Wednesday, September 20

Hotuba ya Trump kwenye Umoja wa Mataifa yakosolewa

US President Donald Trump at the UN General Assembly in New York, 19 SeptemberHaki miliki ya pichaEPA
Image captionHotuba ya Trump kwenye Umoja wa Mataifa yakosolewa
Hotuba ya kwanza kuu ya rais wa Mareknai Donald Tump kwenye Umoja wa Mataifa imekosolewa na baadhi ya chi wanachama.
Rais Trump alizitaja nchi zikiwemo Iran akisema pia kuwa Marekani itaiharibu kabisa Korea Kaskazini ikiwa italazimika kafanya hivyo.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Iran alisema, "hotuba ya Trump ni ya wakati ya mikutano ya wanahabari wala sio kwa Umoja wa Mataifa.
Donald Trump speaks to world leaders at the UN General Assembly at UN headquarters in New York, 19 SeptemberHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHotuba ya Trump kwenye Umoja wa Mataifa yakosolewa
Korea Kaskazini bado haujajibu tisho la Trump kuwa itaharibiwa.
Hotuba ya Trump ilizungumzia zaidi dunia yenye mataifa huru ambayo yana malengo ya kuinua maisha ya watu wao, lakini akatumia muda mwingi akilenga kile alichokija kuwa mataifa yanayoleta matatizo duniani.
Marekani mara kwa mara imeionya Korea Kaskazini kwa majaribio yake ya zana, yanayokiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa.
Kim Jong-un watches a missile launch from North Korea, 16 SeptemberHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionMarekani mara kwa mara imeionya Korea Kaskazini kwa majaribio yake ya zana, yanayokiuka maazimio ya Umoja wa Mataifa
Siku ya Jumanne Trump alimkosoa Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un, akimtaja kuwa mtu wa makombora ambaye yuko katika harakati za kujitia kitanzi.
"Ikiwa Marekani italazimika kujilinda na washirika wake, hatutakuwa na cha kufanya bali tutaiharibu kabisa Korea Kaskazini," aliongeza Trump.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Sweden ambaye alikuwa ameketi katika kikao hicho, alisema kuwa ilikuwa hotuba mbaya, wakati usiofaa na kwa watu wasiostahili.
Trump speaking at the UNHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHotuba ya Trump kwenye Umoja wa Mataifa yakosolewa
Trump pia aliishambulia nchi ya Venezuela akitaja serikali yake kuwa fisadi na ya kiimla na kuonya kuwa Marekani iko tayari kuichukulia hatua.
Waziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Venezuela Jorge Arreaza alipinga kile alichokitaja kuwa vitisho.
"Trump sio rais wa dunia, hata hawezi kuongoza serikaii yake," alisema.
A five-part composite showing reactionHaki miliki ya pichaUN / EVN
Image captionWaakilishi kutoka Israel, Syria, Iran, na Saudi Arabia wakiisikiliza hotuba ya Trump
Akizungumza katika kikao hicho rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, aliteta mkataba wa nyuklia na Iran, akisema kuwa kuuvunja itakuwa makosa makubwa.
Lakini waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alimuunga mkono Bw. Trump. Kwenye hotuba yake aliseka mkataba wa Iran unastali kufanyiwa marekebisho au ufutwe kabisa, na kuonya dhidi ya kukua kwa ushawishi wa Iran eneo la mashariki ya kati.

