Tuesday, November 21

Utafiti: Uvimbe wa saratani ya matiti huwa ''mkubwa'' kwa wanawake wanene kupita kiasi

Mwanamke mneneHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWanawake wenye unene wa mwili wa kupindukia wanahitaji kufanyiwa vipimo cha mara kwa mara cha kubaini saratani ya matiti vya mammograms
Ni vigumu kubaini chembe chembe za saratani ya matiti miongoni mwa wanawake wenye unene kupita kiasi kabla ya uvimbe kuwa mkubwa, umeeleza uchunguzi wa Sweden.
Wanawake wenye unene wa mwili wa kupindukia wanahitaji kufanyiwa vipimo cha mara kwa mara cha kubaini saratani ya matiti cha mammograms kusaidia kubaini uvimbe wa saratani, walisema watafiti, lakini wakaongeza kuwa ushahidi zaidi wa kubainisha hayo unahitajika.
Nchini Uingereza, wanawake wenye umri wa kati ya miaka 50 hadi 70 hualikwa kwa ajili ya uchunguzi wa saratani ya matitikila baada ya miaka mitatu.
Baadhi ya wanawake wenye hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti tayari hupata huduma ya uchunguzi wa mara kwa mara.
Hawa ni wanawake wanaotoka katika familia yenye historia ya saratani ya matiti , kwa mfano.
Kuwa na uzito wa mwili kupita kiasi pia huongeza hatari ya kupata saratani ya matiti, lakini kwa sasa si suala linalozingatiwa inapokuja katika muda wa kufanya vipimo vya saratani.
Taasisi ya Karolinksa iliwahusisha wanawake 2,012 waliopatikana na saratani ya matiti baina ya mwaka 2001 na 2008.
Uchunguzi wa saratani ya matitiHaki miliki ya pichaSPL
Image captionWanawake wenye hatari kubwa ya kupata saratani ya matiti mfano wale wanaotoka katika familia zenye historia ya saratani hiyo wanashauriwa kufanyiwa uchunguzi wa mara kwa mara
Wanawake hao wamekuwa wakifanyika vipimo vya kutambua saratani ya matiti, vinavyofahamika kwa lugha ya kitaalam kama mammograms kila baada ya miezi 18 hadi miaka miwili kama tinavyoshauriwa shauriwa nchini Sweden.
Wanasayansi hao walichunguza juu ya ni vipi uvimbe mkubwa wa saratani wa kila mmoja wakati ulipobainika na pia uzito wa mwili wa mwanamke (BMI), kama kipimo cha uzito wa kupindukia.
Jopo hilo lilibaini kuwa wanawake waliokuwa na uzito wa kupita kiasi wa mwili walikuwa na uwezekano mkubwa wa pia wa kuwa na uvimbe mkubwa ulipobainika kwa kutumia njia ya mammogram ama wakati wa uchunguzi wa kawaida.
Hii ni kwasababu labda matiti yao yalikuwa makubwa na kwa hivyo ilikuwa ni vigumu kubaini uvimbe nama ni kwasababu uvimbe wao ulikua kwa kiwango cha haraka zaidi, aliieleza BBC mkuu wa utafiti huo Fredrik Strand.
Uvimbe mkubwa huwa unakuwa na chembe chembe mbaya za saratani, alisema.
Daktari Strand alisema : " Utafiti wetu unaonyesha kwamba pale daktari wa kliniki anapoonyesha athari na faida za kupima saratani ya matiti kwa mgonjwa mwenye uzito wa kupita kiasi wa mwili(BMI) lazima ieleweke kuwa ni muhimu.
" Zaidi ya hayo utafiti wetu unaonyesha kuwa wenye unene zaidi wa mwili wanapaswa kufanyiwa vipimo baada ya muda mfupi zaidi ."
Lakini Sophia Lowes, kutoka kituo cha utafiti wa saratani nchini Uingereza -Cancer Research UK, anasema kuwa utafiti ambao unawasilishwa kwenye mkutano wa mwaka wa taasisi ya Marekani ya utafiti wa matibabu ya saratani-Radiological Society of North America, haukutoaushahidi wa kutosha juu ya mabadiliko na ni kwa muda gani mwanamke anapaswa kufanyiwa uchunguzi.
Uchunguzi wa matiti unafaida na hasara zake, alisema Daktari Sophia Lowes, na kuongeza kuwa:"Husaidia kunusuru maisha kwa kubaini saratani ya matiti katika hatua zake za mwanzo,lakini kwa upande mwingine huwadhuru.''
Wanawake kwani baadhi ya wanawake hutambua saratani ambazo pengine zisingeweza kusababisha matatizo katika kipindi chao cha maisha.

