Wednesday, February 29

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015 by zittokabwe

Kampeni ya kupunguza umri wa urais haina uhusiano na mimi kutaka kugombea urais 2015
Baadhi ya vyombo vya habari vimehusisha kauli yangu ya kutaka kupunguza umri wa kugombea urais na mimi ‘kuutaka urais’. Mimi nikiwa mwanachama na kiongozi wa chama chama changu cha CHADEMA naelewa na kuziheshimu taratibu na kanuni tulizojiwekea za kuomba nafasi mbalimbali za uongozi, ikiwemo nafasi ya urais. Nafasi ya uongozi ndani ya CHADEMA haiombwi kwenye warsha. Iwapo chama change, wakati muafaka ukifika na kutokana na matakwa ya jamii, kikiona nipewe jukumu lolote sitasita kutekeleza wajibu huo niwe au nisiwe mgombea.
Kwa hivyo, nilichozungumza jana ni kutoa maoni yangu kwamba muda umefika kwa Taifa letu kupunguza umri wa kugombea urais. Maoni yangu haya yanatokana na ukweli kwamba hakuna sababu zozote za kisayansi zinazomfanya mtu aliye chini ya umri wa miaka 40 akose sifa za kuwa Rais. Msimamo huu nimekuwa nao tangu zamani nikisoma shule na haujawahi kubadilika. Hakuna mahala popote katika maoni yangu niliyotoa jana niliposema kwamba nataka umri wa urais upunguzwe ili nipate fursa ya kugombea nafasi ya urais. Pia siwezi kutaka katiba iandikwe kwa ajili yangu. Vilevile kamwe isionekane kwamba matakwa ya muda mrefu ya vijana ya kutaka umri wa kugombea Urais kupunguzwa yanalenga kunipa fursa mimi kwani mimi ni binaadamu naweza nisiwe na sifa za kuwa Rais lakini kukawa na vijana wengine wengi wenye umri chini ya miaka 40 wenye Uwezo na Uzalendo wa kutosha kushika usukani wa nchi yetu. Ni maoni yangu kwamba tupate mabadiliko ya vizazi katika uongozi wa nchi yetu ili kukabili changamoto za sasa zinazokabili Taifa letu.
Tunapojiandaa kutoa maoni kuhusu Katiba Mpya ni vizuri vyombo vya habari vikajikita kutoa taarifa bila kuweka tafsiri au kuwatafasiria maoni ambayo wananchi na viongozi watakuwa wanayatoa kuhusu maudhui ya Katiba Mpya.

Saturday, February 18

Kiama posho serikalini chaja


POSHO za vikao ambazo mjadala wake umechukua takriban mwaka mmoja sasa, huenda zikafikia ukomo mwaka huu kutokana na kuwapo kwa taarifa kwamba wabunge wamepania kuzifuta katika Bajeti ya mwaka ujao wa fedha.

Habari ambazo zimelifikia gazeti hili kutoka bungeni na serikalini zinasema Tume ya Huduma za Bunge tayari imeanza kujadili suala hilo na kwamba uamuzi ni kuanza kufuta posho za vikao kwa wabunge ambazo ni Sh70,000 kwa siku.
Taarifa za kuwapo kwa mpango huo zimekuja siku chache tangu Rais Jakaya Kikwete alipokataa kuidhinisha mapendekezo mapya ya posho za vikao kwa wabunge kutoka kiasi hicho cha Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku.

Ikiwa uamuzi huo utatekelezwa, utakuwa ni ‘ushindi’ kwa wabunge ambao waliasisi vita dhidi ya posho za vikao kiasi cha kusababisha tofauti za wazi na wabunge wenzao ambao wamekuwa wakiwatuhumu kwamba wanatafuta umaarufu wa kisiasa.

Miongoni mwa wabunge hao ni Mbunge wa Bumbuli (CCM), ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, January Makamba na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma, Zitto Kabwe.

