Tuesday, November 21

Kenya yapiga marufuku matangazo ya moja kwa moja ya mikutano ya kisiasa

Polisi Kenya wawatawanya waandamanaji mjini Nairobi waliokuwa wanamsindikiza kiongozi wa upinzani Raila Odinga baada ya kurejea kutoka ziarani Marekani.
mamlaka ya mawasiliano ya Kenya, imetangaza kupigwa marufuku kwa upeperushaji wa matangazo ya moja kwa moja wa mikutano ya kisiasa, katika kile ilichokiita “kusaidiA kupunguza hali ya taharuki nchini.”
SIiku ya Jumapili polisi nchini humo walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliokuwa wanaandamana mjini Nairobi kupinga mauaji ya watu wanne yaliyotekelezwa jaJumamosi usiku katika mtaa mmoja wa mabanda mjini humo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, baadhi ya mitaa ya mji huo imekumbwa na hali ya taharuki tangu Ijumaa, wakati takriban watu watano waliuawa kufuatia makanbiliano kati ya polisi na wafuasi wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, ambaye alikuwa amerejea kutoka ziarani Marekani.
Polisi hata hivyo wamesema waliouawa ni wahalifu.
Haya yamejiri siku moja tu kabla ya mahakama ya juu ya Kenya kutoa uamuzi wake kufuatia kesi zilizowasilishwa kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa tarehe 26 mwezi jana.
Jaji mkuu David Maraga ametangaza kwamba uamuzi huo utatolewa saa tano asubuhui siku ya Jumatatu.

Trump aiweka Korea Kaskazini kwenye orodha wa wafadhili wa ugaidi

Rais Donald Trump wa Marekani ameiweka Korea Kaskazini kwenye orodha ya Mataifa yanayofadhili ugaidi, na kutishia kuimarisha zaidi vikwazo dhidi yake, lakini waziri wa mambo ya nje amesema bado diplomasia inayo nafasi.

UN Generalversammlung in New York | Donald Trump, Präsident USA (Getty Images/S. Platt)
Rais wa Marekani Donald Trump
Kwa tangazo hilo la Rais Trump, Korea ya Kaskazini imeongezwa kwenye orodha ya nchi ambazo Marekani inazichukulia kama wadhamini wa ugaidi duniani, ambayo tayari inazo Iran na Syria. Rais huyo amewashambulia tena watangulizi wake, akisema anayoyafanya leo yalipaswa kufanywa miaka mingi iliyopita.
Mbali na kuishutumu Korea Kaskazini kuendesha mpango haramu wa nyuklia na makombora, vile vile Donald Trump amesema nchi hiyo inaendesha mauaji nje ya ardhi yake, ingawa hakuna visa vya mauaji kama hayo vinavyojulikana kufanywa na serikali ya mjini Pyongyang, mbali na kile kilichomuuwa kaka wa kiongozi wa sasa Kim Jong-un.
Akitangaza uamuzi wake katika kikao cha baraza la mawaziri mjini Washington, Trump amesema baada ya mchakato mzima kukamilika, Korea Kaskazini itakabiliwa na vikwazo vikali kabisa. Amesema, ''Hatua hii inaongeza vikwazo na adhabu kwa Korea Kaskazini na watu wenye mafungamano na nchi hiyo, na itasaidia kuitenga kabisa nchi hiyo inayoongozwa na serikali ya wauaji, kama ambavyo mmekuwa mkisoma na wakati mwingine mkiandika.''
Trump ameongeza kwamba kuwa kuanzia Jumatano wizara ya mambo ya nje itatangaza vikwazo vya ziada, vikali kabisa dhidi ya Korea Kaskazini, na kwamba mchakato huo utadumu kwa wiki mbili.
Tillerson atofautiana na Trump
Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari baada ya tangazo la Rais Trump, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema Marekani bado ina matumaini kwamba mchanganyiko wa vikwazo na juhudi za kidiplomasia unaweza kutumiwa kumshawishi kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kuja kwenye meza ya mazungumzo kuhusu mpango wake wa nyuklia wenye utata.
Nordkorea Kim Jong Un Statement zu Trump und seine UN Rede (Reuters/KCNA)
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un, ambaye waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema vikwazo vimemziba mdomo
Tillerson amesema tayari wanazo taarifa kwamba vikwazo vya bidhaa za petroli ambavyo China imeikea Korea Kaskazini vimeanza kuporomosha mapato ya Korea Kaskazini. ''Ni kutokana na athari hizo kwamba nchi hiyo haijafanya tena uchokozi wake kwa muda wa siku 60 zilizopita,'' amesema Tillerson, akimaanisha Korea Kaskazini.
Hata hivyo, wachambuzi wanasema hatua hii ya Trump dhidi ya Korea Kaskazini ni ya kiishara tu, kwa tayari Marekani imeiwekea nchi hiyo vikwazo chungu nzima.
Korea ya Kaskazini imeizoea orodha hiyo
Hii sio mara ya kwanza Marekani kuiweka Korea Kaskazini katika kundi linalofadhili ugaidi. Nchi hiyo inayoongozwa kwa usiri mkubwa ilikuwa tayari kwenye orodha hiyo hadi mwaka 2008, wakati Rais George W Bush alipoiondoa kwenye orodha hiyo, ili kuweka shinikizo zaidi kwa nchi nyingine ambazo zilikuwa haziibani vya kutosha Korea Kaskazini.
Wataalamu wanaamini kuwa Korea Kaskazini kwamba katika muda wa miezi kadhaa, Korea Kaskazini itapata makombora ya masafa marefu yanayoweza kufyatuliwa kutoka bara moja na kutua bara jingine, yakiwa na uwezo kufanya mashambulizi dhidi ya Marekani. Ikulu ya Rais Donald Trump imesema kamwe haitairuhusu Korea Kaskazini kupata uwezo huo.