Raila Odinga: Hatutambui ushindi wa Uhuru Kenyatta

Raila Odinga asema hatambui ushindi wa rais Kenyatta
Image captionRaila Odinga asema hatambui ushindi wa rais Kenyatta
Kiongozi wa muungano wa upinzani nchini Kenya Raila Odinga amezungumzia kuhusu uamuzi uliotolewa na mahakama ya juu wa kuidhinisha uchaguzi wa Uhuru Kenyatta.
Kulingna na gazeti la daily Nation, Bwana Odinga kupitia taarifa iliotolewa na mshauri wake Salim Lone, amesema kuwa serikali ya Jubilee sio halali akiongezea kwamba uamuzi huo wa mahakama ya juu ulifanywa kupitia shinikizo.
''Sisi watu wa Nasa tayari, tulikuwa tumeamua kabla ya uamuzi wa mahakama kwamba hatuitambui serikali ya Uhuru Kenyatta'', alisema.
''Uamuzi huo haujabadilishwa na uamuzi wa mahakama ya juu ambao haukutushangaza. Ni uamuzi uliotolewa chini ya shinikizo kubwa ,hatushutumu mahakama tunaihurumia''.
Ushindi wa rais Uhuru Kenyatta mnamo mwezi Oktoba 26 uliidhinishwa na mahakama hiyo kupitia uamuzi wa pamoja wa majaji sita wa mahakama ya juu.
Kulingana na gazeti hilo bwana Lone amedai kwamba mahakama ilikutana chini ya shinikizo kubwa, baada ya kushindwa kukutana kutokana na wasiwasi mkubwa wa kiusalama kufuatia kupigwa risasi na kujeruhiwa kwa dereva wa naibu jaji mkuu kabla ya kusikizwa kwa kesi ya uchaguzi wa tarehe 26 Oktoba.

Wezi wachimba handaki na kuiba milioni 50 za benki Kenya

Wezi wachimba handaki na kuiba milioni 50 za benki Kenya
Image captionWezi wachimba handaki na kuiba milioni 50 za benki Kenya
Maafisa wa polisi wanachunguza wizi wa shilingi milioni 50 uliofanyika katika tawi moja la benki ya KCB mjini Thika nchini Kenya.
Kufuatia kisa hicho kamanda wa polisi katika kaunti ya Kiambu Adiel Nyange amesema kuwa watu watatu wamekamatwa.
Kulingana na polisi hao, majambazi hao waliingia katika chumba cha kuhifadhi fedha cha benki hiyo kupitia handaki walilochimba chini ya ardhi na kuiba fedha hizo ambazo zilikuwa zimehifadhiwa ndani ya chumba hicho.
Wanaaminika kukata masanduku mawili ya kuhifadhia fedha hizo kwa kutumia mwako wa moto.
Polisi wanasema kuwa meneja wa benki hiyo aligundua kwamba benki hiyo imeibiwa muda wa saa mbili alfajiri wakati alipofungua chumba hicho cha kuhifadhia fedha.
''Majambazi hao lazima walikuwa na mtu anayefanya kazi katika benki hiyo aliyewaongoza hadi pale masunduku hayo yalipokuwa. Uchunguzi unaendelea'' , alisema naibu wa kamanda wa polisi Bernard Ayoo.