Mwingine ni Kiongozi wa Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe ambaye aliwahi kuziita posho za vikao kuwa ni wizi wa kitaasisi ulioasisiwa hali ukiwa hauna tija kwa Taifa na badala yake kupoteza fedha nyingi za Serikali.
Mmoja wa viongozi waandamizi wa Bunge ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini alisema suala la wabunge kufuta posho za vikao tayari limeanza kujadiliwa na Tume ya Huduma za Bunge ambayo Mwenyekiti wake ni Spika Anne Makinda.
“Kuanzia mwaka ujao wa fedha tunataka kuacha kabisa kulipwa posho za vikao (sitting allowance), kwa hiyo hata hiyo Sh70,000 hatutachukua itakuwa ni ziro kabisa maana tumechoka kuandamwa,” alisema kiongozi huyo na kuongeza:
“Lakini wakati tukifanya uamuzi huo, serikalini, mahakamani na katika mashirika mengine ya umma nako wajiandae, hakuna bajeti yoyote ya posho za vikao itakayopitishwa na hili tutaanza kuwapa maelekezo rasmi wakati wa vikao vya mipango ya bajeti mwezi Aprili mwaka huu.”

Spika wa Bunge, Makinda alipotafutwa juzi na jana kuzungumzia taarifa za taasisi yake kuweka mkakati wa kufuta posho hizo, simu yake ya kiganjani ilikuwa ikiita kwa muda mrefu bila majibu.
Kwa upande wake Naibu Spika, Job Ndugai alipoulizwa iwapo kuna mpango wa wabunge kusimamia kufutwa kwa posho zote za vikao ndani ya Bunge, serikalini na katika Idara ya Mahakama hakukanusha wala kuthibitisha suala hilo, badala yake akashauri kwamba: “usubiriwe wakati mwafaka.”

Alipoulizwa wakati mwafaka ni upi alisema: “Mimi nadhani suala la posho linachosha, hakuna jambo jingine la kuzungumza ina maana ni posho tu? Tumesema sana kama ni kuhusu kufutwa basi mimi nadhani tusubiri wakati mwafaka, wakati wa bajeti maana mchakato wake unaanza Aprili, tusubiri tutapata majibu mwafaka,” alisema Ndugai ambaye amekuwa msemaji wa suala hilo kwa muda mrefu sasa.

Serikalini nako
Wakati wabunge wakiwa wameanza mchakato huo wa kufuta posho, Serikali nayo inatajwa kwamba iko katika mchakato wa kufuta malipo hayo ambayo yamekuwa yakitajwa kwamba hayana tija kwa nchi.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Ramadhani Kijja alisema juzi kuwa: “Ninachofahamu mimi ni kwamba posho ziko nyingi siyo posho za vikao tu, kwa hiyo ni kweli kwamba Serikali inazipitia zote ili kuzihuisha na baadaye kufanya uamuzi sahihi, lakini sasa si rahisi kujua ni uamuzi gani utakaofikiwa.”

Kijja alisema mapitio yatakayofanywa na wataalamu serikalini yatalenga kubaini aina za posho zilizopo, tija yake katika utekelezaji wa kazi za umma na hatimaye kuamua ni zipi zibaki, zifutwe au kuongezwa kwa kuzingatia mapendekezo ya wataalamu.

Katibu Mkuu huyo aliongeza: “Hata kama zipo zitakazobaki mapendekezo ya wataalamu yatatuambia iwapo zinahitaji kuongezwa au la, tusubiri wataalamu wakimaliza kazi basi tutafahamu uamuzi wa Serikali utakuwa ni upi.”

Wakati wa Bunge la Bajeti la Juni mwaka jana, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alisema: “Suala la kupunguzwa kwa posho zisizokuwa na tija ni sehemu ya mpango wa Serikali kupunguza matumizi.”
Licha ya kutoa kauli hiyo, Mkulo pamoja na wabunge kadhaa, walisikika wakiwabeza wenzao waliokuwa wakipinga kuwapo kwa posho za vikao kwa maelezo kwamba wanajitafutia umaarufu wa kisiasa.

Miongoni mwa mabishano yaliyowahi kutokea baina ya pande zinazopingana kuhusu suala hilo yalihusu fedha za posho katika bajeti ya 2011/12 pale Zitto aliposema kuwa Serikali ilitenga kiasi cha Sh987 bilioni kwa ajili ya malipo ya posho mbalimbali na kati ya hizo Sh360 bilioni ni malipo ya posho za vikao (sitting allowance), huku wabunge wakitengewa kiasi cha Sh11 bilioni.

