Thursday, September 14

''Wanawake hupoteza hamu ya ngono ikilinganishwa na wanaume''

Wanawake hupoteza hamu ya tendo la ngono ikilinganishwa na wanaumeHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionWanawake hupoteza hamu ya tendo la ngono ikilinganishwa na wanaume
Wanawake wana uwezo mkubwa wa kupoteza hamu ya kufanya tendo la ngono katika ndoa kulingana na utafiti wa tabia za ngono uliofanywa nchini Uingereza.
Utafiti huo umebaini kwamba huku wanawake na wanaume wakionekana kupoteza hamu ya tendo la ngono kutokana na umri wao, wanawake wengi hupoteza hamu hiyo wanapoishi na wapenzi wao kwa muda mrefu.
Kwa jumla hali mbaya ya afya mbali na ukosefu wa uhusiano wa kihisia unaathiri hamu ya jinsia zote mbili ya kufanya tendo la ngono.
Matokeo hayo yanatokana na mahojiano ya wanaume 5000 na wanawake 6,700 yaliochapishwa na shirika la BMJ Open.
Watafiti hao wa Uingereza wamesema kuwa matatizo ya hamu ya ngono yanafaa kutibiwa kwa kumchunguza mtu badala ya kutumia dawa.
Mtaalam wa maswala ya ngono Ammanda Major amesema kuwa kwa binadamu kukosa hamu ya tendo la ngono sio swala lilisilokuwa la kawaida na kuna sababu nyingi tofauti ambazo wanaume na wanawake wanahitaji mabadiliko.
''Kwa wengine ni kawaida lakini wengine husababisha machungu mengi'' ,alisema.
Kwa jumla asilimia 15 ya wanaume na asilimia 34 ya wanawake waliofanyiwa utafiti huo walisema kuwa walipoteza hamu ya tendo la ngono kwa muda wa miezi mitatu ama hata zaidi katika mwaka uliopita.
Kwa wanaume, ukosefu huo wa hamu ya ngono ulikuwa juu miongoni mwa wanaume wa kati ya umri wa miaka 35-44 huku kwa wanawake ukionekana kati ya umri wa miaka 55 na 64.

Mbunge awasilisha ombi la kuondolewa kwa jaji Maraga Kenya

Jaji mkuu David Maraga
Image captionJaji mkuu David Maraga
Mbunge wa chama tawala cha Jubilee nchini Kenya amewasilisha ombi la kutaka kufutwa kazi kwa jaji mkuu David Maraga.
Mbunge huyo wa Nyeri, Njiri Wambugu amewasilisha ombi lake mbele ya tume ya huduma za majaji akidai kwamba jaji Maraga alihusika katika kufanya makosa.
Akihutubia vyombo vya habari, mbunge huyo anadai kwamba Jaji huyo ''aliwashinikiza'' wenzake kubatilisha matokeo ya uchaguzi wa rais Uhuu Kenyatta wakati alipotoa uamuzi wa kihistoria mnamo tarehe 1 Septemba.
Wambugu amefananisha ubatilishwaji wa matokeo hayo ya urais na mapinduzi ya majaji na sasa anataka nia ya jaji Maraga kuchunguzwa.
Wabunge wa chama cha Jubilee na rais Uhuru Kenyatta wamekuwa wakiukosoa uamuzi wa kufutilia mbali uchaguzi huo na wameendelea na kuwataja majaji hao kuwa ''wakora''.
Naibu wa rais William Ruto amesema kuwa baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa urais wa Oktoba 17, uamuzi huo wa majaji na sababu zao utaangaziwa upya.

