Sunday, June 11

MTOTO WA MIAKA 12 AIBUKA KIDEDEA MASHINDANO YA KUHIFADHI QURAN



  Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza katika kilele cha Mashindano  ya 11 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. 
Waziri Mkuu, Kasssim Majaliwa akizungumza katika kilele cha Mashindano ya 11 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi , Mohammed Abdullah Aden (12) wa Somalia hundi ya shilingi milioni 15, 750,000/= mshindi wa kwaza wa mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akimkabidhi , Mohammed Abdullah Aden (12) wa Somalia hundi ya shilingi milioni 15, 750,000/= mshindi wa kwaza wa mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh. Paul Makonda akizungumza katika mashindano hayo yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo. 
Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili na Mlezi wa Taasisi ya Al- Hikma Foundation, Alhaj Ali Hassan Mwinyi akizungumza katika kilele cha Mashindano ya 18 ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally (kulia) na Sheikh Sharif Abduqadir Mohamed Ahmed Al Ahdar ambaye ni Rais wa Taasisi ya Al – Hikima Foundation na Mlezi Mwenza wa Taasisi hiyo , katika Mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu) 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiteta na Mufti na Sheikh Sharif Abduqadir Mohamed Ahmed Al Ahdar ambaye ni Rais wa Taasisi ya Al – Hikma Foundation na Mlezi Mwenza wa Taasisi hiyo, katika Mashindano ya 18 ya Afrika ya Kuhifadhi Qur-an Tukufu yaliyofanyika kwenye uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam Juni 11, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

…………………………………………………………

MTOTO wa miaka 12 kutoka Somalia, Mohammed Abdullahi Aden ameibuka kidedea na kitita cha dola za Marekani 7,000 (sawa na sh. milioni 15.75) katika mashindano ya 18 ya Afrika ya kuhifadhi Quran kwenye kundi la washiriki wa juzuu 30.

Mohammed ambaye ni miongoni mwa washiriki wadogo zaidi wawili kuliko wote (mwenzake anatoka Burundi), amejishindia pia IPAD, cheti, kompyuta iliyotolewa na Balozi wa Kuwait, ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na ahadi ya kwenda nchi yoyote aitakayo kutoka kwa kampuni ya Sky Bus Travel Agency ya jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na maelfu ya waumini na Watanzania waliofurika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam leo mchana (Jumapili, Juni 11, 2017), Waziri Mkuu Kassim Majaliwa waandaaji wa mashindano hayo ambayo ni Taasisi ya Al-Hikma waangalie uwezekano wa kuboresha zawadi kwa kutoa scholarships (udhamini) kwa washindi au washiriki, hususan kwa washiriki wa Tanzania.

“Ongeeni na nchi marafiki kama Saudi Arabia, waone uwezekano wa kutoa zawadi za ufadhili kwenye masomo ya sekta za kimkakati kama vile mafuta na gesi, ili kuongeza hamasa na chachu ya vijana walioko kwenye sekondari zetu nao waone fursa hii na kuichangamkia, badala ya mashindano kujikita kwenye madrasa peke yake,” amesema.

Waziri Mkuu amewataka wazazi wafuatilie nyendo za vijana wao ili wasijiingize kwenye matumizi ya dawa za kulevya na vitendo vingine viovu vinavyoweza kuhatarisha maisha yao na ustawi wa nchi yetu lakini akasisitiza pia waisaidie Serikali katika mapambano yake dhidi ya rushwa na ufisadi.

“Endeleeni kushirikiana na Serikali katika mapambano yake dhidi ya rushwa na ufisadi na kuwafichua wakwepa kodi. Kila mmoja wetu ahakikishe analipa kodi stahiki kwa mujibu wa sheria. Hii itasaidia Serikali kuboresha huduma kwa wananchi ili waweze kufanya ibada zao vizuri zaidi,” amesema.

