Monday, August 7

RAIS DKT MAGUFULI ATEMBELEA VIWANDA JIJINI TANGA, ATOA MAAGIZO MAZITO KWA WAZIRI MWIJAGE


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na wafanyakazi alipowasili  kufungua rasmi  kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro maeneo ya Maweni jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifunua kitambaa  kufungua rasmi  kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro maeneo ya Maweni jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kufungua rasmi  kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro maeneo ya Maweni jijini Tanga leo Agosti 6, 2017 
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipatiwa maelezo ya uzalishaji baada ya kufungua rasmi  kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro maeneo ya Maweni jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na uongozi wa kiwanda baada ya kufungua rasmi  kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro maeneo ya Maweni jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea risala toka kwa uongozi wa kiwanda kwenye sherehe za kuweka  jiwe la msingi upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh  maeneo ya Kange jijini Tanga leo Agosti 6, 2017 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Mwijage wakifunua kitambaa kama ishara ya kuweka jiwe la msingi upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh  maeneo ya Kange jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na mwandishi wa habari wa TBC Bi. Vumilia Mwasha baada ya kuweka jiwe la msingi upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh  maeneo ya Kange jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembezwa maeneo mbalimbali baada ya kuweka  jiwe la msingi la upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh  maeneo ya Kange jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea kibanda cha maziwa bada ya  kuweka jiwe la msingi upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh  maeneo ya Kange jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigawa maziwa na mtindi kwa wanahabari  katika  kibanda cha maziwa baada ya  kuweka jiwe la msingi upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh  maeneo ya Kange jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigawa maziwa na mtindi kwa wanahabari  katika  kibanda cha maziwa baada ya  kuweka jiwe la msingi upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh  maeneo ya Kange jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimgawaia maziwa na mtindi Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Alhaji Mustapha Selebosi   katika  kibanda cha maziwa baada ya  kuweka jiwe la msingi upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh  maeneo ya Kange jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akigawa maziwa na mtindi kwa watoto katika  kibanda cha maziwa baada ya  kuweka jiwe la msingi upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh  maeneo ya Kange jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wanannchi baada ya kugawa maziwa na mtindi kwa watoto katika  kibanda cha maziwa baada ya  kuweka jiwe la msingi upanuzi wa kiwanda cha maziwa cha Tanga Fresh  maeneo ya Kange jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na mkewe Mama Janeth Magufuli wakicheza ngoma ya Baikoko wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wananchi na wafanyakazi kwenye sherehe za uzinduzi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wananchi na wafanyakazi kwenye sherehe za uzinduzi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipokea risala kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa  GBP Bw. Badar Sood kwenye sherehe za uzinduzi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  Mkurugenzi Mtendaji wa  GBP Bw. Badar Sood kwenye sherehe za uzinduzi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine wakikata utepe kwenye sherehe za  uzinduzi wa wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli na viongozi wengine akifunua kitambaa kwenye sherehe za  uzinduzi wa  matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 Mama Janeth Magufuli na Waziri wa Afya Mhe Ummy Mwalimu wakifurahia jambo kwenye sherehe za  uzinduzi wa  matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga  ngoma ya Baikoko wakati wa sherehe za uzinduzi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga  ngoma ya Baikoko wakati wa sherehe za uzinduzi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipiga  ngoma ya Baikoko wakati wa sherehe za uzinduzi wa matanki ya kuhifadhia mafuta ya kampuni ya GBP yenye ujazo wa lita 300,000 eneo la Raskazone jijini Tanga leo Agosti 6, 2017. Picha na IKULU

MASAUNI APOKEA VIFAA VYA TAMASHA LA USALAMA BARABARANI LITAKALOFAYIKA AGOSTI 12, MWAKA HUU UWANJA WA TAIFA



Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea moja ya tisheti zitakazovaliwa Siku ya Tamasha la Usalama Barabarani kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi na Mauzo wa Benki ya NMB, Omari Mtiga (kushoto), wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi



Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea moja ya tisheti zitakazovaliwa Siku ya Tamasha la Usalama Barabarani kutoka kwa Meneja Masoko wa Kampuni ya Bakhresa, Omary Kuwe (kushoto) wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli



Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akipokea moja ya tisheti zitakazovaliwa Siku ya Tamasha la Usalama Barabarani kutoka kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Bin Slum, wakati wa makabidhiano yaliyofanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam. Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli



Mwenyekiti wa Taifa wa Baraza la Usalama Barabarani, Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akizungumza na Vyombo vya Habari baada ya kupokea vifaa kutoka Kampuni mbalimbali zilizojitokeza kudhamini Siku ya Tamasha la Usalama Barabarani litakalofanyika Agosti 12 katika Uwanja wa Taifa, ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt. John Magufuli. Kulia ni Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani nchini, Fortunatus Musilimu. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.



Meneja Masoko wa Kampuni ya Bakhresa, Omary Kuwe (kushoto) akizungumza na Vyombo vya Habari baada ya kukabidhi vifaa kwa ajili ya udhamini wa Siku ya Tamasha la Usalama Barabarani litakalofanyika Agosti 12 katika Uwanja wa Taifa, ambapo Mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli. Makabidhiano hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Wizara hiyo, jijini Dar es Salaam.

