Saturday, July 22

RAIS MAGUFULI AZINDUA MIRADI MBALIMBALI YA MAENDELEO NA KUHUTUBIA WANANCHI KWENYE MIKUTANO MBALIMBALI YA HADHARA


 Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania,  Dkt. John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Kakonko kabla ya kuzindua Ujenzi wa barabara ya Kibondo -Nyakanazi yenye urefu wa kilometa 54, katika mkoa wa Kigoma.
 Wananchi wa Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma wakisikiliza hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Uzinduzi wa  Ujenzi wa Barabara  ya Kibondo -Nyakanazi yenye urefu wa kilometa 54, kwenye Sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Standi Mpya ya Mabasi Kakonko katika mkoa wa Kigoma Rais yupo mkoani Kigoma kwa ziara ya siku Tatu
Baaadhi ya Viongozi wa vyama vya siasa na wananchi wa Wilaya ya Kakonko Mkoani Kigoma wakisikiliza Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa Uzinduzi wa  Ujenzi  wa Barabara  ya Kibondo -Nyakanazi.
 Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  pamoja na viongozi mbalimbali wakifungua kitambaa kuashiria kuweka jiwe la msingi la ufunguzi wa Barabara  ya Kibondo -Nyakanazi kiwango cha lami.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  pamoja na viongozi mbalimbali serikali wakikata Utepe  kuashiria kuweka jiwe la Msingi la Uzinduzi wa Ujenzi wa  Barabara  ya Kibondo -Nyakanazi 
 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akiwasalimia wananchi wa mji wa Kibondo wakati akiwa safarini kutoka Ngara kuelekea Mkoani Kigoma.
 Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na kijana mwenye ulemavu amabye ni fundi wa kushona nguo ndugu Aron Michael Kapililo mkazi wa Kibondo ambaye alisimiana na Rais Magufuli 
 Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na mamia ya wananchi wa kijiji cha Kifura,  Kibondo Mkoani kigoma waliokuwa wamesimama njiani ili kusalimiana na mh Rais akiwa njiani  safarini kutoka Ngara kuelekea Mkoani Kigoma
 Mamia ya wakazi wa Kasulu Mkoani Kigoma waliojitokeza kumsikiliza Rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 63 Kidawe - Kasulu. 
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  akisalimiana na mamia ya wananchi wa Mamia ya wakazi wa Kasulu Mkoani Kigoma waliojitokeza kumsikiliza wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 63 Kidawe - Kasulu.
 Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli akiwapungia mikono mamia ya wakazi wa Kasulu, Mkoani Kigoma.

Mamia ya wakazi wa Kasulu Mkoani Kigoma waliojitokeza kumsikiliza Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 63 Kidawe - Kasulu.
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya viongozi walioshiriki uzinduzi wa uzinduzi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 63 Kidawe - Kasulu
  Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Mbunge Kigoma Mjini Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe mara baada ya kuzindua  ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 63 Kidawe - Kasulu
 Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Kigoma akikata utepe kuashiria Uzinduzi wa  ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 63 Kidawe - Kasulu Mkoani Kigoma,
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono wananchi waliokuwa wamefurika njiani mara baada ya  Uzinduzi wa  ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa kilometa 63 Kidawe - Kasulu Mkoani Kigoma.

WAJASIRIAMALI WAKIWA KAZINI


 .Kamera imenasa wakazi wa jiji Dar es Salaam wajasiliamali maarufu kama machinga wakiandaa biashara zao leo katika soko la Karume Ilala.
Machinga akisafisha viatu ili kwa kuingiza sokoni katika soko la Karume Ilala jijini Dar es Salaam.
Watembea kwa miguu wakikwepa shimo lililopo katika barabara ya Kilwa jijini Dar s Salaam.

Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.

Dk. Kigwangalla afanya ziara mikoa ya Rukwa, Katavi na Tabora


Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla ameendelea na ziara yake ya kikazi ya kukagua huduma za Afya ‘Imarisha Afya’ katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali mbalimbali kwenye mikoa ya Rukwa, Katavi pamoja na Tabora.  

Akiwa katika mkoa wa Rukwa, Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea Hospitali ya Sumbawanga ambayp ni ya Mkoa wa Rukwa na kujionea mambo mbalimbali huku akiwapongeza kwa namna walivyoboresha huduma zao ikiwemo ile ya Maabara, Chumba cha upasuaji na huduma zingine ambapo aliwaagiza kuhakikisha wanakuwa na hakiba ya kutosha ya damu salama kwa ajili ya dharura kwa wagonjwa wa ukanda huo. 