Washindi wengine kwenye kundi hilo na umri wao kwenye mabano ni Abdulkarim Ahmed Farhina (22) wa Sudan ambaye ameshinda dola za Marekani 5,000, cheti, IPAD, kompyuta iliyotolewa na Balozi wa Kuwait, ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Wa tatu ni Mahamoud Ali Chamfi wa Comoro (18) na Seif Ramadhani Zombe (18) kutoka Taasisi za Tanzania ambao wote wamepata dola za marekani 3,000, cheti, IPAD, kompyuta iliyotolewa na Balozi wa Kuwait, ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Wa nne ni Khalil Mussa Hussein (17) kutoka Tanzania Bara ambaye amepata dola za marekani 1,500, cheti, IPAD, na ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam. Wa tano ni Ismail Issa Qasim (17) kutoka Tanzania Visiwani ambaye dola za marekani 1,000, cheti, IPAD, na ahadi ya sh. milioni moja kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,

Washiriki wengine kwenye kundi la juzuu 30 walitoka nchi za Nigeria, Kenya, Uganda, Djibouti, Afrika Kusini, Rwanda, Ghana, Ethiopia, Congo DRC, Burundi na Msumbiji. Umro wao ulikuwa ni kati ya miaka 12 na 26.

Washiriki wengine waliopewa zawadi ni wale walioweza kuhifadhi Juzuu tatu (washindi watano), Juzuu tano (washindi watatu); Juzuu 10 (washindi watatu) na Juzuu 20 (washindi watatu).

Viongozi wengine waliohudhuria kilele hicho ni Rais Mstaafu wa awamu ya pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, Makamu wa Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Dk. Mohammed Gharib Billal, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Balozi wa Saudi Arabia nchini Tanzania, Mhe. Mohamed Bin Mansour Al Malek. Wengine ni wawakilishi wanne wa Imam Mkuu wa Mskiti Mtakatifu wa Makkah, Sheikh Abdul Rahman Ibn Abdul Aziz as-Sudais; Mufti na Sheikh Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir bin Ally na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu amemuagiza Meya wa Temeke, Bw. Abdallah Chaurembo kesho (Jumatatu, Juni 12, 2017) afuatane na Mkurugenzi wa Manispaa hiyo, Bw. Nassib Mmbaga hadi kwenye kiwanja kilichopo eneo la Matumbi na kukagua kama kuna uwezekano wa kuliongeza kwa taasisi ya Al-Hikma na wampe majibu Jumanne kwani limekaa wazi kwa muda mrefu licha ya kuwa walishaliomba na hawakupata majibu.

“Mstahiki Meya wa Temeke na Mkurugenzi wako, kesho Jumatatu nendeni mkaangalie eneo husika kama linafaa kuongezwa na mfanye maamuzi. Eneo hilo limekaa wazi kwa muda mrefu, na hawa wanataka wanataka kujenga zahanati. Jumanne asubuhi nipate taarifa ya maamuzi yenu,” alisema Waziri Mkuu na kushangiliwa na maelfu ya waumini waliokuwepo kwenye hafla hiyo.

Abiria 75 wanusurika kifo basi likiteketea kwa moto


Butiama. Basi la kampuni ya Batco lililokuwa likitokea Sirari kuelekea Mwanza muda mfupi baada ya kuvuka Mto Mara lilianza kufuka Moshi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, Jaffari Mohamed akizungumzia tukio hilo amesema wanafuatilia kubaini chanzo cha ajili hiyo iliyosababisha mali za abiria kuteketea kwa moto, huku abiria 75 waliokuwamo wakinusurika kifo.
Basi hilo lilianza kuteketea moto leo (Jumamosi) saa saba mchana eneo la Kirumi, Kata ya Bukabwa wilayani Butiama.
Chanzo cha kuteketea basi hilo hakijajulikana, huku zaidi ya abiria 75 waliokuwa ndani wakinusurika. 
Mmoja wa abiria hao, mwalimu Malakwa Asenga amesema basi lilianza kuonyesha kuwa na hitilafu walipokuwa wakitoka mjini Tarime.
Amesema dereva aliendelea na safari na walipofika eneo la Mto Mara alisimama kwa muda akiwa ameegemea usukani na baadaye aliondoka.
Asenga amesema hawakufika mbali dereva alisimama tena, ndipo walipoona moshi ukitoka kwenye injini.
Abiria huyo anasema alimwambia mwenzake washuke kwa kuwa gari linaungua.
“Nikisema hayo tayari abiria wengine walikuwa wameanza kushuka kwa haraka wakiwa na mizigo yao ili kuokoa maisha lakini moto ulikuwa umeanza kuongezeka hivyo ni mizigo michache tu ndiyo iliyookolewa, yangu imeteketea,” amesema Asenga.