Mahakama yaamua Kenyatta ni Rais halali

Rais Uhuru Kenyatta
Mahakama ya Juu ya Kenya, Jumatatu imetoa uamuzi kuwa Rais Uhuru Kenyatta alichaguliwa kihalali katika zoezi la marudio ya uchaguzi wa urais uliyofanyika Oktoba 26.
Kenyatta alipata zaidi ya asilimia 98 ya kura katika uchaguzi uliosusiwa na Muungano wa Upinzani.
Majaji wote sita waliosikiliza kesi hiyo wameamua kwa kauli moja kwamba Kenyatta alichaguliwa kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini humo, IEBC, waliojitokeza kupiga kura walikuwa chini ya asilimia 39 ya Wakenya milioni 19.6 waliojiandikisha.
Mgombea wa upinzani, Raila Odinga, ambaye alijitoa kwenye kinyang'anyiro hicho, aliwataka wafuasi wake kususia uchaguzi huo, na waandamanaji waliwazuia maafisa wa tume ya uchaguzi kufungua vituo vya kupigia kura katika ngome za upinzani. Odinga alisema uchaguzi huo ulikuwa ni aibu.
Maombi ya walalamikaji watatu yaliwasilishwa kwenye mahakama hiyo, na yote yametupiliwa mbali.

Saturday, November 18

ZANU PF yamshinikiza Mugabe ajiuzulu

Chama tawala Zimbabwe ZANU PF kimemtaka Rais Robert Mugabe ajiuzulu. Gazeti la Herald limeandika kuwa matawi ya chama hicho katika majimbo yote10 yalikutana Ijumma na yamemtaka Mugabe na mke wake Grace wajiuzulu.