 Mbali na Hospitali ya Mkoa wa Rukwa, pia aliweza kutembelea kituo ca Laela ambapo pia mbali ya kujionea utendaji kazi wa kituo hicho alipongeza juhudi za Mbunge wa jimbo la Kwera, Mh. Ignas Alloyce Malocha kwa kushirikiana na wananchi wake katika masuala ya huduma za Afya. Ziara hiyo katika mkoa wa Rukwa, aliweza kumalizia katika Kituo cha Afya Wampembe kilichopo Wilayani Nkasi ambapo alijionea shughuli mbalimbali ikiwemo huduma za Upasuaji hata hivyo aliutaka uongozi wa kituo hicho ambacho kipo mwambao wa Ziwa Tanganyika kuhakikisha wanakamilisha mifum ya maji safi na salama ndani ya kituo pamoja na kuboresha huduma za Maabara na usafi kwa ajumla.  

Akiwa katika Mkoa wa Katavi, Dk. Kigwangalla aliweza kufanya ziara ya kushtukiza kituo cha Afya Inyonga,kilichopo Mlele majira ya Saa Sita mchana na kuweza kukagua maeneo mbalimbali ikiwemo Chumba cha Maabara, Chumba cha Upasuaji na wodi ya akina mama wanaosubiria kujifungua.  

Hata hivyo, Dk. Kigwangalla amemtaka Kaimu Mganga Mkuu wa Kituo hicho kumuandikia maelezo juu ya kutokuwepo kwa watoa huduma kwenye jingo la chumba cha upasuaji na eneo la wodi ya akina mama wanaosubiria kujifungua kwani licha ya kufika hapo hakukuta mtoa huduma hata mmoja kwa wakati huo hali ambayo inaweza kuleta hatari.  

“Nataka kupata maelezo kwa maandishi. Kwa nini hakukua na watoa huduma ndani ya Chumba cha upasuaji na kule kwa wodi ya wamama wajawazito. Nilifika kuwakagua kwa upande wa Maabara nimekuta safi mumeweza kuboresha huduma na mumezingatia maelezo yangu niliyoyatoa kipindi nilichofika kukagua mwaka jana. Lakini pia hali niliyoikuta katika maeneo hayo niliyotembelea bila kuwakuta wahusika hii ni hatari nitahitaji maelezo ya kimaandishi” alieleza Dk. Kigwangalla wakati akitoa maagizo kwa Kaimu Mganga Mkuu wa kituo hicho. 

 Aidha, akiwa katika mkoa wa Tabora, aliweza kutembelea eneo la jengo linalojengwa Hospitali ya Wilaya ya Uyui na baadae aliweza kumalizia ziara yake katika Zahanati ya Isikizya ambapo aliagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Uyui kuhakikisha wanatenga bajeti pamoja na kushirikiana na nguvu za wananchi na mbunge wa jimbo hilo wanajenga majengo ya kulazwa wagonjwa, chumba cha upasuaji, maabara na miundombinu mingine ili Zahanati hiyo ije kupanda na kuwa Kituo cha Afya kwani kinahudumia eneo kubwa katika mji huo wa Isikizya ambayo hipo ndani ya Makao makuu ya Wilaya hiyo.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akikaguachumba cha upasuaji Hospitali ya Mkoa wa Rukwa
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua Maabara ya Mkoa wa Rukwa
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akikaguachumba cha upasuaji Hospitali ya Mkoa wa Rukwa
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa viongozi wa Hospitali ya Mkoa wa Rukwa
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akiingia chumba cha Wodi ya wanawake kituo cha Afya Laela Mkoa wa Rukwa
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akielekea kukagua Maabara ya Kituo cha Afya Laela Mkoa wa Rukwa
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Mh. Saidi Mtanda akihutubia wakati Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla alipotembelea kituo cha Afya Wampembe Mkoa wa Rukwa
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua kitanda ndani ya chumba cha kujifungulia katika kituo cha Afya Wampembe Mkoa wa Rukwa
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akitembelea kituo cha Afya Wampembe, Mkoa wa Rukwa. kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Nkasi, Mh. Said Mtanda
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua mfumo wa maji unaoingia kituo cha Afya Wampembe, kutokea Ziwa Tanganyika, Mkoa wa Rukwa
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua chumba cha upasuaji mdogo cha Kituo cha Afya Nkasi alipotembelea hapo majira ya saa mbili usiku, Mkoa wa Rukwa
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua eneo litakalojengwa majengo ya utanuzi wa kituo hicho cha Afya ambapo kikikamilika kinatarajia kuwa Hospitali ya Wilaya ya Nkasi Mkoa wa Rukwa
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akipatiwa maelezo ya maendeleo ya jengo linalojengwa kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Uyui, Mkoani Tabora, kutoka kwa Mbunge wa Jimbo la Tabora Kaskazini Mh. Almasi Maige
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua jengo litakalojengwa Hospitali ya Wilaya ya Uyui, Mkoani Tabora.
Jengo linaloendelea kujengwa kwa ajili ya Hospitali ya Wilaya ya Uyui
 