Tetemeko laua zaidi ya watu 200 Mexico

Waokoaji wakijitahidi kuwatoa watu katika vifusiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionWaokoaji wakijitahidi kuwatoa watu katika vifusi
Tetemeko baya la ardhi limekumba maeneo ya katikati mwa Mexico na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 200.
Tetemeko lenye nguvu ya kipimo cha saba nukta moja limedondosha karibu majengo 30 katika mji mkuu wa Mexico city.
Watu wanaotoa huduma za dharura wakisaidiwa na mamia ya watu wanaojitolea bado wanaendelea kutafuta manusura ambao wamefukiwa na kifusi.
Maafisa wa serikali nchini wanasema idadi ya waliokufa inaweza kuongezeka.
Tetemeko laua zaidi ya watu 100, MexicoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionTetemeko laua zaidi ya watu 200, Mexico
Daniel Lieberson alikuwa katika hotel ya Hilton Mexico City wakati tukio hilo likitokea.
''...Nilikuwa katika ghorofa ya 26. jengo lilikuwa likiyumba mbele na nyuma vioo vyote vilivunjika na tuliogopa kwamba madirisha yatavunjika, lakini haikuwa hivyo. Lakini mashine ya kutengenezea kahawa na vitu vingine vilianguka chini vyote, meza, ilikuwa shida kweli, lilidumu kwa sekunde thelathini tu, lakini ilionekana kama limedumu daima...'' anasema Daniel Lieberson
Kwa upande wake Natasha Pizzey mwandishi wa habari katika mji huo anasema kuna idadi kubwa ya watu waliofukiwa na kifusi baada ya majengo kuporomoka.
Juhudi za uokoaji zikiendeleaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionJuhudi za uokoaji zikiendelea
''..Tunafahamu kuna watu walionusurika katika majengo ya makazi yaliyoporomoka, hatukuwa na uwezo wa kuwaokoa. Kuna mamia ya wafanyakazi wa kujitolea waliokwenda katika eneo la tukio...'' ameongezea kusema
Aidha pia kumetokea madhara mabaya katika majimbo ya jirani ya Morelos na Puebla.
Mapema mwezi huu tetemeko hilo la ardhi pia lilipita katika eneo la pani ya kusini magharibi mwa Mexico na kusababisha vifo vya watu 90.
Tetemeko laua zaidi ya watu 100, Mexico
Image captionTetemeko laua zaidi ya watu 200, Mexico

Nyambizi ya Ujerumani iliyozama wakati wa vita vya kwanza vya dunia yapatikana

Another sketch of the U-boat wreckHaki miliki ya pichaT TERMOTE
Image captionMchoro unaonyesha chombo kikiwa hali nzuri
Mabaki ya nyambizi ya Ujerumani ambayo ilizama wakati wa vita vya kwanza vya dunia imepatikana huko North Sea na maafisa wanasema kuwa huenda bado miili 23 iko ndani ya manowari hiyo.
Nyambizi hiyo ya UB-II ambayo inatajwa kuwa katika hali nzuri iko mita 30 chini ya bahari nje wa pwani ya ubelgiji.
"Nyambizi hiyo iko hali nzuri na tunaamini kuwa huenda miili yote bado imo," alise gavana wa West Flanders ,Carl Decaluwé.
Chombo hicho kinaamiminiwa kuzamishwa na mlipuko.
File pic of German UB-II class submarine from World War OneHaki miliki ya pichaTOMAS TERMOTE
Image captionEneo iliko nyambizi hiyo limewekwa siri kuzuia watu kulikaribia
Bw. Decaluwé aliwaambia waandishi wa hababri siku ya Jumanne kuwa eneo iliko nyambizi hiyo limewekwa siri kuzuia watu kulikaribia
Nyambizi 11 za Ujerumani kutoka kwa vita vya kwanza vya dunia zimepatikana katika maji ya Ubelgiji lakini chombo hiki kinatajwa kuwa kilicho katika hali nzuri zaidi.
Nyambizi za UB-II zilijengwa kati ya mwaka 1915 na 1916 na zilikuwa na uwezo wa kuzama hadi umbali wa mita 50.
File pic of German UB-II class submarine from World War OneHaki miliki ya pichaALAMY
Image captionEneo iliko nyambizi hiyo limewekwa siri kuzuia watu kulikaribia

Mkimbizi wa Iraqi asifiwa kwa kurejesha pesa alizookota

Treni mjini BerlinHaki miliki ya pichaAFP
Image captionMkobaulikuwa na €14,000 sawa na dola $16,800 ulikuwa umeachwa ndani ya treni na kikongwe mwenye umri wa miaka 79
Polisi mjini Berlin wamemsifu mkimbizi wa Iraqi aliyekabidhi pochi aliyoipata ikiwa na kitita cha dola $16,800.
Pochi hiyo iliachwa ndani ya treni Ijumaa iliyopita usiku na mwanamke kikongwe mmoja mwenye umri wa miaka 79.
Muda mfupi baada ya kuiacha pochi yake , aligundua kosa lake na kuwaarifu maafisa wa mamlaka ya usafiri wa relilakini hawakuweza kuipata pochi hiyo.
Aliyeipata ni mwanafunzi wa miaka 16 kutoka Iraqi , ammbaye alimuarifu mama yake . Siku mbili baadae waliikabidhi pochi hiyo kwa Polisi wa Berlin Jumanne.
Polisi wali Tweet wakimpongeza mvulana huyo.
"Mwanafunzi alipata pochi ikiwa na Euro €14,000 na akaikabidhi kwa polisi. Mmiliki wa pesa amefurahi. Tunasema vizuri sana na asante ,"iliandikwa Tweeter ya polisi.
Familia yake ambayo inaishi katika kituo cha kuwapokea wakimbizi, huenda ikazawadiwa kwa uaminifu wao, kulingana na vyombo vya habari vya Ujerumani.
Chini ya sheria ya Ujerumani, zawadi anayopaswa kupewa mtu aliyeokota kitu ama pesa ya mtu ni asilimia tatu ya thamani yake. Kulingana na sheria hii familia ya mtoto huyo inaweza kupata zawadi ya €210.

