Thursday, May 31

Unusual Words

A by no means exhaustive list of rare, obscure, strange and sometimes funny words and their meanings that only seem to crop up in crosswords and dictionaries. Words that are used so seldom, you wonder who invented them and why.

A
abacinate To blind by putting a hot copper basin near someone's eyes
abderian Given to incessant or idiotic laughter
abecedarian A person who is learning the alphabet
abligurition Excessive spending on food and drink
accubation The practice of eating or drinking while lying down
adelphepothia An incestuous desire for one's sister
adelphirexia An incestuous desire for one's nephew
adelphithymia An incestuous desire for one's niece
adoxography Skilled writing on an unimportant subject
aeolist A pompous windy bore who pretends to have inspiration
agelast A person who never laughs
agerasia The state of looking younger than one actually is
agraffe The wire that holds the cork in a champagne bottle
algerining Prowling around with the intent to commit burglary
alphamegamia The marriage between a young woman and an older man
anopisthography The practice of writing on one side of the paper
apodyopsis The act of mentally undressing someone
autohagiographer One who speaks or writes in a smug fashion about their own life and accomplishments
autolatry The worship of one's self
autotonsorialist One who cuts their own hair

B
basorexia An overwhelming desire to neck or kiss
bathykolpian Deep-bosomed
batrachophagous One who eats frogs
blandiloquent Speaking in a flattering or ingratiating manner
bletcherous Pertaining to something poorly or disgustingly designed
bombilate To loudly hum or buzz continuously
borborygmus The rumbling sound of gas passing through the intestine
brevirostrate Having a short nose
bromidrosis Strongly smelling perspiration
brontide The low rumbling of distant thunder

C
cachinnation Loud or hysterical laughter
cacoethes A bad habit or insatiable urge
cagamosis An unhappy marriage
callipygean Having well-shaped buttocks
cancatervate To heap up into a pile
capernoited Slightly intoxicated or tipsy
cataglottism Kissing using the tongue, French kissing
causeuse A sofa built for two people
charientism An artfully veiled insult
cheiloproclitic Being attracted to a person's lips
chirotonsor An alternate title for a barber
cleptobiosis The act of plundering food
clithridiate Key-hole-shaped
colposinquanonia Estimating a woman's beauty based on her chest
concilliabule A secret meeting of people who are hatching a plot
cruciverbalist One who loves doing crossword puzzles

D
dactylion The tip of the middle finger
dactylonomy Counting using one's fingers
decubitis The act or attitude of lying down
defenestrate To throw out of a window
dehisce To burst open, as the pod of a plant
dentiloquent Pertaining to one who talks through their teeth
dephlogisticate To make something fireproof
digamy A second marriage after the death or divorce of a previous spouse
dippoldism The act of beating or whipping school children
dompteuse A woman who trains animals

E
eccedentesiast One who fakes a smile, as on television
emunction The act of removing obstructions from or cleaning bodily passages
estrapade A horses's attempt to remove its rider
exsibilation The collective hisses of a disapproving audience

F
farctate The state of being stuffed with food (overeating)
filipendulous Suspended by a single thread
floccinaucinihilipilification The categorising of something that is useless or trivial
fuscoferuginous Having a dark rusty colour

G
gambrinous Being full of beer
gargalesis Heavy tickling
gargalesthesia The sensation caused by tickling
ginglyform Hinge-shaped
gongoozler An idle spectator
gossypiboma A surgical sponge accidently left inside a patient's body
gowpen A double handful
grapholagnia The urge to stare at obscene pictures
gymnophoria The sensation that someone is mentally undressing you

H
hadeharia The practice of constantly using the word "Hell" in speaking
hamartithia Being likely to make a mistake
hippopotomonstrosesquipedalian Pertaining to extremely long words
honorificabilitudinitatibus With honour

I
inaniloquent Speaking foolishly or saying silly things
interfenestration The space between two windows

J
jentacular Pertaining to breakfast
jumentous Smelling like horse urine

K
knismesis Light tickling
krukolibidinous The act of staring at someone's crotch
kyphorrhinos Having a nose with a bump in it

L
lalochezia The use of foul or abusive language to relieve stress or ease pain
lethologica The inability to recall a precise word for something
liripip The long tail of a hood in medieval or academic costume
lygerastia The condition of one who is only amorous when the lights are out

M
maledicent One who is addicted to abusive speech
mallemaroking The carousing of seamen on board Greenland whaling ships
mammothrept A child who is raised and spoiled by their grandmother
maritodespotism Tyrranical rulership of a woman by her husband
matronolagnia An attraction to older women, especially ones who have children
misocapnist One who hates the smell of tobacco smoke
misodoctakleidist Someone who hates practicing the piano
mulligrubs A state of depression or low spirits
mumpsimus One who sticks obstinately and wrongly to their old ways
mytacism The incorrect or excessive use of the letter M

N
nelipot Someone who walks without shoes
nepheligenous Producing clouds of tobacco smoke
nidorosity Belching with the taste of undigested meat
nudiustertian Pertaining to the day before yesterday

O
oculoplania Letting one's eyes wander while assessing someone's charms
onychophagy The habit of biting one's fingernails

P
pandiculation Stretching and yawning before going to bed or after waking up
petrichor The smell of rain on dry ground
philosophunculist One who pretends to know more than they do to impress others
pogonotomy The act of cutting a beard
polyphloisboian Making a lot of noise or loud racket
preantepenultimate Fourth from last
prosopography The description of a person's appearance
psithurism The sound of wind in trees or rustling leaves
pyknic Short and fat

Q
qualtagh The first person you see after leaving your house
quidnunc One who always wants to know what is going on
quomodocunquize To make money by any means possible

R
recumbentibus A knockout blow, either verbal or physical
runcation The act of weeding

S
sabrage The act of opening a bottle with a sabre
saprostomous Having bad breath
scacchic Pertaining to the game of chess, or to chess pieces
sciapodous Having huge feet
scolecophagous One who eats worms
sgiomlaireached The habit of dropping in at mealtimes
skoptsy The act of self castration
slubberdegullion A filthy, slobbering person
sphallolalia Flirtatious talk that leads nowhere
steatopygic Having a fat behind
strikhedonia The pleasure of being able to say to hell with it

T
tachyphagia Fast eating
tarantism An urge to overcome melancholy by dancing
tetrapyloctomy The act of splitting a hair four ways
thelemic Permitting people to do as they like
tibialoconcupiscent Having a lascivious interest in watching a woman put on stockings

U
ulotrichous Having very wooly hair
ultracrepidarian Of one who speaks or offers opinions on matters beyond their knowledge
usufructuary A person who has use or enjoyment of something, especially property

V
ventripotent Big-bellied, gluttonous
vesthibitionism The flirtatious display of undergarments by a woman
vigesimation The act of killing every twentieth person
viraginity Masculine qualities in a woman

W
wanweird An unhappy fate
witzelsucht A feeble attempt at humour

X
xenobombulate To malinger
xerophagy A diet of bread and water
ximelolagnia The urge to stare at women who are sitting with crossed legs
xylopolist One who sells wood products