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akikagua ndani ya Maabara ya Kituo cha Afya Inyonga, Mlele, Mkoani Katavi
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Mh. Dk.Hamisi Kigwangalla akisaini kitabu cha wageni Kituo cha Afya Inyonga, Mlele, Mkoani Katavi

KOMBE LA MATAIFA AFRIKA SASA KUFANYIKA JUNI NA JULAI 2019 NCHINI CAMEROON



Shirikisho la soka barani Afrika  (CAF) limethibitisha.kuwa Kombe la mataifa bingwa Afrika 2019 litafanyika mwezi Juni na Julai 2019.

Mchuano huo huwa unafanyika mnamo mwezi Januari na Februari na kusababisha migogro na vilabu vya Ulaya ambavyo hulazimika kuwatoa wachezaji katikati ya msimu.
Kinyang'anyiro hicho cha 2019 kitakachoandaliwa Cameroon kitashirikisha timu 24 badala ya 16. Mabadiliko hayo yalitiwa sahihi na kamati kuu ya CAF katika mkutano uliofanyika mji mkuu wa Rabat.
Michuano hiyo imekuwa ikishirikisha timu 16 tangu 1996. Upanuzi wa mechi hizo unaweza kusababisha matatizo kwa Cameroon ambayo itaanda fainali ijayo, huku waziri wa michezo wa taifa hilo la Afrika ya kati akilazimika kukataa ripoti kwamba maandalizi yalikuwa nyuma.
Mashindano hayo yataendelea kila baada ya miaka miwili barani Afrika. Caf ilikuwa inapanga iwapo itaruhusu mataifa kutoka mabara mengine kushiriki ama hata kuandaa mchuano huo.
Tangazo hilo linajiri kufuatia mkutano wa siku mbili ulioandaliwa na rais wa Caf Ahmad kuzungumzia hali ya soka barani Afrika.

NDOTO ZA ZANZIBAR KUSHIRIKI MICHUANO YA CAF ZAFUTIKA, YAVULIWA UANACHAMA




Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limefanya maamuzi ya kuwavua uanachama chama cha soka cha Zanzibar ikiwa ni miezi minne toka  kipewe uanachama na CAF kutoka kwa Rais aliyepita Issa Hayatou.

Rais wa CAF Ahmad Ahmad (pichani)  amesema Zanzibar walipewa uanachama kimakosa na kama sheria zingepitiwa vizuri wasingepewa uanachama. 
“Walipewa uanachama bila kupitia vizuri kanuni ambazo ziko wazi na zinaeleza kila kitu, kama kanuni na sheria zingepitiwa kiufasaha wasingepewa uanachama”, alisema.

Sababu kubwa ambayo CAF wameivua uanachama Zanzibar ni kutokana na kisiwa hicho kuwa ndani ya Tanzania ambao nao ni wanachama wa CAF.

“Jina la nchi linatokana na jina linaloandikwa katika umoja wa mataifa UN na Zanzibar katika umoja huo inafahamika ipo ndani ya nchi iitwayo Tanzania ambao ni wanachama wa CAF” alisema Ahmad.

Hilo ni pigo kubwa kwa Wazanzibari kwani wakati huu walikuwa wakipambana kupata uanachama wa FIFA ambao wameukosa na wa CAF nao pia wamekosa.
Kwa maana hiyo ndoto ya kisiwa cha Zanzibar kushiriki michuano ya CAF kama mwanachama zimekufa rasmi na sasa watakuwa wakishiriki michuano hiyo kama Tanzania (Zanzibar na Tanzania bara).

WAZIRI LUKUVI AONYA MAAFISA ARDHI WASIO WAADILIFU



Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiwaonya maafisa ardhi na maafisa mipango miji wasio waadilifu na kusababisha kero za migogoro ya ardhi nchini wakati wa uzinduzi Master Plan ya mji wa Iringa. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akimkabidhi kitabu cha Master Plan ya mji wa Iringa Meya wa Halmashauri ya Iringa Alex Kimbe. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akiteta jambo na Meya wa Halmashauri ya Iringa Alex Kimbe na Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa. 
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi akipongezwa na Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa mara baada ya Uzinduzi wa Master Plan ya mji wa Iringa. 
Baadhi ya wakazi wa mji wa Iringa waliofika kushuhudia Uzinduzi huo.

……………………………………………………………………………………….

Na Hassan Mabuye Kitengo cha Mawasiliano, Wizara ya Ardhi


Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amewaonya maafisa ardhi na maafisa mipango miji wasio waadilifu na kusababisha kero za migogoro ya ardhi nchini.

