Friday, August 25

DC Temeke awaonya wazoa taka



Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva 

Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva  
Dar es Salaam. Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Felix Lyaniva amesema atawachukulia hatua za kisheria wazabuni waliopewa tenda ya kuzoa taka wanaotupa taka hizo eneo la Mwembe Yanga ikiwemo kulipa faini ya Sh1 milioni.
Lyavina aliyazungumza hayo baada ya kubaini kuwa wazabuni waliopewa tenda ya kuzoa taka wamekuwa wakitupa taka hizo eneo la Mwembe Yanga ambalo si rasmi kwa kutupa takataka hizo badala yake walitakiwa kuzipeleka Dampo la Pugu, Kinyamwezi.
 “Wale wote tuliowapa zabuni ya kuzoa taka wasiende kutupa takataka eneo la Mwembe Yanga, wanatakiwa kwenda kutupa kwenye Dampo la Pugu Kinyamwezi na atakayeshikwa atachukuliwa hatua ikiwemo kulipa faini ya Sh1 milioni,”alisema Lyaniva.
Pia alisema wananchi wajitokeze kufanya usafi kwenye maeneo yao ambapo mkuu huyo atashiriki kufanya usafi kwenye Kata ya Tandika.
Temeke bila uchafu inawezekana hivyo watendaji halmashauri hiyo wanatakiwa kusimamia usafi katika maeneo yao.
Diwani wa Kata ya Mtoni, Bernard Mwakyembe alisema wananchi wamekuwa wakitupa takataka pembezoni mwa barabara zikiwa kwenye mifuko ya plastiki jambo ambalo linaweza kusababisha milipuko ya magonjwa ya kuambukiza ikiwemo Kipindupindu.
Suala la usafi ni lazima si hiari, kila mwananchi anatakiwa kufanya usafi kwenye eneo lake hivyo tunataka wilaya ya Temeke iwe mfano na ikiwezekana tuzishinde wilaya nyingine,”alisema Mwakyembe. 