Y
yclept By the name of; called

Z
zenzizenzizenzic A number raised to the eighth power

Friday, May 18

'Amali Za Kutenda Na Ya Kujiepusha Nayo Katika Mwezi Mtukufu Wa Rajab

Nasiha Za Minasaba Mbalimbali AlhamduliLLaah. Inapasa tumshukuru Allaah (Subhaanahu wa Ta’ala) Kutupa umri hadi kutufikisha mwezi mtukufu wa Rajab ambao ni fursa kwetu kutenda mema yatakayotuchumia thawabu nyingi kuliko miezi mingine. Mema ambayo hatuna budi kuyatenda kwa ajili ya kujenga Aakhirah yetu kabla ya siku hii kufika. Siku ambayo hakuna mmoja wetu yeyote atakayeweza kuikwepa. Basi hebu kila mmoja wetu ajiulize: "Nimetanguliza nini kwa ajili ya siku hiyo?" Siku ambayo safari yake ni ndefu mno. Vyovyote tutakavyobeba kama ni zawadi huko Aakhirah, hazitoshi wala hatuna hakika nazo kama zitapendekezeka au zitakuwa na thamani huko tuendako ambako kuna makazi ya milele tusiyokuwa na hakika nayo; ima moto au Pepo. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala): (( يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اتَّقُوا اللَّهَ وَلْتَنظُرْ نَفْسٌ مَّا قَدَّمَتْ لِغَدٍ وَاتَّقُوا اللَّهَ إِنَّ اللَّهَ خَبِيرٌ بِمَا تَعْمَلُونَ)) ((Enyi mlioamini! Mcheni Allaah, na kila nafsi iangalie inayoyatanguliza kwa ajili ya Kesho. Na mcheni Allaah, Hakika Allaah, Anazo khabari ya mnayoyatenda)) [Al-Hashr: 18]. Vile vile ni miezi miwili tu imebakia kutufikia mgeni wetu tunayemsubiri kwa hamu kila mwaka, mwezi mtukufu wa Ramadhaan. Kwa hiyo ni fursa nyingine pia kujitayarisha kuupokea mwezi huo kwa kujizoesha ibada mbali mbali kama Swawm, tahajjud, na pia kutenda mema mengi ili tutakapofikia mwezi wa Ramadhaan tuwe na nguvu za kufanya zaidi ya tuliyoyazoea kutenda katika miezi hii iliyobakia miwili ijayo. Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala): (( إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللّهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللّهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَات وَالأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ذَلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ فَلاَ تَظْلِمُواْ فِيهِنَّ أَنفُسَكُم )) ((Hakika idadi ya miezi kwa Allaah ni miezi kumi na mbili katika hukumu ya Allaah, tangu Alipoumba mbingu na ardhi. Katika hiyo iko mine mitakatifu. Hiyo ndiyo Dini iliyo sawa. Basi msidhulumu nafsi zenu humo)) [At-Tawbah: 36] Miezi minne hiyo imetajwa katika Hadiyth ifuatayo: عَنْ أَبَى بَكْرَة أَنَّ رَسُول اللَّه - صَلَّى اللَّه عَلَيْهِ وَسَلَّمَ - قَالَ فِي حَجَّة الْوَدَاع : (( إِنَّ الزَّمَان قَدْ اِسْتَدَارَ كَهَيْئَتِهِ يَوْم خَلَقَ اللَّه السَّمَوَات وَالْأَرْض السَّنَة اِثْنَا عَشَر شَهْرًا مِنْهَا أَرْبَعَة حُرُم : ثَلَاث مُتَوَالِيَات ذُو الْقَعْدَة وَذُو الْحِجَّة وَالْمُحَرَّم وَرَجَب مُضَر الَّذِي بَيْن جُمَادَى وَشَعْبَان)) صَحِيح الْبُخَارِيّ Kutoka kwa Abu Bakrah ambaye amesema: "Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa wa sallam) amesema alipokuwa katika Hijjah ya kuaga (Hijjah wa mwisho): ((Mgawanyo wa nyakati umerudi kama ulivyo (wakati) Allaah Alipoumba mbingu na ardhi. Mwaka una miezi kumi na mbili, minne ambayo ni mitukufu; mitatu inafuatana pamoja (nayo ni) Dhul-Qa'adah, Dhul-Hijjah na Muharram, na (wa nne ni) Rajab wa (kabila la) Mudhwar ambao upo baina ya Jumaada na Sha'abaan)) [Al-Bukhaariy] Katika miezi yote kumi na mbili Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Ameichagua hii minne na Ameifanya kuwa ni mitukufu na kusisitiza kuitakasa, na kwamba dhambi zitakazofanyika humo ni zaidi na hali kadhalika thawabu za vitendo vyema zinakuwa maradufu na zaidi. [Atw-Twabariy 14: 238] Ni sawa kama Anavyoonya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kufanya maasi katika sehemu tukufu Alipotaja Masjidul-Haraam (Msikiti Mtukufu Makkah): ((إِنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا وَيَصُدُّونَ عَن سَبِيلِ اللَّهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ الَّذِي جَعَلْنَاهُ لِلنَّاسِ سَوَاء الْعَاكِفُ فِيهِ وَالْبَادِ وَمَن يُرِدْ فِيهِ بِإِلْحَادٍ بِظُلْمٍ نُذِقْهُ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ)) ((Hakika wale waliokufuru na wakazuilia Njia ya Allaah na Msikiti Mtakatifu, ambao tumeufanya kwa ajili ya watu wote sawasawa, kwa wakaao humo na wageni. Na kila atakayetaka kufanya upotofu humo kwa dhulma, basi Tutamwonjesha adhabu iumizayo)) [Al-Hajj: 25] Qataadah amesema kuhusu kauli ya Allaah: (( فَلاَ تَظْلِمُواْ فِيهِنَّ أَنفُسَكُم)) ((Basi msidhulumu nafsi zenu humo)) "Dhulma itakayotendeka katika miezi mitukufu ni mbaya na kubwa (au hatari) kuliko dhulma itakayotendeka katika miezi mingine. Hakika dhulma daima ni