Tuesday, December 5

Mamilioni yalipotea katika mazishi ya Mandela

MandelaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMiaka minne imepita tangu Nelson Mandela tangu afariki
Mazishi ya aliyekuwa rais wa zamani Afrika kusini ,Nelson Mandela yanadaiwa kukumbwa na ufisadi mkubwa ambao unadaiwa kutekelezwa na viongozi wakuu nchini humo.
Mamlaka ya kupambana na rushwa nchini humo imebaini kuwa takriban dollar millioni 22 ilitumika vibaya wakati wa matayarisho ya mazishi ya Mandela miaka nne ilyopita.
MandelaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionNelson Mandela
Ripoti hiyo inasema kwamba viongozi hao walivuja pesa na kukiuka taratibu zilizowekwa huku ikisemekana kwamba gharama za bidhaa ziliongezwa maradufu na matumizi mazishi kutajwa kuwa ya juu sana kwa mfano shati za kumbukumbu ya mazishi zilinunuliwa kwa dollar 25 badala ya dollar19 .
Hata hivyo ripoti hiyo imetaka hatua kali kuchukuliwa dhidi ya wahalifu waliofanya jambo hilo la kushangaza katika jamii.

Rais wa zamani wa Yemen Abdullah Saleh 'auawa'

Picha ya Ali Abdullah Saleh akihutubu Sanaa, Yemen (24 August 2017)Haki miliki ya pichaEPA
Image captionAli Abdullah Saleh alikuwa mshirika wa wapiganaji wa Houthi vita vilipozuka 2015
Aliyekuwa rais wa Yemen Ali Abdullah Saleh ameuawa katika mapigano na washirika wake wa zamani, taarifa zinasema.
Mashirika ya habari yanayodhibitiwa na waasi wa Houthi yamewanukuumaafisa wakitangaza "mwisho wa mzozo wa wanamgambo wahaini na kiongozi wao".
Duru katika chama chake Bw Saleh cha General People's Congress pia wamethibitisha kwamba amefariki, kwa mujibu wa Al Arabiya TV.
Picha na video zilizosambazwa mtandaoni zimeuonesha mwili wa mwanamume anayefanana na Bw Saleh ukiwa na kidonda kichwani.
Hadi kufikia wiki iliyopita, wafuasi wa Bw Saleh walikuwa wanapigana pamoja na wapiganaji wa jamii ya Houthi dhidi ya rais wa sasa wa Yemen Abdrabbuh Mansour Hadi.
Lakini uhasama wa muda mrefu wa kisiasa pamoja na mzozo kuhusu udhibiti wa msikiti mkuu katika mji mkuu wa Sanaa unaodhibitiwa na waasi vilichangia mapigano makali ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 125 na wengine 238 kujeruhiwa tangu Jumatano usiku.
Jumamosi, Bw Saleh aliahidi "kufungua ukurasa mpya" na Bw Hadi anayesaidiwa na muungano wa mataifa yanayoongozwa na Saudi Arabia iwapo majeshi hayo yangeacha kuishambulia Yemen na kuondoa marufuku ya kutoingiza chakula na bidhaa Yemen.
Pande hizo mbili zilipokea kwa furaha tamko la Bw Saleh.
Lakini waasi wa Houthi walitazama hilo kama "mapinduzi" dhidi ya "ushirika ambao hakuwahi kuwa na imani nao."
Watu zaidi ya 8,670 wameuawa na wengine 49,960 kujeruhiwa tangu majeshi ya muungano unaoongozwa na Saudi Arabia yalipoingilia kati vita vya wenyewe kwa wenyewe Machi 2015, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Mzozo huo pamoja na marufuku ya kutoingiza chakula na bidhaa Yemen ambayo imekuwa ikitekelezwa na Saudi Arabia pia umewaacha watu 20.7 milioni wakihitaji kwa dharura msaada wa kibinadamu, na pia kusababisha hitaji kubwa zaidi ya chakula cha dharura duniani.
Aidha, kulitokea mlipuko wa ugonjwa wa kipindupindu ambao unaaminika kusababisha vifo vya watu 2,211 tangu Aprili.