Mkemia mkuu kitanzini

Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele

Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel Manyele akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam 
Dar es Salaam. Mkemia Mkuu wa Serikali, Profesa Samuel Manyele amehojiwa na Mamlaka ya Kuthibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) kwa siku mbili mfululizo kuanzia juzi kuhusu utoaji kiholela wa vibali vya kuingizia nchini kemikali bashirifu.
Uingizaji na usambazaji wa kemikali bashirifu hufanyika chini ya udhibiti wa hali ya juu wa mamlaka za kitaifa na kimataifa kuzuia uwezekano wa kuchepushiwa katika utengenezaji wa dawa za kulevya aina ya heroin na cocaine.
Taarifa zinasema Profesa Manyele, ambaye juzi alihojiwa kwa siku nzima, alichukuliwa tena jana mchana kwa mahojiano zaidi yaliyofanyika makao makuu ya DCEA, Upanga jijini Dar es Salaam.
Hadi tunakwenda mitamboni Profesa Manyele alikuwa bado mikononi mwa DCEA, kwa mujibu wa taarifa ambazo Mwananchi ilizipata, na kuna taarifa zaidi kuwa huenda akaendelea kushikiliwa hadi leo.
Kuhojiwa kwake kwa siku mbili kumetokea sambamba na uamuzi wa Rais Magufuli kumuondoa Mihayo Msikhela kutoka katika nafasi yake ya kamishna wa oparesheni wa DCEA, na kumteua Luteni Kanali Frederick Milanzi kushika wadhifa huo.
Juzi, Rais John Magufuli alifanya mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam na Kamishna Mkuu wa DCEA, Rodgers Siyanga aliyemhakikishia kuwa mapambano dhidi ya biashara na matumizi ya dawa za kulevya nchini yanapata mafanikio makubwa.
Taarifa iliyotolewa juzi na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Gerson Msigwa, inasema Siyanga alimueleza Rais mikakati inayotumika kupambana na tatizo la dawa za kulevya. Haikueleza kwa kina masuala mengine ambayo Rais Magufuli alizungumza na Siyanga.
Ingawa mamlaka haziko tayari kuthibitisha, kuhojiwa kwa Profesa Manyele kunahusishwa kwa kiasi kikubwa na wimbi la kukamtwa kwa kemikali bashirifu ambazo uagizaji, uhifadhi na usambazaji wake husimamiwa na ofisi yake.
Katika miezi ya karibuni, DCEA ilikamata mamia ya tani za kemikali bashirifu katika Bandari ya Dar es Salaam, bandari kavu na kwenye maghala ya watu binafsi.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka DCEA, waagizaji wengi walikiuka utaratibu na kushindwa kueleza wanakosambaza kemikali hizobaada ya kuingizwa nchini.
Tukio la kwanza la kukamatwa kwa kemikali hizo lilitokea Mei baada ya maofisa wa DCEA kukamata lita zaidi ya 5,000 za aina mbalimbali za kemikali bashirifu, mali ya mfanyabiashara wa jijini Dar es Salaam, Benedict Assey.
Baada ya kukamatwa kwa shehena hiyo iliyokuwa katika maghala yaliyopo Mwenge (Dar es Salaam), Bagamoyo (Pwani) na Kilimanjaro (Moshi), iligundulika kuwa kibali cha kughushi kilitumika kuagiza mzigo huo, huku kibali cha usajili cha kampuni iliyoagiza mzigo huo ya Techno Net Solution kikionekana kimekwisha muda wake.
Maghala hayo yalionekana kutokidhi viwango vilivyowekwa kisheria, kama umbali kutoka makazi ya watu.
Mathalani, licha ya ghala la Mwenge kuwa katikati ya makazi ya watu, ofisi ya Mkemia Mkuu haikuchukua hatua pamoja na ukweli kuwa ilikuwa ikifanya ukaguzi mara kwa mara.
Mwezi uliofuata mamlaka hiyo ilikamata tena makontena mawili yaliyokuwa na lita zaidi ya 6,000 za kemikali hizo hatari ndani ya bandari kavu iliyopo Tabata Relini, Dar es Salaam. Shehena hiyo iliyoagizwa kutoka Ufaransa na India, ni mali ya Assey.
DCEA inadai kuwa ilimtaka mmiliki huyo atoe nyaraka na orodha ya watu au taasisi zilizouziwa kemikali hizo, lakini alishindwa kufanya hivyo.
Na mwezi uliopita tu, DCEA ilikamata makontena mengine 10 yenye zaidi ya lita 200, 000 za aina tofauti za kemikali bashirifu katika Bandari ya Dar es Salaam zilizoagizwa kinyume cha sheria kutoka Swaziland.
DCEA ilisema imebaini kampuni inayotuhumiwa kwa uingizwaji huo, ilianza kazi hiyo tangu mwaka 2016 na tayari ilishaingiza lita milioni 1.5 za kemikali hizo na kupelekwa kwa kampuni moja iliyoko Mbezi Luis.
Mamlaka ilisema pia kuwa baada ya uchunguzi zaidi, iligundua kuwa kampuni hiyo inajihusisha na kuuza magari na si kutunza wala kuchakata kemikali, jambo lililowastua na kufanya uchunguzi wa kina.
Kamishna wa ukaguzi na sayansi jinai wa DCEA, Bertha Mamuya aliwahi kuiambia Mwananchi kuwa kwa kawaida kemikali hizo hutumika kutengenezea dawa za binadamu, za wadudu na mbolea lakini magenge ya wahalifu huzitumia kutengeneza heroin na cocaine katika maabara za ufichoni.
Kwa mujibu wa Sheria ya Kemikali za Viwanda na Walaji (Usimamizi na Udhibiti) ya mwaka 2003, Ofisi ya Mkemia Mkuu ndiyo yenye mamlaka ya kutoa vibali vyote vya uingizaji wa kemikali bashirifu, kufanya ukaguzi katika maghala kuona kama yanakidhi viwango na kufuatilia matumizi yake.
Kuna tuhuma kuwa ukwasi wa baadhi ya watumishi wa ofisi hiyo unatokana na kutoa vibali vya uingizaji wa kemikali kinyume cha sheria.
“Imefika wakati watu wanaagiza kiasi kikubwa cha kemikali bashirifu na shehena inapowasili bandarini ndipo wanaanza ku-process (kutafuta) vibali kwa Mkemia Mkuu,” alisema mtaalamu mmoja wa kemikali DCEA aliyeomba kutotajwa jina.
Mapema mwaka jana, Ofisi ya Mkemia Mkuu iliingia katika kashfa kubwa baada ya kontena za kemikali bashirifu aina ya aceti anhydride zenye thamani ya Sh28 bilioni kukamatwa nchini Pakistani likitokea Tanzania.
Inadaiwa kuwa kontena hilo lilitokea China huku wamiliki wake wakipewa vibali vya kuingiza kemikali hizo baada ya kuzieleza mamlaka kuwa zingezitumika katika kiwanda cha korosho. Hata hivyo, habari zinadai kuwa kontena hilo lilihifadhiwa Kurasini jijini Dar es Salaam kabla ya kupata vibali kutoka Ofisi ya Mkemia Mkuu na kupelekwa Pakistan ambako lilikamatwa.
Maofisa wawili wa ofisi ya mkemia mkuu waliwahi kukamatwa na kuhojiwa kuhusiana na utoaji vibali kwa shehena hiyo, lakini kesi dhidi yao ilishindwa kuendelea katika mazingira yasiyoeleweka.
Machi mwaka huu, maofisa wengine wawili wa ofisi hiyo hiyo walikamatwa na DCEA na kuhojiwa kwa saa kadhaa kwa madai ya kusaidia usafirishwaji wa kontena hilo kwenda Pakistan.
Kutokana na wimbi la ukamataji wa kemikali hizo hatari, Profesa Manyele alijitokeza kwenye vyombo vya habari hivi karibuni akionya kuwa Serikali haitasita kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wafanyabiashara wanaokiuka utaratibu wa uingizaji, usafirishaji na uhifadhi wa kemikali bashirifu.
Alikuwa akifafanua kukamatwa kwa tani zaidi ya 6,000 za kampuni ya Tecno Net Scientific.
Profesa Manyele alifanya tena mkutano na waandishi wa habari hivi karibuni na kukiri kwamba ofisi yake imelemewa na kiwango kikubwa cha kemikali za matumizi ya nyumbani na viwandani zinazoingizwa nchini kila siku.
Alisema ongezeko hilo linatokana na watu wengi kuagiza mzigo wa kemikali bila kufuata sheria.
Alisema kabla ya kutoa onyo hilo, waingizaji walikuwa wakifanya hivyo kinyume cha sheria na walikuwa wakiagiza kwanza mizigo na inapowasili au kukaribia kuwasili, ndipo wanaanza kuomba kibali au usajili kwa mara ya kwanza.   