makosa, lakini Allaah Hufanya baadhi ya vitu kuwa ni vizito kuliko vingine kama Anavyopenda". Akaendelea kusema: "Allaah Amechagua baadhi ya viumbe Vyake na baadhi ya vitu kuwa bora zaidi kuliko vingine. Amechagua Wajumbe kutoka Malaika na kutoka binaadamu. Vile vile Amechagua baadhi ya kauli Zake kuwa ni bora kuliko nyingine, Misikiti kuwa bora kuliko sehemu nyingine za ardhi, Ramadhaan na miezi mitukufu kuwa bora kuliko miezi mingine, siku ya Ijumaa kuwa ni bora kuliko siku nyingine, na usiku wa Laylatul-Qadr kuwa ni bora kuliko masiku mengine. Kwa hiyo takasa vile Alivyovitakasa Allaah, kwani kufanya hivyo ni vitendo vya watu wenye akili na wenye kufahamu" [Tafsiyr ya Ibn Kathiyr] Miongoni mwa yaliyokatazwa katika miezi hii mitukufu ni kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala): (( يَسْأَلُونَكَ عَنِ الشَّهْرِ الْحَرَامِ قِتَالٍ فِيهِ قُلْ قِتَالٌ فِيهِ كَبِيرٌ وَصَدٌّ عَن سَبِيلِ اللّهِ وَكُفْرٌ بِهِ وَالْمَسْجِدِ الْحَرَامِ وَإِخْرَاجُ أَهْلِهِ مِنْهُ أَكْبَرُ عِندَ اللّهِ وَالْفِتْنَةُ أَكْبَرُ مِنَ الْقَتْلِ )) ((Wanakuuliza juu ya kupigana vita katika mwezi mtakatifu. Sema: Kupigana vita wakati huo ni dhambi kubwa Lakini kuzuilia watu wasiende katika Njia ya Allaah na kumkanusha Yeye, na kuzuilia watu wasiende kwenye Msikiti Mtakatifu na kuwatoa watu wake humo, ni makubwa zaidi mbele ya Allaah. Na fitina ni mbaya zaidi kuliko kuua..))[Al-Baqarah: 217] Hivyo basi katika mwezi mtukufu wa Rajab, maasi na mema yafuatayo yanatupasa kuzingatia: Maasi Mengine Ambayo Tunatakiwa Tujikumbushe Kuyaacha: - Kuiba; - Kumshirikisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) kama kwenda kwa wachawi na waganga na kuwaamini wanayoyatabiri kwa watu; - Kuzini; - Kulewa; - Kumdhulumu mtu haki yake; - Kugombana, kutukanana, kuvunjiana heshima, kudharauliana n.k.; - Kusengenya (Ghiybah); - Kusema uongo, na kila aina ya uovu mwengine. Mambo Mema Ya Kukumbushana Kufanya Katika Mwezi Huu Mtukufu - Kuongeza Sunnah za Swalah; *(tazama maelezo chini) - Kufunga Swawm za Sunnah kama Jumatatu na Alkhamiys, Masiku meupe (Ayyaamul-biydhw) (tarehe 13, 14 na 15) na Swawm ya Nabii Daawuud (kufunga kila baada ya siku moja); - Kujielimisha mambo ya Dini kwa kusoma vitabu na kusikiliza mawaidha; - Kuomba Maghfirah na Tawbah; - Kufanya kila aina ya dhikr (kumkumbuka na kumtaja Allaah), kwa kusoma Qur-aan kwa wingi, kumshukuru, kumtukuza, kuomba du'aa n.k.; - Kuwasiliana au kutembeleana na ndugu na jamaa; - Kutenda wema kwa jirani, marafiki na watu wote kwa ujumla; - Kutoa sadaka; - Kulisha masikini; - Kupatanisha waliogombana; - Kuamrishana mema na kukatazana maovu, na mengi mengineyo katika vitendo vyema. * Swalah za Sunnah Ratiba Ya Swalah Za Sunnah Zilizosisitizwa Na Zisizosisitizwa ALFAJIRI Kabliya Rakaa 2 ADHUHURI Kabliya Rakaa 4 Baadiya Rakaa2 ALASIRI Kabliya Rakaa 4 MAGHARIBI Kabliya Rakaa 2 Baadiya Rakaa 2 'ISHAA Kabliya Rakaa 2 Baadiya Rakaa 2 Fadhila Zake: (( مَا مِنْ عبْدٍ مُسْلِم يُصَلِّي للَّهِ تَعَالى كُلَّ يَوْمٍ ثِنْتَيْ عشْرةَ رَكْعَةً تَطوعاً غَيْرَ الفرِيضَةِ ، إِلاَّ بَنَى اللَّه لهُ بَيْتاً في الجَنَّةِ ، أَوْ : إِلاَّ بُنِي لَهُ بيتٌ في الجنَّةِ )) رواه مسلم * ((Hatoswali mja Rakaa 12 zisizo za fardhi kwa siku, ila atajengewa [na Allaah] nyumba peponi)) [Muslim] Nazo ni hizo Muakkadah (Zilosisitizwa) jumla yake ni 12 (( ركْعتا الفجْرِ خيْرٌ مِنَ الدُّنيا ومَا فِيها )) رواه مسلم ** ((Rakaa mbili (za Sunnah) kabla ya Alfajiri ni kheri kuliko duniya na yaliyomo ndani yake) [Muslim] ‏‏((ما من عبد يسجد لله سجدة إلا كتب الله له بها حسنة ومحا عنه بها سيئة ورفع له بها درجة فاستكثروا من السجود)) رواه ابن ماجه ((Mja yeyote atakayesujudu sijda moja ataandikiwa wema mmoja, na atafutiwa baya moja, na atapandishwa daraja yake, kwa hiyo zidisheni kusujudu)) [Ibn Maajah] Swalah ya Tahajjud (( أفضل الصلاة بعد الفريضة صلاة الليل)) رواه مسلم ((Swalah iliyo bora kabisa baada ya Fardh ni Swalah ya usiku)) [Muslim] Swalah Ya Dhuhaa na Swalah Ya Witr عـَن أبي هـُريْرَة رضيَ الله عنه قال : أوصـَانـِي خـَليلي صـَلـَّى الله عليه وسلم بـِصـِيامِ ثـَلاثـَة ِ أيـَّام ٍ مـِنْ كـُل شـَهر ٍ، وَ ركـْعـَتي الضـُّحى ، وأنْ أوتـِرَ قبلَ أنْ أرقـُـد " ـ متفق عليه ـ Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiya Allaahu ‘anhu) kwamba “Ameniusia rafiki yangu Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam [mambo matatu]; kufunga siku tatu katika kila mwezi, Rakaa mbili Dhuhaa na niswali Witr kabla ya kulala” [Al-Bukhaariy na Muslim] Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Atuwezeshe kujitenga na maasi na kuzidisha mema katika mwezi huu mtukufu na Atufikishe Ramaadhaan. Aamiyn