Hakimu awataka Kitilya, wenzake kuwa na subira

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemtaka mwenyekiti wa kampuni inayoshughulikia uwekezaji wa mitaji na dhamana (Egma), Harry Kitilya na wenzake kuwa na imani pamoja na subira dhidi ya upelelezi wa kesi ya utakatishaji fedha inayowakabili kwa kuwa unakaribia kufika mwisho.
Hayo yamesemwa leo Jumatano na Hakimu Mfawidhi, Cyprian Mkeha wakati kesi hiyo ilipotajwa.
Kabla ya Hakimu Mkeha kusema hayo, Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kishenyi Mutalemwa alieleza kuwa mara ya mwisho waliomba siku 14 ili waweze kuelezea hali ya upelelezi ulipofikia lakini wameshindwa hivyo wakaomba kuongezewa muda ili tarehe ijayo waweze kueleza.
Alieleza kuwa wanafanya jitihada kuona upelelezi unakamilika na akaomba tarehe ya kutajwa kwa kesi hiyo.
Baada ya Kishenyi kueleza hayo, wakili wa utetezi, Masumbuko Lamwai alidai kuwa kesi ilifikishwa mahakamani hapo Aprili Mosi, 2016, hivyo ni karibu mwaka mmoja na nusu sasa, mashtaka yanayowakabili wateja wake yanahusisha nyaraka ambazo wanazo na kwamba hakuna uchunguzi nje ya nyaraka.
Wakili Lamwai amesema walikuwa wakilalamikia kesi ya utakatishaji fedha kuwa imewekwa kwa makusudi ili wateja wao wakae gerezani.
"Kwa mtu anayekaa gerezani kwa mwaka mmoja na nusu, kuambiwa upelelezi bado haujakamilika inaleta mshangao.
"Hii kesi imekuwa kama ya kukomoana komoana hivi, mheshimiwa wateja wetu ni watu wazima wanashughuli zao na nyingine zimefilisika kwa kukosa usimamizi," ameeleza Wakili Lamwai mahakamani hapo.
"Tunajua mahakama haina uwezo wa kusikiliza kesi hii lakini upande wa mashtaka wanatumia vibaya taratibu za kimahakama."
Baada ya kutolewa kwa maelezo ya pande hizo zote mbili, Hakimu Mkeha amewaambia washtakiwa kuwa upelelezi unaofanywa unakaribia mwisho akaomba wawe na imani, kwa kuwa amejiridhisha yeye mwenyewe kwa macho yake kuwa upelelezi unakaribia kufika mwisho.
Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 5, 2017. Washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni maofisa wa benki ya Stanbic, Shose Sinare na  Sioi Solomon.  
Washtakiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya kula njama, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa dola milioni 6 za Marekani.
Wanadaiwa kutenda makosa hayo kati ya Machi 2013 na Septemba 2015 wakati wa mchakato wa mkopo wa dola za Marekani 550 milioni  kwa  serikali ya Tanzania kutoka Benki ya Standard Uingereza.