TFF YATOA UFAFANUZI KUHUSU SERENGETI BOYS


Kuna taarifa zimekuwa zikienea na kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii, zikidai kuwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewatelekeza wachezaji wa timu ya mpira wa miguu ya Tanzania ya vijana wenye umri wa chini ya miaka 17.

Wadai kwamba eti hawakulipwa posho na kushutumu viongozi wa juu wa shirikisho kuhusu jambo hilo. Hizi taarifa si za kweli.

Aidha, Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kuwajulisha wazazi na umma kwa ujumla kwamba vijana wetu walilipwa posho zao zote wakiwa kambini Morocco na Cameroon na zile za mashindano ya AFCON nchini Gabon.

Vilevile, Shirikisho linafanya taratibu za kupeleka maombi kwenye Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (Football Development Fund FDF) ili kuweza kuwalipa vijana na benchi la ufundi sehemu ya posho zilizokuwa bado hazijakamilishwa wakati wa michuano ya kufuzu kwa AFCON 2017.

Tumeshtushwa na taarifa hizo ambazo tafsiri yake ni kuharibu uhusiano mwema kati ya shirikisho, wazazi na wachezaji ambao wanatarajiwa  kuitumikia timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka  20 maarufu kama Ngorongoro Heroes.

Shirikisho linaendelea kuwatambua vijana wa Serengeti Boys kwani bado ni sehemu ya kikosi cha Ngorongoro Heroes na hivyo ukifika wakati wataitwa kambini kwa ajili ya michezo ya kimataifa ya U-20.

TFF inazidi kuushukuru umma ambao umeendelea kuchangia Mfuko wa FDF ambao kimsingi kazi yake ni kutafuta rasilimali kwa ajili ya maendeleo ya mpira.

Tunaomba michango iendelee kwani bado tuna changamoto za mashindano mbalimbali kwa timu za wanawake na vijana ikiwemo fainali za wanawake Afrika zitakazofanyika Ghana hapo mwakani kwa timu ya Twiga Stars na AFCON 2019 kwa Serengeti Boys ambayo itakuwa mwenyeji.

Mfuko wa Maendeleo ya Mpira - FDF ulianzishwa kwa lengo la kutafuta rasilimali za maendeleo ya mpira wa miguu hasa kwa wanawake na vijana pamoja na miundombinu ya mchezo huo.

Mfuko huo uko chini ya Mwenyekiti Bw. Tido Mhando anayeongoza Bodi na Mtendaji Mkuu (CEO) ni Bw. Dereck Murusuri anayesimamia sekretarieti