Wednesday, May 16

Mzee Makamba awarushia kombora Nape, Pinda

Midraji Ibrahim, Dodoma BAADA ya ukimya wa muda mrefu, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba ameibuka katika kikao cha Halmashauri Kuu ya chama hicho (Nec) na kumtuhumu Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kwamba amekigeuza chama kuwa mali yake binafsi. Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, zimesema kwamba Makamba alisema hatua ya Nape kugeuza chama hicho kama taasisi yake binafsi ndiyo ambayo imesababisha kikose mwelekeo. Makamba licha ya kuelekeza mashambulizi yake kwa Nape, alimrushia pia kombora Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kuwa ana uhusiano mdogo na wananchi. “Mzee (Makamba) amesema hivi sasa CCM imekuwa kama jogoo anayepelekwa kwa mganga, kila anakoelekezwa ndo huko, hali hiyo ndiyo inakikumba CCM hivi sasa. Amemweleza Nape kuwa amegeuza chama kama mali yake binafsi, anafanya mambo nje ya utaratibu na anaangaliwa tu.” Makamba alidai kuwa badala ya sekretarieti kushughulikia matatizo ya chama, imekuwa ikihangaika na watu kwa sababu ya kutofautiana nao misimamo na wakati huo wakijidai kuzika tofauti ili kukiimarisha. Nape alipoulizwa kuhusu suala hilo alipuuza na kusema: “Si kweli, lakini ninyi andikeni tu maana tumewazoea.” Alipotakiwa kueleza kama Kingunge na Makamba walisema nini dhidi yake katika kikao cha Nec alijibu: “Walikuwapo, lakini hakuna kati yao aliyenitaja hata kwa jina.” Nape alitumia muda mwingi kulalamika kuwa taarifa nyingi ambazo zimekuwa zikitolewa kutoka ndani ya mkutano huo uliomalizika jana zimetoka kwa watu aliowataja kuwa wana maslahi nazo binafsi na kuhoji,” Kwa nini msiwe mnasubiri taarifa rasmi (za chama) ili habari iwe ya ukweli zaidi?” Mkongwe mwingine wa chama hicho, Kingunge Ngombale-Mwiru, ambaye anadaiwa kusikitishwa na vitendo vya rushwa na ugomvi vinavyoendelea ndani ya chama huku vikiangaliwa na viongozi kama vile vinakistawisha wakati vinakiporomosha. Kingunge alidai kuwa hivi sasa chama hicho kimetawaliwa na matajiri ambao ndiyo wanaopata nafasi za uongozi na maskini wanawekwa kando. Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja aliunga mkono suala la Pinda kuwa na uhusiano mdogo na wananchi na kwamba, amekuwa mkimya zaidi na hamsaidii Rais Jakaya Kikwete. “Yule Mwenyekiti wa Shinyanga, amemweleza Pinda kuwa ng’ombe wakila mazao mtu wa kwanza kuchapwa viboko ni mchungaji, halafu mmiliki anatozwa faini baadaye. Hivyo, alitakiwa kuwajibika kwanza kabla ya mawaziri walioondolewa,” kilidokeza chanzo chetu. Mgeja alidai kuwa uwajibishwaji wa mawaziri, haukuzingatia haki kwa sababu George Mkuchika, Profesa Jumanne Maghembe na Hawa Ghasia walilalamikiwa, lakini kilichofanywa ni kutoa kafara wengine na hao kubadilishiwa wizara. Pia, inadaiwa kuwa Mwenyekiti Kikwete aliwataka wajumbe kuzika tofauti zao ili kuweka msimamo wa pamoja kwa ajili ya ushindi kwenye Uchaguzi Mkuu ujao wa 2015 na kwamba adui namba moja wa CCM hivi sasa ni Chadema. Rushwa yakishtua chama Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alisema Nec imejadili changamoto zinazokikabili chama kwenye uchaguzi unaoendelea na kubaini kuwa rushwa imekithiri. Nape alisema tishio la rushwa ni kubwa na mgombea atayakayethibitika kujihusisha na vitendo hivyo rushwa ataondolewa mara moja, huku viongozi na watendaji wakitahadharishwa kuchukuliwa hatua za nidhamu. “Kwa kisingizio cha kuwasalimia wajumbe, kuwapa nauli au kujitambulisha. Mgombea atakayethibitika anazunguka au amezunguka ataondolewa bila kuchelewa katika orodha ya wagombea,” alisema na kuongeza: “Kwa watendaji na viongozi wa chama ngazi zote kuanzia sasa ni marufuku kuwatembeza ndani ya maeneo yao, kwa nia ya kuwatambulisha kwa wapiga kura. Mtendaji au kiongozi atakayebainika anakiuka agizo hili, atachukuliwa hatua za nidhamu mara moja.” Pia, Nape alisema kuanzia sasa ni marufuku kwa watendaji na viongozi wa chama ngazi zote kuwaitia wagombea, wajumbe wa mikutano ya uchaguzi kwa lengo lolote, kwani vikao vya aina hiyo havimo katika katiba. Alisema vikao vya aina hiyo ni haramu na vinapalilia rushwa na kuongeza kwamba wanachama wa CCM wanatakiwa kupiga vita rushwa na kutoa taarifa ya vitendo hivyo katika ofisi za chama na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru). Aliitaka Takukuru kutomuonea aibu au kumuogopa mtu anayejihusisha na vitendo vya rushwa badala yake wamchukulie hatua. Mishahara na chakula Kuhusu mishahara ya watumishi wa umma na mfumuko wa bei ya chakula, Nape alisema Nec imeagiza Serikali kuhimiza waajiri kupandisha mishahara na malipo mengine kwa wafanyakazi wao ili waweze kumudu gharama za maisha. Alisema gharama za maisha zimepanda na mishahara inayolipwa haiendani na hali halisi. Alisema nayo Serikali inatakiwa nayo kupandisha mishahara kwa watumishi wake. “Serikali idhibiti malipo ya huduma ya ndani kwa kutumia fedha za kigeni, hasa Dola ya Marekani. Pia, iongeze udhibiti wa maduka na hoteli zinazofanya biashara ya fedha za kigeni ili kuondoa hujuma kwa uchumi wa nchi inayofanywa kutokana na uhuru uliokithiri katika biashara hii,” alisema. Nape alisema Serikali inatakiwa kuweka jitihada zaidi za kudhibiti ulanguzi wa bidhaa muhimu na upandishaji holela wa bei za vyakula, kodi za nyumba na usafiri. Alisema Nec imeagiza Serikali kuendelea kuchukua hatua za muda mrefu na kati za kukabiliana na tatizo la mfumuko wa bei. “CCM inaiagiza Serikali kuchukua hatua za haraka na muda mfupi ikiwamo kuangalia upya baadhi ya kodi katika vyakula pamoja na Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika sukari,” alisema Nape. Pia, Nape alisema wameagiza Serikali kupitia upya utaratibu wa ruzuku ya mbegu na mbolea ili upanuliwe kunufaisha wakulima wengi. Alisema Nec imeitaka Serikali iongeze kasi ya utekelezaji wa mpango wake wa kuongeza uwezo wa kuhifadhi chakula nchini, hasa kupitia Mamlaka ya Hifadhi ya Nafaka ya Taifa (NFRA), ikiwamo kujenga maghala zaidi ya mazao ya chakula maeneo ya uzalishaji na kutenga fedha nyingi zaidi kwa ununuzi wa mazao hayo. “Wakati wa uhaba wa vyakula maeneo ya mijini, kasi ya kupeleka chakula maeneo hayo iongezwe na utaratibu mzuri zaidi wa usambazaji chakula utumike ili walaji na siyo wasafirishaji na wasindikaji, wanufaike,” alisema.

Monday, May 14

Losing Jerusalem

Visiting Jerusalem is up for debate now, and it's good that it is being taken up and understood now. The question is not whether to visit Jerusalem or not, rather it is visiting it under Israeli's occupation. Islamic scholars have different opinions on this, all of which are respected. Let's look at it from the religious perspective first. Jerusalem has always been a sacred place as mentioned in the Holy Quran "... to Masjid Al-Aqsa, whose surroundings we have blessed..." (17:1). It is the land of prophets all of whom are revered and respected. This mosque is the place where all the prophets (May Allah be pleased with them all) met on the night of Isra. When the Holy prophet (PBUH) migrated to Madinah, the Muslims prayed in its direction for more than one and a half year. Being host to the third holiest place of Islam, Jerusalem is equally dear to Muslims, as it is for Jews and Christians. The holy Prophet (PBUH) has specifically mentioned Al-Aqsa Mosque to be visited along with the ones in Makkah and Madinah. So it's more important for Muslims to try and visit there if conditions allow. Though under Israeli occupation, we can still go there via Jordan. According to some scholars, it's like recognizing Israel, and they have a valid point too - in accepting the norms and procedures formed by the occupying Israeli government. But let's look at the other side as well. All these decades we have been "not recognizing Israel", but have also been losing an opportunity to visit Al-Quds. So just by going there, do we "recognize Israel"? No, as long as you are just going to fulfill your religious duty. We have the treaty of Hudaibiyah as an example, where the holy Kaabah was still in control of the Quraysh, but the Prophet (PBUH) and his companions made a pact with them, stayed in Makkah for three days and performed their pilgrimage. Did they recognize the Quraysh's ownership of the Kaabah? Definitely not.
Babri Masjid as it stood once in India Now coming to the political and strategic aspect - Israel has long been trying to drive out all the Palestinians from the remaining lands they hold. And it has been blocking all attempts to even talk of return of refugees to their own country. The only aim is to declare and let the whole world accept Israel as a Jewish state. More importantly there have been concerted efforts to Judaize the surroundings of the Al-Aqsa Mosque. Now if Muslims continue to isolate Jerusalem and Al-Quds, just because its under Israel, will it not boost their efforts to Judaize the whole of Jerusalem? The more number of Muslims visiting Al-Aqsa, the more Islamic right it retains. Of course, the struggle against the Israeli occupation can continue, but the more we shun Jerusalem the stronger will be the Judaization of Jerusalem. If we are honest with ourselves and with the Palestinians, we really don't see even a rare chance of Israel returning back the occupied territories in decades to come. So how long will we be leaving Jerusalem alone? And what do we say about the Muslim countries who already have either full diplomatic ties with Israel or have some tacit (hand in glove) understanding with Israel? Refrain from them as well? An interesting example should be of significance here: The destruction of historic Babri Masjid in India at the hands of right wing Hindu fanatics. The controversy and court cases over this issue were in existence ever since the British rule in India. At one time a court declared the complex locked for both Hindus and Muslims. And after decades the locks were opened and Hindus given access to perform their worship, thereby reducing the Muslims' chances of winning back the right to offer prayers in the Masjid. One of the significant stands taken by right wing propaganda in the run up to opening the locks for Hindus was - "No Muslim prayers were offered there for so many decades, No Muslim ever entered there so it cannot be a Masjid".

Saturday, May 12

ELIMU YA MADRASA TANZANIA:

BISMILLAHIR RAHMANIR RAHIIM
Historia, Matatizo na Taaluma za Walimu
MUHTASARI:
- Madrasa na Kazi zinazonasibishwa nazo.
- Historia ya Elimu ya Madrasa Tanzania.
- Sahihisho kwa madrasah zetu.
- Taaluma muhimu kwa walimu na madrasah.
· Njia na mbinu zakufundishia.
· Uendeshaji wa Madrasah kwa ujumla.
· Saikolojia ya watoto na malezi.
· Maarifa katika fani wanazofundisha.