Kiasi cha Sh360 bilioni kinachodaiwa kutengwa kwa ajili ya fedha za vikao kinatosheleza kujenga vyumba 30,000 vya madarasa ikiwa chumba kimoja kinagharimu Sh12 milioni. Pia kiasi hicho cha fedha kinatosheleza kugharamia barabara ya lami yenye urefu wa kilometa zipatazo 400.

Hata hivyo, Mkulo alikanusha madai ya kutengwa kwa kiwango hicho cha fedha kwa ajili ya posho pale aliposema kwamba posho zote kwa ujumla wake katika bajeti ya mwaka 2011/12 ni Sh352.75 bilioni na kwamba kati ya hizo posho za vikao ni Sh25.68 bilioni huku wabunge wakipata Sh4.92 bilioni.

Mbowe, Makamba na Zitto
Mbowe na January kwa nyakati tofauti wiki hii walisema hawafahamu kuwapo kwa mpango wa kufutwa kabisa kwa posho za vikao, isipokuwa Zitto ambaye alisema amesikia tetesi kwamba Tume ya Huduma za Bunge inalifanyia kazi suala hilo.
Alisema utoaji wa fedha za vikao uliasisiwa na Bunge umesambaa katika taasisi nyingine za umma na kusababisha watendaji kutunga semina na vikao vingi ilimradi wanapata posho huku kazi nyingine zikiendelea kulala.
“Huu ni wizi wa fedha za umma ambao umeasisiwa na sasa unaathiri utendaji katika mfumo mzima wa Serikali, si fedha tu kwani hata kazi zinalala kwani watendaji wote wanakimbilia kwenye vikao vya kutunga kwa sababu kuna posho na si vinginevyo,” alisema Mbowe.

Mbowe aliongeza kuwa kama suala ni mishahara midogo hilo ni jambo linalozungumzika na kwamba Serikali inaweza kujenga hoja na kupandisha mishahara kwa kiwango kinachowezesha watumishi wa umma wakiwamo wabunge kujikimu, lakini si kuweka posho ambazo zinawanufaisha watu wachache na kujenga matabaka miongoni mwa watumishi wa umma.
“Mimi ninaamini watumishi wote wa umma wakiwamo wabunge tunapaswa kulipwa vizuri, kwa hiyo tujenge hoja za malipo mazuri kwa watumishi wote wa ujumla, lakini si kuanzisha posho za vikao kwa kisingizio cha malipo kuwa kidogo halafu hao wengine wadogo wanahudhuria kikao gani?”

Kwa upande wake Zitto alisema: “Nimesikia kwamba kuna mpango huo wa kufuta posho, kama upo ni hatua kubwa sana tutakuwa tumepiga. Msimamo wangu uko palepale kwamba posho za vikao siyo tatizo kwa wabunge tu hata kwa watumishi wengine wa umma na mashirika ya umma.”

Alisema hatua ya Rais Jakaya Kikwete kutoidhinisha nyongeza ya posho za wabunge kama walivyokuwa wamependekeza, ni ushindi wa awali ambao hauna budi kusambazwa katika maeneo mengine kwa kufuta malipo hayo katika mfumo mzima wa Serikali Kuu, Serikali za Mitaa na mashirika yote ya umma.

Naye Makamba alisisitiza kwamba msimamo wake kwamba posho ni tatizo katika mfumo wa utumishi wa umma upo palepale na kwamba ikiwa Bunge litaamua kwamba zifutwe litakuwa ni jambo jema.

“Sifahamu kuhusu mpango wa kufutwa kwake, ila sisi wengine mnatufahamu. Msimamo wangu hauwezi kubadilika katika hili kwa hiyo kama wenzetu wanaungana na sisi kwamba posho hizi za viko zifutwe litakuwa ni jambo jema sana mimi nitakuwa wa kwanza kuliunga mkono,” alisema na kuongeza:

“Nadhani kama kweli hilo lipo na likifanyika kwa nia ya dhati nina hakika tunaweza kusonga mbele kwa ajili ya masuala mengine muhimu badala ya kila siku kubishana kwa mambo ambayo yako wazi”.