Waziri Lukuvi aliyasema hayo leo katika ukumbi wa shule ya sekondari Lugalo mjini Iringa wakati wa Uzinduzi wa Master Plan ya Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.

Amesema mchezo huo wa ufisadi ambao umekuwa ukitumiwa miaka yote na maofisa ardhi nchini ameubaini na kuwataka wakurugenzi wa Halmashauri nchini kutokubaliana na ramani za maeneo mapya zinazoletwa na wataalam hao bila ya wao kufika maeneo husika na kuoneshwa maeneo hayo ili kujiridhisha.

Waziri Lukuvi amefichua kuwa ufisadi unaofanywa na maafisa ardhi nchini kwa kupima viwanja hewa kwa ajili ya maslahi yao na kusema kuwa mbinu ambayo wamekuwa wakiitumia kuiibia serikali amekwisha ibaini na hata kubali kuona mbinu hiyo inapewa nafasi katika serikali hii ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt John Pombe Magufuli .

Maafisa ardhi wakishirikiana na maafisa mipango miji pamoja na wapima wamekuwa wakitajirika sana kwenye idara zao na wanatakata kwa ujanjaujanja na ufisadi wanaoufanya kwa kutengeneza ramani zinazoonesha maeneo mazuri na muhimu katika miji kwamba hayafai kutumika, kumbe wameyauza maeneo hayo kwa mlango wa nyuma na kwa bei za juu.

Unakuta kwenye ramani inayonyesha kuna bonde kubwa lisilofaa kujengwa kumbe ukifuatilia eneo hilo ni zuri kuliko yote na hapo wametenga viwanja vya kuuza. Unakuta ukipima kuna viwanja vingi na vizuri ambavyo ni vyao wao wanachofanya baada ya kuuza viwanja halali za Halmashauri hurudi kupima maeneo hayo walioonyesha ni mabonde na kugawana wao kwa ajili ya kuuza kwa faida yao.



Lukuvi amesema kuwa wathamini nao pi wamekuwa wakiwapunja wananchi wasio elewa kwa kuwafanyia tathimini kubwa zaidi ya uhalisia wake na pindi pesa inapotoka utakuta nyumba inathamani ya milioni 7 wakati wao wanasema inathamani ya milioni 20 ili cha juu wapate wao.

“wakati nilipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam niliweza kubaini ujanja wa wathamini baada ya eneo ambalo nyumba zake zina thamani kati ya milioni 20 hadi 50 kwa maana nyumba hizo ni za udongo ila maofisa hao walimtafuta mtu na kutafuta nyumba nzuri zaidi na kumshikisha kibao kisha kumpiga picha na kuandika kuwa nyumba hiyo inathamani ya zaidi ya milioni 200.

Niliamua kufanya uchunguzi wangu na kumtafuta mtu aliyekwenye picha na kumbana ndipo aliniambia ukweli kuwa mthamini huyo ni ndugu yake hivyo walikubaliana pesa ikitoka atalipwa milioni 70 na milioni 130 ni za afisa huyo”

Hata hivyo alisema kuwa ujenzi holela katika miji na halmashauri imesababishwa na ukilitimba wa utoaji wa vibali kwa wakati na ndio sababu ya wananchi kuvamia maeneo yasiyo pimwa japo kuanzia sasa wote waliopo katika maeneo yasiyo pimwa watapewa leseni ya makazi ya miaka mitano na watalipa kodi ya ardhi na baada ya miaka mitano wahakikishe wamepimiwa ili kupewa hati.

Hivyo Lukuvi aliwataka maafisa ardhi na wathamini wa ardhi manispaa ya Iringa kutofanya kama maeneo mengine kwa kufuata mpango maeneo yote ambayo yameelekezwa kwenye Masta Plan hiyo na kwenda kutenda haki.

Katika hatua nyingine waziri Lukuvi alitoa agizo kwa wale wote waliopewa ardhi kwa ajili ya ujenzi wa hoteli na viwanda na wale waliouziwa viwanda vya serikali, hotel na mashamba ya serikali kuviendeleza haraka kabla ya ardhi hiyo haijapokonywa .

Nae Mkuu wa Mkoa wa Iringa Bibi Amina Masenza akimkaribisha waziri Lukuvi amesema kuwa mkoa wa Iringa umeendelea kuhamasisha wananchi kuzingatia sheria na taratibu za ujenzi na kuachana na ujenzi holela na ndio sababu ya kuja na Masta Plan hiyo ambayo imeanzishwa na aliyekuwa mstahiki meya wa halmashauri hiyo Amani Mwamwindi.