1.0 UTANGULIZI

1.1 Neno la Awali
Kwa muda mrefu sasa taasisi muhimu ya kiislam, taasisi ya “madrasa” imeachwa na kupoteza hadhi yake. Pamoja na hilo, taasisi hii imeacha pengo kubwa ambalo halizibiki kwa urahisi ila kwa kuinua hadhi ya Madrasa zetu.
Umma wa Waislam unazidi kupata kizazi kinachokosa haki za kimsingi za kuandaliwa kama madhalifa. Mwenyezi Mungu katika Qurani 51:56 ametwueleza “SIKU WAUMBA MAJINI NA WATU ILA WANIABUDU” ili kutekeleza lengo hilo, waislamu lazima waipe hadhi Madrasa. Kadhalika ili kufikia hadhi yetu wanaadam kama inavyoelezwa katika Quran 2:30 waislam lazima tuipe madrasah, hadhi yake sahihi. Kwa sababu hizo, kuna haja ya kufanya fikra juu ya kuinua hadhi ya madrasa zetu kwa ajili ya kuuendeleza umma wa kiislam utapotea na kuacha wanaoitwa Waislam lakini ummah wa kiislam haupo.

1.2 Maana ya Madrasa
Ilivyozoeleka, madrasa ni kituo cha kiislam ambapo watu hupata elimu juu ya mambo ya msingi katika uislam. Wengine wameita Shulel za Quran, wengine wamesema, vyuo vya Quran, na wengine wanaelewa kuwa madrasa ni vituo vya watoto ambapo masomo ya Quran, kusoma na kukandika hufundishwa.

1.3 Kazi zinazonasibishwa na Taasisi ya Madrasa
Madrasa zetu Tanzania, kwa muda mrefu tangu Historia ya kuingia kwa uislam nchini zimenasibishwa na kazi zinazofanywa na taasisi hii. Kwa ujumla madrasa zetu zimejikita katika taaluma zifuatazo:-
(i) Kuandika herfu za kiarabu.
(ii) Kuzisoma herfu za kiarabu.
(iii) Kutafsiri llugha ya kiarabu.
(iv) Kusoma Quran kwa ghaibu au kwa kutazamia.
(v) Jinsi ya kufanya ibada maalum na kanuni zake. Mfano, ibada, swala, swaum, hija na utoaji zakat na sadakat.

1.4 Athari za Madrasa kujikita katika shughuli hizo
Kwa kuwa Madrasa ni vituo vya elimu ya kiislam, na kwa vile madrasa zinaoa elimu hizo tu, basi elimu ya kiislam inafahamika kuwa ni ile tu inayohusiana na:
- Kusoma na kuandika Quran.
- Kukariri sura za Quran na tafsiri zake.
- Kanuni za utekelezaji wa nguzo tano.
- Kukariri hadithi kadhaa za Mtume (s.a.w).
- Kukariri visa vilivyo katikak lugha ya kiarabu.
Matokeo ya hilo, Uislam nao umeeleweka kukwa ni mambo ya kimaisha yanayohusiana na shughuli hizo tu. Nje ya shughuli hizo si vitu vya lazima katika uislam. Mfano kuksimamisha dola ya kiislam.

2.0 HISTORIA YA ELIMU YA MADRASA TANZANIA KWA UFUPI
Ø Historia ya Elimu ya Madrasa Tanzania inanasibiana na Historia ya kuenea kwa uislam katika Afrika Mashariki kuanzia Pwani hadi bara.
Ø Elimu itolewayo na Madrasa zetu ilichipuka tangu wakati walivyoanza kuja Waarabu kutoka Saudia, Oman, Uajemi, Hadhramaut na Yemen.
Ø Karne ya 9 na 10 wahamiaji kutoka Saudia walianza kusihi BENADIR (Pwani ya Somalia).
Ø Karne ya 12 Waarabu wageni (Afro-arabs) walianza kufika hadi mji wa Kilwa.
Ø Karne ya 12 wageni kutoka Hadhramawt na Yemen waliingia Afrika Mashariki. Wageni hawa nao pia walitoa elimu inayohusu uislam. Lakini kufahamu uzito wa elimu waliyoitoa kunategemea ufahamu wa sababu zilizowaleta Afrika Mashariki. Hawakuja kueneza uislam na kuufundisha uislam. Bali wali kuja kutokana na:
(i) Njaa iliiyokuwapo Arabuni wakati huo.
(ii) Ukame huko Arabuni.
(iii) Ukandamizaji wa Kisiasa uliotawala huko.

2.1 Kustawi kwa Elimu ya Madrasa Afrika Mashariki
Ø Mwaka 1332, Mwarabu aitwaye IBN BATUTA alipotembelea Kilwa alikuta mji umekaliwa waliokuwa wakitumia lugha ya Kiswahili.
Ø Baadaye miji ya Tanga, Dar-es-Salaam, Mombasa, Lamu, Malindi, na Mikindani vikawa vituo vya kueneza uislam na elimu ya kiislam katika miji ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwandda, Zaire, Msumbiji, Malawi na Burundi.

2.2 Maarifa yaliyotolewa na njia za kufundishia
Ø Maarifa yaliyotolewa na kuonekana hayo ndiyo maarifa ya uislam ni pamoja na:
(i) Zipi ni nguzo za imani na maana yake.
(ii) Zipi nguzo za Swala na maana yake.
(iii) Namna ya kusoma Quran, lugha ya kiarabu na vira kadhaa.
(iv) Sirah ya Mtume (s.a.w)
(v) Kanuni zinazotawalal utendaji wa Ibada Maalumu.
Ø Maarifa haya yalifundishwa kwa njia kuu ya Kipurure. Mwanafunzi hakusoma kwa kuwa mdadisi sana. Wanafunzi walikasirishwa waliyofundishwa.
Ø Walimu wa kufundisha hayo, ni wale tu, walioonekana wanaweza kuyasoma hayo. Hakukuwa na mazingatio kuhusu uwezo na ujuzi wa mfundishaji kufikisha maarifa anayoyatoa.
Ø Kwa sababu hizo, pia njia kuu ya kudhibiti nidhamu, ilibaki kuwa ni viboko tu.
Ø Kwa ujumla taaluma kuu za elimu ya Madrasa zilizotawala ni KUSOMA, KUANDIKA, KUIFADHI na KUIGA ambazo zilitolewa na walioweza kuzipata taaluma hizo.

2.3 Dosari za Elimu ya Madrasa iliyotolewa wakati wa Waarabu
Utangulizi
Ø Dosari hizo zimetokana na asili ya kuenea kwa dini na elimu ya Kiislam Afrika Mashariki, hususan Tanzania.
Ø Tatizo linakuja kwa vile Uislam na elimuk ya Kiisam:-
(i) Vilenea katika taratyibu za walioeneza kkujitafutia maisha yao wala si kwa madhumini ya kufanya umisionari.
(ii) Vilienezwa na wailam ambapo hawakuwa na maandilizi ya kufanya hivyo hivyo hakukuwa na matayarisho yoyote ya malengo ya kieleimu.
Ø Matokeo yake uislam ulifundishwa ili kupata wenzi na washirika katika mas[ala ya kijamii kama vile:
o Misiba
o Harusi n.k..
· Utangulizi

(i) Zilifundishwa Taaluma chache tu.
Mfano: Kusoma, Kuandika, Kukariri Quran.
Taaluma hizo si pana kiasi cha kuwawezesha wanafunzi kuuhani uislam kifikra, au vyovyote Taaluma hizo hazimwezeshi mwanafunzi kumudu changamoto zinazoibuka kila kukicha; Japo uislam haushindwi na changamoto yoyote ile.
(ii) Njia za kuendeleza nidhamu, na maadili zilikuwa viboko tu, ukali tu, pasi na kuchunguza tatizo kwa lengo la kkuondoa tatizo hilo na kusaidia.
(iii) Njia za kkufundishia hazikuzingatia umuhimu wa kuendeleza na kuhusisha nyanja tatu za kujifunza.
(a) Nyanja ya ung’amuzi (Cognitive domain).
(b) Nyanja ya matendo (Psychomotoar domain)
(c) Nyanja ya kuhusisha (Affective domain)
Kila nyanza hapo inaumuhimu katikak uislam wa mtu mmoja mmoja au jamii na hatimaye Ummah.
(iv) Hakukuwapo chombo maalum cha kijamii, kinachosimamia swala zima la utoaji wa Elimu hii. Matokeo yake kila mmoja alifundisha kadiri na namna alivyodhani ni sawa.