Ardhi ya Tanzania yazidi kuumiza wanachama EAC Send to a friend Friday, 17 February 2012 21:13 0 digg Keneth Goliama MVUTANO kuhusu suala la ardhi umeibuka jana katika mkutano wa wataalamu wa kamati za Serikali Kanda ya Afrika Mashariki uliojadili madini, baadhi ya nchi zimepinga kuingiza ardhi kwenye mambo yanayoshughulikiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Wakichangia katika mkutano huo kwa nyakati tofauti, wajumbe walisema itakuwa ngumu kwa baadhi ya nchi kuingia kuingiza suala hilo kwenye mambo ya EAC, kwa sababu bado ndani ya nchi hizo kuna migogoro ya ardhi. Wakati baadhi ya wajumbe wakipinga hilo, wengine kutoka Uganda walisema haiwezekani nchi wanachama kuogopa kuingiza suala hilo kutokana na kuonyesha maendeleo mazuri. Hata hivyo, wajumbe kutoka nchi ya Kenya walionyesha wasiwasi wa uharaka wa kuingia kuingiza ardhi kwenye masuala ya EAC kutokana na mapigano yanayotokea ndani ya baadhi ya nchi wanachama. “Itakuwa ajabu kuingiza shirikisho la ardhi katika jumuiya wakati nchi za Rwanda Burundi na Tanzania zikionyesha kuwa na ugomvi wa ardhi na wawekezaji,” alisema Mkuu wa Sera ya Mipango na Ardhi kutoka Ethiopia, Dk John Kangwanja. Dk Kangwanja alisema kama hatua hiyo itafikia, kuna nchi zinaweza kuathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na migogoro ambayo inaendelea kujitokeza baina ya wazawa na wawekezaji. Wakati suala hilo lilipokuwa likizidi kuzua mvutano kwenye ukumbi, wawakilishi wa Tanzania wakiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha, Gregory Teu, walionekana kutochangia chochote huku waziri akiulizwa suala hilo kutoa maelezo alijibu kuwa hana maelezo. Wachiangiaji hao walisema Sheria ya mwaka 1995 na Sera ya Ardhi ya Tanzania, inapishana kwa kiasi kikubwa kutokana na kupitwa na wakati.Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Profesa Lucugga Kironde, alisema Tanzania ikikubali kuingiza suala hilo, itarajie kukumbwa na migogoro mikubwa kutokana na nchi nyingi za jumuiya hiyo zinanyemelea baada ya kwao kukumbwa na uhaba. Profesa Kironde alisema haiwezekani Tanzania ikiingia kwenye shirikisho bila kufanya marekebisho ya sheria ya ardhi, Watanzania wataendelea kuonekana maskini huku wachache kutoka EAC wakinufaika. “Afrika ina rasilimali za kutosha kila mahali hasa madini,umefika wakati kufuatilia kwa makini sheria ya ardhi ili mikataba ya nchi iweze kunufaisha wazawa kutokana na kumiliki ardhi,” alisema Profesa Kironde.


MVUTANO kuhusu suala la ardhi umeibuka jana katika mkutano wa wataalamu wa kamati za Serikali Kanda ya Afrika Mashariki uliojadili madini, baadhi ya nchi zimepinga kuingiza ardhi kwenye mambo yanayoshughulikiwa na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Wakichangia katika mkutano huo kwa nyakati tofauti, wajumbe walisema itakuwa ngumu kwa baadhi ya nchi kuingia kuingiza suala hilo kwenye mambo ya EAC, kwa sababu bado ndani ya nchi hizo kuna migogoro ya ardhi.
Wakati baadhi ya wajumbe wakipinga hilo, wengine kutoka Uganda walisema haiwezekani nchi wanachama kuogopa kuingiza suala hilo kutokana na kuonyesha maendeleo mazuri.

Hata hivyo, wajumbe kutoka nchi ya Kenya walionyesha wasiwasi wa uharaka wa kuingia kuingiza ardhi kwenye masuala ya EAC kutokana na mapigano yanayotokea ndani ya baadhi ya nchi wanachama.

“Itakuwa ajabu kuingiza shirikisho la ardhi katika jumuiya wakati nchi za Rwanda Burundi na Tanzania zikionyesha kuwa na ugomvi wa ardhi na wawekezaji,” alisema Mkuu wa Sera ya Mipango na Ardhi kutoka Ethiopia, Dk John Kangwanja.

Dk Kangwanja alisema kama hatua hiyo itafikia, kuna nchi zinaweza kuathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na migogoro ambayo inaendelea kujitokeza baina ya wazawa na wawekezaji.