Akitoa taarifa ya uandaaji wa Masta Plan hiyo kwa ajili ya mwaka 2015-2035 Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Dkt William Mafwere, alisema kuwa dhumuni la mpango huo ni kutatua changamoto zilizokuwa zinaikabili Manispaa na kuwa dhana kuu ya mpango huo ni dhana unganishi ikijumuisha dhana nyingine.

Alisema jumla ya miradi 31 itatekelezwa katika awamu ya kwanza 2015-2020 kuwa baadhi ya miradi hiyo ni kituo cha mabasi Igumbilo, kituo hicho kimeanza ujenzi na hatua ya utekelezaji imefikia asilimia 30.

Nae Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa alisema kuwa kazi inayofanywa na Waziri Lukuvi ni tofauti na mawaziri wengine kwani amekuwa ni waziri wa mfano katika kuchapa kazi.

“Kwa mnaonifahamu vizuri mimi sio mbunge wa kusifia sifia ni mbunge mwenye msimamo ila nampongeza sana Waziri Lukuvi ni waziri mchapakazi na kazi zake zinaonekana na ndio maana hata bungeni ni waziri pekee ambaye bajeti yake ilipitishwa kwa kishindo hata na sisi wabunge wa kambi ya upinzani”

Mpango Kabambe ni chombo cha kuchochea utumiaji wa fursa zilizopo katika mji, kuongeza kasi ya upangaji, upimaji na umilikishaji wa ardhi kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii na kupunguza na kumaliza migogoro ya ardhi. kudhibiti ujenzi holela mijini na hutumika pia kuongoza, kusimamia na kudhibiti ukuaji na uendelezaji wa mji na kutoa uhakika kwa wawekezaji katika Halmashauri za Manispaa ya husika.