2.4 Athari za dosari hizo
(i) Kukosekana kwa taaluma muhimu za kifiqih
Mfano:
- Taaluma inayowezesha kkuhusianisha mazingira na fatwa kadhaa za kifiqih.
- Taaluma inayofafanua hukumu kadhaa za kifiqih na yanayotokea katika maisha. Katika hili, kumekosekana taaluma ya kubainisha tofauti ya RIRA na HIBA.
(ii) Watu wachache sana ndio waliweza kwendelea na elimu ya Madrasa kwa
kiwango cha juu kwa kulinganisha na waislam wengine.
Mfano:
Ni Masheikh wachache waliweza kkufikia kiwango Fulani. Matokeo hata vitu vidogo vidogo kuweza kufahamika kwa waislam wote, vinafahamika na masheikh tu.

(iii) Kuibuka kwa Matabaka miongoni mwa waislam kutokana na dosari hizo,
kumeibuka matabaka kadhaa mingoni mwa waislam.

Mfano:
o Tabaka la wasomi wa elimu katika mfumo huu wa madrasa tu.
o Tbaka la waliosoma elimu ya madrasa kidogi na elimu ya kisekula kidogo.
o Tabaka la waliosoma kiasi elimu ya kisekula na kukosa elimu ya madrasa lakini badaye (ukubwani) wakajifunza elimu ya uislam kwa mfumo mwingine.
Mahusiano ya matabaka haya hayasaidii kuendeleza uislam na waislam wa kiislam, ni sumu kwa maendeleo ya jamii ya kiislam.

3.0 MATATIZO YANAYOIKABILI ELIMU YA MADRASA TANZANIA
i) Utangulizi
Taasisi ya Madrasah inazidi kukpoteza hata hadhi yake ndogo iliyokuwa nayo.
Mfano:
Jamii haiipi hadi na thamani stahiki licha ya kuwa madrasa ni taasisi muhimu katika kurithisha mila, na mfumo mzima wa uislam toka kizazi hadi kingine. Wazazi wa watoto wa kiislam leo hii hawana hari ya kupeleka watoto wao kwenye vituo vya madrasa. Wala wazazi hao hawana hata haja ya kujua mikati ya madrasa zinazowazunguka.

(ii) Matatizo

Matatizo yanayoikabili elimu ya madrasa ni:

3.1
Matatizo ya Kitaasisi (Institutional Problems)

(a) Hakuna mfumo wa uendeshaji elimu ya madrasa. Mfumo huo
Mfumo huo hautoi picha halisi juu ya nani hasa ndiye mratibu au msimamizi wa elimu ya Madrasa. Kwa sababu hiyo hakuna upimaji wala tathimini yoyote ili kuelewa mustak bal wa elimu hii muhimu
(b) Kukosekana kwa “usare” (uniformity) katika ufundisjaji.
Matokeo yake anapohama motto kwenda madrasa nyingine anaathirika kitaaluma.
(c) Hakuna utaratibu fasaha/muafaka wa kuwahusisha wazazi wa Kiislam katika kujadili maendeleo na kutathimini uendeshaji wa madrasa. Athari yake ni wazazi kutojihusisha na uendelezaji wa madrasa zetu na ufuatiliaji wa taaluma muhimu zipatikanazo.
(d) Kukosekana kwa utaratibu wa kubadilishana mawazo baina ya walimu tofauti tofauti, juu ya uboreshaji wa njia za ufundishaji na mafanikio katika uendeshaji madrasa.
(e) Kukosekana kwa mipango inayohusiana na madrasa, wanafunzi na walimu. Athari yake ni kupungua kwa idadi ya wanafunzi na walimu wa madrasa.
(f) Kukosekana kwa utaratibu maalumu juu ya vigezo vinavyomuwezesha mtu kuwa mwalimu. Kwa kawaida yeyote anayejua kusoma na kuandika herufi za kiarabu, kusoma Quran na mambo kadhaa katika Ibada maalumu za kifiqih, aweza kuwa mwalimu hata kama sifa za kitabia, na uwezo wa kkurithisha elimu kwake ni vikwazo.

TANBIH:
Aina za walimu zaweza kkuwa kama ifuatavyo:-
(i) Mwenye sifa (Qualified) – Anazo sifa kitabia, anaweza na ujuzi wa kkufundisha na ana elimu.
(ii) Mwenye sifa (Underqualified) – Anayo elimu ila hana mbunu bora za ufundishaji.
(iii) Asiye na sifa (Unqualified) – Hana sifa hata kidogo. Huyu ni hatari sana.

Matatizo ya Kijamii
(a) Fikra za watu juu ya elimu ya madrasa na thamani yake
- Jamii na mtu mmoja mmoja wanachukulia elimu ya msingi ya madrasa ni kusoma Quran na kujua kanuni muhimu za utekelezaji wa Ibada maalumu kama vile Swala, hija, swala ya maiti, kushona sanda na kadhalika.
- Athari yake ni kuwa, mara baada ya watoto kufikia ngazi hiyo huonekana imetosha na kwamba, wana elimu ya kutosha juu ya uislam. Elimu kuhusu uislam inapungua miongoni mwa waislam.
(b) Uchumi duni kwa wazazi na walimu
- Umaskini na kipato kidogo kwa walimu wa madrasa inakuwa tatizo kubwa kwa uendeshaji wa madrasa zetu. Hali hii husababisha walimu wa madrasa kutenga muda kidogo sana kwa ajili ya kazi ya madrasa. Kadhalika kujituma juu ya kuboresha madrasa hupungua.
- Vile vile pato la wazazi kuwa dogo huchangia tatizo. Mara nyingi watu wenyekipato cha chini ndio wanaopeleka watoto wetu madrasa na wenye uwezo na wito wa kiislam wao huwaajiri walimu wa kuwafundisha watoto nyumbani. Kwa sababu hiyo, wazazi wengi hawana uwezo wa kkuchangia fedha muhimu kwa ajili ya madrasa. Wakati mwingine mchango wao huwa kidogo na mgumu kupatikana.
- Athari ya hayo, ni kudorora kwa madrasa zetu na kupatikana kwa watoto, mabarabara, vijana wasio na elimu sahihi ya msingi kuhusu uislam na hatimaye kuporomoka kwa maadili.
(c) Mfumo wa elimu ya nchi na utaratibu wa kisekula
Mfumo wa elimu ya kisekula umembana kiasi motto anayesoma madrasa kutokana na utaratibu ulivyo. Uendeshaji wa elimu ya kisekula umezaa desturi ya “Tuition” (masomo ya ziada), desturi amabyao sit u inamfanya motto achoke bali pia inamkosesha muda wa kuhudhuria katika madrasa zetu.