Wakati suala hilo lilipokuwa likizidi kuzua mvutano kwenye ukumbi, wawakilishi wa Tanzania wakiongozwa na Naibu Waziri wa Fedha, Gregory Teu, walionekana kutochangia chochote huku waziri akiulizwa suala hilo kutoa maelezo alijibu kuwa hana maelezo.

Wachiangiaji hao walisema Sheria ya mwaka 1995 na Sera ya Ardhi ya Tanzania, inapishana kwa kiasi kikubwa kutokana na kupitwa na wakati.Mhadhiri kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi (ARU), Profesa Lucugga Kironde, alisema Tanzania ikikubali kuingiza suala hilo, itarajie kukumbwa na migogoro mikubwa kutokana na nchi nyingi za jumuiya hiyo zinanyemelea baada ya kwao kukumbwa na uhaba.

Profesa Kironde alisema haiwezekani Tanzania ikiingia kwenye shirikisho bila kufanya marekebisho ya sheria ya ardhi, Watanzania wataendelea kuonekana maskini huku wachache kutoka EAC wakinufaika.

“Afrika ina rasilimali za kutosha kila mahali hasa madini,umefika wakati kufuatilia kwa makini sheria ya ardhi ili mikataba ya nchi iweze kunufaisha wazawa kutokana na kumiliki ardhi,” alisema Profesa Kironde.

Friday, February 17

zambia

Zambia fulfills destiny and wins Africa Cup of Nations

Zambia won their first African title after beating Ivory Coast 8-7 on penalties during the final match of the Orange Africa Cup of Nations played at Stade de l’Amitie in Libreville, Gabon. The match had ended goalless after extra time with Didier Drogba missing a penalty in the 69th minute during a pulsating game befitting a final.

Tiote, Bony, Bamba, Gradel , Drogba, Tiene, Ya Kona, converted for Ivory Coast and Kolo Toure and Gervinho missed while Chris Katongo, Mayuka, Chansa, Felix Katongo, Mweene, Sinkala, Lungu converted for Zambia while Kalaba missed before Stoppila Sunzu won it for Zambia.

Zambian goalkeeper Mweene was brilliant throughout the game and deservedly saved Kolo Toure’s spot kick leaving the Elephants still searching for an African title since 1992.

After an impressive closing ceremony display which thrilled the 28th edition of Orange Africa Cup of Nations had kicked off on an equally upbeat tempo with Zambian captain Christopher Katongo forcing Ivorian defender Siaka Tiene to concede a corner kick in the first minute of the game. Zambia worked out a well laid set piece that could have seen the fastest goal but Nathan Sinkala shot was too close to Barry Copa in goal for the Ivorians who dived to his right and smothered the shot hit from inside the box.

Zambia was forced to pull out Joseph Musonda through injury in the 10th minute to be replaced by Henri Nyambe Mulenga and Chipolopolo maintained their early domination of the Elephants. Emmanuel Mayuka headed onto the roof of the net after Chisamba Lungu had found him with a chip as Zambia continued attacks on Ivorian goal.

Ivory Coast’s best chance could have brought the game’s opening goal. One swift move in the 29th minute ended up with Didier Drogba shook off a defender before back heeling to Yaya Toure but the midfielder side footed past Kennedy Mweene’s right-hand post missing the goal by mere centimeters. Zambia had the crowd cheering as their neat passing game left the Elephants second best for the greater part of the first half. Katongo, Mayuka, Chansa and Sinkala a constant menace to the Ivorian back four. The Ivorian midfield of Chiek Tiote, Yaya Toure. Didier Zokora and Kalou was struggling to keep up with the nimble Zambia midfield anchored by Rainford Kalaba

Ivorians started the second half more attack minded and went close from a free-kick after Sinkala fouled Souleyman Bamba . The chip from Tiote was flicked on just beyond on rushing Yaya Toure at the far post. Gervinho came alive on the right flank and was soon making some fruitful runs as the Elephants woke up from their slumber.

Ivorians were awarded a penalty in the 69th minute after Gervinho went down under a challenge from Chansa. Drogba sent his effort over the cross bar and the drama at Stade de l’Amitie continued. At the other end Katongo’s rode a couple of tackles but he did not get the free-kick he was looking for from a Zokora challenge as another Chipolopolo chance went begging. Both coaches Herve Renard for Zambia and Francois Zahoui made changes as the game approached the last twenty minutes. Felix Katongo replaced Henri Nyambe Mulenga while Zokora made way for Didier Ya Konan.

