Tundu Lissu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, Kenya baada ya kujeruhiwa kwa risasi.
Mbunge wa Baraza la Wawakilishi (CCM), Jaku Hashim Ayoub ameomba mwongozo wa Spika akitaka Bunge liteue wabunge wa kwenda kumuona mwenzao wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anayepata matibabu mjini Nairobi, Kenya baada ya kujeruhiwa kwa risasi.
Lissu alijeruhiwa Septemba 7 akiwa ndani ya gari nyumbani kwake Area D mjini hapa na alisafirishwa siku hiyohiyo kwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi. Awali, alipatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Akizungumza baada ya kipindi cha matangazo ya wageni bungeni leo Jumatatu, Jaku amesema Naibu Spika, Dk Tulia Ackson alifanya kitendo cha kibinadamu kuruhusu gari la ndugu zake limpeleke Lissu hospitali.
Amesema kwa ubinadamu, anaomba mwongozo wa Spika wateuliwe wabunge kwenda kumuona Lissu.
Dk Tulia akijibu mwongozo huyo amesema wapo wabunge Nairobi ambao humletea taarifa Spika kila wakati juu ya hali ya mbunge Lissu.
Amewataja wabunge hao kuwa ni Freeman Mbowe ambaye ni Mbunge wa Hai na Mwenyekiti wa Chadema, pia Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni.
Mwingine ni Mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa.
Wakati ofisa kilimo akishambuliwa na wakulima, viongozi wa mtaa aliofuatana nao walikimbia.
Zaidi ya wakulima 19 waliovamia vyanzo vya maji katika bwawa la Mwanzugi wilayani Igunga wamemchapa bakora Ofisa Kilimo wa Kata ya Igunga, Jamila Issa kwa kuwapiga picha.
Tukio hilo lilitokea jana Jumapili ofisa huyo alipokwenda kuangalia utekelezaji wa agizo alilotoa Agosti 27 la kuwapa siku 14 wakulima hao wawe wameondoka katika bwawa hilo.
Ofisa huyo amesema alienda eneo hilo akiwa amefuatana na baadhi ya viongozi wa mtaa kukagua iwapo wakulima wameondoka lakini waliwakuta wakiendelea na kilimo kwenye vyanzo vya maji.
“Nilipofika eneo hilo nilikuta wakulima zaidi ya 19 wakiendelea na kilimo, baadhi wakipanda nyanya na mahindi. Nilianza kuwapiga picha kupata ushahidi, walipobaini walinishambulia kwa fimbo huku viongozi niliofuatana nao wakitimua mbio,” amesema ofisa kilimo Issa.
Amesema baada ya kuanguka, wakulima walitimua mbio na majembe yao na fahamu zilipomrudia alienda kituo cha polisi kuchukua fomu kwa ajili ya matibabu ambayo aliyapata katika Hospitali ya Wilaya ya Igunga na aliruhusiwa kurejea nyumbani.
Hata hivyo, amesema hataogopa kufanya kazi na kuwachukulia hatua wote watakaoendelea kulima kwenye vyanzo vya maji.
Mtendaji wa Kata ya Igunga, Robert Mwagala amesema Polisi kwa kushirikiana na raia wema watawasaka wakulima waliomshambulia ofisa kilimo huyo.
Diwani wa Igunga, Charles Bomani amesema kitendo kilichofanywa na wakulima hao hakikubaliki, hivyo ni lazima hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yao.
Baadhi ya wakulima waliotii agizo la kuondoka kwenye bwawa hilo wamelitaka Jeshi la Polisi kuchukua hatua za haraka juu ya watu waliofanya ukatili huo.
Mkazi wa Kata ya Igunga, Idd Jackson amesema ni aibu na fedheha kumshambulia kiongozi akitekeleza majukumu yake, hivyo ni lazima hatua za kisheria zichukuliwe kwa waliohusika.
Rais Magufuli amemwapisha Profesa Ibrahim Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania.
Rais John Magufuli amefichua siri ya kumteua Profesa Ibrahim Juma kuwa Kaimu Jaji Mkuu akisema hakuwa na historia ya kutosha ya majaji wengi alipoingia madarakani.