Simbabwe Harare Robert Mugabe (picture-alliance/AP Photo/B. Curtis)
Viongozi wa chama hicho wamesema watamshinikiza kiongozi huyo ambaye amekuwa madarakani tangu mwaka 1980 kuondolewa kutoka uongozi wa chama hicho ifikapo hapo kesho Jumapili, na baada ya hilo, bunge litapiga kura ya kutokuwa na imani naye.
Chama cha ZANU PF kitafanya mkutano maalamu wa kamati kuu siku ya Jumapili kujadili yanayojiri kisiasa nchini humo.
Mugabe alionekana kwa mara ya kwanza hadharani, katika mahafali ya chuo kikuu mjini Harare siku ya Ijumaa (17.11.2017) tangu jeshi lilipomuweka chini ya kifungo cha nyumbani wiki hii. Mkewe Grace hajaonekana hadharani tangu jeshi lilipochukua madaraka.
Jeshi la Zimbabwe linapata ugumu wa kuonyesha heshima kwa kiongozi huyo mwenye umri wa miaka 93 kwa kumuita rais na kamanda mkuu wa jeshi.
Madaraka mikononi mwa Jeshi
Taarifa kutoka kwa jeshi hilo imesema kuwa viongozi wake wanashauriana na Kamanda Mkuu wa jeshi Rais Robert Mugabe kuhusu njia bora ya kusonga mbele na litalifahamisha taifa baadaye kuhusu matokeo hayo haraka iwezekanavyo.
President Robert Mugabe poses with General Constantino Chiwenga at State House in Harare (Reuters/Zimpapers/J. Nyadzayo)
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe na mkuu wa majeshi Constantino Chiwenga
Kituo cha televisheni cha serikali ZBC kimeripoti kuhusu kuendelea kwa shinikizo kutoka kwa wanachama wa ZANU PF kwa Mugabe kujiuzulu. ZBC imekuwa ikitumika na serikali ya Mugabe kwa miongo kadhaa kueneza propaganda.
ZANU PF pia imeitisha maandamano Jumamosi (18.11.2017) katika mji mkuu, Harare kuliunga mkono jeshi kwa kuchukua madaraka na kumshinikiza Mugabe ajiuzulu. Gazeti la Herald limeripoti kuwa chama hicho kinataka makamu wa Rais aliyefutwa kazi Emmerson Mnangagwa arejeshwe katika wadhifa huo kwasababu alifutwa kazi bila ya ridhaa ya kamati kuu ya chama hicho.
Wazimbawe wengi wanahisi mipango ya jeshi ni kumkabidhi Mnangagwa madaraka. Huenda viongozi wa kijeshi wanasubiri Mnangagwa ambaye anajulikana kwa jina maarufu kama mamba arejeshwe katika wadhifa wa makamu wa rais kabla ya kumshinikiza Mugabe kuondoka madarakani kwa njia ya amani.
Mugabe anaheshimika sana kama kiongozi aliyepigania uhuru lakini pia wengi wanamuona kama Rais aliyeivuruga nchi yake kwa kusalia madarakani kwa muda mrefu.
Mugabe ameiongoza Zimbabwe tangu 1980
Uchumi wa nchi hiyo umeporomoka vibaya, visa vya ufisadi, usimamizi mbaya, azma ya mke wake Grace kutaka kurithi madaraka na umri wake kuwa mkubwa ni mambo yanayowafanya Wazimbabwe kuhisi hana uwezo tena wa kuliongoza taifa hilo.
Zimbabwe Mugabe Rally (picture-alliance/AP Photo/T.Mukwazhi)
Mugabe na mke wake Grace
Rais wa Botswana Ian Khama amemtaka ajiuzulu akisema hadhani kama kuna mtu yeyote anayestahili kuwa madarakani kwa muda mrefu kama Mugabe akiongeza wao ni marais na sio wafalme.
Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma ambaye aliongoza kikao cha viongozi wa jumuiya ya ushirikiano wa maendeleo wa nchi za Kusini mwa Afrika SADC mjini Gaberone, Botswana amesema wanafuatilia kwa wasi wasi mkubwa matukio ya kisiasa yanayojiri Zimbabwe na anatumai hayatasababisha kuingia madarakani kwa utawala usiotambulika kikatiba.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson aliwaambia mawaziri wa mambo ya nje wa nchi za Afrika wanaohudhuria mkutano mjini Washington kuwa anahimiza kurejea haraka kwa utawala wa kiraia Zimbabwe akisema nchi hiyo ina fursa ya kuanzisha njia mpya ambayo sharti ihusishe chaguzi zinazoendeshwa kwa njia ya kidemokrasia na kuheshimu haki za binadamu. China imesema inatumai kuwa hali ya kisiasa inayoendelea Zimbabwe itasuluhishwa kuambatana na sheria na uthabiti uterejea nchini humo.

Fedha na mgawanyiko vyakwamisha COP23

Mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya tabianchi unaojulikana kama COP23, umekamilika rasmi jana mjini Bonn, Ujerumani, baada ya wajumbe kukutana kwa muda wa wiki mbili.