Mfano:
Mtoto wa darasa la kwanza na pili wanaingia shule kwa zamu, mara asubuhi, mara saa tano, mara mchana. Hii inaleta ugumu kwa madrasa kuratibu jinsi ya kuwasaidia watoto.
Mtoto wa darasa la kwanza atokapo shule, anapumzika kidogi, kasha anaenda “Tuition” masomo ya zaida.
Mtoto wa darasa la tano hadi saba, anakosa muda kabisa. Muda wote, kutwa mzima anashughulishwa na elimu ya kisekula na usiku anajisomea nyumbani.
Athari ya tatizo hili ni kushuka kwa mahudhurio ya watoto katika madrasa zetu, na mara nyingine kuwapo kwa mahudhuria yasiyotabirika na kuelezeka. Mara kuna mahudhurio ya kuridhisha mara mabaya.
(d) Shughuli za Kijamii miongoni mwa Waislam
- Ndani ya jamii ya Kiislam, inapotokea shughuli kama vile harusi na kadhalika, madrasah nyingi kuhusishwa. Mfano kuandaa kaswida kwa ajili ya maulidi harusini. Hili hupunguza za muda wa ufundishaji na kujifunza katika madrasa zetu.
- Athari yake ni kuongezeka kwa tatizo katika madrasa zetu. Wazizi wengine huona kua hakuna haja ya watoto kusoma madrasa hizo.

4.0 SOLUHISHO KWA MADRASA ZETU

4.1 Utangulizi
- Ni vigumu kuliondoa tatizo hili kwa kulifanya jukumu hilo kuwa la watu Fulani tu. Mfano, kulifanya liwe jukumu la masheikh tu, au jukumu la walimu tu, au la wazazi tu. Inapaswa kuwa ni tatizo linalomgusa kihisia kila muislam.
- Kwa hakika elimu hii ni muhimu sana kwa maendeleo ya uislam na waislam kiitikadi, kitaaluma, kielimu n.k.

4.2 Mfumo
- Kunahaja ya kuudhurusi mfumo wa elimu ya madrasa na kuangalia namna ya kuuendeleza na kuuboreha kwa manufaaa ya kikazi cha kiislam.
- Mfumo wa madrasa zetu uendane kabisa na haja iliyopo katika jamii kwa lengo la kuwaendeleza watoto kitaaluma.

4.3 Walimu
- Kuwepo na mpango maalumu wa kuwaendeleza walimu kielimu, kitaaluma na kiuchumi ili kuwaongezea hari ya kujituma na kukfikiri kwa ajili ya maendeleo ya taasisi hii muhimu, “madrasati”.
Mfano:
Kuwepo kwa warsha, makongamano na semina ili kuwawezesha walimu kushirikiana ujuzi na mbinu za kufundishia na kuendeshea madrasa zetu.
- Walimu wawe wabunifu kiuchumi ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuendeleza madrasa zetu.
- Walimu wasijione kuwa wao ni waislam au watu wa daraja la chini sana kimaisha. Bali wajione wao ni watu muhimu na kazi yao ni jukumu lao si jukumu la mtu Fulani na wala hawafanyi kazi hiyo ili tu kuwaridhisha watu Fulani bali ili kumridhisha allah (s.w).

4.4 Jamii ya Kiislam
- Ifanye fikra juu ya jinsi ya kuboresha na kuendeleza madrasa zetu na watoto wetu katika taaluma muhimu za kiislam.
- Jamii nzima ieleweshwe juu ya nafasi sahihi ya Madrasa na Elimu ya Madrasa kwa maisha yua Waislam nchini.

4.5 Taasisi za Kiislam
Zishirikiane kuona jinsi ya kutatua matatizo hayo.

5.0
TAALUMA MUHIMU KWA WALIMU WA MADRASA

5.1 Utangulizi
Kila nyanja inahitaji taaluma Fulani ili kuifanya nyanja hiyo iwe makini na yenye manufaa kwamaisha na ummah kwa ujumla. Hata mitume (radhi za Allah ziwafikie) walipewa taaluma maalumu kwa kazi zao. Katika maisha yetu tunahitaji taaluma zinazowezesha watu kutekeleza majukumu yao katika mazingira wanayoishi.
Mfano:
Mwalimu wa madrasa anahitaji taaluma juu ya;
(i) Uendeshaji wa madrasa.
(ii) Ufundishaji.
(iii) Saikolojia ya watoto na malezi.
(iv) Taaluma inazofundisha kama vile Fiqih, Tareikh, Qurani, Kiarabu, Tawhiid, Sirah, Akhlaq n.k.

5.2 Njia za kkufundishia (Muhtasari)
Zipo njia kadhaa Bwana Mtume (s.a.w) amekuwa akizitumia katika kufundishia watu. Pia Quran imeeleza njia kadhaa kwa ajili ya ufundishaji na uchamasishaji. Kwa muhtasari njia hzo ni pamoja na zifuatazo.

(a) Simulizi (Narration)
- Hii ni njia ambayo mwalimu anafundisha kwa kutumia visa vya kubuni au visa halisi. Njia hii inafaa sana kutumika hususan kwa watoto wadogo.
- Katika Quran njia hii imetumika kutafundisha mara kadhaa. Kanuni na njia yenyewe katika Quran zimeelezwa katika “NJIA ZA KUFUNDISHIA KATIKA MADRASA ZETU”. Hapa ni muhtasari tu.
- Njia hii yaweza kutumika katika kufundisha Sira ya Mtume, Akhlaq, Tareikh, Fiqih hata tawhiid. Alimradi mwalimu afahamu jinsi ya kuitumia njia hiyo kwa ufanisi.
(b) Uelezeaji (Description)
- Njia hii hutumika kuelezea dhana au wazo Fulani katika uislam. Muhimu kwa mwalimu ni kuifahamu misingi ya njia hii pamoja na kuelewa mazingira yanayofaa kwa njia hii.
Mfano:
(i) Ili kutoa maf’hum nzuri kuhusu “UISLAM” kama dini njia hii yafaa kutumika.
(ii) Ili kufunldisha vizuri, mazingira ya vita vya Badr, Uhud, Khandaq n.k. kwa lengo la kkufundisha mazingatio yanayopatikana, mwalimu aweza kutumia njia ya UELEZEAJI (Description)
- Kadhalika, cha muhimu ni maarifa kuhusu njia hii.
(c) Njia ya Uoneshaji (Demonstration)
- Ni njia inayotumika kufundishia mada zinazolenga kutoa ujuzi kwa wanafunzi kutenda matendo maalum:
Mfano:
(i) Swala la mait.
(ii) Swala la Faradh na Sunnah.
(iii) Kushona Sanda.
(iv) Kuosha Maiti.
(v) Kuchukua Udhu n.k.
- Mada kama hizi zikifundishwa pasipokutumia njia hizi, ueleo wa wanafunzi unaathirika.
- Mwalimu anatakiwa kuifahamu njia hii kwa madhumuni ya kuitumia kwa ufanisi.
(d) Njia ya ugunduzi na udadisi
- Njia hii inamtaka mwalimu aoneshe tatizo kasha aongeze wanafunzi katika kugundua suluhisho. Kwa kufanya hivi, milki ya ung’amuzi (Cognitive Facult) itakuwa imeendelezwa. Quran inasisitiza matumizi ya milki ya ung’amuzi (Cognition domain).
Mfano:
(i) Baada ya kufundisha “Tawhid” – Mwalimu anaweza kutoa habari ya kweli kuhusiana na tawhiid kasha wanafunzi wakajadili kwa mnasaba wa tawhid.
(ii) Mwalimu aweza kufundisha “Tareikh” – Hijar kutoka Makka kwenda Madina, alafu wanafunzi watatakiwa kugundua wanachojifunza.
(iii) Mwalimu awezatoa tatizo liliopo katika jamii kwa mnasaba wa uislam, kasha akawataka wanafunzi waonyeshe sabbu na suluhisho.
(e) Njia ya Kuhidadhi
- Hii ni muhimu sna katika elimu na maarifa ya kiislam. Mwalimu anatakiwa kuwawezesha wanafunzi kuhifadhi katika mada kadhaa.
Mfano:
(i) Ktika Swala, mwalimu atumie njia rahisi kwa wanafunzi kuhifadhi.
(ii) Katika Wudhuu, mwalimu atumie njia hii pia ili wnafunzi waweze kuhifadhi maneno muhimu.
(iii) Katika Dua, wanafunzi wahifadhishwe dua.
(iv) Katika Tarekh, wanafunzi wahifadhishwe aya na hadithi mbalimbali zinazonasibiana na matukio katika mada. Mathalani, kufundisha Mkataba wa hudaybiya, Quran 48:1. 48:18 ni vema zikahifhadhiwa. Pia katika kufundisha AKHLAQ mwalimu awahifadhishe watoto, Sura ya 64.4 ikiwekana, kulingana na umri wa watoto, Pia wahifadhi Quran 33:21.
(f) Njia za Kufundisha Quran
Njia na mbinu pamoja na mikakati ni muhimu sana katika ufundishaji wa usomaji Quran, vinginevyo motto atosoma muda mrefu sana ili kuelewa. Baadhi ya mbinu za kufundishia ni pamoja na kusoma herufi bila irobu kwa njia ya ubao, kadi, daftari n.k.