With minutes remaining Ivory Coast almost won it when a flick on from substitute Wilfried Bony who replaced Yaya Toure, found another substitute Max Gradel but he dragged his shot wide as keeper Mweene came off his line.

Zambia were denied by a goal saving timely tackle from Kolo Toure in added time as Mayuka ran onto a delightful ball played in by Chansa. Just as Mayuka was about to shoot Kolo toe-pocked the ball away and the match went into extra time and penalties before Sunzu scored the winning penalty that gave the Southern African side their first title after appearing in their third final.

Tuesday, February 7

Juma Nature avunja ukimya


JUMA Nature amevunja ukimya na kurejea kwa kishindo kwenye muziki ambapo amesisitiza kuwa mwaka huu amepania kuachia kazi za nguvu pamoja na shoo zisizokwisha za Afrika Mashariki kufufua soko lake.

Msanii huyo mahiri wa Bongo ambaye ni kiongozi wa Wanaume Halisi amesema kundi hilo limekamilisha albamu yao ambayo wataitaja miezi michache ijayo, lakini baadhi ya nyimbo tayari zipo redioni zikifanya vizuri.

Muda mwingi nilitulia na wenzangu tulikuwa tunaangalia upepo unavyokwenda na jinsi ya kuibuka tena na kufanya mambo ya uhakika zaidi, kukubalika na mashabiki hasa wa Afrika Mashariki, hatuangalii Tanzania peke yake. Albam za awali za Nature ni 'Nini chanzo' (2001), 'Ugali' (2003), 'Ubinadamu kazi' (2005), 'Zote story' (2006) na 'Tugawane Umaskini' (2009).

Staa huyo alisema kwa ushirikiano wa Dollo, Richie One, JB aliyekuwa Mabaga Fresh, Bob Q, D. Chief, Malipo, Kaka Man, Mzimu na Eddo wanakuja na kazi za mseto ambao mashabiki watajionea tofauti na kuamua.

Nyimbo ambazo tayari zimekamilika ni 'TMK', 'Able' na 'Mguu nje Mguu ndani remix' ambapo kazi kubwa imefanywa na Dolo, KR Mullah na JB.

Nature anasema Halisi Studio ni mali yake na itatumika kutengeneza kazi nyingi zake binafsi na kundi.
Amekiri kuwa studio yake ni ya kawaida kwa mtazamo wa haraka lakini ina vifaa vichache vyenye uwezo mkubwa na baadhi ya wasanii wameanza kufanyia kazi na wanataka kujiondoa katika mfumo wa kutegemea studio za watu.

Studio ipo wazi kwa wasanii wote na siyo Mwanaume Halisi pekee,anasema Nature na kuongeza kuwa licha ya yeye kuwa ndiye prodyuza, lakini wenzake katika kundi pia wanafanya kazi hiyo na wana mpango wa kumpata mtaalam zaidi.

Msanii huyo ambaye kesho jumapili atakuwa na shoo ya pamoja na msanii wa Kenya, Nameless kwenye Ukumbi wa Dar Live, Mbagala jijini Dar es Salaam, alisema; Hii shoo imekuja wakati muafaka kwani hata sisi tunataka kujipima baada ya kujifua kwa muda mrefu.

Thursday, February 2

Posho za wabunge mjadala kila kona - Mwananchi


DK SLAA ATAKA RAIS AZIFUTE, CAG AZISHANGAA, PINDA, MAKINDA WATAKIWA KUJIUZULU
KITENDO cha Rais Jakaya Kikwete kumruka Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Spika wa Bunge, Anne Makinda kuhusu posho za wabunge, kimeibua mjadala mzito nchini, huku wasomi na wanasiasa akiwamo Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa wakimtaka mkuu huyo wa nchi azifute na kulivunja Bunge mara moja kuthibitisha msimamo wake. Juzi, ikiwa ni siku moja baada ya Pinda kusema tayari Rais Kikwete amesaini kuidhinisha ongezeko la posho za vikao (sitting allowance) za wabunge kutoka Sh 70,000 hadi Sh200,000 kwa siku, Ikulu ilitoa taarifa ikisema Rais Kikwete hakuwahi kusaini nyongeza hiyo bali alitaka Waziri Mkuu atumie busara katika kupatia suluhu suala hilo.