COP23 in Bonn - PK Bangladesch (DW)
Wajumbe wa mkutano huo wamekuwa wakifanya vikao mbalimbali vya kutunga sheria zitakazotumiwa katika utekelezwaji wa Mkataba wa Paris, unaonuia kupunguza ongezeko la joto duniani.
Mazungumzo hayo yaliyotakiwa kumalizika jana mchana, yaliendelea hadi saa sita usiku kwa saa za Afrika Mashariki, huku mjumbe mkuu wa China, Xie Zhenhua akisema kwamba kuna masuala mengi ambayo bado yanapaswa kujadiliwa. Wajumbe wa mkutano huo wamesema mazungumzo yamekwama hasa katika masuala makuu mawili likiwemo kuhusu fedha pamoja na kuibuka tena mgawanyiko kati ya mataifa tajiri na yale yanayoendelea.
Mataifa maskini duniani ambayo ndiyo yanayokumbwa zaidi na madhara yatokanayo na mabadiliko ya tabianchi, yanahitaji fedha ili kujiimarisha zaidi katika kujiandaa na kujilinda na athari mbaya za mabadiliko ya tabianchi.
COP23 | Kaliforniens Governeur Jerry Brown (Getty Images/Lukas Schulze)
Gavana wa Marekani, Jerry Brown
Mataifa hayo yanataka uhakika na uwazi zaidi kutoka katika mataifa tajiri kuhusu maendeleo yaliyopatikana ili kutimiza ahadi yao ya kuchangia hadi Dola bilioni 100 kwa mwaka ifikapo mwaka 2020, kama sehemu ya mkataba wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchini.
Marekani chini ya Utawala wa Rais Donald Trump ambayo pia imepunguza ufadhili katika taasisi na miradi inayohusiana na mabadiliko ya tabianchi, imekuwa na misimamo mkali kawenye majadiliano ya kifedha, hatua iliyowakasirisha wajumbe wengi. Mjumbe wa ngazi ya juu wa Ulaya, Jens Mattias Clausen amesema serikali ya Trump ilishindwa kuzuia mazungumzo hayo yasifanyike, lakini hatua hiyo inaweza ikawa imechelewesha mambo. Amesema dunia inahitaji kuchukua hatua haraka.
Mazungumzo yamepiga hatua
Muda mchache kabla ya kumalizika kwa mkutano huo, Waziri Mkuu wa Fiji, Frank Bainimarama amewaambia wanadiplomasia kwamba wanapiga hatua nzuri kuhusu mkataba wa Paris na wataikamilisha kazi hiyo kwa wakati. Bainimarama ambaye aliongoza mazungumzo hayo, alikabiliwa na changamoto ngumu ya kuzipatanisha pande zinazopingana za nchi tajiri na maskini, hasa linapokuja suala la kila upande kufanya juhudi katika kuzuia mabadiliko ya tabianchi.
Wajumbe kutoka karibu nchi 200, wakiwemo wa Marekani, walikusanyika kuandaa sheria muhimu zitakazoidhinishwa mwaka ujao wa 2018 mjini Katowice, Poland kwa ajili ya kuutekeleza Mkataba wa mabadiliko ya tabianchi uliofikiwa mjini Paris, Ufaransa mwaka 2015 na ambao unatarajiwa kuanza rasmi katika muda wa miaka mitatu ijayo.
UN-Klimakonferenz 2017 in Bonn | Angela Merkel, Bundeskanzlerin (Reuters/W. Rattay)
Kansela Angela Merkel akihutubia mkutano wa COP23
Nchi zilizosaini mkataba wa Paris zinataka kupunguza ongezeko la joto duniani hadi chini ya nyuzi joto 2 za Celsius ifikapo mwishoni mwa karne. Lengo hilo halitafanikiwa mpaka nchi hizo zifanye juhudi zaidi katika kupunguza hewa chafu ya carbon inayosababishwa hasa na matumizi ya nishati inayotokanayo na vitu asilia.
Ujerumani kwa upande wake inalenga kupunguza matumizi ya gesi inayochafua mazingira kwa asilimia 40 ifikapo mwaka 2020. Serikali iliamua kuhusu namba hiyo miaka 10 iliyopita, lakini inaonekana kama mpango huo utashindikana. Kulingana na utabiri wa sasa uliotolewa na wizara ya Mazingira ya Ujerumani, nchi hiyo itakuwa na uwezo wa kupunguza matumizi ya gesi hiyo kwa asilimia 34.7 ifikapo mwka 2020.
Desemba 12 mwaka huu, Rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron amewaalika zaidi ya viongozi 100 mjini Paris kuadhimisha miaka miwili tangu ulipofikiwa mkataba wa Paris. Trump anayetaka kujiondoa kwenye mkataba huo, hajaalikwa katika mkutano huo wa kilele uliopewa jina ''One Planet''.

Hariri afunguka kuhusu ziara yake Saudia

Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri akiwa na Mrithi wa Ufalme nchini Saudi Arabia Mohammed bin Salman.
Waziri Mkuu wa Lebanon Saad Hariri amesema Ijumaa amekuwa Saudi Arabia, ambako alikuwa katika mazungumzo yanayohusu mustakbali wa eneo hilo.
Vyanzo vya habari vimeripoti Hariri aliushitua ulimwengu kwa kutangaza kujiuzulu kwake akiwa nje ya nchi yake.
“Kuwepo kwangu Saudi Arabia ni kwa ajili ya kufanya mashauriano juu ya mustakbali wa Lebanon na mahusiano yake na nchi jirani za Kiarabu,” aliandika katika akaunti yake ya Twitter kabla ya kuanza safari yake kuelekea Ufaransa.
Hariri aliongeza kuwa taarifa nyingine zozote kuhusu uwepo wake Riyadh, kuondoka kwake Lebanon au kuhusu familia yake ni “uzushi”.
Hariri amekuwako nchini Saudi Arabia tangu alipotangaza kujiuzulu mapema mwezi huu, akiibua maswali kuhusu ukweli juu ya kushikiliwa kwake Saudia na kupelekea Rais wa Lebanon Michel Aoun kutangaza kuwa anazuiliwa na utawala huo.
Aoun amesema hatakubali kupokea rasmi kujiuzulu kwa Hariri mpaka atapofika Lebanon.
Waziri wa Mambo ya Nje Adel al- Jubeir Alhamisi alitupilia mbalia madai yasiyo na msingi kuwa Saudi Arabia ilikuwa inamshikilia Hariri na ni juu ya Hariri mwenye kuamua wakati gani anataka kuondoka.
Hariri amekubali mualiko wa Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron kwenda Ufaransa katika siku zijazo.