Tanroads yadai kutopata zuio la mahakama, yaendelea kubomoa

Tingatinga la Wakala wa Barabara Tanzania

Tingatinga la Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) likiendelea na kazi ya kubomoa nyumba zinazodaiwa kujengwa katika hifadhi ya Barabara ya Morogoro eneo la Kimara Stop Over jijini Dar es Salaam jana. Picha na Ericky Boniphace 
Dar es Salaam. Wakati Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kikilaani Kitendo cha Wakala wa Barabara Mkoa wa Dar es Salaam (Tanroads) kubomoa nyumba ambazo zina kinga ya mahakama, taasisi hiyo ya Serikali imeendelea na kazi hiyo kwa kuwa haijapewa zuio.
Lakini meneja wa Tanroads wa Dar es Salaam, Julius Ndyamkama amesema hatua hiyo ya kuendelea kubomoa haimaanishi kuwa wameidharau mahakama.
Akizungumza jana na Mwananchi, Ndyamkama alisema wanaiheshimu mahakama na wanaiogopa, lakini kinachowafanya waendelee kubomoa ni kutopewa taarifa ya zuio hilo na mahakama na badala yake habari hizo wanazisikia tu kwenye vyombo vya habari.
“Hivi unategemea mimi nidharau mahakama kweli?” alihoji Ndyamkama.
“Ndiyo nakwambia kweli. Mimi siogopi kweli? Mimi nasikia tu kwenye magazeti kwamba tarehe 18 ndiyo (amri ya zuio) ilitoka. Kwa nini tukaidi agizo la mahakama bwana?
“Jumatatu tulikuwepo ofisini, kwa nini hawakutuletea taarifa au kuja kubandika zuio hilo ofisini kwetu? Hatujaambiwa chochote, hatuwezi kupingana na sheria, kwani sisi tumekuwa nani? Wakituletea taarifa tutatii amri ya mahakama lakini kama hawajaleta tutaendelea.”
Hata hivyo, kazi ya ubomoaji jana iliendea na ilizikumba nyumba za wakazi wawili; Marawa Lyimo na Tedy Marko ambazo ni miongoni mwa majengo yaliyowekewa zuio.
“Niliwaonyesha hati hiyo (ya zuio la mahakama), lakini wakanijibu kuwa ‘sisi hatujui kusoma, tunachojua ni kutekeleza agizo tulilopewa,” alisema Lyimo.
Meya wa jiji la Tanga alia ubomoaji
Sakata la ubomoaji kupisha ujenzi wa reli, pia limeshika kasi mkoani Tanga, ambako Meya wa Jiji, Mhina Mustapha amelaumu wataalamu kuingia eneo lake na kufanya kazi bila kuitaarifu halmashauri hiyo.
Mhina alisema hayo jana jioni alipokutana na wamiliki wa nyumba zilizowekewa alama ya “X”.
“Sisi kama wawakilishi wenu tumefadhaishwa sana na kitendo cha wataalamu wa Rahco kutoka Dar es Salaam na kuja hapa kufanya shughuli za kuweka alama ya “X” kwenye nyumba bila kututaarifu,” alisema Mustapha.
Alisema katika kuonyesha kuwa halmashauri haiungi mkono kazi hiyo, itawasiliana na uongozi wa ngazi za juu serikalini kuona jinsi ya kuwasaidia wakazi.
Wakati Meya akizungumza hayo, wamiliki wa nyumba hizo wamejigawa katika makundi mawili ambayo yatafanya kazi ya kufuatilia haki za wamiliki wa hoteli na wenye nyumba za makazi.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela aliwaomba waandishi wa habari kuwa na subira na kuahidi kulitolea maelezo suala hilo mara baada ya kujiridhisha kuhusu hatua zilizochukuliwa na Rahco kuweka alama hizo.
“Kimsingi kuna dosari ambazo tumeziona katika zoezi zima la uwekaji wa alama za ‘X’ kwenye majengo ya Tanga. Inaonyesha kuna kuchanganya kati ya nyumba za mijini na za vijijini. Haiwezekani ziwekwe alama sawa kwani kwa vyoyote kama itafanyika hivyo basi Tanga itabakiwa na nyumba chache mno,” alisema Shigela.    