Amesema alipoingia madaraka ilikuwa kipindi kifupi ambacho aliyekuwa Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman alistaafu hivyo ilimlazimu achukue muda mrefu wa kujiridhisha na alitumia Ibara ya 118 (4) kumteua Kaimu Jaji Mkuu.
Rais Magufuli amesema hayo leo Jumatatu, Ikulu jijini Dar es Salaam wakati wa kumwapisha Jaji Mkuu, Profesa Juma baada ya kumteua jana Jumapili.
Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.
“Nilifanya hivi si kwa sababu hakuna majaji au walikuwa hawafai, majaji wote ni wazuri na mnafanya kazi nzuri sana lakini sikutaka kuteua jaji baada ya mwaka mmoja nateua tena au baada ya miaka miwili anastaafu, nilitaka nikiteua akae miaka hata 10, awe ‘anatujaji’ wote tutakaokuwepo,” amesema Rais Magufuli.
Amesema kumteua Jaji Mkuu ni kazi ngumu, lazima ujue historia na tabia zake, pia kuangalia iwapo ataweza kuendana na dhamira yake ya kupambana na rushwa.
Rais Magufuli amesema rushwa ipo kila sehemu, hivyo baada ya kuchaguliwa na wananchi mwaka 2015 alikaa chini na kumwomba Mungu apate kiongozi atakayeenda kulisimamia jambo hilo kwa kipindi kirefu zaidi.
Amesema wapo majaji wengi na wenye sifa lakini baadhi yao wamebakisha muda mchache kustaafu.
“Katika kufanya uchambuzi wangu nikamwona Profesa Juma ambaye alikidhi vigezo vyangu. Nakupongeza sana Profesa Juma ni Mungu ambaye amekuchagua kwa hiyo, kawatumikie vizuri watu wa Mungu na utangulize mbele masilahi ya Watanzania,” amesema.
Rais Magufuli amesema ingawa bado kuna changamoto mbalimbali katika Mhimili huo, alimuhakikishia Profesa Juma kwamba Serikali inazitambua na aliwataka majaji kutembea kifua mbele kwa kuwa Serikali inatambua kazi nzuri wanayoifanya.
Amesema kazi nzuri yoyote haikosi watu wa kuiponda, akitumia msemo wa mti wenye matunda ndiyo unaopopolewa kwa mawe.
Kiongozi huyo mkuu wa nchi amesema alipomteua kuwa Kaimu Jaji alipondwa lakini alikuwa mvumilivu na hakupata shinikizo la mtu yeyote la kumteua Jaji Mkuu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto alitoa agizo kumtaka Dk Mashinji kuripoti polisi kulisaidia jeshi hilo.
Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vincent Mashinji ameamua kwenda kuripoti Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini hapa.
Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Chadema, Tumaini Makene imesema Dk Mashinji ameambatana na wasaidizi wake kutoka makao makuu ya chama hicho.
“Katibu mkuu amewasili Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, jijini Dar es Salaam, kuitikia wito wa Polisi uliotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto, kuwa anatakiwa kufika Ofisi ya Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI)” amesema.
Awali, leo Jumatatu Dk Mashinji alisema hawezi kwenda kuripoti kwa kuwa hakuambiwa siku maalumu ya kwenda.
Kamanda Muroto amemtaka Dk Mashinji afike ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai mkoani Dodoma au ofisi kama hiyo iliyopo Kituo Kikuu cha Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam ili kutoa ushirikiano kwa jeshi hilo kuhusu tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
“Nina taarifa za kuitwa Polisi, lakini haziko ‘specific’. Ni wakati wowote naweza kwenda? na hawajasema nikaripoti wapi. Kwa hiyo, wakinihitaji watakuja kuniambia,” amesema Dk Mashinji akizungumza na Mwananchi leo. Lissu alipigwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7 mchana alipokuwa akielekea nyumbani kwake Area D mjini Dodoma. Kwa sasa Lissu anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Aga Khan jijini Nairobi, Kenya.
Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa yupo Nairobi nchini Kenya kumjulia hali Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu aliyelazwa katika Hospitali ya Aga Khan, baada ya kushambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana.