Mahakama nchini Marekani yaruhusu kutekelezwa marufuku ya usafiri ya Trump

trumpHaki miliki ya pichaAFP
Image captionVizuizi vya wageni kutekelezwa
Mahakama kuu nchini Marekani imeamua kuwa toleo la marufuku ya kusafiri ya Rais trump inaweza kutekelezwa kwa ukamilifu.
Huku ikiendelea kukutana na changamoto za kisheria kutoka mahakama za chini.
Nchi sita zinazokutana na zuio hilo ni Iran, Libya, Syria, Yemen, Somalia na Chad.Mahakama za chini tayari zimeruhusu kuzuiwa kwa baadhi ya watu kutoka Korea kaskazini na Venezuela.
Majadiliano Zaidi yatendelea kusikilizwa wiki hii katika mahakama huko San Francisco, California, na Richmond, Virginia.
Mwandishi wa BBC mjini Washington anasema kwamba, kwa sasa, huu ni ushindi mkubwa kwa Donald Trump.
Msemaji wa Ikulu ya White Hogan Gidley alisema kuwa White House haikushangazwa na uamuzi wa mahaka ya juu.
Mwanasheria mkuu Jeff Sessions aliutaja uamuzi huo kama ushindi mkubwa kwa usalama wa watu wa Marekani.

Afisa wa Umoja wa Mataifa afanya ziara nadra Korea Kaskazini

UN under secretary general for political affairs Jeffrey Feltman, attends a press conference in Bogota on 15 November 2017Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionBw Feltman anatarajiwa kukutana na kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un
Afisa wa masuala ya siasa wa umoja wa Mataifa anaanza ziara isiyo ya kawaida wa siku nne huko Pyongyang siku ya Jumanne
Ziara hiyo ya Jeffrey Feltman ndiyo ya kwanza kufanywa na afisa wa cheo cha juu wa Umoja wa Mataifa katika kipindi cha miaka sita.
Korea Kaskazini ilikuwa imetoa mwalika kwa Umoja wa Mataifa mwezi Septemba kufanya ziara.
Ziara hii inakuja baada ya jaribio la wiki iliyopita ambalo Korea kaskazini ilidai kuwa ndilo lenye nguvu zaidi la masafa marefu ikidai kuwa linaweza kushambulia Marekani.
Bw. Feltman, mwanadiplomasia wa zamani wa Marekani na afisa wa cheo cha juu zaidi kufanya kazi na Umoja wa Mataifa atakuwa mjini Pyongyang hadi Ijumaa.
In this handout image taken on December 2 by US Air Force and released on 4 December, A US Air Force F-22 Raptor fighter jet touching down at Gwangju Air Base on 2 December 2017 in Gwangju, South Korea.Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMarekani imepeleka ndeye za aini hii za F-22 fighter jets kushiriki kwennye mazoezi na Korea Kusini
Ziara yake inakuja wakati Korea Kusini na Marekani wanafanya mazoezi makubwa zaidi ya agani kuwai kufanywa.
China ambayo ni mshirika wa jadi wa Korea Kaskazini na mshirika mkubw wa kibiashara ilimtuma mwanadiplomasia wa cheo cha juu kwenda Korea Kaskazini mwezi uliopita kwa majadiliano na maafisa huko.
Umoja wa Mataifa unasema kuwa hakuna mipango kwa sasa kwa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ambaye amejitolea kuwa mpatanishi kwenye mzozo wa Korea Kaskazini kuzuru nchi hiyo.

Kwa nini mji wa Jerusalem ni mtakatifu?