WAZIRI MWAKYEMBE AWAPA BARAKA WATOTO WA TANZANIA KWENDA MAN CITY KWA MAJARIBIO

Waziri wa michezo nchini Tanzania Mh.Dk Harrison Mwakyembe amewatakia safari njema watoto waliochaguliwa na kampuni ya Tecno mobile kwenda kufanya majaribio ya kucheza mpira wa miguu katika academy ya klabu ya Manchester City nchiniUingereza.
Malimi Majaliwa wa kwanza kushoto na Daudi DAmasi wakiwa katika picha ya pamoja baada yakupewa Baraka za safari na Mh. Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe)

Akiongea katika hafla hiyo fupi kutambulisha mbele ya waziri mpango huo, Afisa Mahusiano wa Kampuni ya Tecno Mobile Bwana, Eric Mkomoya alisema kua kampuni ya Tecno Mobile ndio wadhamini pekee wa safari hiyo kupitia simu yao mpya Tecno Camon Cxto leo maalumu la machester city ambapo watoto hao wawili wataenda kupewa mafunzo yenye kiwango cha kimataifa lakin pia endapo watafanya vizuri wanaweza kuchaguliwa kuendelea kucheza katika klabu hiyo. ,(wadhamini wa kuuwa safari 

(Wazazi na walezi wa vijana wanaokwenda Manchester city wakiwa katika picha ya pamoja na wadhamini wa kuu kutokea Tecno Mobile.)

Alisemaa . ”Tumefurahi kukutana na serikali hasa Waziri wa michezo na kuamua kuwapa Baraka zake vijana wetu wanaokwenda huko wataondoka usiku wa tarhe 23 na kurudi tarehe 30 mwezi wa nane”.

Akikaribishwa na mkurugenzi wa michezo, waziri wa michezo Dk. Harrison Mwakyembe amesema kua serikali ina furaha kuona wadau wanajitokeza kukuza vipaji nchini Tanzania, hasa kwa watoto wanao chipukia.

Dk Harrison Mwekyembe pia amesema “niwaombewa dau katika sekta ya michezo tushirikiane katika kukuza michezo, na washukuru kampuni ya Tecno Mobile kwa kuonesha juhudi za wazi katika kufanikisha hili, serikali pia inafanya jitihada kwa nafasi kuhakikisha viwango vya soka na michezo kwa ujumla vinakua.”alimaliza.)

Mzazi wa mtoto mmoja wapo Malimi, Majliwa Mbasa amesema anafuraha kuona kijana wake amepata nafasi hiyo anaamini atafanya vizuri liafungue milango kwa vijana wengine wadogo wa kitanzania walioko nchini waweze kwenda kucheza soka la kulipwa nchini uingereza.

Watoto wawilli Daudi Damasi pamoja na Malimi Majaliwa wanaocheza nafasi ya kipa na ushambuliaji wamepata nafasi hizo kutokana na ushirikiano wa Tecno Mobile naasasi ya michezo ya Magnet, watoto hao ambao wote wana miaka kumi na mbili wataondoka kuelekea manchster city mnamo tarehe 23 mwezi wa nane na kurudi nchini tarehe 30.