Utafiti: Ni hatari kwa wajawazito kulalia migongo yao

Wanawake wameshauriwa kulala kwa kutumia upande katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito wao ili kuzuia kujifungua watoto waliofariki tumboni.Haki miliki ya pichaSCIENCE PHOTO LIBRARY
Image captionWanawake wameshauriwa kulala kwa kutumia upande katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito wao ili kuzuia kujifungua watoto waliofariki tumboni.
Wanawake wameshauriwa kulala kwa kutumia upande katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito wao ili kuzuia kujifungua watoto waliofariki tumboni.
Utafiti wa zaidi ya wanawake 1000 ulibaini kuwa hatari ya mtoto kufariki tumboni miongoni mwa wanawake wajawazito inaongezeka marudufu iwapo watalala kwa kutumia mgongo wao miezi mitatu ya mwisho katika ujauzito.
Utafiti huo ulichunguza mimba 291 zilizoharibika na wanawake 751 waliofanikiwa kupata watoto.
Watafiti wanasema kuwa upande ambao wajawazito hulalia ni muhimu sana na kwamba hawafai kuwa na tashwishi yoyote wanapoamka na kugundua wamelalia migongo yao.
Takriban mimba 225 nchini Uingereza huishia mtoto kuharibika na watafiti wa utafiti huo wanakadiria kwamba takriban maisha ya watoto 130 kila mwaka yataokolewa iwapo wanawake wataendea kulala kwa kutumia upande wa kulia ama kushoto.
Utafiti huo wa MiNESS uliochapishwa katika jarida la Kujifungua ni mkubwa wa aina yake na unathibitisha tafiti ndogo nchini New Zealnd na Australia.

Mugabe akataa kuachia madaraka Zimbabwe licha ya shinikizo

Wengi walitarajia kwamba Robert Mugabe angetangaza kujiuzuluHaki miliki ya pichaSTR/AFP/GETTY
Image captionWengi walitarajia kwamba Robert Mugabe angetangaza kujiuzulu
Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ameapa kuendelea kuongoza taifa hilo kwa wiki kadha, licha ya shinikizo kutolewa kumtaka aachie madaraka.
Akihutubu moja kwa moja kupitia runinga ya taifa, Bw Mugabe amesema anapanga kuongoza mkutano mkuu wa chama mwezi Desemba.
Maafisa wakuu wa chama hicho cha Zanu-PF walikuwa wameidhinisha hatua ya kumvua uongozi wa chama hicho na kumpatia saa 24 ajiuzulu la sivyo wamuondoe madarakani.
Jeshi lilichukua udhibiti wa serikali wiki iliyopita, huku mzozo kuhusu nani atamrithi ukizidi kutokota. Bw Mugabe ameonekana kupoteza udhibiti wa chama chake.
Mzozo wa sasa ulianza Bw Mugabe alipomfuta kazi makamu wake Emmerson Mnangagwa wiki mbili zilizopita, hatua iliyolikera jeshi ambalo lilitazama hatua hiyo kama jaribio la kumteua mke wake Grace kuwa makamu wa rais na mwisho kuwa mrithi wake.
MugabeHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Mapema Jumapili, Bw Mnangagwa alitawazwa kuwa kiongozi mpya wa chama cha Zanu-PF na mgombea wake wa urais uchaguzi mkuu wa 2018.
Katika mkutano huo pia, Grace Mugabe, 52, alifukuzwa kutoka kwa chama hicho pamoja na maafisa wengine wakuu.
"Mkutano mkuu wa chama (cha Zanu-PF) utafanyika wiki chache zijazo na nitauongoza na kusimamia shughuli zake," Rais Mugabe ameliambia taifa kupitia runinga, akiwa ameandamana na majenerali kadha wakuu jeshini.
Amekiri uokosoaji dhidi yake kutoka kwa Zanu-PF, jeshi na umma, na kusisitiza kwamba ipo haja ya hali ya kawaida kurejea.
"Bila kujali faida au madhara ya jinsi (jeshi) walitekeleza operesheni yao, mimi, kama amiri jeshi mkuu, nakiri kwamba kuna matatizo," amesema, akirejelea hatua ya jeshi ya kuchukua udhibiti wa runinga ya taifa wiki iliyopita.
Hata hivyo, hakuzungumzia uwezekano wake kujiuzulu.
Raia wengi nchini Zimbabwe wameonekana kushangazwa na hotuba ya Bw Mugabe ambaye alitarajiwa na baadhi yao kujiuzulu.
Mugabe alikutana na wakuu wa jeshi ambao wamechukua udhibiti wa serikali mapema leoHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionMugabe alikutana na wakuu wa jeshi ambao wamechukua udhibiti wa serikali mapema leo
Kiongozi wa chama chenye ushawishi cha maveterani wa vita vya ukombozi wa Zimbabwe Chris Mutsvangwa, ameambia shirika la habari la AFP kwamba sasa Robert Mugabe huenda akaondolewa madarakani baada yake kukosa kujiuzulu leo.
Amesema hotuba ya kiongozi huyo haijazingatia uhalisia.
"Tutafuata njia ya kumuondoa madarakani na tunawataka watu warejee tena barabarani kuandamana."
Maveterani walikuwa wakati mmoja wafuasi sufu wa Bw Mugabe.
Waliongoza uvamizi wa mashamba yaliyomilikiwa na Wazungu mwaka 2000 na wametuhumiwa kwa kutumia ghasia na fujo uchaguzini kumsaidia Mugabe kusalia madarakani.
Lakini mwaka jana, waliacha kumuunga mkono.
Kiongozi wa upinzani nchini Zimbabwe Morgan Tsvangirai ambaye wakati mmoja alihudumu kama waziri mkuu katika serikali ya umoja wa taifa na Rais Robert Mugabe ameambia shirika la habari la Reuters kwamba ameshangazwa sana na hotuba ya Mugabe.
Sawa na baadhi ya raia wengine Zimbabwe, kiongozi huyo wa chama cha Movement for Democratic Change (MDC) amesema alikuwa anamtarajia Mugabe, 93, ajiuzulu baada ya jeshi kuchukua udhibiti wa serikali wiki iliyopita.
"Nimeshangaa sana. Si mimi pekee, bali taifa lote. Anacheza mchezo fulani. Amevunja matarajio ya taifa lote."
Bado haijabainika ni vipi Rais Robert Mugabe anaweza kuongoza mkutano huo mkuu wa chama cha Zanu-PF mwezi ujao, baada yake kuvuliwa uongozi.
MnangagwaHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionBw Mnangagwa anatarajiwa kuchukua uongozi wa chama cha Zanu-PF
Nyadhifa kwenye chama kuamuliwa kwenye mkutano huo na Bw Emmerson Mnangagwa anaweza kuchukua uongozi wa nchi wakati huo.
Bw Mugabe ameongoza Zimbabwe kwa miaka 37 tangu taifa hilo lilipojipatia uhuru mwaka 1980 kutoka kwa Uingereza.
Hotuba hiyo yake kupitia kwenye runinga Jumapili ilikuwa mara yake ya pili kuonekana hadharani tangu jeshi lilipotangaza kuchukua udhibiti wa taifa hilo katika kile walichosema ni juhudi za kuondoa "wahalifu" ambao wamemzingira rais.
Ijumaa, alihudhuria mahafali katika chuo kikuu wazi cha Zimbabwe, lakini hakutoa tamko lolote wakati huo.