Religious sites in Jerusalem's Old CityHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMaeneo matakatifu ya kidini Jerusalem
Kumekuwa na mzozo wa muda mrefu kuhusu udhibiti wa mji wa Jerusalem kati ya Waisraeli na Wapalestina.
Mji huo kwa sasa huwa umegawanywa mara mbili, Jerusalem Mashariki na Jerusalem Magharibi.
Jerusalem ya Magharibi hutazamwa na Israel kama mji wake mkuu nayo Jerusalem Mashariki hutazamwa kuwa mji mkuu wa taifa la Wapalestina (litakapoundwa), ingawa eneo hilo bado kwa kiwango kikubwa limetawaliwa na Israel tangu vita vya 1967.
Tangu wakati wa vita hivyo, Israel imejengwa nyumba za walowezi wa Kiyahudi takriban 200,000 ambao huishi Jerusalem Mashariki, hatua iliyoshutumiwa na jamii ya kimataifa. Eneo hilo huishi Wapalestina takriban 370,000.
Israel ilitangaza 1980 Jerusalem yote kuwa mji wake mkuu wa milele, lakini nchi nyingi duniani hazikubali azimio hilo.
Hivyo basi, balozi za nchi za kigeni katika Israel ziko nje ya Jerusalem, katika mji wa Tel Aviv.
Mzozo huo umefufuliwa tena kutokana na hatua ya Rais Donald Trump wa Marekani kutarajiwa kuutambua mji huo kama mji mkuu wa Israel.
Mataifa mengi ya Kiarabu yameshutumu hatua hiyo ya Bw Trump na kusema itazidisha uhasama Mashariki ya Kati.
Lakini ni kwa nini mji huu huzozaniwa hivyo? Mwandishi wa BBC Erica Chernofsky anachambua.

Dini tatu

Mji huu huwa na umuhimu mkubwa kwa dini tatu kuu - Ukristo, Uislamu na Uyahudi. Dini zote tatu humuangazia Abraham anayetajwa kwenye Biblia na Koran kama mmoja wa waanzilishi au mababu wa imani.
Ni mji ambao umedhibitiwa na dini hizo kwa vipindi mbalimbali katika historia.
Kwa Kiebrania, mji wa Jerusalem hufahamika kama Yerushalayim na kwa Kiarabu al-Quds. Kwa Kiswahili, jina lake halisi ni Yerusalemu. Mji huo ni miongoni mwa miji ya kale zaidi ambayo ipo hadi sasa duniani.
Ni mji ambao umetekwa, ukabomolewa na kuharibiwa na kisha kujengwa tena.
Kila sehemu ya ardhi yake ukichimba kwenda chini hufichua enzi fulani katika historia yake.
Ingawa umekuwa chanzo cha ubishi na mzozano kati ya dini mbalimbali, dini zote huungana kwa pamoja kuungama kwamba ni eneo takatifu.
Ndani yake kuna Mji Mkongwe, ambao una njia nyembamba, vichochoro na nyumba za kale. Kuna maeneo manne makuu na kila eneo, majengo huwa tofauti. Kuna eneo la Wakristo, Waislamu, Wayahudi na Waarmenia. Eneo hilo huzungukwa na ukuta mkubwa wa mawe. Hapo, kunapatikana baadhi ya maeneo yanayoaminika kuwa matakatifu zaidi duniani.
Kila eneo kati ya maeneo hayo manne (unaweza kuyaita mitaa) huishi watu wa aina moja. Wakristo wana maeneo mawili, kwa sababu Waarmenia pia ni Wakristo. Eneo lililotengewa Waarmenia, ambalo ndilo ndogo zaidi kati ya hao manne, lina vituo vya kale zaidi vya Waarmenia duniani.
Jamii ya Waarmenia imehifadhi utamaduni wake wa kipekee ndani ya Kanisa la St James na nyumba kubwa ya utawala. Maeneo hayo mawili yamechukua sehemu kubwa ya mtaa huo wa Waarmenia.
Image captionNje ya Lango la Damascus