Mbunge kuwajengea wajane nyumba za kudumu Kibiti


 Mbunge wa Kibiti Ally Seif Ungando anatarajia kuanza ujenzi wa nyumba za kudumu kwa wajane wote waishio wilayani Kibiti ambao waume zao wameuwa kwa kupigwa risasi na watu waliokuwa wakifanya mauaji kwa viongozi wa Serikali za vitongoji na vijiji, na wana Chama Cha Mapinduzi.
Hayo ameyazungumza jana kwenye ofsi ya Mkuu wa Wilaya Kibiti,alipokuwa akizungumza na viongozi wa Dini na Wazee juu ya kufanya Kongamano la kuzidi kuiombea Wilaya ya Kibiti iwe na amani.
Ungando amesema mbali na kujenga nyumba hizo,pia atawasomesha watoto wote wa marehemu ambao wameuawa kwa kupigwa risasi kuanzia Mwezi May 2016 hadi sasa.
Amesema tayari ameanza kuwasiliana na wadau mbalimbali ili kumsaidia ujenzi huo kwa kuwa watu waliouawa hawakuwa na makosa yoyote.
Ungando,ambaye ameonekana kuguswa na mauaji yaliyotokea mara kwa mara wilayani hapo kwa nyakati kadhaa alijikuta akitokwa na machozi katika mkutano huo hali iliyoelezwa na baadhi ya Wazee kuwa mauaji hayo yamemuumiza sana.
Amesema kila alipokuwa akifika kwenye maziko ya viongozi wa Serikali za Mitaa au ya mwanachama wa chama cha Mapinduzi aliyeuawa kwa kupigwa risasi alikuwa akiumia sana moyoni mwake hali iliyomfanya kushindwa kuzungumza chochote kutokana na kuwa na machungu mengi moyoni mwake.
"Kila nilipokuwa nakwenda kwenye Msiba wa kiongozi wa Serikali za Mitaa au msiba wa mwanachama wa chama cha Mapinduzi na kwenye maeneo yalipotokea mauaji ya Polisi moyo wangu ulikuwa ukiumia hali iliyokuwa ikisababisha kushindwa kuzungumza" amesema.
Akizungumza katika Kikao hicho Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Juma Mlindo alisema kwa sasa ni wakati muafaka kwa wananchi wote kushikamana pamoja na kuiombea dua wilaya hii irejee kwenye hali yake ya usalama na Utulivu pamoja na wilaya za Rufiji na Mkuranga.
Mlindo amesema wao kama viongozi wa Dini mara kadhaa wamekuwa wakiiombea wilaya hii Dua,ili Mwenyezi Mungu aweze kurejesha hali ya utulivu kama hapo awali.
Mmoja wa wajane ambaye alifiwa na mumewe mwaka jana,bi Mwajuma Mustafa alisema hatua hiyo ya kujengewa nyumba na watoto wao kusomeshwa na Mbunge itakuwa faraja kwao.
Amesema msaada huo utawawezesha waishi katika nyumba zilizo salama wakiwa na watoto wao kwa kuwa wengi wa wajane ambao waume zao waliuawa kwa kupigwa risasi wamelazimika kurudi kwao wakiwa na watoto,huku wakiwa hawapati msaada toka kwa ndugu wa waume zao.
Mwajuma ambaye mumewe alikuwa ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Nyang'undu kilichopo katika kijiji cha Nyambunda aliuawa Desemba 6,2016 kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana akiwa njiani akirejea kwake.

Mgogoro wa Kanisa Anglikana wahamia kwa Askofu wa Mwanza


Nyumba ya Wahudumu wa Dayosisi ya Victoria Nyanza ya Kanisa la Anglikana wamewakataa maaskofu wawili waliokwenda kwa kujitolea kuchunguza mgogoro unaoendelea dhidi ya Askofu wa dayosisi hiyo, Boniface Kwagu.
Maaskofu hao ni Michael Hafidhi kutoka Zanzibar na John Lupaa kutoka Dayosisi ya Manyoni Singida.
Askofu Kwangu amekuwa kwenye mgogoro na viongozi wa kanisa hilo huku baadhi ya waumini wakimtuhumu kutumia madaraka yake vibaya kwa kukiuka katiba ya kanisa.
Akizungumza katika ibada maalumu jana, mwenyekiti wa nyumba ya wahudumu, Mchungaji Andrea Kashirimu alisema wamefikia hatua hiyo baada ya maaskofu hao kukiuka muongozo na hadidu za rejea zilizotumwa Agosti 2 na Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Dk Jacob Chimeledya.
Alisema taarifa za kuwakataa waliitoa polisi na jeshi hilo kuamuru watu hao waondoke.
Lakini Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi alisema, “Sisi hatuwezi kuingilia migogoro ya kanisa. Tunachofanya ni kuhakikisha hakuna ugomvi kwa hiyo tulisema hakuna kufunga milango waache waumni waendele na ibada, hatutaki kuona vurugu kwenye mkoa wetu.”
Walipotafutwa kwa simu Askofu Hafidhi alisema atafutwe baadaye kwani yupo kwenye kikao huku Askofu Lupaa akituma ujumbe mfupi kwamba atafutwe baada ya saa tatu yupo kwani pia kwenye kikao.
Kashirimu alidai kuwa maaskofu hao badala ya kuchunguza mgogogro huo kama hadidu zinavyoelekeza, walisababisha uchochezi na vurugu maeneo mbalimbali ndani ya dayosisi hiyo katika maeneo ya Sengerema, Magu, Ngudu wakati wakifanya vikao mbalimbali.
“Kwa hiyo sasa tunaunga mkono uamuzi wa nyumba ya maaskofu ambao waliufanya Julai 6, walipokaa na kumshauri Askofu Kwangu kustaafu kwa hiari ili kulinda heshima yake ndani na nje ya kanisa,” alisema mchungaji Kashirimu.
Miongoni mwa hadidu za rejea walizopewa na askofu mkuu ni kukutana na makundi mbalimbali kuona chanzo na kiini cha mgogoro, kuchunguza malalamiko ya kutofuatwa kwa katiba, kuchunguza malalamiko juu ya askofu na uhusianao wake na wamisionari, wachungaji na waumini na kuchunguza malalamiko kubadili taratibu za ibada, fedha na kuchunguza malalamiko mengine.
Mchungaji wa Parishi ya Sengerema Mjini, Dk Elisha Ndema alisema, “Walipokuja kwenye kikao walisababisha waumini kuwafungia mlango wasiingie ndani na kutaka kupigwa baada ya kuonekana hawafuati taratibu na kuunda makundi katika Parishi ya Bomani.”
Askofu Chimeledya aliwaagiza maaskofu hao kuchunguza, kubaini chanzo cha migogoro na kumshauri hatua za kuchukua bila wao kufanya uamuzi wowote.