MASHINDANO YA QUR'AN YA AISHA SURURU FOUNDATION 2017



IMG-20170610-WA0108
IMG-20170610-WA0071
IMG-20170610-WA0107
IMG-20170610-WA0110
IMG-20170610-WA0105
IMG-20170610-WA0106
IMG-20170610-WA0036
Pichani za juu, Masheikh na Viongozi mbalimbali wa dini ya Kiislam waliohudhuria katika mashindano ya Qur'an yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
IMG-20170610-WA0046
Mufti wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zubeir akiwapa nasaha waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria katika mashindano ya Qur'an yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
IMG-20170610-WA0112
Sheikh Nurdin Kishki akiwapa nasaha waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria katika mashindano ya Qur'an yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
IMG-20170610-WA0100
Baadhi ya waumini wa Kiislam na washindani wa mashindano ya Qur'an waliohudhuria kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
IMG-20170610-WA0104
Baadhi ya waumini wa Kiislam waliohudhuria kwenye mashindano ya Qur'an kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
IMG-20170610-WA0111
Baadhi ya waumini wa Kiislam waliohudhuria kwenye mashindano ya Qur'an kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
IMG-20170610-WA0103
Baadhi ya waumini wa Kiislam waliohudhuria kwenye mashindano ya Qur'an kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
IMG-20170610-WA0116
Masheikh wa dini ya Kiislam na viongozi wakubwa akiwamo Sheikh Basaleh na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad, kwenye mashindano ya Qur'an yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
IMG-20170610-WA0101
IMG-20170610-WA0049
Maskauti wakimsindikiza kwenye jukwaa mlemavu wa macho aliyehifadhi Qur'an.
IMG-20170610-WA0114
Mgeni wa heshma, Mke wa Makamu wa Rais Mstaafu, Mama Gharib Bilal, akitoa nasaha kwa waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria katika mashindano ya Qur'an yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
IMG-20170610-WA0115
Mwanaharakati wa kijamii, Mwenyekiti na Mlezi wa Mashindano ya Qur'an ya Aisha Sururu Foundation, Bi Aisha Sururu, akitoa nasaha kwa waumini wa dini ya Kiislam waliohudhuria katika mashindano ya Qur'an yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, jijini Dar es Salaam, leo.
IMG-20170610-WA0041
IMG-20170610-WA0117
IMG-20170610-WA0118
Baadhi ya zawadi zilizozawadiwa kwa washindi wa mashindano ya Qur'an yaliyoandaliwa na taasisi ya Aisha Sururu Foundation. Wabillahi tawfeeq.

Naibu Spika Dkt. Tulia Ackson awajulia hali watoto wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji wa Moyo katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI)


 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akimpokea  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Tulia Ackson alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto  wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Prof. Mohamed Janabi akieleza jinsi wanavyotoa  huduma za matibabu ya magonjwa ya Moyo kwa Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  Dkt. Tulia Ackson alipotembelea Taasisi hiyo leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanawaosubiri kufanyiwa upasuaji.
 Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali  mtoto Doreen Sostenes (3) ambaye  Tulia Trust Fund imemlipia gharama za matibabu ya upasuaji wa Moyo ambao utafanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI). Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.
 Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa amembeba   mtoto Doreen Sosthenes (3) ambaye  Tulia Trust Fund imemlipia gharama za matibabu ya upasuaji wa Moyo ambao utafanyika katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI).
 Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimtazama mtoto Johnson Raphael (6) akichora picha ya mtu wakati alipotembelea  Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) leo  ili kuwajulia hali  watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji. Kulia ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.
 Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiwa amembeba mtoto Zuwena Said (4) aliyelazwa katika   Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kusubiri upasuaji wa Moyo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto Naiz Majani.
 Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimjulia hali mtoto Abdukarim Mahilo (2)  aliyelazwa katika   Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa ajili ya kusubiri kufanyiwa upasuaji wa Moyo huku Mama wa mtoto Fatuma Bakari akiangalia.
  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongea na Maria Gervas  ambaye ni mama wa Doreen Sosthenes (3) anayelipiwa gharama za upasuaji wa  Moyo na Tulia Trust Fund. Mhe. Dkt. Tulia alitembelea Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)  leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.

 Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kwa Watoto wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Sulende Kubhoja akimuelezea   Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson magonjwa mbalimbali ya moyo yanayowasumbua watoto. Mhe. Dkt. Tulia alitembelea  Taasisi hiyo  leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.
  Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimbembeleza mtoto Venance  Christopher (14) aliyelazwa katika Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwaajili ya kusubiri upasuaji wa  Moyo. Mhe. Dkt. Tulia alitembelea Taasisi hiyo   leo kwa ajili ya kuwajulia hali watoto wanaosubiri kufanyiwa upasuaji.
 Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akiongea jambo wakati akimjulia hali mtoto Rashid Kombo aliyelazwa katika  chumba cha uangalizi maalum (ICU) baada ya kufanyiwa upasuaji wa Moyo. Kushoto ni Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Moyo kwa watoto kutoka Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Naiz Majani akifuatiwa na  Daktari Bingwa wa Moyo kwa watoto na Mkuu wa Idara ya Magonjwa ya Moyo kwa Watoto Dkt. Sulende Kubhoja. 
Mhe. Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimsikiliza Daktari Bingwa wa upasuaji wa Moyo kwa Watoto na Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Moyo kwa Watoto Godwin Sharau alipotembelea leo chumba cha upasuaji wa Moyo kilichopo Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwetwe (JKCI). Picha na  Anna Nkinda wa JKCI

WAKAAZI WA MBEZI BEACH NA MIKOCHENI B JIJINI DAR ES SALAAM WASAFISHA FUKWE ZA BAHARI.


 Mjumbe wa Serikali za Mtaa wa Mikocheni B, Kamati ya Mazingira Moses Sanga pamoja na Victoria Kileo wa Nipe Fagio wakiwa wamebeba taka wakati wa zoezi la kufanya usafi katika fukwe za Mbezi Beach leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limeshirikisha Marafiki wa Bahari, Nipe Fagio,Mbezi Beach Neighborhoods. 
 Delicia Mwanyika and Cindy Tibazarwa kutoka Mbezi beach Neighborhoods wakishirikiana kuokota taka sugu kama vile Plastiki, makopo, nguo, viatu, nyavu, mataili, sindano, vyupa na taka nyinginezo.
 Beatrice Steyn Muasisi wa Mbezi Beach Neighborhoods akizungumza na waandishi wa habari wakati wa  zoezi la kufanya usafi wa fukwe ya Mbezi Beach katika kuokoa Bahari ambapo alisisitiza ushirikiano kutoka Serikali, Viwanda, Taasisi mbalimbali pamoja na watu binafsi kuungana kwa pamoja kurudisha uhai wa bahari ambayo inaelekea kufa kama hakuna hatua itakayo chukuliwa sasa.
 Boss Brown Muasisi wa Marafiki wa Bahari kutoka Mikocheni B akiwa katika zoezi la kufanya usafi katika fukwe za Mbezi Beach leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi hilo limeshirikisha Marafiki wa Bahari, Nipe Fagio,Mbezi Beach Neighborhoods
Washiriki wa zoezi la usafi wa fukwe wa Mbezi Beach wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kumaliza kwa zoezi hilo leo Jijini Dar es Salaam. Zoezi hiloni harakati za kuunga mkono kampeni ya kuiokoa Bahari ambalo limeshirikisha asasi za Nipe Fagio, Mbezi Beach na Friends Of Ocean kutoka Mikocheni B chini ya udhamini wa Nabaki Africa, Koncept Communication Pamoja na AFM 92.9 ya mjini Dodoma.

Friday, June 9

BARAZA LA TAIFA LA USALAMA BARABARANI LATOA TATHIMINI


 Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Massauni, akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani), kuhusu utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita, mjini Dodoma leo, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa baraza hilo ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani.
 Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Edwin Ngonyani (kulia), akifafanua jambo katika mkutano na Waandishi wa Habari kuhusu hatua za utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita, mjini Dodoma leo, kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandisi  Hamad Massauni.
 Mjumbe wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani, Mhandisi Julius Chambo (Kushoto), akisikiliza kwa makini taarifa ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita, iliyotolewa na Mwenyekiti wa Baraza hilo Mhandisi Hamad Massauni (hayupo pichani), mjini Dodoma leo.
Mwenyekiti wa Baraza la Taifa la Usalama Barabarani ambaye ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Massauni, akitoa taarifa ya utekelezaji wa mpango mkakati wa kupunguza ajali za barabarani nchini katika kipindi cha miezi sita kwa wajumbe na waandishi wa habari, mjini Dodoma leo. 