Rais Museveni aagiza uchunguzi ajali iliyoua Watanzania 13

Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema upelelezi kubaini sababu za ajali iliyosababisha vifo vya Watanzania 13 waliokuwa wakitoka harusini nchini humo unaendelea.
Waziri wa Ofisi ya Rais anayeshughulikia Jiji la Kampala, Bety Kamya akisoma salamu za rambirambi kutoka kwa Rais Museveni amesema licha ya kutoa pole kwa familia, kiongozi huyo ameagiza uchunguzi wa sababu za ajali ufanyike.
Amesema pia amewapongeza maharusi, Dk Aneth na Dk Trease Ibingira na amewatakiwa maisha mema ya ndoa.
Mbali ya hilo, amesema anawaombea ili kukabiliana na kipindi kigumu walichonacho.
Amesema Rais anawashukuru Watanzania kwa kuwa wavumilivu katika kipindi kigumu cha kupoteza wapendwa wao.
"Nakabidhi vyeti hivi vya vifo vya ndugu zetu 13 nawapa pole sana," amesema Waziri Kamya akimkabidhi vyeti hivyo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angellah Kairuki.
Waziri Kairuki amesema Rais John Magufuli amepokea taarifa ya vifo hivyo kwa mshtuko na alitoa maelekezo ya kupokewa miili hiyo, kuhifadhiwa kwenye Hospitali ya Jeshi Lugalo, kuagiwa hapo na kusafirishwa kwa maziko.
Amesema maagizo hayo wanaendelea kuyatekeleza ikiwa ni pamoja na kutoa magari kwa ajili ya kusafirisha miili hiyo.
Waziri Kairuki amesema kwa namna isiyo katika wakati wa kawaida, anawapongeza maharusi na kuwatakia maisha mema.
"Haya ni mapenzi ya Mungu, hili lisiwanyong'onyeshe maharusi," amesema Kairuki.
Ameishukuru Serikali ya Uganda kwa kukodi ndege kuirudisha nyumbani miili hiyo.

Zitto asakwa


Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT –Wazalendo), Zitto Kabwe anatafutwa ili akamatwe na kufikishwa mbele ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge.
Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah amesema leo Jumatano kuwa, Zitto alipewa barua ya wito wa kufika mbele ya kamati hiyo baada ya Spika Job Ndugai kuagiza hilo lifanyike lakini hadi sasa hajaitikia wito huo.
Amesema kamati bado ipo mjini hapa ikiendelea na shughuli baada ya vikao vya Bunge kuahirishwa na inamsubiri.
Dk Kashililah amesema Zitto alipewa barua ya wito lakini alikuwa na udhuru kwa kuwa siku aliyotakiwa kufika mbele ya kamati alikuwa na kikao cha halmashauri
lakini kesho yake angefika kuitika wito.
“Wakati wanamsubiri mara wakamsikia yuko Nairobi (Kenya), kamati inaendelea kumsubiri. Kamati inasema imeagiza wawaone wasije kusema wanatoa hukumu
na wao hawapo,” amesema.
Zitto amepelekwa na Spika Ndugai mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge inayoongozwa na Mbunge wa Newala Mjini (CCM), George Mkuchika akidaiwa kutamka kwenye mitandao ya kijamii kuwa Bunge limewekwa mfukoni na mhimili fulani.
Maneno hayo anadaiwa kuyasema wakati  kamati mbili za Spika kutathmini mfumo wa uchimbaji, usimamizi, umiliki na udhibiti wa madini ya Tanzanite na almasi zilipowasilisha taarifa.

NMB yaipa ‘mkwanja’ Alat


Benki ya NMB imetoa hundi ya Sh100 milioni kuwezesha mkutano mkuu wa Jumuiya ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Alat), utakaofanyika Oktoba 2 hadi 6 jijini Mbeya.
Richard Makungwa, ofisa mkuu wa idara ya wateja wakubwa na Serikali wa NMB   amesema wametoa fedha hizo kuunga mkono jitihada za Alat na kuiwezesha iwajibike ipasavyo kulingana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia.
"Halmashauri zipo karibu na wananchi ambao sisi tunawahudumia, kwa hiyo mchango wetu unalenga kuona malengo waliyopanga yanafikiwa," amesema.
Makamu Mwenyekiti wa Alat, Steven Mhapa amesema pamoja na mambo mengine, mkutano huo utahimiza halmashauri zote kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda vidogo.
"Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Rais John Magufuli, mkutano huu utawahusisha pia wakurugenzi wote wa halmashauri za wilaya, majiji na manispaa nchini," amesema.
Amesema katika mkutano huo watatumia siku moja kuzungumzia mamlaka mpya iliyoundwa kwa ajili ya masuala ya barabara za miji na vijiji kutokana na umuhimu wake katika ukuaji wa uchumi.