Aliyetaka unywele wa Hillary Clinton kutumikia kifungo jela

Aliyekuwa muuzaji dawa Martin Pharma Bro Shkreli kuliaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAliyekuwa muuzaji dawa Martin Pharma Bro Shkreli kulia
Jaji mmoja nchini Marekani amemuhukumu kifungo jela aliyekuwa muuzaji dawa Martin Pharma Bro Shkreli akisubiri hukumu ya kusababisha hofu ya kiusalama.
Jaji Kiyo Matsumoto alisema kuwa chapisho la mtandao wa facebok ambalo Shkreli aliahidi kumzawadi mtu yeyote atakayempatia unywele wa Hillary Clinton lilionyesha kuwa ni hatari kwa umma.
Shkreli aliyewahi kuwa afisa mtendaji wa zamani amekuwa huru baada ya kutoa dhamana ya dola milioni tano tangu alipokamatwa 2015.
Shkreli alitajwa kuwa mtu anayechukiwa zaidi nchini Marekani baada ya kampuni yake ya kuuza dawa kuongeza bei ya dawa zinazotumiwa na wagonjwa wa Ukimwi.
Mnamo mwezi Agosti 2017 alipatikana na hatia ya makosa matatu kuhusiana na usalama na jopo la majaji ambalo pia lilifutilia mbali makosa mengine matano dhidi yake.
Shkreli alikuwa ameshtakiwa kuhusiana na kampuni ya dawa aliyomiliki Retropin mbali na hazina aliyokuwa akisimamia.
Siku ya Jumatano, Jaji Matsumoto aliamua kwamba chapisho hilo la Shkreli mnamo tarehe nne mwezi Septemba lililowekwa muda mfupi kabla ya bi Clinton kuanza ziara yake ya vitabu, lilionyesha kuwa ni hatari akikana hoja ya Shkreli kwamba maneno yake yalilindwa na uhuru wa kujieleza.
Bi Hillary ClintonHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBi Hillary Clinton
Shkreli ambaye amekuwa akisuguana na wakosoaji wake katika mitandao ya kijamii alidai kwamba chapisho hilo lilikuwa la kejeli na la mpangilio wa DNA.
''Hili ni ombi lililochapishwa kwa lengo la kuwazawadi watakaokuletea unywele huo'', alisema jaji huyo.
Wakili wa Shkreli Benjamin Brafmin alisema: Tumekatishwa tamaa.Tunaamini kwamba mahakama ilifanya uamuzi wa makosa .
''Lakini yeye ni jaji na sasa tutalazimika kukubali uamuzi huo''.
Shkreli alipandisha bei ya dawa za ukimwi za Daraprim kwa asilimia 5000 ,2015 na kujipatia jina Pharma Bro.
Bei ya dawa hiyo ilipanda hadi $ 750 kutoka $ 13.50.

Aliyetaka unywele wa Hillary Clinton kutumikia kifungo jela

Aliyekuwa muuzaji dawa Martin Pharma Bro Shkreli kuliaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionAliyekuwa muuzaji dawa Martin Pharma Bro Shkreli kulia
Jaji mmoja nchini Marekani amemuhukumu kifungo jela aliyekuwa muuzaji dawa Martin Pharma Bro Shkreli akisubiri hukumu ya kusababisha hofu ya kiusalama.
Jaji Kiyo Matsumoto alisema kuwa chapisho la mtandao wa facebok ambalo Shkreli aliahidi kumzawadi mtu yeyote atakayempatia unywele wa Hillary Clinton lilionyesha kuwa ni hatari kwa umma.
Shkreli aliyewahi kuwa afisa mtendaji wa zamani amekuwa huru baada ya kutoa dhamana ya dola milioni tano tangu alipokamatwa 2015.
Shkreli alitajwa kuwa mtu anayechukiwa zaidi nchini Marekani baada ya kampuni yake ya kuuza dawa kuongeza bei ya dawa zinazotumiwa na wagonjwa wa Ukimwi.
Mnamo mwezi Agosti 2017 alipatikana na hatia ya makosa matatu kuhusiana na usalama na jopo la majaji ambalo pia lilifutilia mbali makosa mengine matano dhidi yake.
Shkreli alikuwa ameshtakiwa kuhusiana na kampuni ya dawa aliyomiliki Retropin mbali na hazina aliyokuwa akisimamia.
Siku ya Jumatano, Jaji Matsumoto aliamua kwamba chapisho hilo la Shkreli mnamo tarehe nne mwezi Septemba lililowekwa muda mfupi kabla ya bi Clinton kuanza ziara yake ya vitabu, lilionyesha kuwa ni hatari akikana hoja ya Shkreli kwamba maneno yake yalilindwa na uhuru wa kujieleza.
Bi Hillary ClintonHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBi Hillary Clinton
Shkreli ambaye amekuwa akisuguana na wakosoaji wake katika mitandao ya kijamii alidai kwamba chapisho hilo lilikuwa la kejeli na la mpangilio wa DNA.
''Hili ni ombi lililochapishwa kwa lengo la kuwazawadi watakaokuletea unywele huo'', alisema jaji huyo.
Wakili wa Shkreli Benjamin Brafmin alisema: Tumekatishwa tamaa.Tunaamini kwamba mahakama ilifanya uamuzi wa makosa .
''Lakini yeye ni jaji na sasa tutalazimika kukubali uamuzi huo''.
Shkreli alipandisha bei ya dawa za ukimwi za Daraprim kwa asilimia 5000 ,2015 na kujipatia jina Pharma Bro.
Bei ya dawa hiyo ilipanda hadi $ 750 kutoka $ 13.50.