Mwigulu atoa Sh15 milioni ujenzi wa kanisa kutokana na bomoabomoa

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,

Waziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto) akizungumza jambo na Askofu wa Kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk Alex Malasusa  baada ya misa ya harabee kwa ajili ya mchango wa ujenzi wa kanisa la Mbezi Luis jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni Mchungaji wa kanisa hilo, Oscar Mlyuka. Picha na Ericky Boniphace 
Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba amechangia Sh15 milioni katika harambee ya ujenzi wa kanisa jipya la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Usharika wa Mbezi Luisi baada ya kanisa la awali kukumbwa na bomoabomoa ya kupisha upanuzi wa barabara ya Morogoro.
Kanisa hilo ni moja kati ya nyumba zaidi ya 30 za ibada zilizowekewa alama ya X kwa ajili ya kubomolewa na Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads) ili kupisha upanuzi wa barabara hiyo kuanzia Kimara hadi Kiluvya.
Katika harambee hiyo, Mwigulu pia alipiga mnada picha yake na kuiuza kwa Sh 3 milioni kwa ajili ya ujenzi huo.
Akizungumza katika ibada hiyo maalumu iliyoendeshwa na Askofu wa KKKT Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Dk Alex Malasusa, Mwigulu aliwapongeza waumini kwa hatua waliyofikia ya kujenga kanisa kubwa na kuwasihi kuendelea kumuombea Rais John Magufuli na Taifa.
“Kwanza niwapongeze kwa hatua hii mliyofikia ya ujenzi wa kanisa kubwa tena la kisasa, lakini naomba niongee vitu viwili, cha kwanza naomba tuendelee kuliombea Taifa kwani mambo yamebadilika, baadhi ya wananchi wanzetu wamekosa uzalendo na nchi yao wanashiriki kufanya uhalifu,” alisema.
Alisema kuna taarifa ambazo wanazipata za baadhi ya Watanzania kushiriki kufanya mambo mabaya jambo ambalo hajawahi kufikiria kama ipo siku watafikia hatua hiyo, lakini ukweli ni kwamba wapo na wengi ni watoto ambao wanakwenda nje ya nchi kujifunza ugaidi.
“Mfano mzuri ni wilaya yetu ya Kibiti, tumebaini watoto wetu wanafanya mambo haya ukielezwa unaweza usielewe lakini ukifika na kuona utajua kuwa ni mambo ya ajabu yanayofanywa na baadhi ya Watanzania wenzetu,” alisema.
Mwigulu pia aliwaasa waumini hao kuendelea kumuombea Rais kwani hatua anazochukua ni kwa makusudi mazuri ya kuleta maendeleo na kwamba yupo katika vita kali ambayo kwa nguvu ya kibinadamu tu hataweza.
“Ukiona Rais anafanya maamuzi, jua kuna mambo mazuri anataka yafanyike, mkiona anabana matumizi, mjue kabisa kuna mambo mazuri yanakuja na hayo mambo mazuri ni kwa ajili ya manufaa yetu hata Rais akiondoka madarakani hawezi kuondoka nayo,” alisema.
Alisema kuna watu wanamuona Rais ni mkali na kusisitiza kuwa mtu anayepambana na ufisadi kamwe hawezi kuwa mpole, “Lazima awe mkali hata Yesu alipokuwa anakemea mapepo alikemea kwa ukali, ndivyo hata Rais anavyofanya pale anapopambana na uovu wa nchi.”
Pia Mwigulu aliwasihi waumini kujitoa kwa hali na mali katika kuchangia fedha kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa kanisa hilo kwani kuna siri kubwa kwa mtu anayechangia ujenzi wa nyumba za ibada huku akiwaomba waumini kuendelea kujenga makanisa mengi.
“Nimegundua ndani ya nyumba za ibada kuna siri kubwa, utafiti niliofanya mdogo nimekuja kukundua mikoa ambayo ina nyumba nyingi za ibada hawana matatizo mengi kama vile mabaa ya njaa, mfano mzuri ni mikoa ya Mbeya, Iringa, Kilimanjaro, Ruvuma na Njombe, kila mtaa kuna kanisa,” alisema.
Alisema mikoa ambayo haina nyumba nyingi za ibada ni Kagera, Dodoma, Tabora na Shinyanga. “Huko kupata kanisa ni kwa shida angalia sasa kila siku wao wanalia njaa Mbeya, Iringa chakula ni cha kumwaga,” alisema.
Askofu Malasusa
Akiendesha ibada ya harambee ya ujenzi wa kanisa hilo, Askofu Malasusa alisema jambo lolote linapotokea lina makusudi. Alisema kuambiwa kuhama ili kupisha upanuzi wa barabara ni baraka kutoka kwa Mungu hivyo hawana budi kuipokea.
“Hiyo ni baraka, unapopatwa na misukosuko usifikiri itakupeleka pabaya, Mungu yuko pamoja nanyi zaidi naomba muendelee kumwabudu Mungu, kumpenda na kuwa na amani. Mshukuruni Mungu maana amewapa akili ya kujenga kanisa lingine kubwa.”
Alisema wapo wachungaji wengine ambao ni maarufu lakini bado hawajapata baraka ya kujenga makanisa makubwa kama wao.
Katika harambee hiyo, waumini hao walichangia vitu mbalimbali baadhi walitoa mali zao na kuzipiga mnada wakiongozwa na askofu huyo ambaye alipiga mnada picha yake na kuiza kwa Sh3.5 milioni.
Waumini wengine walitoa mali mbalimbali kama vitenge, mbuzi na kuku kwa ajili ya kupigwa mnada ili kupata fedha zitakazosaidia kukamilisha ujenzi wa kanisa jipya.