Lissu ambaye pia ni mwanasheria wa Chadema alijeruhiwa kwa risasi tano Alhamisi Septemba 7 akiwa ndani ya gari nyumbani kwake Area D mjini Dodoma akitokea bungeni.
Katika akaunti yake ya Twitter, Lowassa ame-tweet akisema, “Earlier today i paid a visit at Nairobi Hospital to see our MP, President of TLS and dear friend @tundulissutz He is recovering well. It is Sad times for Tanzania. Let us all keep praying.”
Kwa tafsiri isiyo rasmi amesema “Mapema leo nilitembelea Hospitali ya Nairobi kumwona mbunge, Rais wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS) na rafiki kipenzi Tundu Lissu. Anaendelea vizuri. Ni kipindi cha masikitiko kwa Tanzania. Kwa pamoja tuendelee kuomba.”
Katika tweet hiyo, Lowassa ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, ameweka picha akiwa pamoja na Alicia ambaye ni mke wa Lissu; Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na dereva wa Lissu Simon Mohamed Bakari.
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionRais wa zamani wa Georgia Mikheil Saakashvili (katikati)aingia Ukrain kwa nguvu
Mikheil Saakashvili ambaye ni rais wa zamani wa Georgia na pia gavana wa zamani wa jimbo nchini Ukrain amevuka na kuingia nchini Ukrain aisaidiwa na mamia ya wafuasi wake.
Bwana Saakashvili alisema kuwa alisukumwa bila kutarajia kwenye mpaka na umati wa watu waliokuwa wamekasirika kuwa mpaka ulikuwa umefungwa.
"Walitusukuma na kutebeba hadi nchini Ukarain," alesema Saakashvili.
Maafisa nchini Ukrain wanasema kuwa aliiangia nchini humo kinyume na sheria na walinzi 15 na mpaka walijeruhiwa.
Kulikuwa na mivurutano kwenye mpaka kati ya wafuasi wa bwana Saakashvili na maafisa wa mpaka.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionMikheil Saakashvili na waziri mkuu wa zamani Yulia Tymoshenko
Bwana Saakashvili ambaye awali alikuwa ni raia wa Georgia na kisha raia wa Ukrain kwa sasa hana uraia wa nchi yoyote baada ya uraia wake wa Ukrain kufutwa na mshirika wake wa zamani raid Petro Poroshenko.
Pia anatakiwa nchini Georgia kwa kesi zinazohusu uhalifu ambazo anadai kuwa zimechochewa kisiasa.
Mapema Jumapili treni yake ilizuiwa katika kituo huko Przemysl nchini Poland baada ya walinzi wa Ukrain kumzuia kuingia.
Bwana Saakashivili alijiunga na wafuasi wake kadha akiwemo waziri mkuu wa zamani wa Ukrain na kiongozi wa sasa wa upinzani Yulia Tymoshenko.
Haki miliki ya pichaEPAImage captionRais wa zamani wa Georgia aingia Ukrain kwa nguvu
Mwaka 2015 aliteuliwa gavana wa Odessa na Bw. Poroshenko lakini wawili hao walitofautiana mwezi Novemba mwaka uliopita baada ya Bw Saakashvili kumlaumu rais wa kuzuia jitihada za kumaliza ufisadi.
Haki miliki ya pichaAFPImage captionKimbunga Irma chaingia jimbo la Florida
Kimbunga Irma kimepiga visiwa vilivyo kusini mwa jimbo la Florida nchini Marekani kikiwa katika kiwango cha nne, kwa mujibu wa watabiri wa hali ya hewa.
Kimbuga hicho kumepiga visiwa vilivyo nyanda za chini na upepo wa kasi ya hadi kilomita 209 kwa saa kabla ya kuelekea kaskazini magharibi kwa ghuba ya Florida.
Zaidi ya watu milioni 6.3 waliambiwa waondoke Florida, huko onyo likitolewa kuwa kubunga hicho kinaweza kuwa tisho kwa maisha.
Irma tayari kimeharibu eneo ya Caribbean ambapo takribana watu 25 wameuawa.