Mazoezi ya kijeshi ya Urusi na Belarus yaanza na kuzua hofu Ukraine

Russian tank (file pic)Haki miliki ya pichaMIL.RU
Image captionKifaru cha Urusi kikielekea kwa mazoezi ya kijeshi ya Zapad
Urusi na Belarus zimeanza mazoezi makubwa ya pamoja ya kijeshi, ambayo yamepewa jina Zapad-2017, na ambayo yamezitia wasiwasi nchi jirani wanachama wa shirika la kujihami la nchi za Magharibi la Nato.
Mazoezi hayo ni moja ya mazoezi makubwa kabisa ya kijeshi kuwahi kufanywa na Urusi tangu ilipotwaa rasi ya Crimea kutoka kwa Ukraine mwaka 2014.
Wizara ya ulinzi ya Urusi imesema wanajeshi 12,700 wanashiriki, lakini wataalamu wa Nato wanatarajia kwamba idadi itakuwa juu zaidi ya hiyo.
Mazoezi hayo ya kijeshi yanafanyika ndani na maeneo ya karibu na belarus na yanashirikisha vifaru, ndege za kivita na manowari.
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko ameonya kuwa Zapad-2017 (jina ambalo maana yake kwa Kirusi ni "Magharibi") huenda ikawa ni hatua ya mwisho kabla ya kuivamia Ukraine.
Kiev imeimarisha ulinzi wake mpakani.
Makundi ya wapiganaji wanaoungwa mkono na Urusi wanadhibiti maeneo makubwa ya mashariki mwa Ukraine na wameendelea kukabiliana na wanajeshi wa serikali.
Hii ni licha ya kutiwa saini kwa makubaliano ya kusitisha mapigano Februari mwaka 2015 mjini Minsk.
Nato imeituhumu Urusi kwa kuwapa waasi hao silaha kalikali pamoja na wanajeshi.
Urusi imekanusha tuhuma hizo, lakini imekiri kwamba kuna baadhi ya raia wa Urusi "wanaojitolea" wanaowasaidia waasi hao.
Nato imetuma wanajeshi jumla ya 4,350 Poland, Estonia, Latvia na Lithuania, nchi ambazo zinapakana na Belarus na Urusi.
Nchi 29 wanachama wa Nato pia zinashika doria angani katika mataifa ya eneo la Baltic.
Zapad
Kinachofanyika wakati wa mazoezi ya sasa ya kijeshi ya Zapad-2017 ni kuigiza hali dhahania ya maasi nchini Belarus ikiongozwa na "wasaliti" na "magaidi" wanaoungwa mkono na nchi dhahania kwa jina "Veishnoria".
Wanajeshi wa Urusi wanatumwa Belarus kuisaidia kumaliza maasi hayo.
Lengo kuu ni jinsi ya kuunganisha makao makuu ya kijeshi ya mataifa hayo mawili wakati wa vita.
Belarus imetuma wanajeshi 7,200 na Urusi imetuma wanajeshi 5,500, wizara ya ulinzi ya Urusi imesema.
Jimbo la Urusi la Kaliningrad - ambalo lipo katikati ya Poland na Lithuania ambazo ni nchi wanachama wa Nato - limeshirikishwa katika mazoezi hayo ya kijeshi.
Rais wa Belarus Alexander Lukashenko ana uhusiano wa karibu na Urusi, ingawa kumekuwepo na mzozo wa mara kwa mara kati ya serikali yake na Urusi kuhusu biashara.