Rais Magufuli ‘awakaanga’ mawaziri wake


“Nimekueleza tukiwa wachache ofisini nikajua utanisikia bado, nimezungumza tukiwa kwenye Baraza la Mawaziri (cabinet) bado,” hayo ni maneno ya Rais John Magufuli jana aliyoyatoa kwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage akimhoji kwa nini hajavirejesha serikalini viwanda ambavyo vilibinafsishwa lakini haviendelezwi.
Mwezi uliopita akiwa mjini Morogoro, Rais Magufuli aliwaagiza wafanyabiashara walionunua viwanda wakati Serikali ilipoamua kuvibinafsisha na kushindwa kuviendeleza wavirudishe serikalini akiwamo Mbunge wa Morogoro Mjini.
Jana, alirejea kauli hiyo na kumtaja waziwazi Waziri Mwijage alipokuwa akizungumza na wananchi wakati wa uzinduzi wa kiwanda kipya cha saruji cha Kilimanjaro kilichopo mjini Tanga, akielezea kushangazwa jinsi viwanda vingi vilivyobinafsishwa kwa miaka zaidi ya 20 iliyopita lakini haviendelezwa.
Alisema vipo viwanda ambavyo walipewa baadhi ya wawekezaji kwa urafiki wa viongozi waliopita hivyo akamuagiza Waziri Mwijage kuvifuta bila kuangalia sura.
“Sasa wewe waziri usiangalie sura za marafiki wa wenzako waliotangulia, wewe wakung’ute kisawasawa, hicho ndicho ninachotaka ukafanye wewe na makatibu wakuu wako. Nataka kuona kiwanda kimefutwa, hiki kimefutwa atakayejidai anakwenda mahakamani ninajua tuta-deal naye vipi najua sheria zipo.
“Waziri nakuomba nimezungumza mara nyingi, sitaki kukaa narudia hili kila siku. Si vizuri kulizungumzia hili hapa Tanga lakini napenda nizungumze, nisingezungumza ningeondoka moyo unauma, nataka muelewe.”
Alimtaka Waziri Mwijage asiogope kuvifuta viwanda vilivyokaa bila kuendelezwa akimkumbusha kuwa yeye ndiye aliyemteua.
Pia Rais Magufuli aliwaagiza wakuu wa mikoa kufanya tadhimini kwenye mikoa yao kubaini viwanda ambavyo vilibinafsishwa lakini vimekaa kwa muda mrefu bila kuendelezwa.
“Kama wapo wawekezaji wanaotaka kujenga viwanda nyang’anya, mtu huyu na mpe masharti ya miezi mitatu au minne naye akishindwa kuendeleza nyang’anya.’’
Katika uzinduzi huo, Rais Magufuli alitumia muda mwingi akikumbusha historia ya viwanda ya Mkoa wa Tanga akivitaja baadhi, cha Mkonge, Amboni Plastic, Nondo na Saruji.
“Tanga kulikuwa na kila aina ya viwanda, leo tujiulize vimeenda wapi? Tanga kuna reli, bandari, mawasiliano na umeme, lazima tujiulize wapi tumeshindwa? alihoji.
Jana haikuwa siku mbaya kwa Waziri Mwijage peke yake, akifungua Kiwanda cha Maziwa Tanga Fresh, Rais alieleza kushangazwa kwake na Waziri wa Kilimo, Chakula na Mifugo, Dk Charles Tizeba kutokufika katika kiwanda hicho kutatua matatizo waliyo nayo.
Rais Magufuli alisema anakifahamu vyema kiwanda hicho kwa sababu wakati wa Serikali ya Awamu ya Nne alipokuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, alikuwa akikitembelea.
Akizungumza baada ya Meneja wa Tanga Fresh, Michael Karata kueleza changamoto nne zinazokikabili zikiwamo kubwa mbili; Tume ya Ushindani wa Kibiashara (FCC) kukifikisha mahakamani na kutakiwa kulipa faini ya Sh 2.8 bilioni, Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuzuia hati ya biashara kutokana na kampuni iliyokiuzia bidhaa ya Azania kuwa na limbikizo la kodi na hivyo kushindwa kuendesha biashara.
Baada ya taarifa hiyo, Rais Magufuli ambaye aliweka jiwe la msingi na upanuzi wa kiwanda hicho alisema changamoto hizo zimetokana na Waziri wa Mifugo kutokitembelea na kuzifanyia kazi.
“Tanga Fresh nakijua vizuri iweje waziri, katibu mkuu na wakurugenzi wengine hawajafika? Naagiza waziri afike hapa ndani ya wiki moja na changamoto azifanyie kazi,” alisema Rais Magufuli.
Rais pia alimwagiza Waziri Mwijage kuangalia kama maziwa ya Tanzania yakizuiwa kupelekwa nje ya nchi basi na yeye azuie ya nje yasiiingie nchini.
Alisema anafahamu kuwa sekta ya maziwa imekuwa na changamoto ya kupigwa vita na masoko ya nje. Aliahidi kuvilinda viwanda vya maziwa nchini.
Aliagiza hati iliyozuiliwa na TRA ipatikane haraka ili kiwanda hicho kifanye kazi bila vikwazo kwa sababu Tanga Fresh inamilikiwa na wananchi kwa asilimia 42 huku kikipokea maziwa kutoka kwa wafugaji 6,000.
Dk Magufuli hakuishia kwa mawaziri hao tu, pia alieleza kukasirishwa kwake na kitendo cha mawaziri wa wizara zinazohusika na usimamizi wa ujenzi wa flow meter bandarini kushindwa kutoa uamuzi baada ya mwaka mmoja kupita bila kujengwa huku akisema baadhi yao ni wapumbavu.
Alisema licha ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kuagiza zijengwe, mwaka umepita na mawaziri wapo.
“Mawaziri wengine ni wapumbavu, hawatoi decision (uamuzi) haraka ndiyo maana nasema ni wapumbavu,”
Awali, akimkaribisha Rais Magufuli katika uzinduzi wa Kiwanda cha Saruji cha Kilimanjaro, Waziri Mwijage alimuomba Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Marten Shigella kutenga ekari 2,000 kutoka kwenye ekari 14,000 za mashamba matano yaliyofutwa na Rais Magufuli ili aweze kuwakaribisha wawekezaji kujenga viwanda.
Imeandikwa na Emmanuel Mtengwa, Burhan Yakubu na Raisa Said