Kanisa

Ndani ya mtaa wa Wakristo, kuna Kanisa Kuu la Kaburi na Ufufuo wa Yesu Kristo, ambalo ni muhimu sana kwa Wakristo kote duniani.
Hupatikana katika eneo ambalo lina umuhimu mkubwa katika kisa cha kusulubiwa, kufariki na kufufuka kwa Yesu.
Kwa mujibu wa utamaduni wa Kikristo, Yesu alisulubiwa hapo, katika Golgotha, au mlima wa Calvary. Kaburi lake linapatikana ndani ya kanisa hilo la kaburi na inaaminika kwamba hapo ndipo alipofufuka.
Kanisa hilo husimamiwa kwa pamoja na madhehebu mbalimbali ya Kikristo.
Sana huwa ni wahudumu wa kanisa la Kiothodoksi la Ugiriki, watawawa na mapadri wa Francisca kutoka Kanisa Katoliki la Roma na wengine kutoka kanisa la Waarmenia.
Kuna pia wahuudmu kutoka kanisa la Waothodoksi kutoka Ethiopia, Coptic na Syria.
Ni eneo ambalo mamilioni ya mahujaji wa Kikristo husafiri kila mwaka kwenda kuliona kaburi wazi la Yesu na kutafuta ufunuo na kuomba katika eneo hilo.

Msikiti

Mtaa wa Waislamu ndio mkubwa zaidi kati ya maeneo hayo manne na ndani yake kunapatikana madhabahu ya Dome of Rock (Kuba ya Mwamba) na Msikiti wa al-Aqsa kwenye eneo linalofahamika na Waislamu kama Haram al-Sharif, au Mahali/Hekalu Patakatifu.
Msikiti huo ndio eneo la tatu kwa utakatifu katika dini ya Kiislamu na husimamiwa na wakfu wa Kiislamu ambao hufahamika kwa Kiarabu kama Waqf.
Waislamu huamini kwamba Mtume Muhammad alisafiri kutoka hapo hadi Mecca usiku na aliomba pamoja na roho za manabii wengine wote. Hatua chache kutoka hapo kunapatikana Dome of the Rock (Kuba ya Mwamba) ambapo kuna jiwe la msingi. Waislamu huamini kwamba ni kutoka hapo ambapo Mtume Muhammad alipaa mbinguni.
Waislamu hutembelea eneo hilo takatifu kila wakati katika mwaka, lakini kila Ijumaa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhan, mamia ya malelfu ya Waislamu hufika kuomba kwenye msikiti huo.

Ukuta

Katika mtaa wa Wayahudi, kunapatikana Kotel, au Ukuta wa Magharibi ambao ni masalio ya ukuta wa nje uliozunguka lililokuwa Hekalu Takatifu.
Ndani ya hetalu hilo kulikuwa na Patakatifu pa Patakatifu, eneo takatifu zaidi katika dini ya Kiyahudi.
Wayahudi huamini kwamba hapo ndipo kulikuwa na jiwe la msingi ambapo kutoka kwake dunia iliumbwa.
Kadhalika, wanaamini ni hapo ambapo Abraham alikuwa amejiandaa kumtoa kafara mwanawe Isaac. Wayahudi wengi huamini kwamba Dome of the Rock ndipo lilipokuwa eneo takatifu zaidi ndani ya hekalu lililofahamika kama Patakatifu pa Patakatifu.
Leo hii, Ukuta wa Magharibi ndilo eneo la karibu zaidi ambalo Wayahudi wanaweza kufanya maombi yao.
Husimamiwa na Rabbi wa Ukuta wa Magharibi na kila mwaka hutembelewa na mamilioni ya mahujaji.
Wayahudi kutoka kila pembe ya dunia hutembelea eneo hilo kuomba na kukumbuka utamaduni wao, hasa nyakati za siku kuu za kidini.
Ukuta huo pia hufahamika kama Ukuta wa Maombolezo.