Amuua mkewe kwa kukataa kushiriki tendo la ndoa

Migogoro ya kiyumbani ndio yenye visa vingi vilivyoripotiwa dhidi ya wanawake nchini India kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.
Image captionMigogoro ya kiyumbani ndio yenye visa vingi vilivyoripotiwa dhidi ya wanawake nchini India kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.
Maafisa wa polisi wanasema kuwa mwanamume mmoja katika jimbo la kaskazini mwa India la Haryana amemuua mkewe baada ya kukataa kushiriki naye tendo la ndoa.
Sanjiv Kumar mwenye umri wa miaka 35 alidaiwa kumyonga mkewe ,Suman wakati wa vita siku ya Jumanne.
Mwanamume huyo alikiri kutekeleza kitendo hicho baada ya kukamatwa , afisa wa polisi Ramesh Jaglan aliambia BBC.
Migogoro ya kiyumbani ndio yenye visa vingi vilivyoripotiwa dhidi ya wanawake nchini India kwa zaidi ya muongo mmoja sasa.
''Alikuwa akikataa kufanya ngono kwa muda .Siku ya Jumanne alikataa tena, hatua iliomuudhi na kuamua kumnyonga.Tumemkamata'', bwana Jaglan aliambia BBC.
Wanandoa hao walikuwa wameoana kwa zaidi ya muongo mmoja. Wana watoto wawili.