Makamba njia panda


Maswali mazito yameibuka juu ya uamuzi wa Serikali kuwarudisha kazini kimyakimya wajumbe saba wa bodi na watendaji waandamizi wanne wa Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), siku chache baada ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), January Makamba, kuwasimamisha.
Mwananchi limedokezwa kuwa hivi sasa watumishi hao, akiwamo Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Vedasto Makota wanaendelea na kazi zao kama kawaida kwa maelekezo ya mamlaka za juu.
Wiki mbili zilizopita, Makamba alitangaza kutengua uteuzi wa wajumbe saba wa Bodi ya NEMC na kuwasimamisha wakurugenzi wake wanne ---Manchare Heche, Deus Katwale, Andrew Kalua na Benjamin Dotto--- kwa tuhuma kadhaa ikiwamo ya ucheleweshaji wa vibali vya ukaguzi wa mazingira na tuhuma za rushwa.
Alisema NEMC ina upungufu mkubwa kiutendaji huku akiwatuhumu baadhi ya watendaji kwa kuwasaidia watu wenye masilahi nao na kushindwa kutoa maelezo ya kuridhisha pale walipotakiwa kufanya hivyo.
“Kulingana na mamlaka niliyonayo chini ya Sheria ya Mazingira Kifungu cha 19 (2), nimeamua leo kutengua uteuzi wa wajumbe wote saba wa Bodi ya NEMC ili baadaye niteue wajumbe wapya ambao wataenda na kasi na ari tunayoihitaji sasa katika kuelekea uchumi wa viwanda. Mwenyekiti wa Bodi, ambaye mamlaka yake ya uteuzi ni Mheshimiwa Rais, ataendelea kuwepo hadi Mheshimiwa Rais atakapoteua mwingine.”
Pia alisema, “Tumewasimamisha kazi baadhi ya watendaji wa NEMC kuruhusu uchunguzi dhidi ya tuhuma zinazowakabili kabla ya kuchukua hatua zaidi.”
Makamba alimteua Dk Elikana Kalumanga kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NEMC.
Hata hivyo, baada ya hatua hiyo, imeelezwa kwamba wote walioondolewa wamerejeshwa kimyakimya. Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Vedasto Makota hakupatikana kuzungumzia suala hili na mmoja wa waliosimamishwa kazi, Heche hakukataa wala kukubali kwamba amerudishwa kazini, akisema hawezi kuzungumzia suala hilo kwa kuwa liko chini ya mamlaka ya waziri.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa tangazo hilo la Makamba halikudumu kwa zaidi ya wiki moja baada ya mamlaka za juu kuagiza hali irudi kama ilivyokuwa awali.
Baadhi ya watu walio ndani ya NEMC wamedai kuwa uamuzi huo wa Serikali utaathiri kwa kiasi kikubwa utendaji wa Baraza hilo la Mazingira linalokabiliwa na changamoto nyingi kiasi cha mchango wake katika masuala ya uhifadhi wa mazingira kuhojiwa mara kwa mara.
“Hapa palishageuka kama himaya ya watu fulani tu. Hakuna kinachoenda. Malalamiko ni mengi kutoka jumuiya ya wafanyabiashara na wenye viwanda. Sio siri tena kwamba rushwa imetawala hasa katika eneo la utoaji vibali vya mazingira,” alisema ofisa mmoja wa daraja kati wa NEMC kwa sharti la kutotajwa jina.
“Kuna ukiritimba mkubwa kutoa cheti cha mazingira na mtu kama akiwa tayari kutoa pesa anapata hata ndani ya siku mbili tu. Kama huna utasumbuka sana,” alisema ofisa huyo.
Wizara ya Viwanda na Biashara imewahi kusikika mara kadhaa ikilalamikia ucheleweshaji wa utoaji wa vibali vya mazingira kama moja ya mambo yaliyozorotesha jitihada za Serikali za ujenzi wa viwanda nchini.
Akiwa katika ziara ya kikazi Mkoa wa Pwani mwezi uliopita, Rais John Magufuli alionyesha waziwazi kukerwa na ucheleweshaji wa vibali vya mazingira unaofanywa na NEMC na alizungumzia suala hilo mara mbili katika mikutano yake ya hadhara.
Mbali na ucheleweshaji wa vibali vya mazingira, rushwa inatajwa kukithiri ndani ya wakala huyo wa mazingira huku watendaji wakidaiwa kuwatoza faini wenye viwanda kinyume cha sheria na wakati mwingine kuwatisha ili watoe rushwa kwa ahadi ya kuwapunguzia faini.
Akitoa mfano, ofisa mwingine wa NEMC aliyeomba kutotajwa jina amesema baadhi ya maofisa waliwahi kukitoza kiwanda cha kuchinja nyama ya punda mjini Dodoma kinachomilikiwa na raia wa China faini ya Sh240 milioni kinyume na Sheria za Mazingira.
Suala hilo linadaiwa kufika mezani kwa waziri Makamba ambaye baada ya uchunguzi na kuweka vielelezo mezani zikiwamo risiti za tozo, ikagundulika wawekezaji hao walilipa Sh20 milioni tu huku watu wa NEMC wakiondoka na Sh100 milioni baada ya kukubali kuwapunguzia Wachina hao kiasi cha faini.
Ofisa huyo alidai kuwa watendaji hao waliamua kughushi mukhtasari kuonyesha kwamba mwekezaji huyo aliomba kupunguziwa faini.
Taarifa zinasema kuwa watendaji wote wa NEMC waliotajwa kwenye mukhtasari huo baada ya kubanwa walikikiri kuwa hawakuhudhuria mkutano uliozaa mukhtasari huo na kwamba hawana mamlaka ya kumpunguzia mtu faini isipokuwa waziri peke yake.