Wakati Ikulu ikitoa taarifa hiyo juzi jioni, tayari mchana wa siku hiyo, Spika wa Bunge, Anne Makinda aliitisha mkutano wa waandishi wa habari na kusema, "Siyo kwamba tutaanza kutoa, tulishaanza kutoa na Rais ameshatoa kibali chake na mbunge atalipwa katika vikao tu, si kila siku na tena baada ya kukaa kwenye vikao na kusaini."

Mgongano huo wa kauli kuhusu posho hizo ulijitokeza tangu Novemba mwaka jana baada ya Mwananchi kuripoti kwa mara ya kwanza kwamba wabunge waliongezewa posho na Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashillilah kukanusha, akisema Rais hakuwa ameziidhinisha. Hata hivyo, siku tatu baadaye, Spika Makinda alithibitisha juu ya wabunge kuanza kulipwa viwango hivyo vipya vya posho akisema, Rais Kikwete tayari alishaidhinisha zilipwe kwa wawakilishi hao.

Jana, kwa nyakati tofauti wakizungumzia utata huo watu wa kada mbalimbali wakiwamo viongozi wa dini, wanasiasa na wasomi, walielezea mkanganyiko huo kama kitendo cha hatari katika kipindi hiki ambacho nchi inatikiswa na mgomo wa madaktari.

Wanasiasa Katibu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alienda mbali zaidi kwa kusema kutofautiana kwa viongozi hao wa Serikali na Bunge kuhusu suala la posho mpya za wabunge, ni sawa na kutokuwa na Serikali.

Alifafanua kwamba posho hizo ni sawa na bomu ambalo limetegwa na sasa linakaribia kulipuka wakati wowote. “Rais na Waziri Mkuu wanatofautiana kuhusu posho, hivi hapo kuna Serikali kweli? Ndiyo maana tunasema posho hizi ni bomu litakalolipuka wakati wowote,” alionya Dk Slaa. Dk Slaa alisema wabunge hao kulipwa posho ya Sh330,000 huku wakiwa wamekaa kwenye viyoyozi wakati madaktari wanafanya kazi katika mazingira magumu ni laana. “Laana hii, ndiyo inawafanya Rais Jakaya Kikwete na Waziri Mkuu Mizengo Pinda wanatofautiana na bado wasubiri sasa bomu litakalolipuka,” alisema Dk Slaa.

Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Julius Mtatiro alisema Rais Kikwete anatakiwa kulivunja Bunge kwa kitendo hicho cha taasisi hiyo kujiongezea posho kinyemela. “Kama ingekuwa enzi za Mwalimu Julius Nyerere, kitendo hicho kilichotokea cha kujiongezea posho kingesababisha Bunge kuvunjwa, lakini, kwa Rais wetu mambo yataendelea kama kawaida,” alisema Mtatiro.

Kwa upande wa CCM, kimetoa tamko kikisema huu si wakati wa kupandisha posho na kupongeza hatua ya Rais Kikwete kuweka mambo wazi kwamba hakuzithibitisha. Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nauye alisema jana katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuwa huu si muda mwafaka kwa wabunge kujiongezea posho.

CAG abaki mdomo wazi Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG), Ludovick Utouh alisema kuwasilishwa kwa taarifa za mchanganyiko kuhusu posho za wabunge kunachanganya wananchi. Akizungumza na Mwananchi jijini Dar es Salaam jana, Utouh alisema wabunge hawawezi kulipana posho bila Rais kuidhinisha.

“Ninachojua mimi ni kwamba, Serikali haiwezi kulipa wabunge bila ya fedha kuidhinishwa na Rais na kwamba hakuna kibali kinachotolewa zaidi yake, kutokana na hali hiyo taarifa zao zinatuchanganya,"alisema Utouh. Viongozi wa dini Rais wa Baraza la Maaskofu Tanzania (TEC), Askofu Yuda Thadeus Ruwaichi, alisema kugongana kwa kauli hizo, kunatoa taswira kwamba kuna jambo linafichwa kuhusu suala hilo. “Kugongana kwa hizi kauli kunaonyesha wazi kuwa, kuna kitu kimejificha hapa..., ni vyema ukweli ukaelezwa,” alisema Ruwaichi.