Rais Magufuli aagiza ukuta mkubwa kujengwa migodi ya Tanzanite


Rais John Magufuli ameagiza kujengwa uzio katika eneo linalozunguka machimbo ya Tanzanite liliko Simanjiro ikiwa ni hatua yake ya kutaka kukabiliana na utoroshwaji wa rasilimali hiyo.
Amelisisitiza Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuanza kazi hiyo haraka iwezekanavyo.
Rais Magufuli ambaye yuko ziarani mkoani Manyara amesema vikosi vya ulinzi na usalama vinapaswa kushirikiana kujenga ukuta huo ambao utaanzia eneo la block A hadi D la machimbo hayo.
Baada ya ujenzi huo kukamilika ametaka kufungwa mitambo maalumu ikiwamo kamera zitakazokuwa na uwezo kutambua na kubaini matukio yoyote yanayotendeka katika eneo hilo.
“Nataka ukuta huu uanze mara moja tena JWTZ kupitia Suma JKT waanze kazi hii mara moja na baada ya kukamilika eneo hili liwe na mlango mmoja tu ambao utaweka mtambo wa ukaguzi... wewe ukiweka Tanzanite tumboni tutakubaini, ukiweka kwenye kiatu uonekane pia,” amesema Rais Magufuli.
Amesema lengo la Serikali kufanya hivyo ni kuhakikisha inapata sehemu ya mapato yake na wawekezaji waondoke na haki yao bila kupunjwa upande wowote.
Amesema hataki kuona rasilimali za Taifa zinatoroshwa kienyeji na kwenda kuwafaidisha wajanja wachache walioko nje ya nchi hivyo ili kudhibiti hali hiyo ameamua kuchukua hatua madhubuti.
“Hapa adui yetu siyo CCM au Chadema ama mwingine yeyote, adui yetu ni yule anayopora mali zetu, hatupaswi kugombana sisi wenyewe na kumuacha adui yetu yuko pembeni, naomba tushikamane katika hili maana hii vita ya uchumi siyo lelemama lazima tuwe wamoja,” amesema.
Pia, amesema ndoto yake ni kuona soko la Tanzanite linakuwa Simanjiro ili wafanyabiashara kutoka ng’ambo kama Marekani, India na Ulaya wanafika kwenye eneo hilo kufanya biashara.
“Tunataka soko la Tanzanite linakuwa hapa Simanjiro ili hawa wafanyabiashara wafunge safari waje kununulia hapa na hiyo itakuwa na manufaa pia kwa wafanyabiashara wa eneo hilo maana hata yule mchinja mbuzi ama mwenye gesti atafaidika na ujio huo,” amesema.
Rais Magufuli amesema hayo leo Jumatano wakati akizindua barabara ya kiwango cha lami ya Mererani yenye urefu wa kilometa 26 ambayo imegharimu kiasi cha Sh 32.5 bilioni.  Rais ameahidi kuendelea na kipande kilichobakia ili lami hiyo ifike makao makuu ya Mkoa wa Manyara ambayo ni Babati.

VIDEO-Vigogo mradi wa mwendokasi wapeta mahakamani

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imewaachia huru vigogo watatu wa Mradi wa Mabasi Yaendayo Haraka(DART), akiwemo mtendaji mkuu wa mradi huo, Asteria Mlambo na mwenzao.
Akitoa hukumu hiyo leo Jumatano ni Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage amesema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi 10 wa upande wa mashtaka, vielelezo na ushahidi wa upande wa utetezi ameona upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka yote yaliyokuwa yakiwakabili vigogo hao pasipo kuacha shaka.
Mbali na Mlambo wengine walioachiwa huru ni Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Evodius Katale, Mwanasheria Mkuu wa DART, Francis Kugesha na mkurugenzi wa kampuni ya Yukan, Yuda Mwakatobe.
Washtakiwa hao walikuwa wakikabiliwa na mashtaka ya uhujumu uchumi kwa kula njama, kusababisha hasara ya Sh 83.5 milioni.
Katika kesi hiyo ilidaiwa kuwa Septemba Mosi na Oktoba Mosi, mwaka 2013 maeneo ya  Kinondoni Dar es Salaam, Mlambo, Katale na Kugesha wakiwa wafanyakazi wa mradi huo, walishindwa kutekeleza majukumu yao vizuri na kuisababishia Serikali hasara ya Sh 83.5 milioni.