Pope Francis awataka polisi kuwa na ''huruma'' kwa madereva

Wiki iliyopita, Papa alibariki gari alilopewa kama zawadi ambalo sasa linapigwa mnada kwa ajili ya kupata pesa za msaadaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionPapa Francis anasema mitaa imebadilishwa kuwa kama njia za magari ya mashindano ya ''Formula One''
Madereva wanaokamatwa na polisi kwa kuendesha magari kwa kasi kubwa wanaweza kumnukuu Papa wanapoomba msamaha kwa polisi.
Katika mkutano na maafisa wa polisi wa usalama barabarani nchini Italia, Pope Francis aliwaomba waonyeshe "huruma " kwa madereva wanaovunja sheria za barabarani.
"huruma sio ishara ya udhaifu", alisema Papa. "Nawala haimaanishi kuacha kutumia nguvu ."
Aliongeza kusema kuwa polisi wanapaswa kutambua ni kwa nini mtu amefanya kosa.
Papa alikiri kuwa wakati mwingine husinzia akiwa kwenye maombi.
Hata hivyo alizungumzia kuhusu "ongezeko kubwa la makosa'' ya barabarani.
Alisema kuwa hali ya maisha ya watu kuwa na " haraka na ushindani " vimesababisha watu kuwaona madereva wenzao barabarani ''kama vizuwizi " ama washindani wao wanaopaswa kupitwa barabarani, na hivyo kuibadili mitaa kuonekana kama njia za mashindano ya magari ya Formula One".
Papa, ambaye amekuwa kiongozi wa kanisa Katoliki la Roma tangu mwaka 2013, pia aliwakosoa watu wanaotumia simu zao za mkononi wakati wanapoendesha magari.
"lazima tuangalie uwezo mdogo wa madereva wengi wa uwajibikaji, ambao mara kwa mara hawatambui madhara makubwa yanayotokana na kutokuwa kwao makini ," alisema.
Wiki iliyopita, Papa alibariki gari alilopewa kama zawadi ambalo sasa linapigwa mnada kwa ajili ya kupata pesa za msaada.

Kenya yapiga marufuku matangazo ya moja kwa moja ya mikutano ya kisiasa

Polisi Kenya wawatawanya waandamanaji mjini Nairobi waliokuwa wanamsindikiza kiongozi wa upinzani Raila Odinga baada ya kurejea kutoka ziarani Marekani.
mamlaka ya mawasiliano ya Kenya, imetangaza kupigwa marufuku kwa upeperushaji wa matangazo ya moja kwa moja wa mikutano ya kisiasa, katika kile ilichokiita “kusaidiA kupunguza hali ya taharuki nchini.”
SIiku ya Jumapili polisi nchini humo walitumia mabomu ya machozi kuwatawanya watu waliokuwa wanaandamana mjini Nairobi kupinga mauaji ya watu wanne yaliyotekelezwa jaJumamosi usiku katika mtaa mmoja wa mabanda mjini humo.
Kwa mujibu wa shirika la habari la Reuters, baadhi ya mitaa ya mji huo imekumbwa na hali ya taharuki tangu Ijumaa, wakati takriban watu watano waliuawa kufuatia makanbiliano kati ya polisi na wafuasi wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga, ambaye alikuwa amerejea kutoka ziarani Marekani.
Polisi hata hivyo wamesema waliouawa ni wahalifu.
Haya yamejiri siku moja tu kabla ya mahakama ya juu ya Kenya kutoa uamuzi wake kufuatia kesi zilizowasilishwa kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais wa tarehe 26 mwezi jana.
Jaji mkuu David Maraga ametangaza kwamba uamuzi huo utatolewa saa tano asubuhui siku ya Jumatatu.

Trump aiweka Korea Kaskazini kwenye orodha wa wafadhili wa ugaidi

Rais Donald Trump wa Marekani ameiweka Korea Kaskazini kwenye orodha ya Mataifa yanayofadhili ugaidi, na kutishia kuimarisha zaidi vikwazo dhidi yake, lakini waziri wa mambo ya nje amesema bado diplomasia inayo nafasi.