Jeshi la Polisi lasema uhalifu umepungua, ubakaji umeongezeka


ZIARA YA KIKAZI: Msemaji mpya wa Jeshi la
ZIARA YA KIKAZI: Msemaji mpya wa Jeshi la Polisi, Kamishina Msaidizi (ACP), Barnabas Mwakalukwa akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL), Francis Nanai (kulia) alipotembelea ofisi za kampuni hiyo jana. Katikati ni Mhariri Mtendaji Mkuu wa MCL, Bakari Machumu. Picha na Anthony Siame 
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi limesema hali sasa ni shwari kwa kuwa vitendo vya unyang’anyi vimepungua, lakini likasema hali ya ubakaji na ulawiti kwa watoto wadogo ni mbaya.
Jeshi hilo pia limesema limefanikiwa kudhibiti kwa kiasi kikubwa mauaji yanayofanywa na watu wasiojulikana katika wilaya tatu za mkoani Pwani.
“Tatizo kubwa kwa sasa ni ubakaji na ulawiti. Hii inatokana na makosa mengi sasa yanaripotiwa kwa sababu ya ufahamu wa wananchi kuongezeka,” alisema msemaji huyo wa Jeshi la Polisi, Kamishna Msaidizi (ACP), Barnabas Mwakalukwa alipotembelea ofisi za kampuni ya Mwananchi Communications Limited zilizopo jijini Dar es Salaam jana.
Mwakalukwa, ambaye alikuwa katika ziara yake ya kwanza kwenye vyombo vya habari tangu ateuliwa kushika nafasi hiyo alisema kwa sasa nchi ina amani na utulivu kwa kuwa vitendo vya unyang’anyi wa kutumia silaha, uporaji, mauaji ya vikongwe na albino yamepungua.
Mwakalukwa, ambaye pia ni mchambuzi wa uhalifu, alisema vitendo vya ubakaji na ulawiti vinakua kwa kuwa sasa wananchi wengi wamesahau maadili yao kama Watanzania.
Alisema kwa sasa mitandao ya kijamii imeathiri jamii, lakini pia watu hawana maadili tena kiasi kwamba wanaona  hawana wajibu wa kuwaelekeza watoto wa wenzao.
“Hata wazazi nao wamesahau majukumu yao ya malezi, lakini pia tunaaminiana kupita kiasi. Mgeni anakuja nyumbani kwako, unaruhusu alale na watoto bila kujua athari wanazoweza kuzipata,” alisema.
“Mgeni anamnajisi mtoto lakini kwa sababu ni mtu wa karibu na familia taarifa hazifiki kituoni. Kunakuwa na mgogoro katika familia. Mama analalamika sana, lakini baba anataka wayamalize katika level (ngazi) ya familia. Matokeo yake taarifa zinaletwa zikiwa zimechelewa sana.”
Mwakalukwa, ambaye hakutoa takwimu za kukua kwa vitendo hivyo, alisema kesi nyingine za ubakaji zinatokana na wanawake wanaofanya biashara ya kuuza miili.
 “Wanakutana na mteja, lakini wasipokubaliana, wanafanyiwa vitendo vya unyanyasaji na wanakuja kuripoti polisi kwamba wamebakwa,” alisema kamanda huyo.
Kuhusu wizi, Mwakalukwa ambaye amechukua nafasi ya Advera Bulimba aliyehamia Mwanza, alisema umepungua mitaani kutokana jeshi hilo  kushirikina na wadau kutoa elimu na kuhamasisha.
“Mabenki sasa yamewaelimisha wateja wao kutotembea na fedha nyingi, lakini pia watu hawakai na fedha nyingi nyumbani hivyo hata wahalifu wanaona wakivamia hawawezi kupata kitu,” alisema.
Alisema suala jingine lililopunguza uhalifu ni kupiga marufuku pikipiki za abiria, maarufu kama bodaboda kuingia mijini.
Alisema bodaboda zilikuwa zinatumiwa na wahalifu na kwamba waathirika wakubwa wa vitendo hivyo walikuwa wanawake kutokana na kupenda kutumia usafiri huo.
Alisema wengi waliporwa mikoba yao, fedha na hata kubakwa.
“Unajua wakati tunasema pikipiki zisiingie mjini, watu hawakutuelewa lakini niwaambie tu uamuzi ule umeleta mafanikio sana. Wanawake walikuwa waathirika wakubwa wa matukio ya uvamizi, walikuwa wakiibiwa mikoba yao na kunyang’anywa vitu vya thamani lakini sasa hali ni tofauti,” alisema.
Hata hivyo, Mwakalukwa ambaye kabla ya kuteuliwa kuwa msemaji wa jeshi hilo alikuwa kitengo cha operesheni mkoani Mwanza, alisema pamoja na uhalifu kupungua mitaani, wahalifu wamebuni mbinu mpya; sasa wanaiba kwa njia ya mitandao.
Kazi kubwa
“Kwa sasa  kuna kazi kubwa ya kumaliza uhalifu wa njia ya mtandao kwa sababu baada ya teknolojia kupanuka, wahalifu hawatumii tena silaha na badala yake wanaiba kwa njia ya mtandao,” alisema.
“Unajua wengi wanatapeliwa na kuibiwa ila hawasemi, wananchi wanafikiri wanasiasa ndiyo waathirika wakuu. Ngoja nikwambie hao ni idadi ndogo sana ukilinganisha na wananchi wa kawaida.
“Sasa wahalifu wanakuja moja kwa moja kwenye wallet (pochi) yako kupitia ATM. Wanachofanya ni kutumia mitandao. Hivyo kazi bado kubwa na kinachotakiwa zaidi ni kutoa elimu ili watu wasihamishe fedha kwa mtu aliyemtumia tu ujumbe mfupi wa simu kwamba atume fedha,” alisema.
Sirro anastahili sifa
Mwakalukwa pia alizungumzia mauaji yanayoendelea katika wilaya za Kibiti, Rufiji na Mkuranga akisema hali sasa ni shwari na kumsifu mkuu mpya wa Jeshi la Polisi (IGP), Simon Sirro kwamba amefanya kazi kubwa.
“Kibiti sasa kuna amani. Kibiti itabadilika kwani hata sasa  hatusikii tulivyokuwa tukiyasikia. Waandishi tusifanye propaganda kuwa Kibiti haikaliki. Hali sasa shwari na sisi tumeanzisha mkoa maalumu wa kipolisi, maana yake usalama sasa upo,” alisema Mwakalukwa.
Alisema kwa jinsi hali inavyoendelea, itafikia wakati Kibiti itakuwa sehemu nzuri ya kuwekeza tofauti na watu wanavyosema sasa kuwa ekari kumi inauzwa Sh1,000 kuonyesha kuwa wilaya hiyo si salama .
“Ninachowashauri ni kwamba andikeni habari nzuri za Kibiti,” alisema.
Wilaya hizo tatu zimekuwa zikibaliwa na mauaji ya viongozi na watendaji wa vijiji na vitongoji tangu Mei mwaka jana.
Katika matukio machache, wauaji hao waliacha ujumbe kuwa viongozi hao wamekuwa wakidhulumiwa na watendaji wa Serikali, lakini mauaji hayo ya visasi yamekuwa yakitia shaka kutokana na matumizi ya silaha na kulenga polisi pia.