Mtoa taarifa wetu anadokeza kuwa hata bodi ilipofikishiwa suala hili ikasema watu hao wapewe onyo wakati kosa ni la wazi kabisa.
“Huku ni kulindana tu na NEMC isipokuwa overhauled (fumuliwa) tusitegemee chochote. Hizi ni zama za accountability (uwajibikaji) na kwa kweli kuna mambo hayaendi sawa humu mwetu. Sisi tukiboronga madhara kwa nchi ni makubwa kuliko watu wanavyoona,” alisema ofisa huyo wa NEMC.
Alipotafutwa kwa simu, waziri Makamba alikataa katakata kuzungumzia suala hilo. “Sisi tuko vizuri tu na tunatekeleza mipango ya Serikali kama kawaida. Sina zaidi ya hilo,” alisema.
Habari kutoka ndani ya wizara zinasema kukithiri kwa matatizo ndani ya NEMC kuliwahi kumsukuma Waziri Makamba kuwaita watendaji wake na kuandaa mkakati wa kuyashughulikia, wakilenga zaidi suala la utoaji vibali vya mazingira kwa kuangilia muda unaotumika kwa kazi hiyo, gharama na kuziba mianya yote ya rushwa.
Vyanzo vyetu vinasema kuna wakurugenzi ambao wanakabiliwa na tuhuma za wazi za kukiuka sheria za utumishi wa umma ikiwamo rushwa na ndizo zilizomsukuma Waziri Makamba kuwasimamisha kazi akijipanga kufanya mabadiliko makubwa ndani ya NEMC.
Watu wanaofuatilia kwa karibu sakata hili wanasema makundi yenye masilahi ya kiuchumi na NEMC hawakupendezwa na mwelekeo wa Makamba katika kuifumua NEMC ndipo wakaanza mkakati wa chini kwa chini kukabiliana naye.
Makundi hayo ndiyo yanayodaiwa kuiteka NEMC na yanalaumiwa kwa kukwamisha juhudi mbalimbali za wizara na Serikali kwa miaka mingi sasa kama vile kuzuia matumizi ya mifuko ya plastiki na kudhibiti viwanda dhidi ya uchafuzi wa mazingira na kujenga jumba za kifahari ndani ya hifadhi za fukwe mbalimbali.
Haijulikani ni nani, katika mazingira gani na kwa sababu ipi aliamuriwa ‘kumzima’ Waziri Makamba lakini vyanzo vyetu ndani ya NEMC vinaonya kuwa uamuzi huo utaadhiri utendaji kazi wa baraza na kumpunguzia waziri mamlaka ya kiutawala dhidi ya Baraza hilo.
Habari zinasema tayari Wangwe, alikwishapewa barua ya kuondolewa NEMC na kurudishwa Hazina.
Wafuatiliaji wanahoji pia ni jinsi gani Makamba atapeleka uso wake na kuanza kufanya kazi na kundi la watu ambao hana imani nao tena na alikwishaamua kuwaondoa kazini.
“Huu uamuzi sijui umechukuliwa na nani lakini jambo lililo wazi ni kwamba utamuondolea kabisa waziri moral authority (mamlaka ya kimaadili) kutimiza mipango yake na watu hawa waliorudishwa. Hali hii nina hakika imemshushia hadhi hapo wizarani na itakuwa imemvunja sana moyo,” alisema mtoa taarifa huyo.
Wadadisi pia wanahoji endapo mikakati iliyopo ya kuifumua NEMC na kuifanya ifanye kazi kwa ufanisi na uadilifu zaidi itatekelezwa katika mazingira ya sasa.
Kwa upande mwingine, suala hili kwa namna moja au nyingine limeiweka majaribuni vita ya Rais Magufuli dhidi ya rushwa na utendaji usioendana na kasi yake hasa ikizingatiwa hata aliwahi kuonyesha kutoridhishwa na ufanisi wa NEMC.
“Tatizo ni wazi kabisa hawa watu walishafeli kabisa katika majukumu na Makamba aliona ili mambo yaende lazima awaondoe. Sasa changamoto kwa huyu bwana (Makamba) ni kuhakikisha kazi na mipango yake vinaendelea katika hali ya vikwazo vilivyo mbele yake,” anasema.
Wachambuzi wa masuala ya kisiasa wanasema inawezekana waziri huyo kijana hakufanya mawasiliano ya kutosha kabla ya kuchukua uamuzi wake.
“Hili haina tafsiri nzuri. Nchi nyingine waziri huwa anajiuzulu kwa sababu mamlaka yake yamevizwa. Inawezekana alichukua hatua hiyo bila mawasiliano ya kutosha. Sidhani kama walimpa go ahead (ruhusa) halafu wa-reverse (wageuke),” anasema Profesa wa Chuo Kikuu Katoliki cha Ruaha (RUCU), Gaudence Mpangala.
“Unajua mfumo wa utawala wetu wa sasa walio chini ya Rais mara nyingi wanachukua hatua kwa kudhani wanampendeza Rais au waonekane wanafanya kazi lakini si mara zote hiyo inafanya kazi.”
Profesa wa Sayansi ya Siasa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Benson Bana alisema hatua ya Serikali kubadili uamuzi ya Makamba inaashiria kuwa hakufanya mawasiliano ya kutosha kabla ya kuchukua uamuzi wake.
“Nafikiri inawezekana ni tatizo la mawasiliano na mamlaka. Unajua kimsingi Makamu wa Rais ndiye mwenye dhamana. Waziri hana instruments. (mamlaka). Sasa kuvunja bodi ni dhamana ya Makamu wa Rais. Swali kubwa la kujiuliza hapa ni je, Makamu wa Rais alijulishwa na kuridhia mpango wa Makamba? Kama hakuridhia inawezekana ndiyo sababu mambo yamekuwa hivyo,” alisema Bana.