UN Generalversammlung in New York | Donald Trump, Präsident USA (Getty Images/S. Platt)
Rais wa Marekani Donald Trump
Kwa tangazo hilo la Rais Trump, Korea ya Kaskazini imeongezwa kwenye orodha ya nchi ambazo Marekani inazichukulia kama wadhamini wa ugaidi duniani, ambayo tayari inazo Iran na Syria. Rais huyo amewashambulia tena watangulizi wake, akisema anayoyafanya leo yalipaswa kufanywa miaka mingi iliyopita.
Mbali na kuishutumu Korea Kaskazini kuendesha mpango haramu wa nyuklia na makombora, vile vile Donald Trump amesema nchi hiyo inaendesha mauaji nje ya ardhi yake, ingawa hakuna visa vya mauaji kama hayo vinavyojulikana kufanywa na serikali ya mjini Pyongyang, mbali na kile kilichomuuwa kaka wa kiongozi wa sasa Kim Jong-un.
Akitangaza uamuzi wake katika kikao cha baraza la mawaziri mjini Washington, Trump amesema baada ya mchakato mzima kukamilika, Korea Kaskazini itakabiliwa na vikwazo vikali kabisa. Amesema, ''Hatua hii inaongeza vikwazo na adhabu kwa Korea Kaskazini na watu wenye mafungamano na nchi hiyo, na itasaidia kuitenga kabisa nchi hiyo inayoongozwa na serikali ya wauaji, kama ambavyo mmekuwa mkisoma na wakati mwingine mkiandika.''
Trump ameongeza kwamba kuwa kuanzia Jumatano wizara ya mambo ya nje itatangaza vikwazo vya ziada, vikali kabisa dhidi ya Korea Kaskazini, na kwamba mchakato huo utadumu kwa wiki mbili.
Tillerson atofautiana na Trump
Hata hivyo, akizungumza na waandishi wa habari baada ya tangazo la Rais Trump, waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema Marekani bado ina matumaini kwamba mchanganyiko wa vikwazo na juhudi za kidiplomasia unaweza kutumiwa kumshawishi kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kuja kwenye meza ya mazungumzo kuhusu mpango wake wa nyuklia wenye utata.
Nordkorea Kim Jong Un Statement zu Trump und seine UN Rede (Reuters/KCNA)
Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un, ambaye waziri wa mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson amesema vikwazo vimemziba mdomo
Tillerson amesema tayari wanazo taarifa kwamba vikwazo vya bidhaa za petroli ambavyo China imeikea Korea Kaskazini vimeanza kuporomosha mapato ya Korea Kaskazini. ''Ni kutokana na athari hizo kwamba nchi hiyo haijafanya tena uchokozi wake kwa muda wa siku 60 zilizopita,'' amesema Tillerson, akimaanisha Korea Kaskazini.
Hata hivyo, wachambuzi wanasema hatua hii ya Trump dhidi ya Korea Kaskazini ni ya kiishara tu, kwa tayari Marekani imeiwekea nchi hiyo vikwazo chungu nzima.
Korea ya Kaskazini imeizoea orodha hiyo
Hii sio mara ya kwanza Marekani kuiweka Korea Kaskazini katika kundi linalofadhili ugaidi. Nchi hiyo inayoongozwa kwa usiri mkubwa ilikuwa tayari kwenye orodha hiyo hadi mwaka 2008, wakati Rais George W Bush alipoiondoa kwenye orodha hiyo, ili kuweka shinikizo zaidi kwa nchi nyingine ambazo zilikuwa haziibani vya kutosha Korea Kaskazini.
Wataalamu wanaamini kuwa Korea Kaskazini kwamba katika muda wa miezi kadhaa, Korea Kaskazini itapata makombora ya masafa marefu yanayoweza kufyatuliwa kutoka bara moja na kutua bara jingine, yakiwa na uwezo kufanya mashambulizi dhidi ya Marekani. Ikulu ya Rais Donald Trump imesema kamwe haitairuhusu Korea Kaskazini kupata uwezo huo.

Mahakama yaamua Kenyatta ni Rais halali

Rais Uhuru Kenyatta
Mahakama ya Juu ya Kenya, Jumatatu imetoa uamuzi kuwa Rais Uhuru Kenyatta alichaguliwa kihalali katika zoezi la marudio ya uchaguzi wa urais uliyofanyika Oktoba 26.
Kenyatta alipata zaidi ya asilimia 98 ya kura katika uchaguzi uliosusiwa na Muungano wa Upinzani.
Majaji wote sita waliosikiliza kesi hiyo wameamua kwa kauli moja kwamba Kenyatta alichaguliwa kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.
Kwa mujibu wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini humo, IEBC, waliojitokeza kupiga kura walikuwa chini ya asilimia 39 ya Wakenya milioni 19.6 waliojiandikisha.
Mgombea wa upinzani, Raila Odinga, ambaye alijitoa kwenye kinyang'anyiro hicho, aliwataka wafuasi wake kususia uchaguzi huo, na waandamanaji waliwazuia maafisa wa tume ya uchaguzi kufungua vituo vya kupigia kura katika ngome za upinzani. Odinga alisema uchaguzi huo ulikuwa ni aibu.
Maombi ya walalamikaji watatu yaliwasilishwa kwenye mahakama hiyo, na yote yametupiliwa mbali.