MUHIMU:
- Mwalimu afundishe kwanza herfu bila irabu. Yaani: ALIF, BE …….
- Kisha afundishe Irabu. Yaani: FAT’HA, KISRA, ……
- Afundishe kuchanganya herufi hizo na rabu;
Mfano: BE FAT’HABA, TE FAT’HATA …….
- Mwalimu atumie michezo kadhaa kwa watoto kuzitambua herufi.
Mfano: NGAZINGAZI, KIKAPU, UPANGAJI, GURUDUMU ZA GARI, NYUMBA …. n.k.
- Mwalimu afundishe kuchanganya SILABI ili kupata neno. Ni vizuri Mwalimu akaanza na kinachoeleweka kwenda kisichoeleweka.
Mfano: Kumwezesha motto kuandika BABA kwa herufi za Kiarabu, kasha aandike neno la kiarabu kwa herfu hizo.

6.0 HITIMISHO
Mwalimu anapaswa sit u kujua anachokifundisha, bali pia kufahamu na kuweza kutumia njia na mbinu muafaka. Kwa kawaida hatupaswi kulenga kusema sana, au kueleza mengi, bali tulenge kuwezesha mengi kufahamika kwa urahisi zaidi.

7.0 MWISHO
Kwa muda mrefu MADRASA zimesahaulika na kusababisha athari mbaya. Ili kuzikuisha tunapaswa kuzingatia kazi zinazotakiwa kukfanywa na madrasa na zipi zinafanywa. Kuelewa tatizo kwa undani. Historia ya Madrasa Tanzania ni muhimu kufahamika ili kurudisha mzizi wa tatizo. Kadhalika, Matatizo yanayoikabili taasisi ya Madrasa na ufumbuzi wake ni muhimu vikajadiliwa. Aidha , kuna haja ya kukumbuka taluma muhimu kwa walimu wa Madrasah na kuona kama wengi wanazo. Kama si hivyo, basi mikakati iwepo kuwawezesha walimu wa Madrasa kuendesha madrasa zetu (Uendeshaji Madrasa) pamoja na kuwa na mbinu bora za kufundishia katika madrasah zetu.
Mbinu zilizomo humu ni muhtasari tu, hazijaelezwa zote. Na wala hazijafafanuliwa hasa.
ALLAH NDIYE MJUZI WA YOTE

Saturday, May 5

Mawaziri, hakuna sherehe, nendeni mkawajibike! by zittokabwe

Juhudi za kurejesha misingi ya uwajibikaji katika utumishi wa umma zimeanza kuzaa matunda Baada ya Rais kutekeleza shinikizo la Bunge la kuwafukuza kazi baadhi ya Mawaziri ambao Wizara zao zimetuhumiwa kwa ubadhirifu wa fedha za umma, rushwa na utendaji mbovu. Mawaziri 6 wamefukuzwa kazi baada ya kugoma kujiuzulu wao wenyewe, manaibu Waziri 2 wamefukuzwa pia.

Ndugu George Mkuchika alitakiwa kujiuzulu, akajiuzulu lakini Rais amemrudisha kwenye Baraza kama Waziri wa Utawala Bora. Yeye nampongeza kwani hakuwa na makuu ya kuanza kujitetea kama wengine. Atakuwa ametoa funzo kwa wenzake.

Kwa kawaida wateule hufanya sherehe kwa kuteuliwa kwao. Nitawashangaa watakaofanya sherehe safari hii kwani hakuna cha kufurahia. Nitawashangaa Watakaokwenda kuapa na Maua kwa furaha kwani furaha itakuwa ya muda mfupi tu. Mkutano wa Bunge wa Bajeti ni mwezi ujao tu na Wateule wote watakuwa kikaangoni. Too short honeymoon.

Hakuna cha kusherehekea kwa sababu nchi in a changamoto nyingi sana. Changamoto ya kuzalisha umeme wa kutosha na kuusambaza kwa wananchi wengi, changamoto ya kukuza uchumi wa vijijini na kukuza uzalishaji viwandani ili kutengeneza ajira kwa vijana, changamoto ya kuongeza mapato ya Utalii kutoka katika hifadhi zetu na kuvutia watalii zaidi katika nchi yetu.

Nimewapigia simu wateule wengi na kuwaambia, siwapi pongezi Bali nawatakia kazi njema. Nawatakia uwajibikaji mwema. Uwajibikaji ndio msingi wa kupambana na rushwa, uvivu na uzembe.

Kwa Waziri wa Fedha, ambaye mimi ni Waziri Kivuli wake (Kama Kiongozi wa Upinzani Bungeni hataniwajibisha pia), namwambia uteuzi wake ni changamoto kubwa sana katika maisha yake.

Hivi sasa eneo lenye Bajeti kubwa kuliko zote nchini ni huduma kwa Deni la Taifa (services to national debt). Lazima kuangalia upya Deni la Taifa. Hivi sasa Deni la Taifa ukijumlisha na Dhamana za Serikali (government guarantees) limefikia tshs 22trn mpaka Desemba 2011. Nimewahi kutaka ukaguzi Maalumu katika 'account' ya Deni la Taifa. Linarejea wigo huu. Tunalipa takribani 1.9trn tshs kwa mwaka kuhudumia Deni la Taifa. Zaidi ya Bajeti ya miumbombinu, Afya, Maji, Umeme nk.

Mfumuko wa Bei, misamaha ya kodi na kodi zinazozuia watanzania kujiajiri ni changamoto kubwa sana Wizara ya Fedha lazima ihangaike nayo.

Usimamizi wa Mashirika ya Umma kupitia Ofisi ya Msajili wa Hazina na hasa usimamizi wa Hisa za Serikali katika kampuni binafsi ni masuala yanayohitaji masuluhisho sasa na sio baadaye.

Kwa Mwalimu wangu Dkt. Mwakyembe, utakumbukwa kwa Jambo moja tu. RELI. 'make our Railway system work'. Hutakuwa na 'legacy' nyingine isipokuwa Reli maaana Bandari bila Reli ni sawa na Bure.

Tunatumia zaidi ya tshs 300bn kwa mwaka kukarabati barabara wakati tunahitaji tshs 200bn kukarabati Reli iweze kusafirisha mzigo kwenda Bandarini na kukupa Bandarini.

Ndio maana nasema hakuna Jambo la kusherehekea maana wajibu mliopewa na Rais ni mtihani mkubwa kwenu katika kukitumikia Taifa letu. Msipowajibika, mtakumbwa na fagio la chuma!

Mkisha kula kiapo, kimbieni kazini. Nothing to celebrate. Hit the ground running.

ZZK

Dar-es-Salaam

Jumamosi, Mei 5 2012