Msafara huo utaongozwa na wazazi na walezi wa watoto hao akiwemo kocha mwenye utalaamu wa kulea vipaji vya vijana kocha Juma Maswanya. Tecno mobile ndio wadhamini wakuu wa safari hii wanajumuisha vijana kutoka nchi za afrika ambako kampuni hii inapofanyakazi hivyo Nigeria, misri ,Tanzania, Ghana pamojana Kenya.
Afisa Mahusiano wa Tecno Mobile Eric Mkomoya wa kwanza kushoto, meneja Masoko Franck Luo, wa kwanza kulia)
aziriwaHabari, Utamaduni, Utalii na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na watoto wawili Daudi Damasi na Malimi Majaliwa wanaokwenda kufanya Majaribio,

DOLA MILIONI 9.5 KUTATUA TATIZO LA MAJI MJI MDOGO WA ILULA


 Mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah akiwa sambamba na mkuu wa mkoa wa iringa wakizungumza na waandishi wa habari katika eneo la chanzo cha mradi huu wa maji katika mji mdogo waIlula
 Mkuu wa mkoa wa iringa Amina masenza akifurahia kufika kwenye chanzo cha maji pamoja na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah kwa kuwa wanajua hilo ndio litakuwa suluhisho la mda mrefu kwa wakazi wa mji mdogo wa Ilula
viongozi wa kamati ya siasa ya mkoa wa iringa wakiwa wanaelekea kwenye chanzo cha maji kwa ajili ya kujua jinsi gani kitaweza kutatua kero za wananchi wa mji wa mafinga
 mjumbewa kamati ya siasa ya mkoa wa iringa ndugu mosha akiwa njiani kuelekea kukikagua chanzo hicho cha maji
 katibu msaidizi wa chama cha mapinduzi mkoani iringa akiwa sambasamba na mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdalla wakielekea kukagua chanzo kipya cha maji kwa ajili ya wananchi wa mji mdogo wa mafinga


Na Fredy Mgunda,Iringa

Halmashauri ya wilaya ya kilolo inatarajia kutatua kero ya maji iliyodumu kwa miaka mingi katika mji mdogo wa Ilula mkoani Iringa kwa kutenga kiasi cha dola za kimarekani 9,548,827 kwa ajili ya kujenga chanzo kipya cha maji yatakayo weza kutatua changamoto hiyo.

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua utekeleza wa ilani ya chama cha mapinduzi  wilayani kilolo mkuu wa mkoa wa iringa ambaye ndio mwenyekiti wa kamati ya siasa ya mkoa bi Amina Masenza alisema kuwa wameamua kutafuta chanzo kipya ili kutatua tatizo la maji katika mji mdogo wa Ilula.

“Leo nimefika hadi huku kwenye chanzo cha maji ambacho naamini kuwa kitafanikiwa kutatua kero ya muda mrefu kwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula hivyo lazima waisimamie ipasavyo ilani ya chama na kuhakikisha kuwa wanatatua  matatizo ya wananchi”alisema Masenza

Aidha Masenza alisema kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kumuunga mkono rais wa jamhuri ya muuungano wa Tanzania dr John Pombe Maguli kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa wananchi wake.

Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya kilolo Asia Abdallah alivitaja baadhi ya vyanzo ya maji na uwezo wa uzalishaji ambavyo vinatoa huduma kwa mji mdogo wa Ilula ni Ilomba kutoka kijiji cha Imalutwa na Idemule kutoka kijiji cha Mazombe kwa ujumla vinazalisha wastani wa uzalishaji wa maji wa mita za ujazo 1,142 kwa siku.

Abdallah alisema kuwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula unamahitaji makubwa ya matumizi ya maji ambapo kwa siku wanahitaji maji ya mita za ujazo 2687 kwa siku hivyo hadi sasa kunaupungufu wa mita za ujazo 1545 kwa siku.

“Mji huu unakuwa kwa kasi kubwa hivyo matumizi ya maji yamekuwa makubwa mno ndio maana tumeanza  kujenga chanzo kingine ambacho kitakuwa na suluhisho kwa wananchi wa mji mdogo wa Ilula na kutaua kabisa tatizo la maji” alisema Abdallah 

Abdallah aliwataka wananchi na viongozi wa ngazi zote kuacha tabia ya kuharibu vyazo vya maji na mazingira kwa ujumla hivyo atakaye kamatwa anafanya uhalibifu wowote ule sheria itachukua mkondo wake.

“Ni malufuku kwa wakulima kulima kwenye vyanzo vya maji,wafugaji kufujia mifugo kwenye vyanzo vya maji pamoja na ukaji wa miti hovyo hapo nitakuwa mkali sana kwa watu ambao watakiuka haya nayoyasema hii leo kwa kuwa kila kitu kipo kisheria “ alisema Abdallah

Naye meneja wa mamlaka ya maji wa mji mdogo wa Ilula Enock Ngoyinde aliiomba serikali ya na kamati ya siasa ya mkoa wa iringa kusaidia upatikanaji wa pesa kwa wakati za kumaliza mradi huu wa maji ili wananchi waanze kupata huduma bora mapema iwezekanavyo.

Ngoyinde alisema kuwa mradi huo ukikamilika utakuwa umeongeza eneo la utoaji wa huduma vya maji kutoka wastani wa asilimia 62 hadi asilimia 75 na kuwahudumia wananchi zaidi ya elfu ishirini na tano (25000) ambao watakuwa na mtandao wa bomba za maji.