Tillerson ahimiza utawala wa kiraia Zimbabwe

Rais Robert Mugabe akiwa na Jenerali Constantino Chiwenga ikulu mjini Harare, Zimbabwe, Novemba 16, 2017.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Rex Tillerson ametoa wito Ijumaa Zimbabwe kurejea katika utawala wa kiraia.
Shirika la habari la AP limeripoti kuwa Tillerson amesema Zimbabwe bado inayofursa ya kuanza "utaratibu mpya" wakati kuna dalili kuwa uongozi wa mabavu wa Robert Mugabe utalazimishwa kuachia madaraka katika mapinduzi yaliyofanyika bila ya kumwaga damu.
"Sisi sote lazima tushirikiane ili kurejesha kwa haraka utawala wa kiraia katika nchi hiyo kwa mujibu wa katiba, Tillerson aliuambia mkusanyiko wa mawaziri wa mambo ya nje na wanadiplomasia waliokusanyika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani.
Amesema ni lazima Zimbabwe ifanye uchaguzi uliyo huru na haki. Mugabe alishinda katika chaguzi zilizopita ambazo wasimamizi waliokuwepo wakati wa uchaguzi huo waligundua kuwa ulivurugwa.
“Mwisho wa yote wananchi wa Zimbabwe ni lazima wapewe fursa ya kuchagua serikali yao,” aliongeza
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ameonekana Ijumaa hadharani kwa mara ya kwanza leo Ijumaa, tangu jeshi la nchi hiyo kumzuilia nyumbani kwake siku ya Jumatano, kuchukua udhibiti wa taasisi za serikali na kuanziisha mazungumzo yanayotarajiwa kumruhusu baba wa taifa kustahafu.
Kiongozi huyo mkongwe, akiwa amevaa kofia na mavazi ya rangi ya samawati na manjano, alihudhuria sherehe ya kuhitimu wanafunzi elfu moja katika chuo kikuu, mjini Harare, huku akishangiliwa na umati wa watu.
Wazimbabwe wanatumai kwamba mzozo wa kisiasa unaoikabili nchi hiyo utatatuliwa kwa haraka, huku viongozi wa upinzani, wanaharakati na viongozi wa kidini wakimtaka Mugabe kuondoka madarakani, baada ya jeshi kuchukua udhibiti wa serikali.
Hata hivyo, ripoti zilieleza kuwa Mugabe hajasalimu amri. Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma aliliambia bunge la nchi yake kwamba ni mapema mno kuchukua msimamo wowote kuhusiana na mzozo huo.

Sudan kukatiza mahusiano na Korea Kaskazini

Marekani imesema kwamba nchi ya Sudan itakata mahusiano yote ya kijeshi na kibiashara na Korea Kaskazini.