Onyo jipya kuhusu Trump kuutambua mji wa Jerusalem latolewa

The Israeli flag flutters in front of the Dome of the Rock mosque and the city of Jerusalem, on December 1, 2017.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionOnyo jipya kuhusu Trump kuutambua mji wa Jerusalem latolewa
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amemuambia Donald Trump kuwa ana wasiwasi kuwa rais huyo wa Marekani anaweza kuutambua Jerusalem kuwa mji mkuu wa Israel.
Uamuzi wowote kuwa mji huo unastahili kuwa katika viwango vya mazungumzo kati ya Israel na Palestina, Bw Macron alisema.
Mapema onyo kama hilo lilitolewa na nchi za kiarabu na mataifa ya kiislamu.
Ripoti zinasema kuwa rais wa Mareknia atautambua mji wa Jerusalem kuwa mji wa mkuu wa Israel.
Israel na Palestina wote wanadai kuwa mji huo ni mji wao mkuu.
Image captionRais Macron alimpigia Trump simu kuelezea wasi wasi wake
Ikulu ya White House iliseam kuwa anaweza kukosa siku ya mwisho ya Jumamosi kuweka sahhihi agizo la kuzuia kuhamishwa ubalozi wa Marekani kutoka Tel Avivi kwenda Jerusalem.
Kila rais akiwemo Trump ametia sahhihi agizo kila baada ya miezi sita tangu bunge le Congress lipitishe mswada mwaka 1995 wa kutaka ubalozi huo kumamsihwa,
Hali ya mji wa Jerusalem ndio channzo cha mzozo kati ya Israel na Palestina wanaoungwa mkono na nchi za kiarabu na ulimwengu wa kiislamu.

Mtalii kutoka Ujerumani auawa kwa kupigwa risasi Ethiopia

Watalii wengi hutembelea mlima wa volkano wa Erta AleHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWatalii wengi hutembelea mlima wa volkano wa Erta Ale
Mtalii mmoja kutoka Ujerumani amepigwa risasi na kuuawa kaskazini mashariki mwa Ethiopia.
Dereva wake pia alijeruhiwa wakati wa tukio hilo, ambalo lilifanyika katika jimbo la Afar, karibu na mpaka wa Eritrea.
Ripoti zanasema raia huyo wa Ujerumani alikuwa miongoni mwa kundi la watalii ambao walikuwa kwenye ziara ya volkano ya Erta Ale - kivutio kikubwa kwa watalii wanaozuru Ethiopia.
Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza anasema hadi kufikia sasa haijabainika ni nani hasaa aliyetekeleza shambulio hilo lakini serikali ya Ethiopia inasema inachunguza mauaji hayo.
Serikali pia inasema vikosi vya usalama vimetumwa kuimarisha usalama huko.
Eneo hilo la mpakani linatumika sana na kundi la waasi linalotaka kujitenga na Ethiopia.
Mnamo mwaka 2012, watalii watano waliuawa na wengine wanne kutekwa nyara baada ya wapiganaji kuwashambulia katika eneo hilo.
Kundi lililojihami la Afar Revolutionary Front lilidai kuhusika kwenye shambulio hilo.