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA ENEO NA FERI MAPEMA LEO JIJINI DAR


  Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimia na baadhi ya vijana aliokutana nao wakati akisubiri kivuko mapema leo asubuhi alipotembelea eneo la Feri, na kuvuka kwa kutumia kivuko cha Mv Kigamboni kwenda Kigamboni.



 Rais Dkt John Pombe Magufuli akimsikiliza mmoja wa walemavu mapema leo asubuhi alipotembelea eneo la Feri, na kuvuka kwa kutumia kivuko cha Mv Kigamboni kwenda Kigamboni.



  Rais Dkt John Pombe Magufuli ( wa pili kulia) akiwa na baadhi ya Wananchi wengine walipokuwa wakisubiri kivuko mapema leo asubuhi,alipotembelea eneo la Feri, na kuvuka kwa kutumia kivuko cha Mv Kigamboni kwenda Kigamboni

Maadhimisho ya siku ya majeshi


Jeshi la Ulinzi la Wananch wa Tanzania linapenda kutoa ufafanuzi kuhusu maadhimisho ya siku ya majeshi yanayoanza tarehe 25 Agosti 2017. Sherehe hizi ni za kuadhimisha siku ya kuanzishwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) ambazo hufanyika kila mwaka tarehe 01Septemba, mwaka huu sherehe hizo zitaadhimishwa wakati Jeshi linatimiza miaka 53 tangu lilipo asisiwa na Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa kwanza Marehemu Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere  Septemba Mosi 1964.
Mwaka huu 2017 maadhimisho hayo yatafanyika kwa wanajeshi kufanya shughuli mbalimbali kuanzia tarehe 25 Agosti 2017 hadi tarehe 31 Agosti 2017 na kilele cha maadhimisho hayo kitakuwa tarehe 01 Septemba 2017.Shughuli hizo ni pamoja na kufanya shughuli za huduma za kijamii katika maeneo jirani na vikosi vya Jeshi, Wanajeshi kuchangia damu salama katika hospitali mbalimbali nchini, kutoa huduma za tiba na ushauri nasaha kwa Dar es salaam huduma za tiba zitatolewa katika viwanja vya mnazi mmoja kuanzia saa 2:00 asubuhi siku ya tarehe 01 Septemba, aidha wanajeshi watafanya michezo mbalimbali na wananchi Pamoja na kushiriki kufanya usafi kwenye maeneo ya kijamii (Hospitali, Masoko, Mashule n.k) na pia watafanya michezo Shirikishi na jamii inayowazunguka.
Kauli Mbiu ya maadhimisho haya ni Wiki ya Majeshi na Afya yako.
Imetolewa  na  Kurugenzi  ya  Habari  na  Uhusiano
Makao Makuu ya Jeshi, Upanga
S.L.P  9203,   Dar es Salaam,  Tanzania.

Kwa Mawasiliano zaidi: 0756-716085

NMB BANK


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kulia) akiwasilisha mada katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini. Wajumbe hao walikutana Makao Makuu ya Ofisi za Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujenga mtandao na ushirikiano. Katika mada yake kwa washiriki wa mkutano huo, Bi. Bussemaker alielezea benki ya NMB ilivyo na fursa mbalimbali kwa makundi tofauti na hasa inavyowasaidia wafanyabiashara kupitia bidhaa yake ya Trade Finance.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kushoto) akimkaribisha mmoja wa washiriki katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini.Sehemu ya washiriki katika mkutano ulioandaliwa na Benki ya NMB na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini. Wajumbe hao walikutana Makao Makuu ya Ofisi za Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujenga mtandao na ushirikiano.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kulia) akiwasilisha mada katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini. Wajumbe hao walikutana Makao Makuu ya Ofisi za Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujenga mtandao na ushirikiano. Katika mada yake kwa washiriki wa mkutano huo, Bi. Bussemaker alielezea benki ya NMB ilivyo na fursa mbalimbali kwa makundi tofauti na hasa inavyowasaidia wafanyabiashara kupitia bidhaa yake ya Trade Finance.Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NMB Plc, Ineke Bussemaker (kulia) akiwasilisha mada katika mkutano ulioandaliwa na benki hiyo na kushirikisha mabalozi, wawakilishi wa taasisi za maendeleo kimataifa, wanadiplomasia pamoja na asasi za kiraia nchini. Wajumbe hao walikutana Makao Makuu ya Ofisi za Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam lengo likiwa ni kujenga mtandao na ushirikiano. Katika mada yake kwa washiriki wa mkutano huo, Bi. Bussemaker alielezea benki ya NMB ilivyo na fursa mbalimbali kwa makundi tofauti na hasa inavyowasaidia wafanyabiashara kupitia bidhaa yake ya Trade Finance.