USA Heather Nauert (picture-alliance/AA/Y. Ozturk )
Ni hatua ambayo huenda ikawa ushindi mkubwa wa juhudi za utawala wa Trump za kulitenga taifa hilo la Asia  licha ya kuzidi kwa mvutano kufuatia majaribio ya silaha za nyuklia na makombora yanayofanywa na Korea Kaskazini.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje wa Marekani Heather Nauert alisema Sudan inachukua hatua hiyo kutokana na "tishio kubwa" linalotokana na mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini.
Alisema Marekani imekaribisha uamuzi huo, uliotangazwa baada ya ziara ya naibu waziri wa mambo ya nchi za kigeni John Sullivan mjini Khartoum.
Ziara hiyo ilikuja wakati Marekani na Sudan, zikihimizwa na Israeli na Saudi Arabia, wakielekea kuimarisha  mahusiano bora zaidi baada ya miongo kadhaa ya uadui.
"Kuitenga serikali ya Korea Kaskazini ni kipaumbele kwa Marekani, na ni kipengele muhimu cha kudumisha amani na utulivu duniani kote," Nauert alisema katika taarifa.
"Marekani inaishukuru Sudan kwa kutimiza ahadi ya kuchukua hatua hizi muhimu kwa sababu ya kitisho kikubwa kinachosababishwa na" Korea ya Kaskazini.”
Utawala wa Trump umekuwa ukizitia msukumo  nchi za kigeni kukata mahusiano ya kiuchumi, kidiplomasia na mengine na Korea Kaskazini katika jitihada za kuitenga nchi hiyo na kuirudisha kwenye meza ya majadiliano.
Katika wiki za hivi karibuni, utawala huo umekuwa ukiyalenga mataifa ya Kiafrika na Kusini mwa Asia na kadhaa wamekubaliana.
Sudan imekuwa mtazamo maalum wa juhudi hiyo kama sehemu ya jaribio la kuboresha uhusiano kati ya Marekani na Sudan, ambayo ilisababisha kuondolewa kwa baadhi ya vikwazo vya Marekani  dhidi ya Sudan.
Huku Korea ya Kaskazini ikiendelea kutengwa na mataifa ya magharibi, nayo imezidi kutafuta mahusiano na mataifa ya Afrika, Mashariki ya Kati na kusini mwa Asia ili kukusanya fedha zinazohitajika.
Nordkorea Kim Jong Un bei Besuch einer Fabrik fĂ¼r Nuklearwaffen (Reuters/KCNA)
Rais wa Korea Kaskazini Kim Jong Un akitoa mwelekeo kwenye mpango wa silaha za nyuklia
Barani Afrika, imeimarisha uhusiano wa kijeshi na kiuchumi na nchi kadhaa, ikiwa Sudan, Uganda na Angola, kwa kutoa mipango ya mafunzo ya kijeshi, ujenzi na miradi ya viwanda na usambazaji wa wafanyakazi wageni.
Mwezi uliopita, Uganda ilitangaza kuwa imewaondoa wataalam wa kijeshi wa Korea Kaskazini na wawakilishi wa makampuni ya ya Korea Kaskazini, ikiwa ni pamoja na muuzaji wake mkuu wa silaha, kama sehemu ya jitihada za kuzingatia vikwazo vipya vya umoja wa mataifa dhidi ya Korea Kaskazini.
Korea Kaskazini kwa miaka mingi imekuwa ikiwapa mafunzo wanajeshi wa  Uganda ,ya vita vya bahari na utunzaji wa silaha.
Moussa Faki Mahamat, mwenyekiti wa Halmashauri ya Umoja wa Afrika, alijibu tangazo la Sudan kwa kusema Umoja wa Afrika umeshutumu uenezaji  wa silaha za nyuklia katika bara hilo na mahali pengine.
"Maendeleo na utengenezaji wa silaha hizi inakuwa tishio la kweli kwa amani na usalama duniani," mkuu huyo wa AU alisema katika mahojiano na shirika la habari la  AP.
Tangazo hili la Alhamisi lilikuja kabla ya uamuzi uliotarajiwa hivi karibuni kwa Marekani  kuiorodhesha tena Korea ya Kaskazini kama "serikali inayodhamini ugaidi," jina ambalo liliondolewa na utawala wa Rais George W. Bush mnamo mwaka wa 2008 kwa kuwa ulitaka makubaliano ya kidiplomasia kuzuia mpango wa silaha za atomiki wa Korea kaskazini.
Sarah Huckabee Sanders (picture alliance/AP Images/P.M. Monsivais)
Msemaji wa ikulu ya White House Sarah Huckabee Sanders aliwaambia waandishi wa habari kwamba anatarajia uamuzi juu ya hali ya Korea Kaskazini kuamuliwa mapema wiki ijayo.
Sudan ni moja ya nchi tatu tu - nyingine ni Iran na Syria - ambazo kwa sasa zimeteuliwa wafadhili wa ugaidi na wizara ya nchi ya kigeni, jina linalobeba vikwazo vya uchumi na kifedha. Tangazo la Sudan kukata mahusiano na Korea ya Kaskazini kunaweza kusaidia kesi yake kuondolewa kutoka kwenye orodha hiyo.
Hata hivyo, afisa wa wizara ya mambo za kigeni alisema uwezekano wa mabadiliko ya uteuzi ya Sudan na Korea Kaskazini hauhusiani na kwamba ukaguzi wa nchi zote mbili unaendelea.
Afisa huyo, ambaye hakuwa na mamlaka ya kuzungumza jambo hilo kwa umma na aliyezungumza katika hali ya kutojulikana, alisema uamuzi juu ya Sudan unaweza kutegemea jinsi itakavyotelekeza ahadi yake ya kukata mahusiano na Korea Kaskazini.
Taarifa ya Nauert ilisema Marekani  "itaendelea kushirikiana juu ya suala hili ili kuhakikisha kuwa ahadi hii imetekelezwa kikamilifu."