Kenya kuzalisha kawi ya nyuklia kufikia 2027

Cattenom October 17, 2017.Haki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionPicha ya kiwanda cha kuzalisha kawi ya nyuklia cha Cattenom mashariki mwa Ufaransa
Kenya imesema kwamba itaendelea na mpango wake wa kuhakikisha kwamba ina kiwanda cha kuzaliwa umeme kwa kutumia nguvu za nyuklia kufikia 2027.
Afisa Mkuu Mtendaji wa Bodi ya Umeme wa Nyuklia ya Kenya Collins Juma ameambia mkutano wa wadau kuhusu kawi jijini Nairobi kwamba ujezi wa kiwanda cha kuzalisha kawi hiyo unatarajiwa kuanza 2024.
Bodi hiyo imesema nishati hiyo itatumiwa kuongeza uzalishaji wa umeme nchini humo na si kuchukua nafasi ambayo imekuwa ikitekelezwa na vyanzo vingine vya kawi nchini humo.
Kufikia mwaka 2030, ambapo Kenya inatazamia kuwa taifa lenye viwanda la mapato ya wastani kufikia wakati huo, Kenya itakuwa ikihitaji megawati 17,000.
Kawi ya mvuke itachangia megawati 7,000. Kwa sasa, kawi hiyo kwa sasa hutumiwa kuzaliwa megawati 2,400 za umeme nchini humo.
Kaimu afisa mkuu mtendaji wa kukinga dhidi ya miali nururishi nchini Kenya Joseph Maina amesema Wakenya hawafai kuwa na wasiwasi kuhusu usalama wa nishati ya nyuklia.
"Kumekuwa na ajali tatu pekee kubwa za nyuklia katika historia. Kisiwa cha Three Mile Marekani, 1978; Chenorbyl nchini Ukraine, 1986 na Fukushima nchini, Japan, 2011. Usalama umeimarishwa kutokana na mafunzo kutoka kwa mikasa hiyo," amesema.
Kenya imekuwa na mpango wa kuzalisha kawi ya nyuklia kwa muda.
Machi mwaka huu, Waziri wa nishati na mafuta wa nchi hiyo Bw. Charles Keter alisema Kenya itatimiza vigezo vikali vilivyowekwa na Shirika la kimataifa la nishati ya atomiki IAEA kabla ya kutekeleza mpango huo.
Alikadiria kwamba Kenya itatumia dola 5 bilioni za Marekani kujenga kiwanda cha kuzalisha kawi hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti ya IAEA ya mwaka 2015, zaidi ya nchi 30 duniani, theluthi moja zikitoka Afrika zinajiandaa kuanzisha mipango ya nyuklia kwa ajili ya kuzalisha umeme kwa usaidizi wa wataalamu kutoka shirika hilo.

Monday, December 4

UTARATIBU UNAOSTAHILI KUFUATWA KABLA YA KUFUTIWA UMILIKI WA ARDHI.

Image result for HATI MILIKI
NA  BASHIR  YAKUB -

Yafaa  kujua  utaratibu unaotakiwa  kufuatwa  kabla  ya kufutiwa  hati miliki  ya  ardhi (nyumba/kiwanja).  Unapojua utaratibu  huu  ndipo  unapojua kama  ulionewa  au  hapana. Na kuonewa ni  pamoja na  kukiuka utaratibu.  Na  kukiuka  taratibu yoyote  ya  kisheria kunabatilisha  mchakato wa  kufutwa  kwa  hati yako na  kutakiwa  kurudishiwa  eneo  lako  au  fidia.

Makala  yaliyopita  tulieleza mambo  ambayo  ukifanya  unahesabika  kukiuka  masharti  ya  umiliki wa  ardhi   na ni hapo  unapoweza   kufutiwa  umiliki. Leo  tuangalie  utaratibu  wa  kufuta umiliki  ikiwa imethibitika  kuwa   tayari  umekiuka  masharti  hayo. Sheria  namba 4 ya 1999 , Sheria  Ya  ardhi  imeeleza  utaratibu  wa  kufuta  umiliki  wa  ardhi.

 UTARATIBU.

1.Ni  lazima  uwe umekiuka  masharti  au  moja  ya  masharti uliyopewa  wakati unakabidhiwa  ardhi/hati kwa  mujibu  wa  kifungu  cha 48 ( 1) cha  Sheria  ya  ardhi. Usikubali  kufutiwa  umiliki  ikiwa  hujakiuka  sharti/masharti ya umiliki uliyopewa,  labda   iwe  vinginevyo.