PROFESA NDALICHAKO AVUTIWA NA KITUO CHA MAFUNZO KWA VITENDO CHA KIKULETWA WILAYANI HAI


Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(kushoto) akifurahia madhari ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Kituo cha kuzalisha umeme cha Kikuletwa kilichopo wilayani Hai mkoa wa Kilimanjaro kinachotumika kwa mafunzo ya wanafunzi wanaosomea kozi ya Umeme,kulia ni Mkuu wa Chuo hicho,Dk Richard Masika.Picha kwa hisani ya ATC
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(kulia) akifurahia madhari ya Chuo cha Ufundi Arusha(ATC),Kituo cha kuzalisha umeme cha Kikuletwa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro kinachotumika kwa mafunzo ya wanafunzi wanaosomea kozi ya Umeme,kulia ni Mkuu wa Chuo hicho,Dk Richard Masika.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(kulia) akipewa maelezo na Mkuu wa Chuo chaUfundi Arusha(ATC),Dk Richard Masika wakati ya ziara yake kwenye Kituo cha kuzalisha umeme cha Kikuletwa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro kinachotumika kwa
mafunzo ya wanafunzi wanaosomea kozi ya Umeme,kushoto ni Naibu Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Mhandisi Stella Manyanya.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako(kushoto) akiangalia moja ya mitambo ya kuzalisha umeme kwa njia ya maji iliyokua ikitumika zaidi ya miaka 50 iliyopita,kulia ni Mkuu wa Chuo hicho,Dk Richard Masika.
Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia,Profesa Joyce Ndalichako akisisitiza jambo wakati akizungumza na jumuiya ya wana Chuo cha Ufundi Arusha(ATC) kwenye Kituo cha kuzalisha umeme cha Kikuletwa wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro kinachotumika kwa mafunzo ya wanafunzi wanaosomea kozi ya Umeme.

NAIBU WAZIRI AAGIZA HALMASHAURI KUTAMBUA MAENEO YASIYOENDELEZWA NA YASIYOMIKILIWA KIHALALI


Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
Mhandisi Baraka Felix kutoka Kampuni ya EAU Consult akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kulia) alipotembelea kuona Ujenzi wa Ofisi ya Mamlaka ya Maji Lamadi itakayosimamia mradi wa maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali .
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb)(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari katika mahojiano maalum mara baada ya kutembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) (kushoto) akipokea maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya wakati alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali.
Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe.Angelina Mabula(Mb) (wa pili kushoto) akizungumza na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Busega mara baada ya kutembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali, (kushoto) Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhe.Tano Mwera.
Msajili Msaidizi wa Baraza la Ardhi Kanda ya Ziwa, Dorothy Moses akitoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizowasilishwa na watumishi wa Idara ya Ardhi katika kikao cha Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi , Mhe.Angelina Mabula(Mb) na watumishi hao Wilayani Busega(hawapo pichani).


Na Stella Kalinga, Simiyu

Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb), ameziagiza Halmashauri nchini, kuyatambua na kuyatolea taarifa maeneo yanayohodhiwa na watu bila kuendelezwa na yale ambayo hayakupatikana kihalali ili Wizara iweze kuchukua hatua stahiki.

Naibu Waziri huyo ameyasema hayo alipotembelea eneo la hekta 13 katika Kijiji cha Kalago, Kata ya Lamadi, Wilayani Busega lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji Hermati Pateli kinyume cha sheria, ambaye amefutiwa hati na Serikali, kisha Halmashauri ya Busega Mkoani Simiyu kuanza ujenzi wa mradi wa maji katika eneo hilo utakaonufaisha vijiji vinne vya kata ya Lamadi.

Mhe.Mabula amesema Halmashauri zinapaswa kutambua maeneo yasiyoendelezwa na yanayomilikiwa kinyume cha sheria na kuwasilisha taarifa katika Wizara ya Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ili yaweze kuyarejesha kwa wananchi na kupangiwa matumizi mengine yenye manufaa zaidi kwa jamii.

“Maeneo yote yaliyohodhiwa ambayo hayajaendelezwa na ambayo pengine hayakupatikana kihalali, ni jukumu la Halmashauri kuyatambua na kuleta taarifa zake Wizarani ili Wizara iweze kuchukua hatua ya kuweza kuyarudisha katika matumizi kwa Umma na yaweze kufaidisha watu wengi zaidi badala ya mtu mmoja” amesema Naibu Waziri Angelina Mabula

Aidha,Naibu Waziri Mabula amebainisha sababu zilizopelekea Mwekezaji Hermati Pateli kufutiwa hati ya eneo hilo na Serikali kuwa ni udanganyifu wa Uraia pamoja na upatikanaji wa hati ambao haukuzingatia sheria na taratibu za nchi.