Rais Mugabe amtunuku shahada mke wa Jenerali aliyemzuia

Rais wa Zimbabwe's Robert Mugabe amewatunuku shahada zaidi ya wanafunzi 3,300 katika chuo kikuu cha ZimbabweHaki miliki ya pichaEPA
Image captionRais wa Zimbabwe's Robert Mugabe amewatunuku shahada zaidi ya wanafunzi 3,300 katika chuo kikuu cha Zimbabwe
Rais wa Zimbabwe's Robert Mugabe amewatunuku shahada zaidi ya wanafunzi 3,300 katika chuo kikuu cha Zimbabwe, akiwemo mke wa jenerali aliyemzuia siku ya Jumatano.
Marry Chiwenga alipata shahada ya MBA kulingana na shirika la habari la Zimbabwe.
Awali Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameonekana hadharani kwa mara ya kwanza tangu jeshi la nchi hiyo lichukue madaraka siku ya Jumatano.
Alihudhuria sherehe za kuhitimu kwa mahafala kwenye mji mkuu Harare.
Bwana Mugabe amekuwa chini ya kuzuizi cha nyumbani kwa siku kadhaa huku kukiwa na mvutano kuhusu ni nani atamrithi.
Jeshi lilisema Ijumaa kuwa lilikuwa kwenye mazungumzo na Mugabe na litaujulisha umma kuhusu matokeo ya mazunngumoz hayo haraka iwezekanavyo.
Mtu moja aliyeshuhudia alinukuliwa na Reuters akisema kuwa Mugabe alishangiliwa wakati wa sherehe baada ya kuzungumza.
Jeshi lilichukua madaraka baada ya Mugabe kmfuta kazi makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa wiki iliyopita, na kuashiria kuwa alimpendelea mkewe kuweza kuchukua ungonizi wa Zanu-PF na urais.

Mwanajeshi wa Korea Kaskazini aliyetorokea K Kusini apatikana na minyoo mingi

Minyoo yapatikana ndani ya mwili wa mwanbajeshi wa Korea Kaskazini aliyetorokea Korea KusiniHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMinyoo yapatikana ndani ya mwili wa mwanbajeshi wa Korea Kaskazini aliyetorokea Korea Kusini
Mwanajeshi wa Korea Kusini aliyepigwa risasi alipokuwa akitorokea Korea Kusini katika mpaka wa mataifa hayo mawili amepatikana na vimelea vingi katika matumbo yake , kulingana na daktari wake.
Mtoro huyo alivuka eneo linalolindwa sana mpakani siku ya Jumatatu , lakini akapigwa risasi kadhaa na walinzi wa Korea Kaskazini.
Madaktari wanasema mwanajeshi huyo kwa sasa yuko katika hali nzuri , lakini idadi kubwa ya minyoo katika mwili wake unafanya hali yake kuwa mbaya.
Hali yake inaonyesha hali ya maisha yalivyo nchini Korea Kaskazini.
''Sijawahi kuona kitu kama hiki katika miaka yangu 20 kama daktari , daktari wa Korea Kusini Lee Cook-jong aliwaambia waandishi wa habari, akielezea kwamba kimelea mrefu katika tumbo lake alikuwa na urefu wa sentimita 27.
Mwanajeshi wa Korea Kaskazini akikimbizwa hospitalini Korea KusiniHaki miliki ya pichaEPA
Image captionMwanajeshi wa Korea Kaskazini akikimbizwa hospitalini Korea Kusini
Mwanadamu anaweza kupata vimelea kupitia kula chakula kichafu kwa kuumwa na wadudu ama vimela waliongia kupitia katika ngozi.
Kwa upande wa mwanajeshi huyo huenda vimelea hao waliingia kupitia chakula kichafu.
Korea Kaskazini inatumia kinyesi kama mbolea. Iwapo vinyesi hivyo havitibiwi na kutumiwa kama mbolea katika mboga ambayo haijapikwa ,vimelea hivyo vinaingia mdomoni hadi katika matumbo ya mwanadamu.

Pentagon yamtaka Trump kujiuzulu kimakosa

Ujumbe huo ambao pia uliwataka wanasiasa wengine wawili wa Marekani kujiuzulu kufuatia madai ya unyanyasaji wa kijinsia ulitumwa kutoka kwa akaunti ya @ProudResisterHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionUjumbe huo ambao pia uliwataka wanasiasa wengine wawili wa Marekani kujiuzulu kufuatia madai ya unyanyasaji wa kijinsia ulitumwa kutoka kwa akaunti ya @ProudResister
Ndio idara inayosimamia nambari za siri makombora, Idara inayosimamia usalama wa Marekani na mkuu wake ni rais wa Marekani ambaye hupendelea sana kutumia mtandao wa Twitter.
Lakini inapofikia wakati wa kusimamia akaunti yake ya mtandao huo, the Pentagon inafaa kuimarisha uwezo wake.
Siku ya Alhamisi idara hiyo ya ulinzi ilituma ujumbe kimakosa katika mtandao wake wa Twitter ukimtaka rais Trump kujiuzulu.
Ujumbe huo ambao pia uliwataka wanasiasa wengine wawili wa Marekani kujiuzulu kufuatia madai ya unyanyasaji wa kijinsia ulitumwa kutoka kwa akaunti ya @ProudResister, mwanaharakti ambaye ni mkosaji mkuu wa Trump.
Akaunti hiyo ilisema: Suluhu ni rahisi. Roy More jiuzulu katika kinyanganyiro. AI: Jiuzulu katika bunge la Congres, Donald Trump Jiuzulu katika urais. GOP: Wacha kulifanya swala la unyanyasaji wa kijinsia kuwa la kibinafsi.Ni uhalifu kama unafiki wao.
Ujumbe wa Trump uliosambazwa na akaunti ya idara ya ulinzi ya marekani kimakosaHaki miliki ya pichaTWITTER
Image captionUjumbe wa Trump uliosambazwa na akaunti ya idara ya ulinzi ya marekani kimakosa
Akaunti ya Idara hiyo ya ulinzi iliusambaza ujumbe huo kimakosa kwa takriban wafuasi wake milioni 5.2 kabla ya kuufuta.
Lakini makosa hayo yalionekana.
Picha ya ujumbe huo wa Pentagon lisambazwa na majibu yake pia yakawa ya haraka sana.