Mwanafunzi wa sekondari apatikana akiwa na bunduki shuleni Kenya

Mwanafunzi wa sekondari apatikana akiwa na bunduki shuleni KenyaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMwanafunzi wa sekondari apatikana akiwa na bunduki shuleni Kenya
Mwanafunzi mmoja wa shule ya sekondari katika kaunti ya Homabay nchini Kenya, anashikiliwa na polisi akitarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kupatikana akiwa na bunduki, kwa mujibu wa gazeti la Daily Nation.
Mwanafunzi huyo wa umri wa miaka 17 alikamatwa siku ya Jumanne baada ya wanafunzi wawili kuripoti kuwa amekuwa akiwatisha kwa bunduki hiyo.
Mwalimu mkuu wa shule hiyo Dickens Bula, alisema kuwa usimamizi wa shule ulijulishwa na wanafunzi waliodai kuwa mwenzao amekuwa akiwatisha kuwa angewapiga risasi.
Gezeti hilo linasema kuwa baada ya mwanafunzi huyo kukamatwa na kuhojiwa, aliwapeleka polisi kwa kichaka kilichokuwa karibu ambapo alikuwa ameificha bunduki hiyo.
Daily Nation linasema kuwa bunduki hiyo ni ya kimarekani na hajaruhusiwa kutumiwa nchini Kenya.
Linasema kuwa licha ya uchunguzi kugundua kuwa bunduki hiyo haikuwa na risasi, usimamizi wa shule na wanafunzi walishikwa na hofu, na kusababsisha wanafunzi zaidi kuhojiwa kuhusu silaha hiyo.
Mkuu wa polisi eneo hilo Esau Ochorokodi, alisema mwanafunzi huyo aliwaambia wachunguzi kuwa alipata bunduki hiyo kutoka kwa jamaa wake anayeishi nchini Marekani.
Sasa mwanafunzi huyo anasubiri kushtakiwa kwa kumiliki bunduki bila kibali katika hakama ya Homa Bay.

India kujenga treni ya kwanza ya mwendo kasi

This handout photograph released by India"s Press Information Bureau (PIB) on September 14, 2017 shows Indian Prime Minister Narendra Modi (L) and Japanese Prime Minister Shinzo Abe looking at a railway station model at a ground breaking ceremony for the Mumbai-Ahmedabad high speed rail project in Ahmedabad. India"s first bullet train project, a $19-billion initiative linking Ahmedabad to Mumbai, was launched September 14Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMradi huo unafadhiliwa na mkopo wa dola bilioni 17 kutoka Japan na utatoa huduma kati ya miji ya Ahmedabad na Mumbai.
Waziri mkuu wa Japan shinzo Abe amezindu mradi wa kujengwa kwa treni ya kwanza ya mwendo kasi katika jimbo la nyumbani mwa waziri mkuu wa wa India Narendra Modi la Gujarat.
Mradi huo unafadhiliwa kwa mkopo wa dola bilioni 17 kutoka Japan na utatoa huduma kati ya miji ya Ahmedabad na Mumbai.
Wakati mradi huo utaanza kutoa huduma katika kipindi cha miaka mitano, safari ya kilomita 500 inatarajiwa kupunguzwa hadi masaa matatu kutoka masaa manane ya kawaida.
Bw. Abe anafanya ziara ya siku mbili nchini India ambayo ni mshirika mkuu wa Japan.
A Shinkansen bullet train moves on tracks above traffic in Tokyo on August 14, 2017.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionJapan ndiye mwanzilishi wa treni za mwendo kasi
"Rafiki yangu waziri mkuu Narendra Modi ni kiongozi mwenye kuona mbali. Alifanya uamuzi miaka miwili iliyopita kuleta treni ya mwendo kasi nchini India na kujenga India mpya," alisema baada ya kuweka jiwe la msingi leo Alhamisi.
"Nina matumani ya kufurahia mandhari mazuri ya India kupitia kw\ madirisha ya treni wakati nitarudi hapa miaka michache inayokuja".
Treni hiyo ya viti 750 inatarajiwa kuanza kuhudumua kuanzia Agosti mwaka 2022.
Mifumo ya usafiri wa treni nchini India husafirisha zaidi ya watu milioni 22 kwa siku na baadhi ya treni zimepitwa na wakati hali ambayo huchangia ajali za mara kwa mara.
An Indian Railways passenger train travels on a railway track in New Delhi on November 10, 2015.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMifumo ya usafiri wa treni nchini India husafirisha zaidi ya watu milioni 22 kwa siku na baadhi ya treni zimepitwa na wakati hali ambayo huchangia ajali za mara kwa mara