Muigizaji akiri kuchepuka


MCHEKESHAJI na pia muigizaji nguli kutoka katika ardhi ya Rais Dolad Trump, Kelvin Hart ameamua kuweka wazi juu ya shutuma alizokuwa amezushiwa juu ya kumsaliti mke wa sasa anaefahamika kwa jina la Eniko Parrish ambaye ni mjamzito kwa sasa.
Katika video aliyoweka katika mtandao wa Instagram Hart aliomba radhi na kusema yeye ni binadamu hivyo anaomba msamaha kwa kitendo hicho alichokifanya huku akitumia dakika moja ipasavyo kwa kumzungumzia mke wake na familia yake kiujumla.
““Niombe radhi kwa mke wangu, watoto wangu nimefanya makosa najua nilipitiwa na nikafanya ujinga huo, hilo kosa nilibebe mimi kweli nilifanya. Mimi ni binadamu daima sijakamilika, nilitegeka katika mazingira ambayo sikutarajia kufanya hivyo,“ alisema.

Rita yazifuta taasisi 230

Kubebea apelekwa zahanati ya Bunge


Mbunge wa Ubungo (Chadema), Saed Kubenea amepelekwa katika zahanati ya Bunge baada ya kujihisi vibaya.
Katibu wa wabunge wa Chadema, David Silinde amesema leo Jumatano kuwa, Kubenea amefika mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge na amewaeleza kwamba hali yake si nzuri.
Kutokana na hilo, amesema amepelekwa kwenye zahanati hiyo na hali yake itakapoimarika atahojiwa na kamati.
Mbunge huyo ambaye alipelekwa Dodoma kwa ndege leo asubuhi, jana Jumanne alisema alikuwa Kituo cha Polisi cha Oysterbay  wilayani Kinondoni akisubiri utaratibu wa safari hiyo ya kwenda kuhojiwa kama Spika wa Bunge Job Ndugai alivyoagiza.

Nyuki waamsha kizaazaa nje ya Mahakama


 Polisi na kundi la waandamanaji waliokusanyika katika eneo la Mahakama Kuu mjini Nairobi wametimua mbio baada ya kuvamiwa na nyuki  wanaodaiwa kuwadhuru watu kadhaa.
Tukio hilo limetokea wakati majaji wa Mahakama wakiongozwa na Jaji Mkuu, David Maraga wakisoma hukumu kamili kuhusu kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa Rais yaliyompa ushindi mgombea wa Jubilee, Uhuru Kenyatta.
Kulikuwa na hali ya taharuki wakati kundi la nyuki lilipovamia eneo hilo ambalo lilikuwa limezingirwa na askari wakiwa na magari ya doria.
Mmoja wa watu waliokuwepo eneo hilo ambaye ni mlemavu alipatiwa msaada kwa kuondolewa kwa gari la wagonjwa baada ya kujeruhiwa na nyuki hao.
Waandishi wa habari walikuwa sehemu ya waliotimua mbio wakinusuru maisha yao kutokana na uvamizi huo.
Kabla ya nyuki kuvamia eneo hilo, baadhi ya wafuasi wa Nasa walisikika wakiwashambulia kwa maneno askari waliokuwa wamezuia barabara kuelekea Mahakama Kuu.
Inadaiwa nyuki walikuwa wameweka maskani karibu na eneo hilo lakini hakuna aliyejua.
Kwa mujibu wa taarifa, kelele za waandamanaji ndizo zilizowafanya nyuki kutoka na kuwashambulia.

Serikali ya Tanzania yalifungia gazeti la mwanahalisi kwa miaka 2


Serikali ya Tanzania yalifungia gazeti la mwanahalisi kwa miaka 2
Image captionSerikali ya Tanzania yalifungia gazeti la mwanahalisi kwa miaka 2

Serikali ya Tanzania imelifungia gazeti la Mwanahalisi kwa miaka miwili zuio hilo pia linahusisha machapisho ya mtandaoni.
Gazeti hilo linafungiwa kwa kile kilicho arifiwa kuwa ni kuchapisha habari za uongo na uchochezi ambazo zinadaiwa kuwa zinaweza kuhatarisha usalama wa taifa hilo.
Mwanahalisi linakuwa gazeti la pili kufungiwa kwa kipindi cha miezi minne .
Gazeti hilo limepigwa kufuli kutokana na kuchapisha mlolongo wa habari ambazo zinasemekana kuwa za kichochezi ikiwemo yenye kichwa cha habari 'Tumwombee Magufuli au Tundu Lissu' iliyochapishwa katika toleo la 409 la tarehe 18-24 Septemba 2017 .
Hivi karibuni vyombo vya habari vimekuwa vikimulikwa kwa ukaribu nchini humo. Mapema mwaka huu Raisi Magufuli alionya vyombo vya habari 'visifikiri viko huru kwa kiwango hicho.'