Naibu Waziri huyo amesema eneo lililokuwa linamilikiwa na Mwekezaji huyo isivyo halali ambalo limefutiwa hati miliki limegawanyika katika ploti mbili, ploti Namba 01 na Namba 02 Block C lenye ukubwa wa hekta 7.62 na Block Namba 03 C hekta 5.45.

Akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Angelina Mabula(Mb), Mhandisi Mshauri wa Mradi wa Maji wa Lamadi kutoka Kampuni ya EAU Consult, Baraka Felix amesema Tanki la Maji litakalojengwa katika eneo hilo litakuwa na uwezo wa kuzalisha mita za ujazo 3000 kwa siku.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega, Anderson Njiginya amesema Mradi wa Maji wa Lamadi unaojengwa katika eneo hilo utawanufaisha wananchi wa Vijiji Vinne vya Kalago, Lamadi, Lukungu na Mwabayanda.

Mradi huu wa maji unaojengwa katika eneo hili lililokuwa linamilikiwa isivyo halali na Mwekezaji Pateli, utagharimu kiasi cha Yuro milioni 2.8, na unatarajiwa kukamilika ifikapo Mei, 2019.

Soko la Wazi la Mkulima Market Chuo Kikuu cha Dar es salaam kuanza Agosti 30 hadi septemba 2, 2017


25 Agosti 2017
Ni msimu mwingine wa Soko la Wazi la Mkulima Market maarufu kama Mkulima Soko. Tunakukaribisha kuungana na wazalishaji na wachakataji bidhaa mbalimbali za kilimo, ufugaji, uvuvi na uwindaji kuona wazalishaji kutoka kila pembe ya Tanzania. Katika Mkulima Soko utapata fursa ya kuona, kupata elimu na kununua bidhaa bora zinazozalishwa Tanzania.

Soko hili la Wazi litafanyika kuanzia tarehe 30 Agosti hadi 2 Septemba 2017 (Jumatano, Alhamisi, Ijumaa na Jumamosi). Karibu ujifunze ufugaji wa sungura, samaki na nyuki. Kama kawaida soko litafanyika kwenye Maegesho ya Magari ya Research Flats, mbele ya Jengo la Ndaki ya Kilimo na Teknolojia za Uvuvi ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Msimu huu kutakuwa na wazalishaji wapatao 60 watakaoleta bidhaa mbalimbali fresh na zilizochalatwa.

Katika soko hili kutakuwa na mambo makubwa manne:

1.     Mkulima Market itazindua rasmi kidokozi (app) pamoja tovuti yake ya mkulimamarket.com ili kuwezesha Watanzania wengi zaidi kunufaika na fursa zilizopo katika sekta ya Kilimo, Uvuvi, Ufuaji na Uwindaji.
2.     Uzinduzi wa masoko ya wazi ya kila mwisho wa wiki yatakayofanyika kwenye eneo la Organic Farmer Supermarket iliyopo eneo la Kijitonyama mita 300 toka kwenye taa za Sayansi, mkabala na Hoteli ya Colubus. Hivyo basi wakati wa soko la wazi, wazalishaji watapata fursa ya kujiunga na mtandao huu mkubwa wa wazalishaji wa bidhaa zenye ubora kutoka shambani hususani nyanya, vitunguu, pilipili hoho, karoti, viazi, mchele, unga wa mahindi, kuku samaki na asali.
3.     Uhabarishaji kuhusu huduma mpya ya kupata bidhaa mlangoni kwako iitwayo Mkulima Basket kwa kushirikiana na Organic Farmer Supermarket.
4.     Pia tutakuwa elimu kuhusu ufugaji sungura itakayotolewa Uhuru Rabbits.  Pamoja na kutoa elimu kuhusu ufugaji wa sungura wataendesha onesho la kuonja nyama choma ya sungura.

Tunamkaribisha kila mwana Dar es Salaam kuja kuona ubunifu na maendeleo yanayotokana na biashara katika sekta kilimo nchini Tanzania. Kama kawaida kutakuwa na burudani mbalimbali pamoja na michezo ya watoto. Hakuna kiingilio

Unaweza kuwasiliana na Mratibu kupitia namba 0767 254 887 au 0629 042 678 au kwa kuandika barua pepe kupitia mkulimamarket@gmail.com au kwenye mitandao ya kijamii ya twitter, facebook, instagram na youtube.

Shukrani za kipekee kabisa ziende kwa Kilimanjaro Audiovisual Services (KAVS), Michuzi Blog, Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) pamoja na TanTrade kwa kuendelea kuuunga mkono kazi za Mkulima Market.