Trump afanya mazungumzo na viongozi wa Demokrat

Trump na wanachama wa Democrats nancy Pelosi na Chuck SchumerHaki miliki ya pichaEPA
Image captionTrump na wanachama wa Democrats nancy Pelosi na Chuck Schumer
Rais wa Marekani Donald Trump amekutana na wanasiasa wawili waandamizi kutoka chama cha Demokrat katika bunge la Congress kujadili maswala tata, huku pande zote mbili zikisema mazungumzo hayo wakati wa chakula cha jioni ikulu ya white house yalikuwa yenye manufaa.
Katika taarifa, Chuck Schumer na Nancy Pelosi wamesema wamekubaliana kuunda mpango wa pamoja kuhusu usalama wa mipakani na Donald Trump.
Wanasema mpango huo unajumuisha kuwalinda wahamiaji wenye umri mdogo lakini haukujumuisha ujenzi wa ukuta kwenye mpaka na taifa la Mexico.

Pacha walioshikamana wajiunga na chuo kikuu Tanzania

Maria na Consolata wakiwa darasani
Image captionMaria na Consolata wakiwa darasani
Ni ndoto iliozaa matunda kwa pacha walioshikana Maria na Consalata nchini Tanzania baada ya kuanza masomo yao katika chuo kikuu ili kujifunza kuwa walimu.
Kulingana na gazeti la The Citizen, waliwashukuru walimu wao wapya kwa mapokezi mema waliopata mbali na mazingira mazuri ya kusoma waliopata yalioandaliwa na chuo kikuu cha Ruaha Catholic University.
Waliwasili katika chuo hicho mbele ya wanafunzi wengine ili kuweza kujiandaa na mazingira yaliyopo.
Walianza masomo yao ya Kompyuta siku ya Jumatano .Waliwashukuru Wamishenari wa Consalata kwamba wamefikia kiwango hicho cha maisha yao.
Wamishenari hao waliwalea na kuwashawishi kuendelea na masomo.
Pacha walioshikana Tanzania walio na ndoto kuu
Wasichana mapacha walioshikana Tanzania
Mtawa mmoja katika Chuo hicho amesema kuwa kuwasili kwa pacha hao mbele ya wanafunzi wengine katika chuo hicho kutawawezesha kujiandaa ili kuweza kuwa sawa na wengine.
Vyumba vitatu vilivyopo na fanicha zote vimeandaliwa kwa pacha hao, ikiwemo jiko na sebule.
Naibu Chansela anayesimamia maswala ya fedha na usimamizi wa chuo hicho , Fr Kelvin Haule alionyesha furaha baada ya kuwapokea pacha hao.
Amesema kuwa masomo yataanza mwisho wa mwezi Oktoba lakini masomo ya kompyuta yanaanza mara moja.