHA VIJANA NCHINI


Filbert Rweyemamu,Arusha

Benki ya Dunia imetoa Sh 200 Milioni ili kuwezesha miradi ya elimu na ujuzi kwa ajili ya kazi zinazoleta uzalishaji wenye tija pamoja na vituo viwili vya umahiri vya kikanda vitakavyofungua ajira kwa vijana mara baada ya kuhitimu elimu. 

Akizungumza katika uzinduzi wa miradi hiyo,Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako alisema kuwa miradi hiyo itasaidia kuongeza watu wenye ujuzi wa kati ambao watafanya kazi katika sekta za kilimo,utalii,ujenzi ,nishati na madini.

Alisema kuwa miradi iliyofadhiliwa ni pamoja na vituo vinne vya umahiri katika masuala ya utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu pia ipo miwili iliyochini ya taasisi ya Chuo Kikuu ya Nelson Mandela pamoja na vituo vingine viwili vilivyopo katika Chuo cha Kilimo cha Sokoine(Sua).

Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania,Malawi ,Burundi na Somalia, Bella Birds alisema kuwa uboreshwaji wa rasilimali watu kwa kuongeza ujuzi uliokosekana utasaidia taifa kufikia malengo yake ya kufikia uchumi wa viwanda.

Bella alisema inakadiriwa kuwa vijana milioni 1 huitimu katika vyuo na kuingia katika soko la ajira kila mwaka hivyo anatarajia kuwa nafasi za ajira kwa vijana hao zitatengenezwa na sekta binafsi iwapo zitashirikiana vyema na serikali .

Makamu wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela Karoli Njau alisema kuwa mradi huo utasimamiwa kwa makini ili kuhakikisha kuwa malengo yanafikiwa hususan katika vituo vya umahiri pamoja na mradi wa ujuzi.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye amesema kuwa kulikua na upungufu mkubwa wa watu wenye ujuzi nchini kutokukidhi mahitaji ya soko la ajira hivyo kulazimu waajiri kuajiri watu kutoka nje jambo linalogharimu fedha nyingi hivyo mradi huo utasaidia vijana 30,000 kupata ujuzi utakaokidhi mahitaji ya soko la ajira.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(wa pili kushoto) akiwasili katika taasisi ya Chuo cha Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela(NM-AIST) kuzindua mradi wa Vituo vya umahiri katika utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu pamoja na mradi wa kuongeza ujuzi kwa kazi za uzalishaji zinazoleta tija uliofadhiliwa na Benki ya Dunia,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo,Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya NM-AIST,Profesa David Mwakyusa na Makamu Mkuu wa taasisi hiyo,Profesa Karoli Njau .
Waziri wa Elimu ,Mafunzo na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako (wa pili kulia) akipata maelekezo juu ya utendaji wa Kituo hicho 
Waziri wa Elimu ,Mafunzo na Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akizindua mradi wa Vituo vya Umahiri katika utafiti wa kilimo na magonjwa ya binadamu kulia ni Mkurugenzi wa Benki ya Dunia kwa nchi za Tanzania,Malawi ,Burundi na Somalia Bella Bird. 

NEEMA YA UPATIKANAJI WA MAJI YA KUTOSHA DAR ES SALAAM


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda leo amefanya ziara ya ukaguzi wa Ujenzi wa Miundombinu ya Maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa Maji ya kutosha kwa Wakazi wa Dar es Salaam.

Katika ziara hiyo Makonda ametembelea Ujenzi wa Vituo vya Usambazaji wa Maji, Visima pamoja na maeneo yatakayojengwa mifumo ya kisasa ya kusafirisha na kutibu Maji taka.

Makonda amesema lengo la Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli ni kumtua Mama Ndoo kichwani na kuhakikisha huduma ya Maji inawafikia Wananchi wote.

Amesema kukamilika kwa miradi ya Ujenzi wa Vituo Vinne vikubwa vya usambazaji wa Maji vinavyojengwa maeneo ya Changanyikeni, Makongo, Wazo na Bunju*vitasaidia kuzalisha Maji ya kutosha na kutatua kero kwa Wananchi.

Katika ziara hiyo pia Makonda ametembelea Visima 10 ambavyo aliahidi kwenye Ziara ya Dar Mpya ambavyo Ujenzi wake umekamilika vikiwa na uwezo wa kuzalisha Lita 16,000 kwa kila kisima ambavyo vitahudumia wakazi wa Wilaya ya Ubungo.

Aidha Makonda ametembelea eneo la Jangwani ambapo 
kutajengwa Mfumo wa Maji taka utakaogharimu kiasi cha Bilion 200 na eneo la Kilongawima Mbezi Beach kunakojengwa mfumo wa Maji taka utakaogharimu kiasi cha Bilion 135 chini ya ufadhili wa Bank ya Dunia na Serikali ya Japan.

Hata hivyo amesema bado Serikali inaendelea kufanya jitiada za kuhakikisha Wakazi wa Wilaya ya Kigamboni na Temeke wanapata maji ya kutosha kupitia miradi mbalimbali inayoendelea.

Amewataka Wananchi ambao bado hawajaunganishwa na huduma ya Maji kufika Ofisi za DAWASCO ili waunganishiwe Maji bila malipo ambapo baada ya hapo watawekewa utaratibu wa malipo.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitazama  Ujenzi wa moja ya Vituo vya Usambazaji wa Maji, Visima pamoja na maeneo yatakayojengwa mifumo ya kisasa ya kusafirisha na kutibu Maji taka.
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitazama mambo ya kupitishia maji ikiwa ni pia sehemu ya miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akipewa maelezo mafupi juu ya muundo mzma mzima wa miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akitazama miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akishiriki kuchimba mtaro wa kupitisha bomba la maji ikiwa ni sehemu ya miundo mbinu ya maji ambayo kukamilika kwake kutaongeza wigo wa upatikanaji wa maji ya kutosha kwa wakazi wa jiji la Dar