Rambo akana kumnyanyasa kingono shabiki wake mwenye umri wa miaka 16

Nyota wa filamu Sylvester StalloneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNyota wa filamu Sylvester Stallone
Nyota wa filamu Sylvester Stallone amekana ripoti kwamba yeye na mlinzi wake walimnyanyasa kingono shabiki wake wa miaka 16 mjini Las Vegas mapema miaka ya themanini.
Gazeti la mtandao la The Mail limechapisha kile linasema ni ripoti ya polisi kutoka 1986 ambayo ilielezea madai hayo.
Mwanamke huyo hakuwasilisha mashtaka dhidi ya Stallone kwa sababu alinyanyaswa na kuaibishwa mbali na kuwa na hofu.
Hakuna hatua iliochukuliwa.
Msemaji wa nyota huyo wa filamu ya Rocky alisema kuwa taarifa hiyo ilikuwa ya uwongo.
Michelle Bega aliyaelezea madai hayo kuwa ya uwongo, akiongezea : hakuna mtu aliyekuwa akijua kuhusu habari hiyo hadi ilipochapishwa leo, akiwemo bwana Stallone.
''Bwana Stallone hakuwasiliana na mtu yeyyote ama malaka ama mtu yeyote yule kuhusu swala hilo''.

Muswada kuwabana wenye nyumba waandaliwa


Dodoma. Serikali iko katika mchakato wa maandalizi ya muswada wa sheria ambayo itasimamia sekta ya nyumba, hivyo kuondoa changamoto ya wamiliki kudai kodi ya pango ya zaidi ya mwezi mmoja.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Angelina Mabula amesema hayo bungeni leo Ijumaa Novemba 17,2017 akijibu swali la nyongeza la mbunge wa Viti Maalumu (CCM), Halima Bulembo.
Halima katika swali lake amesema vijana ambao ni kati ya asilimia 56 na 60 nchini, wanashindwa kutimiza ndoto zao kutokana na gharama kubwa ya kodi ambayo hutakiwa kulipa kwa kipindi cha mwaka mmoja au miezi sita.
"Serikali inasemaje kuhusu kuleta sheria itakayofuta tabia ya wenye nyumba kulazimisha kulipwa kodi ya mwaka?" amehoji mbunge huyo.
Akijibu swali hilo, Mabula amesema Serikali imeliona tatizo hilo na ipo katika mchakato wa kuandaa muswada wa sheria utakaosimamia sekta hiyo.
Mabula amesema baada ya kukamilika kwa sheria ambayo itaunda chombo cha kusimamia sekta hiyo, wapangaji hawatalipa kodi ya mwaka wala miezi sita tena bali watalipa kwa mwezi na kuweka amana ya miezi mitatu.
Katika swali la msingi, Halima amesema kumekuwa na upandaji holela wa gharama za pango kwa nyumba za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC).
"Je Serikali haioni kuna haja ya kudhibiti upandaji holela ambao unaathiri wananchi wengi kutokana na kipato chao?" amehoji.
Akijibu, Mabula amesema utaratibu wa urekebishaji wa viwango vya kodi za shirika hilo husimamiwa na bodi ya wakurugenzi ambayo imepewa mamlaka ya kisheria ya kusimamia kodi ya pango na kuidhinisha viwango vya kodi vinavyotozwa kwa wapangaji wa nyumba za shirika.
"Kwa mara ya mwisho bodi ya wakurugenzi ya Shirika la Nyumba la Taifa iliidhinisha viwango vipya vya kutoza kodi kwenye nyumba za shirika mwaka 2011 ambavyo ndivyo vinavyotumika mpaka sasa," amesema.