Imetolea na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano

JK aeleza changamoto anazokumbana nazo kwenye kilimo cha mananasi



Pwani. Rais mstaafu, Jakaya Kiwete amezungumzia  shughuli za kilimo anazozifanya huku akianika changamoto mbalimbali zinazomkabili.

Akizungumza leo Ijumaa muda mfupi mara baada ya Mwenge wa Uhuru kufika kwenye shamba lake la mananasi lenye ukubwa wa eka zaidi ya 200 mkoani hapa, amesema ingawa kilimo alianza tangu mwaka 1989, lakini suala la palizi na ukosefu wa maji ni moja ya changamoto anazokabiliana nazo.
"Nilianza kilimo miaka mingi sana na mpaka nastaafu nilikuwa naendelea na kilimo, lakini changamoto kubwa katika kilimo ni suala la palizi hususan haya mananasi unaweza palilia zaidi ya mara tatu," amesema.
Amesema kuwa ingawa mananasi yanazaa vizuri kama yatapata huduma zote kikamilifu, lakini mkulima anaweza kupambana na ukosefu wa masoko pindi unapofikia msimu wa mavuno.
"Hata kama viwanda vitajengwa kwa wingi lakini ili mkulima apate faida ya juu ya kilimo hasa cha mananasi ni lazima kuwe na bei nzuri, lakini kama wanunuzi watakuwa wananunua bei isiyo na masilahi hakutakuwa na maendeleo kwa wakulima,"amesema.
Amesema kuwa mikakati aliyonayo kwa kushirikiana na taasisi na wakulima mbalimbali ni kutafuta mbegu za  mananasi kutoka nje ya nchi na mkakati wa kuanzisha kilimo cha mananasi kwa njia ya umwagiliaji hali aliyosema itawainua wakulima wengi na kujikwamua katika janga la umaskini.
Mkimbiza Mwenge wa Uhuru kitaifa, Amour Hamad Amour amempongeza Kikwete kwa kuonyesha mfano bora hususan kuendeleza kilimo cha mananasi huku amiwahimiza Watanzania kuiga mfano huo.

Mwanafunzi wa darasa la sita abakwa hadi kufa



Sumbawanga. Mwanafunzi wa darasa la sita  katika Shule ya Msingi Kapanga, Kata ya Katuma Wilaya ya Tanganyika, Mkoa wa Katavi, amekutwa amekufa kwenye shimo baada ya kubakwa na watu wasiojulikana.
Kaimu  Kamanda wa  Polisi wa  Mkoa wa  Katavi,   Benedict  Mapujila  amesema tukio  hilo  lilitokea juzi saa 11 jioni katika kata hiyo.
Amesema  siku hiyo mwanafunzi huyo aliondoka  nyumbani  kwenda  shule,  lakini ilipofika jioni hakurejea.
Kaimu kamanda amesema hali hiyo ilisababisha wazazi wake wapate shaka kwa kuwa marehemu hakuwa na tabia ya kutorudi nyumbani.
Amesema siku iliyofuata wazazi wake walikwenda kufuatilia  shuleni lakini hawakumkuta na kwenda kutoa taarifa kwenye uongozi wa kijiji hicho.
“Viongozi wa kijiji na wananchi walianza msako wa kumtafuta binti huyo kutwa nzima  na ilipofikia saa 11 jioni  walikuta mwili wake umetupwa  kwenye  shimo  la kolongo,” amesema.
Kaimu Kamanda Mapujila amesema  sehemu za siri za binti huyo zilikutwa zimeharibika vibaya.
Amesema uchunguzi wa kitabibu umebaini mwanafunzi huyo alitokwa damu  nyingi hali iliyosababisha kifo.
Kaimu kamanda hakuna aliyekamatwa kutokana na tukio hilo ila polisi inaendelea na msako kuwabaini waliohusika.