Alisema kuongeza posho za wabunge katika wakati huu ambapo kuna kada nyingi za utumishi wa umma kama walimu na madaktari wakiwa na hoja ambazo hazijapatiwa majibu, hakuleti taswira nzuri kwa Serikali. “Huku kunaonyesha kwamba, hakuna busara katika kufanya maamuzi ya mambo mazito yanayohusu hatima ya taifa hili. Kuchukua uamuzi kama huu wakati huu ambao watumishi wengi wa umma kama madaktari na walimu wana madai mbalimbali, siyo busara kabisa,” alisisitiza Ruwaichi.

Shekhe wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhaji Alhad Mussa Salim alisema kauli hizo tata za viongozi si ishara nzuri kwa mustakabali wa taifa. “Mgongano wa kauli za viongozi siyo sura nzuri. Tunashangaa kuona Mtendaji Mkuu akisema tofauti na bosi wake hiki ni kitu cha kushangaza," alisema Salim.

Wasomi Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Benson Bana alisema kama viongozi hao wa Serikali wanatofautiana kuhusu posho ni ishara kwamba kuna mtikisiko mkubwa wa kiutendaji. Alisema, “Pamoja na kwamba sijafuatilia vizuri viongozi hao kutofautiana katika suala la posho, dalili zinaonyesha kwamba kuna matatizo makubwa katika mihimili hiyo miwili,” alisema Dk Bana. “ Sina tatizo kama wabunge wakiongezewa mishahara yao, lakini kulipwa posho wakiwa kazini ni makosa makubwa,” alisema.

Mhadhiri mstaafu wa Chuo cha Ushirika Moshi, Akwiline Kinabo aliwataka wabunge na Serikali kusoma alama za nyakati kwani posho hizo za wabunge zimewaudhi wananchi kwa kiwango cha kutisha.

Wanasheria, wanaharakati
Mkurugezi Mtendaji wa Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC), Hellen Kijo-Bisimba alisema utawala wa sheria haupo au umekufa kabisa. " Haiwezekani leo mhimili mmoja useme posho za wabunge zimepitishwa, halafu kesho yake mwingine ukanushe, sasa nchi inakwenda wapi?’’ alihoji Bisimba. Wakili wa kujitegemea, Harold Sungusia alisema tatizo kubwa lipo katika Katiba ya nchi ambayo imeshindwa kuonyesha mgawanyo wa madaraka ulipo katika mihimili yetu mitatu ya dola.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Fordia, Buberwa Kaiza amemtaka Rais Kikwete kufuta posho hizo ili kuthibitisha madai yake kwamba hajazibariki.

“Kauli hizi zinawachanganya wananchi maana haiwezekani Rais atoe msimamo wake halafu kiongozi wa chini yake apinge tamko la Rais, ni dhahiri kwamba Rais anaonekana kushindwa kutekeleza wajibu wake na kusimamia mamlaka yake kwa madaraka aliyonayo,”alisema Kaiza.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake (Tamwa), kimemtaka Rais aeleze ni wapi wabunge wamepata idhini ya kupitisha posho badala ya kusema tu kwamba hajazibariki na kukaa kimya.

“Haiwezekani wabunge wajipitishie posho bila idhini ya Rais, maana hapa Serikali inataka kutuchanganya tu. Waziri Mkuu ni kiongozi wa Serikali, Rais ni kiongozi wa Serikali, lakini kila mmoja anasema lake, hii maana yake nini?" alihoji Mkurugenzi wa shirika hilo, Ananilea Nkya

Mjini Moshi, baadhi ya wakazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro wamemtaka Waziri Mkuu na Spika Makinda wajiuzulu kwa kuwaongezea wabunge posho bila idhini ya Rais. Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, walisema Pinda anapaswa kujiuzulu kwa kuwa ameidhalilisha Serikali na Makinda kwa sababu amewasaliti Watanzania maskini.

“Angalau kwa hili Rais ametukuna, lakini bado tunataka Pinda na Makinda wajiuzulu kwa kutoa kauli za kuudhi eti gharama za maisha zimepanda kwa wabunge ndiyo maana posho zipande,”alisema mmoja wa wakazi hao.

Habari hii imeandaliwa na Gedius Rwiza, Patricia Kimelemeta, Fredy Azzah, Raymond Kaminyoge, Shakila Nyerere, Daniel Mwingira, Dar, Moses Mashalla, Arusha na Daniel Mjema, Moshi.