BALOZI WA ISRAEL NCHINI MHE. YAHEL VILAN AWAAGA WAFANYAKAZI WA TAASISI YA MOYO JAKAYA KIKWETE (JKCI) BAADA YA KUMALIZA MUDA WAKE WA KUFANYA KAZI HAPA NCHINI



Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimshukuru Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan (kulia) kutokana na nchi yake kuisaidia Taasisi hiyo kuwapatia mafunzo madaktari, wauguzi na kutoa matibabu kwa watoto. Katikati ni Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo Sulende Kubhoja. 
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akizungumza na Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo kuwaaga wafanyakazi baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini. Israel imekuwa ikiisadia JKCI kwa kutoa mafunzo kwa madaktari, wauguzi na matibabu kwa watoto. 
Balozi wa Israel nchini mwenye makazi yake jijini Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi wakati alipotembelea Taasisi hiyo leo kuwaaga wafanyakazi baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini. Israel imekuwa ikiisadia JKCI kwa kutoa mafunzo kwa madaktari, wauguzi na matibabu kwa watoto. 
Mwanamuziki kutoka nchini Israel Maestro Nir Brand akiwaimbia wimbo watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakati balozi wa nchi hiyo Mhe. Yahel Vilan alipotembelea Taasisi hiyo kuwaaga wafanyakazi baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini. 
Balozi wa Israel nchini ambaye makazi yake yapo Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan (watatu kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi pamoja wa wafanyakazi wa Taasisi hiyo na wageni kutoka nchini Israel. 
Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo Sulende Kubhoja wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) akizungumza na Daktari Bingwa wa mfumo wa chakula kwa watoto Cohen Shlomi kutoka nchini Israel wakati wa ziara ya balozi wa nchi hiyo alipotembelea Taasisi hiyo kwa ajili ya kuwaaga wafanyakazi. 
Baadhi ya watoto wanaotiba katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) wakimsikiliza Balozi wa Israel nchini ambaye makazi yake yapo Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan alipokuwa akiwaaga wakati wa ziara yake aliyoifanya leo katika Taasisi hiyo. Serikali ya Israel kupitia Taasisi ya Save Child Heart (SACH) imegharamia matibabu ya watoto 40 tangu Novemba 2015 hadi sasa ambao walitibiwa nchini humo. 
Balozi wa Israel nchini ambaye makazi yake yapo Nairobi nchini Kenya Mhe. Yahel Vilan akizungumza na wafanyakazi pamoja na watoto wanaotibiwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete wakati wa ziara yake ya kuwaaga aliyoifanya leo baada ya kumaliza muda wake wa kufanya kazi hapa nchini. Israel imekuwa ikiisadia Taasisi hiyo kutoa mafunzo kwa madaktari, wauguzi na matibabu kwa watoto. 

WAZIRI MKUU ATOA MIEZI MITATU WALIOJENGA NDANI YA MPAKA WA TANZANIA NA ZAMBIA KUBOMOA NYUMBA ZAO


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametoa miezi mitatu kwa wananchi wote waliojenga ndani ya eneo la mpaka wa Tanzania na Zambia kubomoa nyumba zao .

Pia ameiagiza Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuanza kuweka alama za X katika nyumba 252 zilizojengwa ndani ya mpaka huo ili wahusika wazibomoe.

Agizo hilo amelitoa leo jioni (Ijumaa, Julai 21, 2017) alipotembelea eneo la ujenzi wa Kituo cha Pamoja cha Forodha (OSBP) katika mpaka wa Tanzania na Zambia, ambacho kinajengwa na Serikali ya Tanzania na kitagharimu sh. bilioni 12.

“Kuna watu wamejenga ndani ya mpaka wa Tanzania na Zambia na kuendesha biashara zao jambo ambalo ni kinyume cha sheria na linazikosesha Serikali mapato.”Kufuatia hatua hiyo Waziri Mkuu ametoa muda wa miezi mitatu kwa watu wote waliojenga kuanzia umbali wa mita 50 kutoka Tanzania na mita 50 kutoka Zambia kuzibomoa nyumba hizo kwa hiari.

“Hatuna msamaha kwa watu waliojenga katika eneo hili kwa sababu wamesababisha tupoteze kodi nyingi, hivyo baada ya kumalizika muda huo mamlaka husika zibomoe nyumba zote zitakazosalia.”

Awali Waziri Mkuu alikutana na Mkuu wa wilaya ya Nakonde nchini Zambia, Bw. Field Simwinga ambaye alisema wamekubaliana na utekelezaji wa agizo hilo kwa kuwa jambo hilo linaathiri shughuli za mipakani kwa pande zote mbili.

Bw. Simwinga alisema tayari wameshaanza kuwaeleza wananchi wao waliojenga ndani ya mpaka huo kuanza kuondoka, ambapo Waziri Mkuu amesema wanataka eneo hilo liwe wazi ili iwe rahisi kuutazama mpaka huo kwa umakini.

Mkuu huyo wa wilaya ya Nakonde alisema utekelezaji wa jambo utafanikiwa kwa urahisi kutokana na ushirikiano wa Serikali za Tanzania na Zambia.

IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, JULAI 21, 2017


 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwapungia wananchi wakati alipokagua eneo la ujenzi wa jengo la pamoja la forodha kwenye mpaka wa Tanzania na Zambia katika mji mdogo wa Tunduma. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Songwe Julai 21, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Waziri aivunja Bodi ya soko la Kariakoo


Waziri wa Nchi Ofisi  ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa George Simbachawene ameivunja bodi ya Shirika la Masoko Kariakoo baada ya kushindwa  kutekeleza majukumu yake ya msingi.
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyosainiwa na Msemaji wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Rebecca Kwandu ilisema kwamba  uamuzi huo ni baada ya uongozi kushindwa kutekeleza majukumu yao ya msingi waliyopewa ya kumshauri Waziri wa Nchi Tamisemi juu ya uendeshaji wa Soko hilo.

Coaster yagonga treni leo


Dar es Salaam. Watu kadhaa wamejeruhiwa kufuatia ajali iliyotokea asubuhi ya leo, Jumamosi, Julai 22, baada daladala aina ya coaster kuigonga treni maeneo ya Tandika.
Mashuhuda waliokuwepo eneo la tukio wamedai kuwa kuna majeruhi kadhaa ambao wamenza kufanya jitihada za kuwaokoa kutoka katika gari hilo.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Gilles Muroto amezungumza na Mwananchi kwa njia ya simu na kuthibitisha ajali hiyo.
Muroto amesema bado hana taarifa ya uhakika juu ya ajali hiyo na atazungumza pindi atakapofika sehemu ajali ilipotokea.
“Ni kweli ajali imetokea ila sina taarifa sahihi hadi nikifika, ndiyo naelekea,” amesema Muroto.

Friday, July 21

Mamba atishia amani Tanga



Tanga. Wakazi wa Mitaa ya Kange na Mkurumuzi jijini Tanga wamesema maisha yao yapo hatarini kutokana na bwawa lilioibuka baada ya kubomoka bwawa la samaki la kiwanda cha Rhino kuwa na mamba wakubwa.
Wakazi hao wamedai kuwa mwanamke mmoja alinusurika kuliwa na mamba mkubwa ambaye alikuwa amejificha katika kichaka.
Licha ya kufikisha malalamiko yao katika mamlaka husika na
kamati ya maafa ya Wilaya ya Tanga kutembelea, lakini ni miezi mitatu sasa hakuna hatua za kwuadhibiti wanyama hao zilizofanyika.
Mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama cha Maopinduzi (CCM) Kata ya Maweni, Said Bindo (72) amesema hali ilivyo inavyohatarisha usalama wa wakazi wa mtaa huo na kuitaka Serikali kutosubiri maafa yatokee.
“Tatizo hapa ni kwamba ni sababu huku wanaishi watu wa hali ya chini… kama wangekuwa wanaishi vigogo, hili bwawa lisingekuwepo. Kinachohitajika ni kutengeneza daraja litakalokuwa na uwezo wa kupitisha maji kwa wingi ili bwawa likauke,” amesema Kada huyo wa CCM.
Bindo, ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya siasa ya CCM tawi la Kange, amesema ameishi hapo  kwa kipindi cha zaidi ya miaka 50 na haijawahi kutokea hali kama hiyo.
“Sababu zinazotolewa tunaona kama ni visingizio… wanasema eti mara Halmsahuri itakapopata fungu, lakini kwa umri wangu na uzoefu nilionao, tatizo kama hili ni janga ambalo linahitaji kutatuliwa kwa fungu la dharura au kukiamuru kiwanda cha Rhino kujenga daraja kwa sababu ndiyo chanzo,” amesema Bindo.
Issa Shaaban, ambaye nyumba anayoishi inapakana na mto huo alilalamika kuwa jana jioni mke wa kaka yake alikurupshwa na mamba mkubwa lakini alifanikiwa kukimbia na kujiokoa.
Diwani wa kata ya Kange, Joseph Colyvirs, amesema tayari Baraza la Madiwani la Halmashauri ya jiji la Tanga limeshapitisha katika mpango wake wa kujenga makaravati katika mto huo ulioibuka hivi karibuni ili kuruhusu maji yapite.
“Yupo mwekezaji alifanya kazi ya kuzibua pale lakini kutokana na maji kuwa mengi iimeshindikana,” amesema diwani huyo.
Mkuu wa Wilaya ya Tanga, Thobias Mwilapwa, amesema taarifa za kuibuka kwa bwawa katika eneo hilo anazo lakini tukio la kuonekana mamba halijamfikia na akaahidi kufanyia kazi haraka iwezekanavyo ili kunusuru maisha wananchi.