Haki miliki ya pichaMALCOLM TURNBULLImage captionPicha ya waziri mkuu wa Australia akishika mtoto na bia mkononi yazua maoni mitandaoni
Watu nchini Australia wamejitokeza kumtetea waziri mkuu Malcolm Turbull baada ya picha yake akimshika mjukuu wake na bia mkononi kuzungumziwa kwa wingi,.
Bwana Turbull alisambaza picha hiyo mwenyewe akimshika mjukuu wake kwenye uwanja mmoja wa kandanda mjini Sydney siku ya Jumamosi.
Picha hiyo ilichapishwa kwenye ukurasa wake wa Facebook.
Lakini ilizua maoni ya kumkosoa Bw Turnbul kutokana na kuwepo kwa bia.
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionZaidi ya watu 300,000 waisilamu wa Rohingya, wamekimbia kwenda Bangaladesh tangu ghasia zianze mwezi uliopita
Oparesheni ya kiusalama inayowalenga waislamu wa Rohingya nchini Myanmar ni mfano wa mauaji ya kikabila, mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa amesema.
Zeid Raad Al Hussein ameitaka Mynamar kusitisha oparesheni mbaya ya kijeshi katika jimbo la Rakhine.
Zaidi ya watu 300,000 waisilamu wa Rohingya, wamekimbia kwenda Bangaladesh tangu ghasia zianze mwezi uliopita.
Jeshi linasema kuwa linajibu mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa Rohingya na kukana kuwalenga raia.
Ghasia hizo zilianza tarehe 25 mwezi Agosti wakati wapiganaji wa Rohingya walishambulia vituo vituo vya polisi kaskazini mwa Rakhine na kuwaua maafisa 12 wa ulinzi.
Rohingya ambao wameikimbia Myanmar tangu wakati huo, wanasema kuwa wanajeshi walijibu vikali kwa kuchoma vijiji na kuwashambulia raia kwa minajili ya kuwafukuza.
Rohinga ambayo ni jamii ndogo ya waislamu wasio na utaifa wamekumbwa na mauaji kwa muda mrefu nchini Myanmar ambayo inasema kuwa wao ni wahamiaji haramu.
Haki miliki ya pichaREUTERSImage captionWatu 7 wauawa kwa kupigwa risasi Dalllas Marekani
Mtu mwenye bunduki amewaua watu saba kwenye nyumba moja mjini Dallas, Texas nchini Marekani, kabla ya kuuliwa kwa kipigwa risasi na polisi.
Watu wawili ambao nao walipigwa risasi wako hospitalini.
Msemaji wa polisi David Tilley alisema kuwa mshambuliaji aliuawa na polisi kwa kwanza ambaye alifika wakatin wa ufyatulianaji wa risasi. Polisi huyo hakujeruhiwa.
Kile kilichochangia shambulizi hilo bado hakijulikani au ikiwa mshambuliaji aliwafahamu waathiriwa.
"Tunajaribu kuangalia suala hili kwa kina," Bwa Tilley alisema.
Gazeti moja huko Dallas liliripoti kuwa wale waliouawa walikuwa wakitazama timu ya Dallas Cowboys, ambayo ni timu ya kandanda ya Marekani wakati walishambuliwa.
Polisi hawajatoa jina la mshambuliaji au muathirwa yeyote lakini wote wametajwa kuwa watu wazima.
Apple inatarajiwa kuzindua kifaa kipya kwenye makoa yake makuu siku ya Jumanne.
Kampuni hiyo yenye makao yake huko California hujitahidi kuficha siri za teknlojia yake hadi wakati wa uzinduzi wa vifaa vyake.
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGESImage captionMkuu wa Apple Tim Cook
Hata hivyo taarifa kuhusu vigaa vipya vya Apple zlifichuliwa Agosti,
Wakati hilo likionekana kufanyika kimakosa, imedaiwa lakini ufujaji wa hivi majuzi ulikwa wa makusudi.
Hata hivyo BBC imebaini kuwa mtu asiyejulikana alichapisha anwani za iOS 11 zinazofahamika kama golden master (GM) ambazo zilifungua teknolojia katika komputa za Apple.