Selcom yaipa shavu T-Junction ya Kijiweni Production

Uzinduzi wa filamu hiyo ambayo wahusika wake nji wasanii wa hapa nchini, umewezekana kutokana na ufadhili kutoka kampuni kadhaa ikiwemo Selcom.

Kampauni ya uzalishaji wa filamu ya Kijiweni Productions wiki hii itazindua filamu yake mpya ya T-Junction katika ukumbi wa Molimani City.
Uzinduzi wa filamu hiyo ambayo wahusika wake nji wasanii wa hapa nchini, umewezekana kutokana na ufadhili kutoka kampuni kadhaa ikiwemo Selcom.
Mkurugenzi wa Kijiweni Productions, Amil Shivji anasema wamefurahishwa na hatua ya Selcom kuwa mmoja wa wadhamini wa kundi lao.
”Tumefurahi kwamba Selcom wametudhamini. Ni kweli kwamba kampuni nyingi kwenye sekta binafsi wanaogopa kuunga mkono wasanii kwa namna yoyote kwa kuamini kwamba hawanufaiki kupitia udhamini wa Sanaa,” amesema.
Hata hivyo, amebainisha kuwa hayo ni mawazo potofu kwa sababu wanasahau kuwa sanaa inawezesha maisha ya watu wengi nchini.
“Sanaa Inaakisi mwenendo wa maisha ya kila situ. Tangazo ni sanaa, bango ni sanaa na kuna bajeti maalumu ambayo kitengo cha masoko wanapewa kutumia ili kutangaza shughuli zao.
“Ila unakuta mara nyingi hakuna ubunifu hata kidogo. Selcom wamejitokeza kama washupavu kubadilisha hali ya mambo na kukiri kwamba kama kampuni kubwa ni jukumu lao kusaidia kujenga tasnia ya sanaa na kurudisha hadhi ya wasanii ndani ya jamii.”
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Selcom, Benjamin Mpamo, amesema udhamini huo kwa Kijiweni Productions si wa kwanza na wala hautakuwa wa mwisho kufanywa na kampuni yake.
“Wiki iliyopita tulidhamini kampeni inayolenga kuelimisha na kupanua uelewa wa umma juu ya umuhimu wa kujua njia za kuzuia na kupambana moto majumbani. Katika kampeni hiyo itakayoendeshwa kwa miaka mitatu, tumeungana na kampuni ya Alaf kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Tanzania na taasisi isiyo ya kiserikali ya United Against Crime (UAC).
“Mwaka jana tulikuwa kampuni ya kwanza ya Kitanzania kudhamini shughuli za Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani. Tunayafanya hayo katika kutimiza wajibu wetu wa kurejesha kwenye jamii kidogo tunachopata kutokana shughuli zetu za biashara.
Kwa miaka mingi sasa tasnia ya filamu imekuwa kapu la kukusanya ajira za vijana katika nyanja mbalimbali zikiwamo uigizaji, utayarishaji filamu, usambazaji kazi za wasanii na hata kuzitangaza.
Lakini pamoja na hayo yote bado tasnia hiyo haifuatiliwi kwa karibu na vyombo husika. Kama ingefuatiliwa vyema bila shaka mambo yangebadilika, walau hivyo ndivyo anavyoona Shivji.
Kijiweni Productions si jina geni ni kampuni iliyoanzishwa  mwaka 2013, filamu yake  ya mwanzo ikiwa katika mtindo wa filamu fupi iitwayo Shoeshine.
Filamu hiyo ilishinda tuzo ya People’s Choice Award katika tamasha la ZIFF mwaka 2013 na iliendelea kushinda tuzo na kushiriki kwenye matamasha ya filamu nyingi duniani.