2.   Baada  ya  kuwa  umekiuka  masharti  yafaa  upewe  taarifa  maalum( notice) kwa  mujibu  wa  kifungu 48(2). Ni  taarifa inayoeleza  masharti  ya  umiliki  uliyokiuka  na  onyo  la  kufutiwa  umiliki.  Taarifa  hiyo  ni  ya  siku  90(miezi  mitatu).  Taarifa  hiyo utapewa wewe  mmiliki  na  kila  mwenye  maslahi  katika  ardhi  hiyo  mf, mpangaji, mrehani nk.

3.   Baada  ya  siku 90  kuisha na  pengine  hujajirekebisha  au  kufanya  kile  ulichoambiwa  kufanya  basi  kamishna  wa  ardhi  atatakiwa  kupeleka  pendekezo  kwa  rais  ili  kufutiwa umiliki. Ni  rais  tu  mwenye  mamlaka  ya  kufuta  umiliki  wa  ardhi. 

Zingatia, barua  au  nyaraka  nyingine yoyote  ambayo inasema  umefutiwa  umiliki  lakini  aliyefuta  sio  rais  wa  nchi,  sio  halali.

4.  Ikiwa rais  atakubali  kukufutia  umiliki  wa  ardhi basi  inatakiwa kufutwa  huko  kutangazwe  katika  gazeti  maalum  la  serikali/taarifa ya  serikali(GN)  na  katika  gazeti  la  kawaida(newspaper)  ambalo  linafika  eneo  ardhi  yako  ilipo.  Hii  ni  kwa  mujibu  wa  kifungu  cha 49(1).  Ili  utaratibu  uhesabike  umefuatwa  ni  lazima  matangazo  haya  yatolewe  la  sivyo  kufutiwa  huko  kunabatilika.

5.  Rais  atakapofuta  umiliki  wa  ardhi basi  ardhi  hiyo  itahama  kutoka  kwa  mmiliki  wa  awali  kwenda  serikalini  au  vinginevyo itakavyoamriwa kwa  mujibu  wa  kifungu cha 49(2).  

6. Ikiwa  kuna  maendelezo  yoyote  ya  kudumu  ambayo  ulifanya  kwenye  hiyo  ardhi  basi   ni  lazima  ulipwe  fidia  ya  maendelezo  hayo  kwa  mujibu  wa  kifungu  cha  49(3). 

Isipokuwa maendelezo  hayo  yawe  yalikuwa  ni sehemu  ya  masharti  ya  umiliki  wa  ardhi  hiyo.  Yasiwe  nje  ya  yale  uliyokuwa  umepewa kwenye umiliki.

7. Ikiwa   ardhi  hiyo  ilikuwa  inadaiwa  kodi au tozo  za ardhi basi  kodi  na  tozo  hizo  zinaondolewa  na  deni  hilo  linakufa, mpaka  isemwe  vinginevyo.  Hii  ni  kwa  mujibu  wa  kifungu cha 49(2)(e)..

NAMNA  YA  KUDAI  HAKI  YAKO  IKIWA  TARATIBU  ZIMEKIUKWA.

Kwanza, waweza  kupeleka  malalamiko  yako  kwa  kamishna  wa  ardhi    na  baadae  kwa  rais. Utaandika  barua  ikieleza kile  ambacho  unahisi  kuonewa au  taratibu  kukiukwa.

Pili, ni  kupeleka  malalamiko  yako  mahakamani. Hapo  sio barua  bali utapeleka  nyaraka  maalum  za  kufungulia  shauri(Plaint/Application). Humo  pia  utaeleza  pahala  unapohisi  kuonewa au  taratibu  kukiukwa pia.
Pia  unaqweza  kuchukua  hatua  hizi  kwa  pmoja na  kwas  wakati moja.

MWANDISHI   WA   MAKALA  HAYA   NI   MWANASHERIA  NA  MSHAURI   WA  SHERIA  KUPITIA  GAZETI   LA  JAMHURI   KILA   JUMANNE.  0784482959,  0714047241bashiryakub@ymail.com