Ujazo wa mkaa mwisho kilo 50


Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) umewataka wasafirishaji na wauzaji wa mkaa nchini, kuhakikisha ujazo wa mkaa hauzidi kilo 50 ili kuepuka adhabu inayotokana na kukiuka Sheria ya Vipimo nchini.
Hata hivyo, katika maeneo mbalimbali nchini, bado wauzaji wa bidhaa hiyo wanauza kwa ujazo unaozidi kiwango hicho huku wengine wakiwa hawafahamu kuhusu uwapo wa sheria hiyo.
Akizungumza katika maonyesho ya Wakulima maarufu kwa jina la Nanenane jana, Meneja wa Habari na Mawasiliano wa TFS, Glory Mziray alisema sheria ya vipimo inataka bidhaa hiyo kupimwa katika ujazo wa kilo 50.
“Tunawataka wauzaji na wasafirishaji kuzingatia sheria hii ili kuepuka adhabu inayotokana na ukiukwaji wa sheria,” alisema Mziray.
Pia, alisema ushuru wa vitanda umepungua kutoka Sh120,000 mwaka uliopita hadi Sh 20,000 mwaka huu, huku ushuru wa mlango ukipungua kutoka Sh90,000 mwaka jana hadi Sh50,000 mwaka huu.
Hata hivyo, alisema watu wanaotaka maelezo zaidi kufika katika ofisi za wakala huo, kuangalia katika tovuti na mitandao ili kukidhi matakwa ya sheria hizo.
Muuzaji mkaa mkoani hapa, Rashid Maulid alisema ni vigumu kutekeleza sheria hiyo kutokana na wengi kutokuwa na mizani ya kupimia.

Bawacha wageukia mimba za utotoni

Mbunge wa Viti Malum, Susan Lyimo na wajumbe wa

Mbunge wa Viti Malum, Susan Lyimo na wajumbe wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) wa mkoa wa Dar es Salaam wakimkabidhi Mkurugezi wa Kituo cha Yatima group, Winifrida Lubaza (aliyevaa gauni la kitenge) msaada wa mifuko ya Simenti 35, kituoni hapo jana. Bawacha wametoa misaada mbalimbali kituoni hapo ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za chama hicho kusherehekea kutimiza miaka 25. Picha na Omar Fungo 
 Baraza la Wanawake Chadema Mkoa wa Dar es Salaam (Bawacha), limemuunga mkono Mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuhusu kuwataka wanafunzi watakaopata mimba waruhusiwe kurudi shuleni.
Kwa nyakati tofauti, walisema hayo jana wakati wakitoa msaada wa vitu mbalimbali kwenye kituo cha kulelea watoto cha Yatima Group Trust Fund (YGTF).
Msaada huo wa mifuko ya saruji 35, sukari kilo 25, unga kilo 50, sabuni, vifaa vya watoto shuleni, nguo pamoja na mahitaji mengine yenye thamani ya Sh2 milioni, ni sehemu ya kuazimisha miaka 25 ya Chadema tangu kuanzishwa kwake.
Mwenyekiti wa Bawacha Mkoa wa Dar es Salaam, Magreth Mugyabuso alisema wanathamini hali ya watu wa chini hasa wenye uhitaji, ndiyo maana imewasukuma kuwapatia msaada ikiwamo vifaa vya shule ili kupata elimu bora.
“Watoto hawa wanahaki kama wengine ambao wanasoma, imetugusa kufanya haya Mkoa wa Dar es Salaam... suala la elimu lipewe kipaumbele hasa kwa watoto wa kike tukiamini ukimwelimisha msichana umeelimisha jamii,” alisema Mugyabuso.
Mbunge wa Viti Maalumu Ilala, Anatropia Theonest alisema hawawezi kwenda tofauti na kauli ya Mdee.
Aliitaka jamii iunge mkono suala la mtoto wa kike kurudi shuleni akipata ujauzito na kujifungua.
“Wasichana hawapati mimba kwa kujitakia, wengi wanapitia magumu, mfano katika halmashauri ya Ilala, miezi mitatu iliyopita watoto 156 wamefanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia na watu wanaowazunguka. Jamii inapaswa kulikemea hili kwa kuwa matatizo humkuta kila mtu,” alisema Theonest.
Alisema kumnyima mtoto elimu ni kukiuka haki yake na misingi ya katiba ya nchi inayomtaka kila mtu apate elimu.
“Serikali inapaswa kuliangalia hili kwa makini, wengi wananyanyaswa wakiwa wadogo, hivyo bila kukemea baadhi ya kauli ni miongoni mwa ishara ya kuwakandamiza,” alisema.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Catherene Vallence alisema wanawapa kipaumbele wasichana na watoto wenye uhitaji katika kuhakikisha wanapata elimu bora huku wakiendelea kumuunga mkono Mwenyekiti wa Bawacha Taifa.
“Mwenyekiti Mdee, amepambana katika kupinga ukatili dhidi ya wanawake na sisi hatuko nyuma, ndiyo maana tunatekeleza haya kwa kuwafikia wananchi wa hali ya chini,” alisema Vallence. Aliaema hata idadi ya wapigakura wengi ni wanawake na ndilo kundi kubwa linalotaka maendeleo, hivyo kwa kumnyima elimu ni njia ya kumkwamisha kufikia ndoto zake.
Mkurungenzi wa YGTF, Winfrida Lubanza alisema kituo hicho kina watoto 151.
Pia, alisema wengine 300 waliokuwapo kituoni hapo wameondoka baada ya kumaliza shule na kuajiriwa.